Nguzo za swaumu
NGUZO YA KWANZA: Ni kujizuia kufanya mambo yatakayo Haribu swaumu
kuanzia kutokeza kwa alfajiri hadi kuzama kwa jua kwa kuingia jioni
Dalili ni kauli yake Mwenyezi Mungu U: {…Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa
alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni saumu mpaka usiku…} (Al-Baqarah- Aya 187).
NGUZO YA PILI: Ni kutia nia ya Kufunga
Nako ni kukusudia kwa anayefunga saumu ya kwamba huku kujizuia
na vitu vinavyofungua saumu ni ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwa
dalili ya kauli ya Mtume (saw): (
Hakika kila jambo analolifanya (mwanadamu) ni kulingamana na nia yake, na
hakika kila mtu atalipwa kulingana na alivyonuilia)[Imepokewa na Bukhari na Muslim.] Endelea Kupata Zaidi