Tuesday, 12 May 2020

MFUMO WA KUANDAA MATOKEO NA RIPOTI ZA TAALUMA (SARPS) A LEVEL



Mfumo wa kuandaa matokeo na ripoti za kitaaluma kwa shule kidato cha tano na sita sasa upo tayari. Kama ulivyo mfumo wa kuandalia ripoti kwa kidato cha I hadi IV pia mfumo huu unachakata matokeo ya aina nane kwa wakati mmoja ambayo ni ripoti ya kila mwanafunzi, mkeka wa matokeo ya wanafunzi unaonesha alama tu, mkeka wa matokeo ya wanafunzi unaonesha madaraja tu, mkeka wa matokeo ya wanafunzi unaonesha alama na madaraja, dondoo ya matokea ya jumla, Orodha ya wanafunzi waliofanya vizuri, Orodha ya wanafunzi waliofanya vibaya na ISAL kama inavyoonesha picha hapa chini Endelea Kupata Zaidi

Wednesday, 6 May 2020

Nguzo za swaumu

Nguzo za swaumu
NGUZO YA KWANZA: Ni kujizuia kufanya mambo yatakayo Haribu swaumu kuanzia kutokeza kwa alfajiri hadi kuzama kwa jua kwa kuingia jioni
Dalili ni kauli yake Mwenyezi Mungu U: {…Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni saumu mpaka usiku…} (Al-Baqarah- Aya 187).

NGUZO YA PILI: Ni kutia nia ya Kufunga
Nako ni kukusudia kwa anayefunga saumu ya kwamba huku kujizuia na vitu vinavyofungua saumu ni ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwa dalili ya kauli ya Mtume (saw): ( Hakika kila jambo analolifanya (mwanadamu) ni kulingamana na nia yake, na hakika kila mtu atalipwa kulingana na alivyonuilia)[Imepokewa na Bukhari na Muslim.] Endelea Kupata Zaidi

Friday, 24 April 2020

Fadhila za swaumu

Swaumu ni Nini?
Saumu Katika Lugha
Ni kujizuia na kujiepusha kufanya jambo fulani.
Saumu Kisheria
Ni kufanya ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu U kwa kujizuia kula, kunywa na kufanya tendo la ndoa kuanzia kutokeza kwa alfajiri hadi kutwa kwa Jua. Endelea Kupata Zaidi

Monday, 20 April 2020

Abu Hurayrah-mpokezi wa hadithi

Mamilioni ya waislam tokea mwanzo mwanzo mwa historia ya kiislam hadi hii leo wanaisoma kauli hii ‘kutoka kwa Bwana Abu Hurayrah radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie amesema, mjumbe wa Mwenyezi Mungu amesema…….”   Endelea Kupata Zaidi

Monday, 20 May 2019

Katika mambo yanayoleta changamoto kubwa kwa walimu katika shule nyingi tangu muda mrefu ni kuandaa ripoti za kitaaluma za wanafunzi. Walimu wa madarasa na wataaluma hujikuta wakiangukia katika wakati mgumu sana mara tu baada ya kusahihisha kazi walizofanya wanafunzi kwenye mitihani yao, iwe ni mitihani ya kila mwezi au ya robo muhula au nusu muhula au ya kumaliza mwaka. Imefikia hatua hata ripoti zenyewe hazitolewi kwa wakati kwa sababu ya kutumia muda mrefu kuchakata matokeo na ripoti za wanafunzi ili kupata nani ameshika nafasi gani kwa wastani na daraja gani kati ya wanafunzi wangapi na mambo mengine mengi ambayo hayawezi kufikiwa lakini ni muhimu sana. Endelea Kupata zaidi

Monday, 12 November 2018

HAQQIY ANDROID APP


Haqqiy blog tumekurahisishia kwa kukutengenezea android app. Unaweza download kupitia link Haqqiy App Sasa 

Monday, 13 February 2017

Huyu Ndiyo Abdullah ibn Abbass- msomi wa umma huu

Abdullah ibn Abbas bin Abdul Muttalib ni mtoto wa ami yake Mtume (SAW). Alizaliwa miaka mitatu kabla ya Hijra.  Na Mtume alipofariki, Abdullah alikuwa na umri wa miaka kumi  na mitatu.   Endelea Kupata Zaidi

Saturday, 9 July 2016

HAQQIY: Vitabu vya Dini


Vitabu vya Dini:
Haqqiy imekurahisishia upatikanaji wa vitabu mbalimbali vya Kiislamu vya wanachuoni wa kuaminika na kufanyiwa tarjama katika lugha ya Kiswahili. Una fursa ya kupata vitabu hivyo sasa na tutaendelea kukusanyia vitabu vingine vingi zaidi Inshaallah.

Thursday, 20 August 2015

Abu Ubaydah ibn Al-Jarraah-mtihani wake ulikuwa mzito !

Alikuwa na umbo la kuvutia, mwembamba na mrefu uso wake mwingi huwa na tabasamu na kuwa na ndevu ziliachana achana.  Alikuwa mkarimu sana mpole na mwenye haya.  Hata hivyo, katika mazingira magumu huwa mkakamavu na mkali mfano wa upanga.
Jina lake kamili ni Amr ibn Abdullah ibn Al-Jarraah...... Endelea Kupata Zaidi

Monday, 20 October 2014

Mvua Kubwa Yanyesha Mtwara


Maeneo Mengi Yaliyopo Wilaya Ya Masasi Yamenyesha Mvua Kubwa Zilizoambatana Na Radi. Mvua Hizo Zilidumu Kwa Muda Wa Taklibani Saa Moja  

Thursday, 23 January 2014

Haqqiy: Hadiyth Ya Al-Jassaasah

Haqqiy: Hadiyth Ya Al-Jassaasah: Hadiyth Ya Al-Jassaasah Imetafsiriwa na Muhammad Faraj Salem Al Saiy Utafiti mwingi uliofanywa na wazungu wenye kufuatilia mam...

Sunday, 17 November 2013

Madrasa Chigugu yachangamka kwa kasi ikiwa ni mwitiko wa kipekee baada kukosekana kwa kitambo kirefu

Miaka takribani Sita sasa kumekosekana  madrasa yenye uhakika kutokana na kuhamishwa Sheykh aliyekuwa akifundisha wakati huo kutokana chuki za vigogo wa kijiji cha Chigugu. Sheykh Abillah  mwenye kipaji cha ufundishaji wa Elimu ya dini ya Kiislam, ujuzi wa kuwavuta watu wenye rika tofauti tofauti kuwa na ari ya kusoma dini alijikuta akinyanyasika, kutukanwa na kufukuzwa kwa kashifa, kutokana na Nuru aliyokuwa akiieneza katika jamii hiyo ilyo totoro na Ushirikina, Ulevi, Zinaa na Uislamu wa kurithishana.  Endelea Kupata Zaidi>>>>