Maana ya swaumu
Saumu
Katika Lugha
Ni kujizuia na kujiepusha
kufanya jambo fulani.
Saumu
Kisheria
Ni kufanya ibada kwa
ajili ya Mwenyezi Mungu U kwa kujizuia kula, kunywa na kufanya tendo la ndoa
kuanzia kutokeza kwa alfajiri hadi kutwa kwa Jua.
Fadhla za swaumu
Asema Mwenyezi Mungu { Enyi mlo Amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andkikwa
walio kuwa kabla yenu ili mpate kucha mungu.(Mfunge) siku maalumu za
kuhisabika.na atakaye kuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimiza
hisabu katika siku nyingine. Na wale wasio weza watoe fidiya kwa kumlisha
masikini na atakaye fanya wema kwa kujitolea, Basi ni bora kwake na Mkifunga ni
bora kwenu kama mnajua.} (Al-Baqarah- Aya 183: 185)
Saumu ina fadhila kubwa
sana, na thawabu nyingi mno tena maradufu, na kwa hakika Mwenyezi Mungu
ameinasibisha saumu kwake yeye kwa ajili ya kuipa utukufu na kuitukuza. Katika
Hadithi Al-Qudsy iliyopokewa na swahaba Abu Hurayrah, t Anasema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): “kila tendo la
mwanadamu huongezwa malipo ya wema wake mara kumi ya mfano wa jema hilo
alilolitenda mpaka hufikia kuongezwa (huku kwa malipo ya wema huo) hadi nyogeza
mara sabiini. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Isipokuwa saumu, kwani hiyo saumu
ni yangu mimi, na mimi ndiye mwenye kutoa malipo yake; (mja wangu) anaacha
matamanio yake na chakula chake kwa ajili yangu. Katika kufunga saumu kuna furaha
mbili: furaha (ya kwanza) ni pale anapofungua saumu aliyefunga, na furaha (ya
pili) ni wakati (aliyefunga) atakapokutana na Mola wake. Na harufu inayotoka
kwenye kinywa cha aliyefunga ni nzuri sana mbele ya Mwenyezi Mungu kushinda
harufu ya miski”. [Imepokewa na Bukhari
na Muslim.]
Hekima za kufaradhishwa
kufunga
1)
Ni
mja kupata ucha Mungu kwa kuitika amri ya Mola wake amri hii ya kufunga na
kujitolea muhanga kuitekeleza sheria ya Mola wake. Anasema Mwenyezi Mungu
Mtukufu: {Enyi mlioamini! Mmelazimishwa
kufunga (saumu) kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha
Mungu} (Al-Baqarah-
Aya 183).
2)
Kuipa
nafsi mazoezi ya kusubiri, na kujipa nguvu ili kuweza kushinda matamanio.
3)
Kujizoezesha
mtu kufanya hisani, na kuwa na huruma kwa wanaohitaji masikini na mafukara; kwa
sababu mtu anapoonja hisia ya njaa itampelekea mtu huyu kuwa na moyo laini na
kuhisi jinsi wanavyohisi ndugu zake wahitaji wasio na chochote cha kula.
4)
Kupata
raha ya kiwiliwili na afya bora katika kufunga.
Hukumu ya kufunga swaumu Imegawanyika saumu ambayo
Mwenyezi Mungu ameiweka katika sheria vigawanyo vifuatavyo:
1.
Saumu
ya wajibu
Nayo iko sampuli mbili:
i)
Saumu
aliyoiwajibisha Mwenyezi Mungu U kuanzia mwanzo wake (mwanzo wa hii saumu –
chanzo chake) kwa mja wake, nayo ni saumu ya kufunga mwezi wa ramadhani, na
saumu hii ni nguzo moja wapo katika nguzo za Uislamu.
ii) Saumu ambayo kwamba mja ndiye anayekuwa sababu
ya kuwajibishwa yeye mwenyewe kuifunga, kama vile saumu ya nadhiri na saumu ya
kafara.
2.
Saumu
za Sunna
Nayo ni kila saumu ambayo
kwamba sheria ya kiislamu imependekeza saumu hiyo kufungwa, kama kufunga siku
ya Jumatatu na Alhamisi, na kufunga siku tatu za kila mwezi, na kufunga siku ya
A’shura, na kufunga masiku kumi ya mwanzo wa mwezi wa Dhilhijja, na kufunga siku
ya A’rafah.
Masharti ya mtu
kuwajibika Kufunga
1.
Uislamu:
Haimlazimu kafiri kufunga.
2.
Kubaleghe:
Sio lazima kwa mtoto mdogo kufunga, lakini huamrishwa kufunga akiwa anaweza ili
kumpa mazoezi ya saumu naye azoee.
3.
Kuwa
na akili: Sio wajibu kwa mwendawazimu kufunga.
4.
Uwezo
wa kufunga: Sio wajibu kufunga kwa mtu ambaye hawezi kufunga (labda amekuwa
mzee sana ama afya yake haimruhusu kuhimili saumu).
Kufunga Ramadhani
Kufunga mwezi wa
Ramadhani ni nguzo mojawapo kati ya nguzo za Uislam, na ni lazima kufunga mwezi
huu. Mwenyezi Mungu amewalazimisha waja wake kufunga.
Anasema Mwenyezi Mungu
mtukufu: {Enyi mlioamini! Mmelazimishwa
kufunga (Saumu) kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha
Mungu} (Al-Baqarah
–Aya 183).
Na amesema Mtume (saw): “Uislamu umejengwa kwa mambo matano” [Imepokewa na Bukhari.] na
akataja miongoni mwa mambo hayo: “kufungu
saumu ya mwezi wa Ramadhani”.
Fadhila za Mwezi wa
Ramadhani
1.
Kufunga
na kusimama usiku katika mwezi wa Ramadhani hali ya kuwa mtu ana imani na
kutaraji malipo basi husamehewa madhambi yake yote yaliyopita. Amesema Mtume
Mtume (saw): “Atakayefunga mwezi wa
Ramadhani hali ya kuwa ana imani na kutaraji malipo husamehewa yote
yaliyotangulia katika madhambi aliyoyafanya” [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
Na akasema Mtume Mtume (saw): “Atakayesimama (kuswali usiku) katika mwezi
wa Ramadhani hali ya kuwa na imani na kuridhia atasamehewa yote yaliyotangulia
katika madhambi aliyoyafanya” [
Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
2.
Ndani
ya mwezi wa Ramadhani kuna ‘Lailatu Al-Qadr’ – ‘Usiku wenye hishima kubwa’
ambao kwamba Mwenyezi Mungu amesema kuhusu usiku huu: <> (Al-Qadr – Aya 3).
3.
Atakayesimama
usiku huu basi atasamehewa madhambi yake yote yaliyotangulia. Amesema Mtume
Mtume (saw): “Yoyote atakayesimama
usiku wa cheo hali ya kuwa na imani na kuridhia atasamehewa yote yaliyotangulia
katika madhambi yake” [Imepokewa na
Bukhari na Muslim.].
4.
Kufanya
U’mrah ndani ya mwezi wa Ramadhani ni sawa na kuhiji pamoja na Mtume Mtume (saw). Amesema Mtume Mtume (saw): “Kufanya U’mrah ndani ya Ramadhani ni sawa
na kuhiji pamoja nami” [Imepokewa na
Muslim.].
5.
Mwezi
wa Ramadhani hufunguliwa milango ya peponi, na hufungwa milango ya motoni, na
hutiwa minyororo (hufungwa) mashetani, na nafsi huelekea katika kufanya mambo
ya kheri. Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtume (saw): “Unapoingia mwezi wa Ramadhani hufunguliwa milango ya
mbinguni, na hufungwa milango ya motoni, na hutiwa minyororo mashetani” [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
6.
Mwezi
wa Ramadhani ni mwezi wa Qur’an, na ndiyo mwezi ulioteremshwa Qur’an, kwa hivyo
inafaa kuzidisha kusoma Qur’an ndani ya mwezi huu, Anasema Mwenyezi Mungu
Mtukufu: {Mwezi wa Ramadhani ni mwezi
ambao imeteremshwa Qur’an katika mwezi (huo)} [Al-Baqarah – Aya 185]
7.
Mwezi
wa Ramadhani ni mwezi wa ukarimu na kutoa sana sadaka. Imepokewa kutoka kwa Ibn
Abbas t akisema: “Alikuwa
Mtume (saw) mkarimu sana kushinda watu wote katika kufanya mambo ya kheri,
na alikuwa mkarimu zaidi wakati wa mwezi wa Ramadhani, hakika Jibril alikuwa
akikutana na Mtume kila mwaka katika mwezi wa Ramadhani mpaka uishe mwezi, basi
ikawa Jibril wakati kama huu anampitishia Mtume (anaregelea kusoma pamoja na
Mtume) Qur’an, basi pindi Mtume anapokutana na Jibril alikuwa Mtume mkarimu
sana katika mambo ya kheri kushinda upepo mkali uliotumwa” [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
Kitu gani
kitathibitishia kuingia kwa Mwezi wa Ramadhani?
Inathibiti kuingia mwezi
wa Ramadhani kwa kuonekana kwa mwezi, utakapoonekana mwezi baada ya kuzama kwa
jua siku ya ishirini na tisa katika mwezi wa shabani, basi itakuwa umeshaingia
mwezi wa Ramadhani, na ikiwa haukuonekana mwezi baada ya kuzama kwa jua siku ya
thelathini ya mwezi wa shabani, au hali ikatanda wingu bila kuonekana mwezi, au
kukawa na vumbi kali, au kukawa na moshi (wa umande wa baridi), itakamilishwa
mwezi wa shabani siku thelathini; kwa kauli ya Mtume Mtume (saw): “Fungeni kwa kuonekana kwa mwezi na fungueni kwa
kuonekana kwa mwezi, na ikiwapitikieni kwamba hamuuoni mwezi basi hisabuni siku
thelathini (kukamilika shabani)” [Imepokewa
na Bukhari na Muslim.].
Ruhusa za mtu kula
ndani ya mwezi wa Ramadhani
Kula ndani ya mwezi wa
Ramadhani (yaani nyakati za mchana) ni haramu na ni katika madhambi makubwa, na
atakayefungua siku moja tu bila ya udhuru wowote na wala asitubie basi
hatokubaliwa saumu ya mwaka mzima hata akifunga, kwa kauli ya Mtume Mtume (saw): “Atakayekula siku moja katika mwezi wa Ramadhani bila ya
ruhusa yoyote aliyoiruhusu Mwenyezi Mungu hatokubaliwa mtu huyu saumu ya mwaka
mzima” [Imepokewa na Abuu Daud.].
Na dhambi la kula ndani
ya mwezi wa Ramadhani ni kubwa sana, kutoka kwa Abi Umaamatu Albaahiliy
amesema: “Nilimsikia Mtume Mtume (saw)
yuwasema: Pindi mimi nilikuwa nimelala walinijia watu wawili ….., kisha
wakaniondokea, nikawa nimefika mahali pa watu ambao wamefungwa sehemu zao za
nyuma ya magoti wametanuliwa sehemu za pambizoni mwa midomo yao, sehemu zao za
pambizoni mwa midomo inatona damu. Akasema: Nikauliza: Ni kina nani watu hao?.
Akasema: Hao ni wale ambao kwamba wanakula kabla ya kukamilika kwa saumu zao) [Imepokewa na Ibnu Hibbaan.]
Hali ya watu wema
katika mwezi wa Ramadhani
Kielelezo cha watu wema ni
Mtume Muhammad (saw)
Asema Ibnul-Qayyim Mungu
amrehemu (Na alikuwa mtume (saw) Katika muongozo wake kwnye mwezi mtukufu wa Ramadhani
huzidisha sampuli nyingi za Ibada, Alikuwa jibril (AS) Akimsomesha yeye Qur’ani
katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Alikuwa anapo kutana na jibril ni mkarimu
zaidi kwa mambo ya kheri kushinda upepo uliotumwa, na Alikuwa ni mtowaji zaidi
wa kushinda watu na Ramadhani alikuwa zaidi akizidisha kutoa sadaka na kufanya
wema na kusoma Qur’ani na kuswali na kumtaja Mwenyezi Mungu na kukaa Itikafu na
alikuwa akiukhusisha mwezi wa Ramadhani kwa ibada Asiyo yakhusisha katika miezi
mengine mpaka mara nyingine akiunganisha saumu ili akapate masaa mengi ya
kufanya Ibada).
Watu wema na kusoma Qur’ani
katika mwezi wa Ramadhani
Imependekezwa katika
nyakati bora kama Mwezi wa Ramadhani haswa katika masiku kuzidisha kusoma
Qur’ani kwa ijili yakufaidika kwa Wakati.
Huyu hapa imamul –Bukhari
mungu amrehemu alikuwa usiku wa kwanza wa mwezi wa Ramadhani Wakijikusanya
kwake marafiki zake akiwaswalisha na akisoma kila rakaa aya ishirini, akifanya
hivyo mpaka akimaliza Qur’ani. Na alikuwa wakati wa maladaku akisoma kati ya
nusu na thuluthi ya Qur’ani, na akikhitimisha Qur’ani wakati wa kufunguwa saumu
kila usiku na Akisema kila unapo maliza msahafu kuna dua isiyo rudishwa
Na imepokewa kuwa imamu
shafi alikuwa akikhitisha Qur’ani mara sitini mbali na zile anazo soma katika
Swala