Miaka takribani Sita sasa kumekosekana madrasa yenye uhakika
kutokana na kuhamishwa Sheykh aliyekuwa akifundisha wakati huo kutokana
chuki za vigogo wa kijiji cha Chigugu. Sheykh Abillah mwenye kipaji cha
ufundishaji wa Elimu ya dini ya Kiislam, ujuzi wa kuwavuta watu wenye
rika tofauti tofauti kuwa na ari ya kusoma dini alijikuta akinyanyasika,
kutukanwa na kufukuzwa kwa kashifa, kutokana na Nuru aliyokuwa
akiieneza katika jamii hiyo ilyo totoro na Ushirikina, Ulevi, Zinaa na
Uislamu wa kurithishana.
Mafanikio yaliokuwa yakipanda kwa
kasi, na juhudi za wazi za Sheykh Abillah na wenzake walioamua
kuikomboa jamii yao iliyokithiri katika ujinga yakadhoofishwa na na
Mamwenye wachache wa mji na kusababisha kizuri kuwa kibovu.
Waliyeshuhudia tukio la kufedheheshwa Sheykh walilaumu hatua iliyofikia
ya kumwagiwa Pombe mahala pa Kuswalia, na matusi kejeli za Usuni n.k.
Tunamuomba Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) amjaalie subira.
Baada
ya kipindi hicho chote Chigugu yaanza madrasa kwa watoto, watu wazima
wake kwa waume baada ya kituo kimoja cha Kisunnah kung'amua tatizo hilo
na kuamua kulivalia njuga kwa hali na mali.Imam wa Masjid Al -Ansaar
Chigugu Sheykh Hamisi Nachembe amehakikisha ya kwamba awamu hii madrasa
itasimamiwa vizuri. Kwa upande wake mwalimu wa mmoja kati yao Ustaadh
Juma naye ameamua kujitoa kweli kweli katika jambo hili kwa kusema hii
ni sehemu ya fadhila na Mas'ul kwa Allah (Subhaanahu wa Ta'ala).
Allah
(S.W) awatilie wepesi walewaliojitoa kwa ajili ya kuitafuta fardhi hii
ya elimu na wengine wengi wawe wenye kujitokeza. Aamiin!