Ash-Shu’araa: 26

الشُّعَرآء
Ash-Shu’araa: 26


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ



طسم ﴿١﴾
1. Twaa Siyn Miym.



تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ ﴿٢﴾
2. Hizo ni Aayaat za Kitabu kilicho bayana.



لَعَلَّكَ بَاخِعٌ نَّفْسَكَ أَلَّا يَكُونُوا مُؤْمِنِينَ ﴿٣﴾
3. Huenda utaiangamiza nafsi yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa sikitiko kwamba hawawi wenye kuamini.



إِن نَّشَأْ نُنَزِّلْ عَلَيْهِم مِّنَ السَّمَاءِ آيَةً فَظَلَّتْ أَعْنَاقُهُمْ لَهَا خَاضِعِينَ ﴿٤﴾
4. Tungetaka Tungewateremshia kutoka mbinguni Aayah, (muujiza, ishara) kisha zingebakia shingo zao zenye kuinyenyekea.



وَمَا يَأْتِيهِم مِّن ذِكْرٍ مِّنَ الرَّحْمَـٰنِ مُحْدَثٍ إِلَّا كَانُوا عَنْهُ مُعْرِضِينَ ﴿٥﴾
5. Na hauwafikii ukumbusho wowote ule mpya kutoka kwa Ar-Rahmaan isipokuwa walikuwa ni wenye kuupuuza.



فَقَدْ كَذَّبُوا فَسَيَأْتِيهِمْ أَنبَاءُ مَا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿٦﴾
6. Basi kwa yakini wamekadhibisha, basi itawafikia khabari ya yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.



أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَى الْأَرْضِ كَمْ أَنبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوْجٍ كَرِيمٍ ﴿٧﴾
7. Je, hawaioni ardhi, mimea mingapi Tumeiotesha humo ya kila aina nzuri?



إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٨﴾
8. Hakika katika hayo pana Aayah (ishara, zingatio n.k.), lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.



وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿٩﴾
9. Na hakika Rabb wako bila shaka Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika,Mwenye kurehemu.



وَإِذْ نَادَىٰ رَبُّكَ مُوسَىٰ أَنِ ائْتِ الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿١٠﴾
10. Na Rabb wako Alipomwita Muwsaa kwamba: “Nenda kwa watu madhalimu.”



قَوْمَ فِرْعَوْنَ ۚ أَلَا يَتَّقُونَ ﴿١١﴾
11. “Watu wa Fir’awn; je, hawamchi Allaah?”



قَالَ رَبِّ إِنِّي أَخَافُ أَن يُكَذِّبُونِ ﴿١٢﴾
12. (Muwsaa) Akasema: “Rabb wangu! Hakika mimi nakhofu wasije kunikadhibisha.”



وَيَضِيقُ صَدْرِي وَلَا يَنطَلِقُ لِسَانِي فَأَرْسِلْ إِلَىٰ هَارُونَ ﴿١٣﴾
13. “Na kinadhikika kifua changu, na wala ulimi wangu haukunjuki vizuri basi mtume Haaruwn.”



وَلَهُمْ عَلَيَّ ذَنبٌ فَأَخَافُ أَن يَقْتُلُونِ ﴿١٤﴾
14. “Nao wana (madai ya) dhambi juu yangu, basi nakhofu wasiniue.”



قَالَ كَلَّا ۖ فَاذْهَبَا بِآيَاتِنَا ۖ إِنَّا مَعَكُم مُّسْتَمِعُونَ ﴿١٥﴾
15. (Allaah) Akasema: “Hapana! Nendeni kwa Aayaat (ishara, dalili) Zetu, hakika Sisi Tuko pamoja nanyi Wenye kusikiliza.”



فَأْتِيَا فِرْعَوْنَ فَقُولَا إِنَّا رَسُولُ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٦﴾
16. “Basi mfikieni Fir’awn, na mseme: “Hakika sisi ni Rasuli wa Rabb wa walimwengu.”



أَنْ أَرْسِلْ مَعَنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿١٧﴾
17.  “Waachilie wana wa Israaiyl waondoke pamoja nasi.”



قَالَ أَلَمْ نُرَبِّكَ فِينَا وَلِيدًا وَلَبِثْتَ فِينَا مِنْ عُمُرِكَ سِنِينَ ﴿١٨﴾
18. (Fira’wn) Akasema: “Je, hatukukulea kwetu ulipokuwa mtoto, na ukaishi kwetu miaka mingi ya umri wako.



وَفَعَلْتَ فَعْلَتَكَ الَّتِي فَعَلْتَ وَأَنتَ مِنَ الْكَافِرِينَ ﴿١٩﴾
19. “Na ukafanya kitendo chako ambacho ulikifanya nawe ni miongoni mwa wasio na shukurani.”



قَالَ فَعَلْتُهَا إِذًا وَأَنَا مِنَ الضَّالِّينَ ﴿٢٠﴾
20. (Muwsaa) Akasema: “Nilikifanya hapo wakati nilikuwa miongoni mwa waliokosea.



فَفَرَرْتُ مِنكُمْ لَمَّا خِفْتُكُمْ فَوَهَبَ لِي رَبِّي حُكْمًا وَجَعَلَنِي مِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٢١﴾
21. “Nikakukimbieni nilipokukhofuni, na Rabb wangu Akanitunukia hikmah na Akanijalia ni miongoni mwa Rusuli.



وَتِلْكَ نِعْمَةٌ تَمُنُّهَا عَلَيَّ أَنْ عَبَّدتَّ بَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿٢٢﴾
22. “Na hiyo ni neema unayonisimbulia, kwamba umewatia utumwani wana wa Israaiyl.”



قَالَ فِرْعَوْنُ وَمَا رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٢٣﴾
23. Fir’awn Akasema: “Na ni nani kwani Rabb wa walimwengu?”



قَالَ رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ ﴿٢٤﴾
24. (Muwsaa) Akasema: “Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake mkiwa ni wenye yakini.”



قَالَ لِمَنْ حَوْلَهُ أَلَا تَسْتَمِعُونَ ﴿٢٥﴾
25.  (Fir’awn) Akawaambia waliomzunguka: “Je, hamsikilizi kwa makini?”



قَالَ رَبُّكُمْ وَرَبُّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ ﴿٢٦﴾
26. (Muwsaa) Akasema: “Rabb wenu na Rabb wa baba zenu wa awali.”



قَالَ إِنَّ رَسُولَكُمُ الَّذِي أُرْسِلَ إِلَيْكُمْ لَمَجْنُونٌ ﴿٢٧﴾
27. (Fir’awn) Akasema: “Hakika Rasuli wenu ambaye ametumwa kwenu bila shaka ni majununi.”



قَالَ رَبُّ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ ﴿٢٨﴾
28. (Muwsaa) Akasema: “Rabb wa Mashariki na Magharibi na vilivyo baina yake, mkiwa nyinyi ni wenye kutia akilini.”



قَالَ لَئِنِ اتَّخَذْتَ إِلَـٰهًا غَيْرِي لَأَجْعَلَنَّكَ مِنَ الْمَسْجُونِينَ ﴿٢٩﴾
29. (Fir’wan) Akasema: “Ukichagua mwabudiwa mwengine badala yangu, nitakufanya miongoni mwa wafungwao gerezani.”



قَالَ أَوَلَوْ جِئْتُكَ بِشَيْءٍ مُّبِينٍ ﴿٣٠﴾
30. (Muwsaa) Akasema: “Je, hata kama nikikujia na kitu bayana?”



قَالَ فَأْتِ بِهِ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٣١﴾
31. (Fir’wan) Akasema: “Kilete ukiwa wewe ni miongoni mwa wakweli.”



فَأَلْقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ ثُعْبَانٌ مُّبِينٌ ﴿٣٢﴾
32. (Muwsaa) Akatupa fimbo yake, tahamaki hiyo ikawa joka kubwa bayana.



وَنَزَعَ يَدَهُ فَإِذَا هِيَ بَيْضَاءُ لِلنَّاظِرِينَ ﴿٣٣﴾
33. Na akavuta mkono wake; tahamaki huo ukawa mweupe kwa watazamao.



قَالَ لِلْمَلَإِ حَوْلَهُ إِنَّ هَـٰذَا لَسَاحِرٌ عَلِيمٌ ﴿٣٤﴾
34. (Fir’awn) Akawaambia wakuu waliomzunguka: “Hakika huyu bila shaka ni mchawi mjuzi.



يُرِيدُ أَن يُخْرِجَكُم مِّنْ أَرْضِكُم بِسِحْرِهِ فَمَاذَا تَأْمُرُونَ ﴿٣٥﴾
35. “Anataka kukutoeni kutoka ardhini mwenu kwa sihiri yake; basi mnaamrisha nini?”



قَالُوا أَرْجِهْ وَأَخَاهُ وَابْعَثْ فِي الْمَدَائِنِ حَاشِرِينَ ﴿٣٦﴾
36. Wakasema: “Muakhirishe kidogo na kaka yake, na tuma katika miji wakusanyao wachawi.”



يَأْتُوكَ بِكُلِّ سَحَّارٍ عَلِيمٍ ﴿٣٧﴾
37. “Watakujia na kila mchawi mjuzi.”



فَجُمِعَ السَّحَرَةُ لِمِيقَاتِ يَوْمٍ مَّعْلُومٍ ﴿٣٨﴾
38. Basi wakakusanywa wachawi katika mahali na wakati siku maalumu.



وَقِيلَ لِلنَّاسِ هَلْ أَنتُم مُّجْتَمِعُونَ ﴿٣٩﴾
39. Na wakaambiwa watu: “Je, mmekwishakusanyika?



لَعَلَّنَا نَتَّبِعُ السَّحَرَةَ إِن كَانُوا هُمُ الْغَالِبِينَ ﴿٤٠﴾
40. “Ili tuwafuate wachawi, wakiwa wao ndio watakaoshinda.”



فَلَمَّا جَاءَ السَّحَرَةُ قَالُوا لِفِرْعَوْنَ أَئِنَّ لَنَا لَأَجْرًا إِن كُنَّا نَحْنُ الْغَالِبِينَ ﴿٤١﴾
41. Basi walipokuja wachawi walimwambia Fir’awn: “Je, tutapata ujira wowote   ikiwa sisi tutakuwa wenye kushinda?”



قَالَ نَعَمْ وَإِنَّكُمْ إِذًا لَّمِنَ الْمُقَرَّبِينَ ﴿٤٢﴾
42. (Fir’awn) Akasema: “Naam! Na bila shaka nyinyi hapo mtakuwa miongoni mwa waliokurubishwa (kwangu).”



قَالَ لَهُم مُّوسَىٰ أَلْقُوا مَا أَنتُم مُّلْقُونَ ﴿٤٣﴾
43. Muwsaa akawambia: “Tupeni vile mnavyotupa.”



فَأَلْقَوْا حِبَالَهُمْ وَعِصِيَّهُمْ وَقَالُوا بِعِزَّةِ فِرْعَوْنَ إِنَّا لَنَحْنُ الْغَالِبُونَ ﴿٤٤﴾
44. Wakatupa kamba zao na fimbo zao; na wakasema: “Kwa utukufu wa Fir’awn! Hakika sisi ni wenye kushinda.”



فَأَلْقَىٰ مُوسَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ تَلْقَفُ مَا يَأْفِكُونَ ﴿٤٥﴾
45. Basi Muwsaa akatupa fimbo yake, tahamaki inameza vyote walivyovizua.



فَأُلْقِيَ السَّحَرَةُ سَاجِدِينَ ﴿٤٦﴾
46. Basi wale wachawi wakaanguka wakisujudu.



قَالُوا آمَنَّا بِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٤٧﴾
47. Wakasema: “Tumemwamini Rabb wa walimwengu.



رَبِّ مُوسَىٰ وَهَارُونَ ﴿٤٨﴾
48. “Rabb wa Muwsaa na Haaruwn.”



قَالَ آمَنتُمْ لَهُ قَبْلَ أَنْ آذَنَ لَكُمْ ۖ إِنَّهُ لَكَبِيرُكُمُ الَّذِي عَلَّمَكُمُ السِّحْرَ فَلَسَوْفَ تَعْلَمُونَ ۚ لَأُقَطِّعَنَّ أَيْدِيَكُمْ وَأَرْجُلَكُم مِّنْ خِلَافٍ وَلَأُصَلِّبَنَّكُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٤٩﴾
49. (Fira’wn) Akasema: “Je, mmemwamini kabla sijakupeni idhini? Hakika bila shaka kubwa lenu ndiye amekufunzeni sihiri. Basi mtakuja kujua. Nitakukatenikateni mikono yenu na miguu yenu kinyume (kulia kwa kushoto), kisha nitakusulubuni nyote.”
                                     


قَالُوا لَا ضَيْرَ ۖ إِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا مُنقَلِبُونَ ﴿٥٠﴾
50. Wakasema: “Hakuna dhara yoyote! Hakika sisi tunarudi kwa Rabb wetu.



إِنَّا نَطْمَعُ أَن يَغْفِرَ لَنَا رَبُّنَا خَطَايَانَا أَن كُنَّا أَوَّلَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٥١﴾
51. “Hakika sisi tunatumai kwamba Rabb wetu Atatughufuria madhambi yetu kwa vile tumekuwa wa kwanza wenye kuamini.”



وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ أَنْ أَسْرِ بِعِبَادِي إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ ﴿٥٢﴾
52. Na Tukamfunulia Wahy Muwsaa kwamba: “Safiri usiku pamoja na waja Wangu, hakika nyinyi ni wenye kufuatwa.”



فَأَرْسَلَ فِرْعَوْنُ فِي الْمَدَائِنِ حَاشِرِينَ ﴿٥٣﴾
53. Basi Fir’awn akawatuma wakusanyao wachawi katika miji. 



إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ لَشِرْذِمَةٌ قَلِيلُونَ ﴿٥٤﴾
54. (Akisema): “Hakika hawa ni kikosi kidhaifu kidogo, wachache.”



وَإِنَّهُمْ لَنَا لَغَائِظُونَ ﴿٥٥﴾
55. “Na hakika wao wanatughadhibisha.



وَإِنَّا لَجَمِيعٌ حَاذِرُونَ ﴿٥٦﴾
56. “Na hakika sisi, bila shaka ni jamii wenye kuchukua hadhari mno.”



فَأَخْرَجْنَاهُم مِّن جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ ﴿٥٧﴾
57. Basi Tukawatoa katika mabustani na chemchemu.



وَكُنُوزٍ وَمَقَامٍ كَرِيمٍ ﴿٥٨﴾
58. Na mahazina na vyeo vya heshima.



كَذَٰلِكَ وَأَوْرَثْنَاهَا بَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿٥٩﴾
59. Hivyo ndivyo (Tulivyofanya); na Tukayarithisha hayo wana wa Israaiyl.



فَأَتْبَعُوهُم مُّشْرِقِينَ ﴿٦٠﴾
60. Basi wakawafuata walipopambazukiwa.



فَلَمَّا تَرَاءَى الْجَمْعَانِ قَالَ أَصْحَابُ مُوسَىٰ إِنَّا لَمُدْرَكُونَ ﴿٦١﴾
61. Yalipoonana makundi mawili, wakasema watu wa Muwsaa: “Hakika sisi bila shaka tutadirikiwa kukamatwa.”



قَالَ كَلَّا ۖ إِنَّ مَعِيَ رَبِّي سَيَهْدِينِ ﴿٦٢﴾
62. (Muwsaa) akasema: “Hapana! Hakika Rabb wangu Yu pamoja nami Ataniongoza.”



فَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ أَنِ اضْرِب بِّعَصَاكَ الْبَحْرَ ۖ فَانفَلَقَ فَكَانَ كُلُّ فِرْقٍ كَالطَّوْدِ الْعَظِيمِ ﴿٦٣﴾
63. Tukamfunulia Wahy Muwsaa kwamba: “Piga kwa fimbo yako bahari.” Basi ikatengana ikawa kila sehemu kama jabali kubwa mno.



وَأَزْلَفْنَا ثَمَّ الْآخَرِينَ ﴿٦٤﴾
64. Na Tukawaleta karibu hapo wengine.



وَأَنجَيْنَا مُوسَىٰ وَمَن مَّعَهُ أَجْمَعِينَ ﴿٦٥﴾
65. Tukamuokoa Muwsaa na walio pamoja naye wote.



ثُمَّ أَغْرَقْنَا الْآخَرِينَ ﴿٦٦﴾
66. Kisha Tukawagharikisha wengine.



إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٦٧﴾
67. Hakika katika hayo pana Aayah (ishara, zingatio n.k.), lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.



وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿٦٨﴾
 68. Na hakika Rabb wako bila shaka Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kurehemu.



وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ إِبْرَاهِيمَ ﴿٦٩﴾
69. Na wasomee (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) khabari za Ibraahiym.



إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ مَا تَعْبُدُونَ ﴿٧٠﴾
70. Alipomwambia baba yake na watu wake: “Mnaabudu nini?”



قَالُوا نَعْبُدُ أَصْنَامًا فَنَظَلُّ لَهَا عَاكِفِينَ ﴿٧١﴾
71. Wakasema: “Tunaabudu masanamu, na tutaendelea kuyakalia kwa kuyaabudu.”



قَالَ هَلْ يَسْمَعُونَكُمْ إِذْ تَدْعُونَ ﴿٧٢﴾
72. Akasema: “Je, yanakusikieni mnapoyaomba?”



أَوْ يَنفَعُونَكُمْ أَوْ يَضُرُّونَ ﴿٧٣﴾
73. “Au yanakunufaisheni au yanakudhuruni?”



قَالُوا بَلْ وَجَدْنَا آبَاءَنَا كَذَٰلِكَ يَفْعَلُونَ ﴿٧٤﴾
74. Wakasema: “Tumewakuta baba zetu wakifanya hivyo.”



قَالَ أَفَرَأَيْتُم مَّا كُنتُمْ تَعْبُدُونَ ﴿٧٥﴾
75.  Akasema: “Je, mnaona hivyo mlivyokuwa mkiviabudu?



أَنتُمْ وَآبَاؤُكُمُ الْأَقْدَمُونَ ﴿٧٦﴾
76. “Nyinyi na baba zenu waliotangulia?



فَإِنَّهُمْ عَدُوٌّ لِّي إِلَّا رَبَّ الْعَالَمِينَ ﴿٧٧﴾
77. “Basi hakika hao ni adui zangu isipokuwa Rabb wa walimwengu.



الَّذِي خَلَقَنِي فَهُوَ يَهْدِينِ ﴿٧٨﴾
78. “Ambaye Ameniumba, Naye Ananiongoza.”



وَالَّذِي هُوَ يُطْعِمُنِي وَيَسْقِينِ ﴿٧٩﴾
79. “Na Ambaye Ndiye Anayenilisha na Ananinywesha.



وَإِذَا مَرِضْتُ فَهُوَ يَشْفِينِ ﴿٨٠﴾
80. “Na ninapokuwa mgonjwa, basi Yeye Ananiponyesha.


وَالَّذِي يُمِيتُنِي ثُمَّ يُحْيِينِ ﴿٨١﴾
81. “Na Ambaye Atanifisha kisha Atanihuisha.



وَالَّذِي أَطْمَعُ أَن يَغْفِرَ لِي خَطِيئَتِي يَوْمَ الدِّينِ ﴿٨٢﴾
82. “Na Ambaye natumai Atanighufuria makosa yangu Siku ya Malipo.



رَبِّ هَبْ لِي حُكْمًا وَأَلْحِقْنِي بِالصَّالِحِينَ ﴿٨٣﴾
83. “Rabb wangu! Nitunukie hikmah; elimu ya Dini na Unikutanishe na Swalihina.



وَاجْعَل لِّي لِسَانَ صِدْقٍ فِي الْآخِرِينَ ﴿٨٤﴾
84. “Na Nijaalie kusifika kwa heshima kwa vizazi watakaokuja baadaye.



وَاجْعَلْنِي مِن وَرَثَةِ جَنَّةِ النَّعِيمِ ﴿٨٥﴾
85. “Na Nijaalie miongoni mwa warithi wa Jannah ya neema.



وَاغْفِرْ لِأَبِي إِنَّهُ كَانَ مِنَ الضَّالِّينَ ﴿٨٦﴾
86. “Na Mghufurie baba yangu, hakika yeye amekuwa miongoni mwa waliopotea.



وَلَا تُخْزِنِي يَوْمَ يُبْعَثُونَ ﴿٨٧﴾
87. “Na wala Usinihizi Siku watakayofufuliwa.



يَوْمَ لَا يَنفَعُ مَالٌ وَلَا بَنُونَ ﴿٨٨﴾
88. “Siku hayatofaa mali wa watoto.



إِلَّا مَنْ أَتَى اللَّـهَ بِقَلْبٍ سَلِيمٍ ﴿٨٩﴾
89. “Isipokuwa yule atakayemfikia Allaah na moyo uliosalimika.



وَأُزْلِفَتِ الْجَنَّةُ لِلْمُتَّقِينَ ﴿٩٠﴾
90. Na itakurubishwa Jannah kwa wenye taqwa.



وَبُرِّزَتِ الْجَحِيمُ لِلْغَاوِينَ ﴿٩١﴾
91. Na utadhihirishwa moto uwakao vikali mno kwa wapotofu.



وَقِيلَ لَهُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ تَعْبُدُونَ ﴿٩٢﴾
92. Na wataambiwa: “Wako wapi wale mliokuwa mkiwaabudu?”



مِن دُونِ اللَّـهِ هَلْ يَنصُرُونَكُمْ أَوْ يَنتَصِرُونَ ﴿٩٣﴾
93. “Badala ya Allaah. Je, wataweza kukunusuruni au kujinusuru wenyewe?”



فَكُبْكِبُوا فِيهَا هُمْ وَالْغَاوُونَ ﴿٩٤﴾
94. Watapinduliwa gubigubi humo wao na wapotofu.



وَجُنُودُ إِبْلِيسَ أَجْمَعُونَ ﴿٩٥﴾
95. Na majeshi ya Ibliys yote.



قَالُوا وَهُمْ فِيهَا يَخْتَصِمُونَ ﴿٩٦﴾
96. Watasema na huku wao wanakhasimiana humo.  



تَاللَّـهِ إِن كُنَّا لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٩٧﴾
97. “Wa-Allaahi! Hakika tulikuwa bila shaka katika upotofu bayana.”



إِذْ نُسَوِّيكُم بِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٩٨﴾
98. “Tulipokusawazisheni na Rabb wa walimwengu.



وَمَا أَضَلَّنَا إِلَّا الْمُجْرِمُونَ ﴿٩٩﴾
99. “Na hakuna aliyetupoteza isipokuwa wakhalifu.



فَمَا لَنَا مِن شَافِعِينَ ﴿١٠٠﴾
100. “Basi hatuna waombezi wowote.



وَلَا صَدِيقٍ حَمِيمٍ ﴿١٠١﴾
101. “Na wala rafiki khalisi.



فَلَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٠٢﴾
102. “Basi lau tungelikuwa tuna fursa ya kurudi (duniani) tungekuwa miongoni mwa Waumini.”



إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١٠٣﴾
103. Hakika katika hayo pana Aayah (ishara, zingatio n.k.), lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.



وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿١٠٤﴾
104. Na hakika Rabb wako bila shaka Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kurehemu.



كَذَّبَتْ قَوْمُ نُوحٍ الْمُرْسَلِينَ ﴿١٠٥﴾
105. Watu wa Nuwh walimkadhibisha Rusuli.



إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ نُوحٌ أَلَا تَتَّقُونَ ﴿١٠٦﴾
106. Alipowaambia ndugu yao Nuwh: “Je, hamtokuwa na taqwa?”



إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ ﴿١٠٧﴾
107. “Hakika mimi kwenu ni Rasuli mwaminifu.



فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿١٠٨﴾
108. “Basi mcheni Allaah na nitiini.



وَمَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٠٩﴾
109. “Na wala sikuombeni ujira wowote juu yake.  Ujira wangu hauko isipokuwa kwa Rabb wa walimwengu.”



فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿١١٠﴾
110. “Basi mcheni Allaah na nitiini.”



قَالُوا أَنُؤْمِنُ لَكَ وَاتَّبَعَكَ الْأَرْذَلُونَ ﴿١١١﴾
111. Wakasema: “Je, tukuamini na hali kuwa waliokufuata ni wadhalilifu?”



قَالَ وَمَا عِلْمِي بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١١٢﴾
112.  Akasema: “Na najuaje kwa ambayo waliyokuwa wanayatenda?



إِنْ حِسَابُهُمْ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّي ۖ لَوْ تَشْعُرُونَ ﴿١١٣﴾
113. “Hesabu yao haiko isipokuwa kwa Rabb wangu, lau mngetambua.



وَمَا أَنَا بِطَارِدِ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١١٤﴾
114. “Nami sitowafukuza walioamini.



إِنْ أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ مُّبِينٌ ﴿١١٥﴾
115. “Mimi si yeyote ila mwonyaji dhahiri.”



قَالُوا لَئِن لَّمْ تَنتَهِ يَا نُوحُ لَتَكُونَنَّ مِنَ الْمَرْجُومِينَ ﴿١١٦﴾
116. Wakasema: “Usipoacha ewe Nuwh bila shaka utakuwa miongoni mwa wenye kurajimiwa.”



قَالَ رَبِّ إِنَّ قَوْمِي كَذَّبُونِ ﴿١١٧﴾
117. Akasema: “Rabb wangu! Hakika watu wangu wamenikadhibisha.



فَافْتَحْ بَيْنِي وَبَيْنَهُمْ فَتْحًا وَنَجِّنِي وَمَن مَّعِيَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١١٨﴾
118. “Basi Hukumu baina yangu na baina yao hukumu (Yako), na Uniokoe mimi na wale walio pamoja nami miongoni mwa Waumini.”



فَأَنجَيْنَاهُ وَمَن مَّعَهُ فِي الْفُلْكِ الْمَشْحُونِ ﴿١١٩﴾
119. Tukamuokoa pamoja na wale waliokuwa naye katika jahazi iliyosheheni.



ثُمَّ أَغْرَقْنَا بَعْدُ الْبَاقِينَ ﴿١٢٠﴾
120. Kisha Tukawagharikisha baada ya hapo waliobakia.



إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١٢١﴾
121.  Hakika katika hayo pana Aayah (ishara, zingatio n.k.), lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.



وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿١٢٢﴾
122. Na hakika Rabb wako bila shaka Ndiye Mwenye Nguvu, Mshindi Asiyeshindika, Mwenye Kurehemu.



كَذَّبَتْ عَادٌ الْمُرْسَلِينَ ﴿١٢٣﴾
123. Kina ‘Aad walimkadhibisha Rusuli.



إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ هُودٌ أَلَا تَتَّقُونَ ﴿١٢٤﴾
124. Alipowaambia ndugu yao Huwd: “Je, hamtokuwa na taqwa?”



إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ ﴿١٢٥﴾
125. “Hakika mimi kwenu ni Rasuli mwaminifu.



فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿١٢٦﴾
126. “Basi mcheni Allaah na nitiini.



وَمَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٢٧﴾
127. “Na wala sikuombeni ujira wowote juu yake.  Ujira wangu hauko isipokuwa kwa Rabb wa walimwengu.”



أَتَبْنُونَ بِكُلِّ رِيعٍ آيَةً تَعْبَثُونَ ﴿١٢٨﴾
128. “Je, mnajenga katika kila sehemu maarufu za mnyanyuko, majengo marefurefu kwa ajili ya burudani tu?



وَتَتَّخِذُونَ مَصَانِعَ لَعَلَّكُمْ تَخْلُدُونَ ﴿١٢٩﴾
129. “Na mnafanya mangome madhubuti kama kwamba mtaishi milele?



وَإِذَا بَطَشْتُم بَطَشْتُمْ جَبَّارِينَ ﴿١٣٠﴾
130. “Na mnapokamata kushambulia mnatumia nguvu kwa uadui na ujabari.   



فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿١٣١﴾
131. “Basi mcheni Allaah na nitiini.



وَاتَّقُوا الَّذِي أَمَدَّكُم بِمَا تَعْلَمُونَ ﴿١٣٢﴾
132. “Na mcheni Ambaye Amekupeni yale mnayoyajua.



أَمَدَّكُم بِأَنْعَامٍ وَبَنِينَ ﴿١٣٣﴾
133. “Amekupeni wanyama wa mifugo na watoto.



وَجَنَّاتٍ وَعُيُونٍ ﴿١٣٤﴾
134.  “Na mabustani na chemchemu.



إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿١٣٥﴾
135. “Hakika mimi nakukhofieni adhabu ya Siku adhimu.”



قَالُوا سَوَاءٌ عَلَيْنَا أَوَعَظْتَ أَمْ لَمْ تَكُن مِّنَ الْوَاعِظِينَ ﴿١٣٦﴾
136. Wakasema: “Ni sawa sawa kwetu, ukiwaidhi au usipokuwa miongoni mwa wanaowaidhi.



إِنْ هَـٰذَا إِلَّا خُلُقُ الْأَوَّلِينَ ﴿١٣٧﴾
137. “Haya si chochote isipokuwa ni desturi ya watu wa awali.



وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ ﴿١٣٨﴾
138. “Na wala hatutoadhibiwa.”



فَكَذَّبُوهُ فَأَهْلَكْنَاهُمْ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١٣٩﴾
139. Wakamkadhibisha; basi Tuliwaangamiza. Hakika katika hayo pana Aayah (ishara, zingatio n.k.), lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.



وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿١٤٠﴾
140. Na hakika Rabb wako bila shaka Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kurehemu.



كَذَّبَتْ ثَمُودُ الْمُرْسَلِينَ ﴿١٤١﴾
141. Kina Thamuwd walimkadhibisha Rusuli.



إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ صَالِحٌ أَلَا تَتَّقُونَ ﴿١٤٢﴾
142. Alipowaambia ndugu yao Swaalih: “Je, hamtokuwa na taqwa?”



إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ ﴿١٤٣﴾
143. “Hakika mimi kwenu ni Rasuli mwaminifu.



فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿١٤٤﴾
144. “Basi mcheni Allaah na nitiini.



وَمَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٤٥﴾
145. “Na wala sikuombeni ujira wowote juu yake.  Ujira wangu hauko isipokuwa kwa Rabb wa walimwengu.”



أَتُتْرَكُونَ فِي مَا هَاهُنَا آمِنِينَ ﴿١٤٦﴾
146. “Je, mtaachwa mkiwa katika amani kwenye haya hapa mliyonayo? 



فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ ﴿١٤٧﴾
147. “Katika mabustani na chemchemu.



وَزُرُوعٍ وَنَخْلٍ طَلْعُهَا هَضِيمٌ ﴿١٤٨﴾
148. “Na mimea na mitende makole yake laini, yamewiva.



وَتَنْحِتُونَ مِنَ الْجِبَالِ بُيُوتًا فَارِهِينَ ﴿١٤٩﴾
149. “Na mnachonga majabalini nyumba kwa uhodari kabisa.



فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿١٥٠﴾
150. “Basi mcheni Allaah na nitiini.



وَلَا تُطِيعُوا أَمْرَ الْمُسْرِفِينَ ﴿١٥١﴾
151. “Na wala msitii amri ya wenye kupindukia mipaka.



الَّذِينَ يُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ وَلَا يُصْلِحُونَ ﴿١٥٢﴾
152. “Ambao wanafanya ufisadi katika ardhi na wala hawatengenezi.”



قَالُوا إِنَّمَا أَنتَ مِنَ الْمُسَحَّرِينَ ﴿١٥٣﴾
153. Wakasema: “Hakika wewe ni miongoni mwa waliorogwa.



مَا أَنتَ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُنَا فَأْتِ بِآيَةٍ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿١٥٤﴾
154. “Wewe si chochote isipokuwa mtu kama sisi; basi lete Aayah (dalili, muujiza) ukiwa wewe ni miongoni mwa wakweli.”



قَالَ هَـٰذِهِ نَاقَةٌ لَّهَا شِرْبٌ وَلَكُمْ شِرْبُ يَوْمٍ مَّعْلُومٍ ﴿١٥٥﴾
155. Akasema: “Huyu hapa ngamia jike ana zamu ya kinywaji, nanyi mna zamu ya kinywaji siku maalumu.



وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابُ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿١٥٦﴾
156. “Na wala msimguse kwa uovu, ikaja kukuchukueni adhabu ya Siku adhimu.”



فَعَقَرُوهَا فَأَصْبَحُوا نَادِمِينَ ﴿١٥٧﴾
157. Basi wakamuua wakapambazukiwa wenye kujuta.



فَأَخَذَهُمُ الْعَذَابُ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١٥٨﴾
158. Ikawachukuwa adhabu. Hakika katika hayo pana Aayah (ishara, zingatio n.k.), lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.



وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿١٥٩﴾
159. Na hakika Rabb wako bila shaka Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kurehemu.



كَذَّبَتْ قَوْمُ لُوطٍ الْمُرْسَلِينَ ﴿١٦٠﴾
160. Watu wa Luwtw walimkadhibisha Rusuli.



إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ لُوطٌ أَلَا تَتَّقُونَ ﴿١٦١﴾
161. Alipowaambia ndugu yao Luwtw: “Je, hamtokuwa na taqwa?”



إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ ﴿١٦٢﴾
162. “Hakika mimi kwenu ni Rasuli mwaminifu.



فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿١٦٣﴾
163. “Basi mcheni Allaah na nitiini.



وَمَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٦٤﴾
164. “Na wala sikuombeni ujira wowote juu yake.  Ujira wangu hauko isipokuwa kwa Rabb wa walimwengu.”



أَتَأْتُونَ الذُّكْرَانَ مِنَ الْعَالَمِينَ ﴿١٦٥﴾
165. “Je, mnawaendea wanaume miongoni mwa walimwengu?



وَتَذَرُونَ مَا خَلَقَ لَكُمْ رَبُّكُم مِّنْ أَزْوَاجِكُم ۚ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ عَادُونَ ﴿١٦٦﴾
166. “Na mnawaacha wale Aliyekuumbieni Rabb wenu kati ya wake zenu. Bali nyinyi ni watu mliopindukia mipaka.”



قَالُوا لَئِن لَّمْ تَنتَهِ يَا لُوطُ لَتَكُونَنَّ مِنَ الْمُخْرَجِينَ ﴿١٦٧﴾
167. Wakasema: “Usipoacha ee Luwtw, bila shaka utakuwa miongoni mwa watakaofukuzwa.”



قَالَ إِنِّي لِعَمَلِكُم مِّنَ الْقَالِينَ ﴿١٦٨﴾
168. Akasema: “Hakika mimi ni katika wanaochukia mno kitendo chenu.



رَبِّ نَجِّنِي وَأَهْلِي مِمَّا يَعْمَلُونَ ﴿١٦٩﴾
169. “Rabb wangu! Niokoe na ahli zangu kutokana na yale wanayotenda.”



فَنَجَّيْنَاهُ وَأَهْلَهُ أَجْمَعِينَ ﴿١٧٠﴾
170. Basi Tukamuokoa na ahli zake wote.



إِلَّا عَجُوزًا فِي الْغَابِرِينَ ﴿١٧١﴾
171. Isipokuwa kikongwe katika waliobaki nyuma.



ثُمَّ دَمَّرْنَا الْآخَرِينَ ﴿١٧٢﴾
172. Kisha Tukadamiri wengineo.



وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِم مَّطَرًا ۖ فَسَاءَ مَطَرُ الْمُنذَرِينَ ﴿١٧٣﴾
173. Na Tukawanyeshea mvua (ya adhabu). Basi uovu ulioje mvua ya walioonywa.



إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١٧٤﴾
174. Hakika katika hayo pana Aayah (ishara, zingatio n.k.), lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.



وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿١٧٥﴾
175. Na hakika Rabb wako bila shaka Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kurehemu.



كَذَّبَ أَصْحَابُ الْأَيْكَةِ الْمُرْسَلِينَ ﴿١٧٦﴾
176. Watu wa Al-Aykah wamemkadhibisha Rusuli.



إِذْ قَالَ لَهُمْ شُعَيْبٌ أَلَا تَتَّقُونَ ﴿١٧٧﴾
177. Alipowaambia Shu’ayb: “Je, hamtokuwa na taqwa?”



إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ ﴿١٧٨﴾
178. “Hakika mimi kwenu ni Rasuli mwaminifu.



فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿١٧٩﴾
179. “Basi mcheni Allaah na nitiini.



وَمَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٨٠﴾
180. “Na wala sikuombeni ujira wowote juu yake.  Ujira wangu hauko isipokuwa kwa Rabb wa walimwengu.”



أَوْفُوا الْكَيْلَ وَلَا تَكُونُوا مِنَ الْمُخْسِرِينَ ﴿١٨١﴾
181. “Timizeni kipimo na wala msiwe miongoni mwa wenye kupunja.



وَزِنُوا بِالْقِسْطَاسِ الْمُسْتَقِيمِ ﴿١٨٢﴾
182. “Na pimeni mizani kwa uadilifu iliyosawa.



وَلَا تَبْخَسُوا النَّاسَ أَشْيَاءَهُمْ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ ﴿١٨٣﴾
183. “Na wala msiwapunje watu vitu vyao, na wala msieneze uovu katika ardhi hali ya kuwa ni wenye kufanya ufisadi.



وَاتَّقُوا الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالْجِبِلَّةَ الْأَوَّلِينَ ﴿١٨٤﴾
184. “Na mcheni Ambaye Amekuumbeni na viumbe vingi wa awali.”



قَالُوا إِنَّمَا أَنتَ مِنَ الْمُسَحَّرِينَ ﴿١٨٥﴾
185. Wakasema: “Hakika wewe ni miongoni mwa waliorogwa.



وَمَا أَنتَ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُنَا وَإِن نَّظُنُّكَ لَمِنَ الْكَاذِبِينَ ﴿١٨٦﴾
186. “Nawe si chochote isipokuwa ni mtu kama sisi, na hakika tunakudhania ni miongoni mwa waongo.



فَأَسْقِطْ عَلَيْنَا كِسَفًا مِّنَ السَّمَاءِ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿١٨٧﴾
187. “Basi tuangushie vipande vipande vya mbingu, ukiwa ni miongoni mwa wakweli.”



قَالَ رَبِّي أَعْلَمُ بِمَا تَعْمَلُونَ ﴿١٨٨﴾
188. Akasema: “Hakika Rabb wangu Anajua zaidi yale mnayoyatenda.”



فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَهُمْ عَذَابُ يَوْمِ الظُّلَّةِ ۚ إِنَّهُ كَانَ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿١٨٩﴾
189. Wakamkadhibisha; basi adhabu ya siku ya kivuli (cha mawingu) ikawachukua. Hakika hiyo ilikuwa ni adhabu ya Siku kubwa mno.



إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١٩٠﴾
190. Hakika katika hayo pana Aayah (ishara, zingatio n.k.), lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.



وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿١٩١﴾
191. Na hakika Rabb wako bila shaka Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kurehemu.



وَإِنَّهُ لَتَنزِيلُ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٩٢﴾
192. Na hakika hii (Qur-aan) ni uteremsho wa Rabb wa walimwengu.



نَزَلَ بِهِ الرُّوحُ الْأَمِينُ ﴿١٩٣﴾
193. Ameiteremsha haya Ar-Ruwh (Jibriyl) mwaminifu.



عَلَىٰ قَلْبِكَ لِتَكُونَ مِنَ الْمُنذِرِينَ ﴿١٩٤﴾
194. Juu ya moyo wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ili uwe miongoni mwa waonyaji.



بِلِسَانٍ عَرَبِيٍّ مُّبِينٍ ﴿١٩٥﴾
195. Kwa lugha ya Kiarabu bayana.



وَإِنَّهُ لَفِي زُبُرِ الْأَوَّلِينَ ﴿١٩٦﴾
196. Na hakika hii bila shaka imo katika Vitabu vya awali.



أَوَلَمْ يَكُن لَّهُمْ آيَةً أَن يَعْلَمَهُ عُلَمَاءُ بَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿١٩٧﴾
197. Je, haikuwa kwao ni Aayah (ishara, dalili), kwamba waitambue wanavyuoni wa wana wa Israaiyl? 



وَلَوْ نَزَّلْنَاهُ عَلَىٰ بَعْضِ الْأَعْجَمِينَ ﴿١٩٨﴾
198. Na lau Tungeliiteremsha (hii Qur-aan) juu ya yeyote miongoni mwa wasio Waarabu.



فَقَرَأَهُ عَلَيْهِم مَّا كَانُوا بِهِ مُؤْمِنِينَ ﴿١٩٩﴾
199. Na akawasomea, wasingelikuwa wenye kuiamini.



كَذَٰلِكَ سَلَكْنَاهُ فِي قُلُوبِ الْمُجْرِمِينَ ﴿٢٠٠﴾
200. Hivyo ndivyo Tunavyoingiza katika nyoyo za wakhalifu.



لَا يُؤْمِنُونَ بِهِ حَتَّىٰ يَرَوُا الْعَذَابَ الْأَلِيمَ ﴿٢٠١﴾
201. Hawaiamini mpaka waione adhabu iumizayo.



فَيَأْتِيَهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٢٠٢﴾
202. Basi itawajia kwa ghafla, nao hawatambui.



فَيَقُولُوا هَلْ نَحْنُ مُنظَرُونَ ﴿٢٠٣﴾
203. Kisha watasema: “Je, sisi tutapewa muhula?”



أَفَبِعَذَابِنَا يَسْتَعْجِلُونَ ﴿٢٠٤﴾
204. Je, wanahimiza adhabu Yetu?



أَفَرَأَيْتَ إِن مَّتَّعْنَاهُمْ سِنِينَ ﴿٢٠٥﴾
205. Je, unaonaje kama Tukiwastarehesha miaka.



ثُمَّ جَاءَهُم مَّا كَانُوا يُوعَدُونَ ﴿٢٠٦﴾
206. Kisha ikawajia yale waliyokuwa wameahidiwa.



مَا أَغْنَىٰ عَنْهُم مَّا كَانُوا يُمَتَّعُونَ ﴿٢٠٧﴾
207. Hayatowafaa yale waliyokuwa wakistarehe nayo.



وَمَا أَهْلَكْنَا مِن قَرْيَةٍ إِلَّا لَهَا مُنذِرُونَ ﴿٢٠٨﴾
208. Na Hatukuangamiza mji wowote isipokuwa ulikuwa na waonyaji.



ذِكْرَىٰ وَمَا كُنَّا ظَالِمِينَ ﴿٢٠٩﴾
209.  Ni ukumbusho na Hatukuwa madhalimu.



وَمَا تَنَزَّلَتْ بِهِ الشَّيَاطِينُ ﴿٢١٠﴾
210. Na wala hawakuteremka nayo (hii Qur-aan) mashaytwaan.



وَمَا يَنبَغِي لَهُمْ وَمَا يَسْتَطِيعُونَ ﴿٢١١﴾
211. Na wala haipasi kwao na wala hawawezi.



إِنَّهُمْ عَنِ السَّمْعِ لَمَعْزُولُونَ ﴿٢١٢﴾
212. Hakika wao bila shaka wametengwa mbali kuisikiliza.



فَلَا تَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ فَتَكُونَ مِنَ الْمُعَذَّبِينَ ﴿٢١٣﴾
213. Basi usiombe pamoja na Allaah mwabudiwa mwengine ukaja kuwa miongoni mwa watakaoadhibiwa.



وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ ﴿٢١٤﴾
214. Na onya (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) jamaa zako wa karibu.



وَاخْفِضْ جَنَاحَكَ لِمَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٢١٥﴾
215. Na inamisha ubawa wako kwa anayekufuata miongoni mwa Waumini.



فَإِنْ عَصَوْكَ فَقُلْ إِنِّي بَرِيءٌ مِّمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٢١٦﴾
216. Wakikuasi; basi sema: “Hakika mimi niko mbali na hayo mnayoyatenda.”



وَتَوَكَّلْ عَلَى الْعَزِيزِ الرَّحِيمِ ﴿٢١٧﴾
217. Na tawakali kwa Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kurehemu.



الَّذِي يَرَاكَ حِينَ تَقُومُ ﴿٢١٨﴾
218.  Ambaye Anakuona wakati unaposimama.



وَتَقَلُّبَكَ فِي السَّاجِدِينَ ﴿٢١٩﴾
219. Na mageuko yako katika wenye kusujudu. 



إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٢٢٠﴾
220. Hakika Yeye Ndiye Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.



هَلْ أُنَبِّئُكُمْ عَلَىٰ مَن تَنَزَّلُ الشَّيَاطِينُ ﴿٢٢١﴾
221. Je, nikujulisheni wanaowateremkia mashaytwaan?



تَنَزَّلُ عَلَىٰ كُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٍ ﴿٢٢٢﴾
222. Wanateremka juu ya kila mzushi mkubwa mwingi wa kutenda dhambi. 



يُلْقُونَ السَّمْعَ وَأَكْثَرُهُمْ كَاذِبُونَ ﴿٢٢٣﴾
223. Wanaotega sikio na wengi wao ni waongo.



وَالشُّعَرَاءُ يَتَّبِعُهُمُ الْغَاوُونَ ﴿٢٢٤﴾
224. Na washairi wanafuatwa na wapotofu.



أَلَمْ تَرَ أَنَّهُمْ فِي كُلِّ وَادٍ يَهِيمُونَ ﴿٢٢٥﴾
225. Je, huoni kwamba wao katika kila bonde wanatangatanga?



وَأَنَّهُمْ يَقُولُونَ مَا لَا يَفْعَلُونَ ﴿٢٢٦﴾
226. Nao wanasema yale wasiyoyafanya.



إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَذَكَرُوا اللَّـهَ كَثِيرًا وَانتَصَرُوا مِن بَعْدِ مَا ظُلِمُوا ۗ وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنقَلَبٍ يَنقَلِبُونَ ﴿٢٢٧﴾
227. Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema, na wakamdhukuru Allaah kwa wingi, na wakapata nusura baada ya kudhulumiwa. Na hivi karibuni watakuja kujua wale waliodhulumu mgeuko gani watakaogeuka.




Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com