Abu Ubaydah ibn Al-Jarraah-mtihani wake ulikuwa mzito !
Alikuwa
na umbo la kuvutia, mwembamba na mrefu uso wake mwingi huwa na tabasamu na kuwa
na ndevu ziliachana achana. Alikuwa mkarimu sana mpole na mwenye
haya. Hata hivyo, katika mazingira magumu huwa mkakamavu na mkali mfano
wa upanga.