Katika mambo yanayoleta changamoto kubwa kwa walimu katika shule nyingi tangu muda mrefu ni kuandaa ripoti za kitaaluma za wanafunzi. Walimu wa madarasa na wataaluma hujikuta wakiangukia katika wakati mgumu sana mara tu baada ya kusahihisha kazi walizofanya wanafunzi kwenye mitihani yao, iwe ni mitihani ya kila mwezi au ya robo muhula au nusu muhula au ya kumaliza mwaka. Imefikia hatua hata ripoti zenyewe hazitolewi kwa wakati kwa sababu ya kutumia muda mrefu kuchakata matokeo na ripoti za wanafunzi ili kupata nani ameshika nafasi gani kwa wastani na daraja gani kati ya wanafunzi wangapi na mambo mengine mengi ambayo hayawezi kufikiwa lakini ni muhimu sana.
Endelea Kupata zaidi