Sunday 17 November 2013

Madrasa Chigugu yachangamka kwa kasi ikiwa ni mwitiko wa kipekee baada kukosekana kwa kitambo kirefu

Miaka takribani Sita sasa kumekosekana  madrasa yenye uhakika kutokana na kuhamishwa Sheykh aliyekuwa akifundisha wakati huo kutokana chuki za vigogo wa kijiji cha Chigugu. Sheykh Abillah  mwenye kipaji cha ufundishaji wa Elimu ya dini ya Kiislam, ujuzi wa kuwavuta watu wenye rika tofauti tofauti kuwa na ari ya kusoma dini alijikuta akinyanyasika, kutukanwa na kufukuzwa kwa kashifa, kutokana na Nuru aliyokuwa akiieneza katika jamii hiyo ilyo totoro na Ushirikina, Ulevi, Zinaa na Uislamu wa kurithishana.  Endelea Kupata Zaidi>>>>