Wednesday 6 May 2020

Nguzo za swaumu

Nguzo za swaumu
NGUZO YA KWANZA: Ni kujizuia kufanya mambo yatakayo Haribu swaumu kuanzia kutokeza kwa alfajiri hadi kuzama kwa jua kwa kuingia jioni
Dalili ni kauli yake Mwenyezi Mungu U: {…Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni saumu mpaka usiku…} (Al-Baqarah- Aya 187).

NGUZO YA PILI: Ni kutia nia ya Kufunga
Nako ni kukusudia kwa anayefunga saumu ya kwamba huku kujizuia na vitu vinavyofungua saumu ni ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwa dalili ya kauli ya Mtume (saw): ( Hakika kila jambo analolifanya (mwanadamu) ni kulingamana na nia yake, na hakika kila mtu atalipwa kulingana na alivyonuilia)[Imepokewa na Bukhari na Muslim.] Endelea Kupata Zaidi