Yuwnus: 10

  يُونُس
Yuwnus: 10

(Imeteremka Makka)


Sura hii ya Makka imeteremka Makka, na ina Aya 109. Imeanzia kuashiria cheo cha Kitabu hiki Kitukufu, na wasemayo washirikina yaliyo mkhusu Nabii s.a.w. Kisha ikataja ulimwengu na ishara za Mwenyezi Mungu Mtukufu ziliomo humo, na malipo ya Siku ya Kiyama, na mwendo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwatendea makafiri, na kuwakemea kwake kwa hizo itikadi zao, na hali ya watu wakati wa shida na neema, na uwezo wa Mwenyezi Mungu juu ya kila kitu, na kuemewa  masanamu kufanya lolote. Na katika Sura hii wanatakiwa kama wanaweza makafiri walete Sura japo moja ya kuzua. Na pia ndani yake kuna vitisho vikali vya adhabu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hali za nafsi za watu, na vipi Mwenyezi Mungu anavyo vichunguza vitendo vyao. Kisha baada ya hayo ikaingia kumwondolea Nabii s.a.w. kuungulika kwake kwa ukafiri wao, pamoja na kutoa hoja ya kuwavunja kabisa, na ikampoza kwa kumtajia hadithi za Manabii wengine na kaumu zao. Ikaja hadithi ya Nuhu, na hadithi ya Musa na Harun na Firauni na Wana wa Israili; kisha ikaashiriwa hadithi ya Yunus, na kwa jina hilo Sura hii ikaitwa. Na mwisho ikaelekea  Sura hii kubainisha mambo ya Mtume huyu ili kutimiza mawaidha na mazingatio.
 


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

الر ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْحَكِيمِ﴿١﴾
1. Alif Laam Raa. Hizo ni Aayaat za Kitabu chenye hikmah.


أَكَانَ لِلنَّاسِ عَجَبًا أَنْ أَوْحَيْنَا إِلَىٰ رَجُلٍ مِّنْهُمْ أَنْ أَنذِرِ النَّاسَ وَبَشِّرِ الَّذِينَ آمَنُوا أَنَّ لَهُمْ قَدَمَ صِدْقٍ عِندَ رَبِّهِمْ ۗ قَالَ الْكَافِرُونَ إِنَّ هَـٰذَا لَسَاحِرٌ مُّبِينٌ﴿٢﴾
2. Je, imekuwa ni ajabu kwa watu kwamba Tumemfunulia Wahy mtu miongoni mwao kwamba: “Waonye watu (adhabu ya Allaah) na wabashirie wale walioamini kwamba watapata cheo kitukufu mbele ya Rabb (Mola) wao.” Makafiri wakasema: “Hakika huyu bila shaka ni mchawi bayana.”


إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۖ يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۖ مَا مِن شَفِيعٍ إِلَّا مِن بَعْدِ إِذْنِهِ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ﴿٣﴾
3. Hakika Rabb (Mola) wenu ni Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha Istawaa juu ya ‘Arsh (Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah). Anadabiri mambo (ya kila Alichokiumba). Hakuna mwombezi yeyote ila baada ya idhini Yake. Huyu Ndiye Allaah Rabb Wenu, basi mwabuduni. Je, hamkumbuki?


إِلَيْهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا ۖ وَعْدَ اللَّـهِ حَقًّا ۚ إِنَّهُ يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ لِيَجْزِيَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ بِالْقِسْطِ ۚ وَالَّذِينَ كَفَرُوا لَهُمْ شَرَابٌ مِّنْ حَمِيمٍ وَعَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ﴿٤﴾
4. Kwake ni marejeo yenu nyote. Ni ahadi ya Allaah ya kweli. Hakika Yeye Anaanzisha uumbaji, kisha Anaurejesha ili Awalipe kwa uadilifu wale walioamini na wakatenda mema. Na wale waliokufuru watapata kinywaji cha maji ya kuchemka, na adhabu iumizayo kwa yale waliyokuwa wakikufuru.


هُوَ الَّذِي جَعَلَ الشَّمْسَ ضِيَاءً وَالْقَمَرَ نُورًا وَقَدَّرَهُ مَنَازِلَ لِتَعْلَمُوا عَدَدَ السِّنِينَ وَالْحِسَابَ ۚ مَا خَلَقَ اللَّـهُ ذَٰلِكَ إِلَّا بِالْحَقِّ ۚ يُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ﴿٥﴾
5. Yeye Ndiye Aliyejaalia jua kuwa ni mwanga na mwezi kuwa ni nuru; na Akaukadiria vituo ili mjue idadi ya miaka na hesabu (nyingine).  Allaah Hakuumba hivyo ila kwa haki. Anafasili Aayaat (na dalili, hoja n.k) kwa watu wanaojua.


إِنَّ فِي اخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَمَا خَلَقَ اللَّـهُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَّقُونَ﴿٦﴾
7. Hakika katika mabadiliko (ya mfuatano) ya usiku na mchana na Alivyoviumba Allaah katika mbingu na ardhi, bila shaka ni Aayaat (ishara, hoja) kwa watu walio na taqwa.



إِنَّ الَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَاءَنَا وَرَضُوا بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَاطْمَأَنُّوا بِهَا وَالَّذِينَ هُمْ عَنْ آيَاتِنَا غَافِلُونَ﴿٧﴾
7. Hakika wale wasiotaraji kukutana Nasi, na wakaridhika na uhai wa dunia na wakakinaika nayo, na wale ambao wanaghafilika na Aayaat Zetu.


أولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمُ النَّارُ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿٨﴾
8. Hao makazi yao ni Moto, kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.



إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ يَهْدِيهِمْ رَبُّهُم بِإِيمَانِهِمْ ۖتَجْرِي مِن تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ﴿٩﴾
9. Hakika wale walioamini na wakatenda mema, Rabb (Mola) wao Atawaongoza kwa iymaan zao. Zitapita chini yao mito katika Jannaat za neema (za kila aina).

دَعْوَاهُمْ فِيهَا سُبْحَانَكَ اللَّـهُمَّ وَتَحِيَّتُهُمْ فِيهَا سَلَامٌ ۚوَآخِرُ دَعْوَاهُمْ أَنِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴿١٠﴾
10. Wito wao humo (utakuwa) ni: “Subhaanaka-Allaahumma” (Utakasifu ni Wako ee Allaah). Na maamkizi yao humo ni “Salaam” (amani). Na wito wao wa mwisho ni ‘AlhamduliLLaahi (Himidi zote Anastahiki Allaah) Rabb (Mola) wa walimwengu.


وَلَوْ يُعَجِّلُ اللَّـهُ لِلنَّاسِ الشَّرَّ اسْتِعْجَالَهُم بِالْخَيْرِ لَقُضِيَ إِلَيْهِمْ أَجَلُهُمْ ۖ فَنَذَرُ الَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَاءَنَا فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ﴿١١﴾
11. Na lau Allaah Angeliwaharakizia watu shari (wanayoihimiza iwafike) kama wanavyojihimizia kheri, bila shaka wangetimiziwa muda wao (wa kuangamizwa). Basi Tunawaacha wale wasiotarajia kukutana Nasi katika upindukaji mipaka ya kuasi kwao, wakitangatanga kwa upofu.


وَإِذَا مَسَّ الْإِنسَانَ الضُّرُّ دَعَانَا لِجَنبِهِ أَوْ قَاعِدًا أَوْ قَائِمًا فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُ ضُرَّهُ مَرَّ كَأَن لَّمْ يَدْعُنَا إِلَىٰ ضُرٍّ مَّسَّهُ ۚ كَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلْمُسْرِفِينَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١٢﴾
12. Na inapomgusa insani dhara hutuomba (katika kila hali); anapolala ubavu, au anapokaa au kusimama. Tunapomuondolea dhara, hupita (kuendelea na maasi) kama kwamba hakutuomba (Tumuondoshee) dhara iliyomgusa. Hivyo ndivyo walivyopambiwa wapindukao mipaka yale waliyokuwa wakiyatenda.


وَلَقَدْ أَهْلَكْنَا الْقُرُونَ مِن قَبْلِكُمْ لَمَّا ظَلَمُوا ۙ وَجَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ وَمَا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْقَوْمَ الْمُجْرِمِينَ﴿١٣﴾
13. Na kwa yakini Tuliangamiza karne nyingi kabla yenu walipodhulumu, na wakawajia Rasuli wao kwa hoja bayana, na hawakuwa wa kuamini. Hivyo ndivyo Tunavyowalipa watu wahalifu.


ثُمَّ جَعَلْنَاكُمْ خَلَائِفَ فِي الْأَرْضِ مِن بَعْدِهِمْ لِنَنظُرَ كَيْفَ تَعْمَلُونَ﴿١٤﴾
14. Kisha Tukakufanyeni makhalifa katika ardhi baada yao, ili Tutazame vipi mtatenda.


وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ ۙ قَالَ الَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَاءَنَا ائْتِ بِقُرْآنٍ غَيْرِ هَـٰذَا أَوْ بَدِّلْهُ ۚ قُلْ مَا يَكُونُ لِي أَنْ أُبَدِّلَهُ مِن تِلْقَاءِ نَفْسِي ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ ۖ إِنِّي أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّي عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ﴿١٥﴾
15. Na wanaposomewa Aayaat Zetu bayana, wale wasiotarajai kukutana Nasi husema: “Lete Qur-aan isiyokuwa hii au ibadilishe.” Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم):  “Hainipasii mimi kuibadilisha kwa khiyari ya nafsi yangu. Mimi sifuati ila tu yale nilofunuliwa Wahy. Hakika mimi nakhofu nikimuasi Rabb (Mola) wangu, adhabu ya siku kubwa mno.


قُل لَّوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا تَلَوْتُهُ عَلَيْكُمْ وَلَا أَدْرَاكُم بِهِ ۖ فَقَدْ لَبِثْتُ فِيكُمْ عُمُرًا مِّن قَبْلِهِ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ﴿١٦﴾
16. Sema: “Kama Angetaka Allaah nisingelikusomeeni (hii Qur-aan) na wala Asingelikujulisheni nayo. Kwani nimekwishaishi nanyi umri (mwingi) kabla yake.  Je, basi hamtii akilini?”


فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْمُجْرِمُونَ﴿١٧﴾
17. Basi nani dhalimu zaidi kuliko (yule) anayemtungia Allaah uongo au amekadhibisha Aayaat (na ishara, hoja n.k) Zake? Hakika wahalifu hawatofaulu.


وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ ۚ قُلْ أَتُنَبِّئُونَ اللَّـهَ بِمَا لَا يَعْلَمُ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿١٨﴾
18.  Na wanaabudu asiyekuwa Allaah ambao (hawawezi) kuwadhuru na wala (hawawezi) kuwanufaisha, na wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.” Sema: “Je, mnamjulisha Allaah kwa yale Asiyoyajua katika mbingu na ardhini? Subhaanahu wa Ta’alaa! (Utakasifu ni Wake Na Ametukuka kwa ‘Uluwa) kwa yale yote wanayomshirikisha.


وَمَا كَانَ النَّاسُ إِلَّا أُمَّةً وَاحِدَةً فَاخْتَلَفُوا ۚ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ فِيمَا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ﴿١٩﴾
19. Na wala watu hawakuwa ila ni ummah mmoja (wote wanampwekesha Allaah), kisha wakakhitilafiana. Na kama si neno lililotangulia kutoka kwa Rabb (Mola) wako; bila shaka ingehukumiwa baina yao katika yale waliyokuwa kwayo wakikhitilafiana.


وَيَقُولُونَ لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ آيَةٌ مِّن رَّبِّهِ ۖ فَقُلْ إِنَّمَا الْغَيْبُ لِلَّـهِ فَانتَظِرُوا إِنِّي مَعَكُم مِّنَ الْمُنتَظِرِينَ﴿٢٠﴾
20. Na wanasema: “Kwanini haikuteremshwa juu yake Aayah (ishara, dalili) kutoka kwa Rabb (Mola) wake?” Basi sema: “Hakika (‘ilm) ya ghayb ni ya Allaah Pekee. Basi ngojeeni; hakika mimi niko pamoja nanyi miongoni mwa wanaongojea.” 


وَإِذَا أَذَقْنَا النَّاسَ رَحْمَةً مِّن بَعْدِ ضَرَّاءَ مَسَّتْهُمْ إِذَا لَهُم مَّكْرٌ فِي آيَاتِنَا ۚ قُلِ اللَّـهُ أَسْرَعُ مَكْرًا ۚ إِنَّ رُسُلَنَا يَكْتُبُونَ مَا تَمْكُرُونَ﴿٢١﴾
21. Na Tunapowaonjesha watu Rahmah baada ya dhara iliyowagusa; tahamaki wanafanyia hila katika Aayaat (ishara n.k) Zetu. Sema: “Allaah ni Mwepesi zaidi wa kuvurumisha hila. Hakika Wajumbe wetu wanaandika yale mnayofanya hila.”


هُوَ الَّذِي يُسَيِّرُكُمْ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا كُنتُمْ فِي الْفُلْكِ وَجَرَيْنَ بِهِم بِرِيحٍ طَيِّبَةٍ وَفَرِحُوا بِهَا جَاءَتْهَا رِيحٌ عَاصِفٌ وَجَاءَهُمُ الْمَوْجُ مِن كُلِّ مَكَانٍ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ أُحِيطَ بِهِمْ ۙ دَعَوُا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ لَئِنْ أَنجَيْتَنَا مِنْ هَـٰذِهِ لَنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ﴿٢٢﴾
22. Yeye Ndiye Anayekuendesheni katika bara (nchi kavu) na bahari. Mpaka mnapokuwa katika majahazi na yanakwenda nao kwa upepo mzuri, na wakafurahia; mara ukawajia upepo wa dhoruba, na yakawajia mawimbi kutoka kila upande, na wakayakinisha kwamba wameshazungukwa. Hapo humwomba Allaah mukhliswiyn (wenye kumtakasia) Dini (wakisema): “Ukituokoa katika haya, bila shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru.”


فَلَمَّا أَنجَاهُمْ إِذَا هُمْ يَبْغُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ ۗ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّمَا بَغْيُكُمْ عَلَىٰ أَنفُسِكُم ۖ مَّتَاعَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ ثُمَّ إِلَيْنَا مَرْجِعُكُمْ فَنُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٢٣﴾
23. Lakini Anapowaokoa, tahamaki wao wanafanya ufidhuli katika ardhi bila ya haki. Enyi watu! Hakika ufidhuli wenu ni dhidi ya nafsi zenu. Ni starehe ya uhai wa dunia. Kisha Kwetu marejeo yenu; Tutakujulisheni kwa yale   mliyokuwa mkiyatenda.


إِنَّمَا مَثَلُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَاءٍ أَنزَلْنَاهُ مِنَ السَّمَاءِ فَاخْتَلَطَ بِهِ نَبَاتُ الْأَرْضِ مِمَّا يَأْكُلُ النَّاسُ وَالْأَنْعَامُ حَتَّىٰ إِذَا أَخَذَتِ الْأَرْضُ زُخْرُفَهَا وَازَّيَّنَتْ وَظَنَّ أَهْلُهَا أَنَّهُمْ قَادِرُونَ عَلَيْهَا أَتَاهَا أَمْرُنَا لَيْلًا أَوْ نَهَارًا فَجَعَلْنَاهَا حَصِيدًا كَأَن لَّمْ تَغْنَ بِالْأَمْسِ ۚ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴿٢٤﴾
24. Hakika mfano wa uhai wa dunia ni kama maji Tuliyoyateremsha kutoka mbinguni, kisha yakachanganyika nayo mimea ya ardhi katika wanayoila watu na wanyama, mpaka ardhi ilipokamilisha uzuri wake na ikapambika na wakayakinisha watu wake kwamba wanao uwezo juu yake (ya kuivuna); tahamaki amri Yetu ikaijia usiku au mchana, Tukaifanya kama iliyofekwa kama kwamba haikusitawi jana. Hivyo ndivyo Tunavyofasili Aayaat (ishara, hoja n.k) kwa watu wanaotafakari.


وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَىٰ دَارِ السَّلَامِ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٢٥﴾
25. Na Allaah Anaitia Daarus-Salaam (nyumba ya amani Jannah), na Anamwongoza Amtakaye kuelekea njia iliyonyooka.

لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ ۖ وَلَا يَرْهَقُ وُجُوهَهُمْ قَتَرٌ وَلَا ذِلَّةٌ ۚ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴿٢٦﴾
26. Kwa wale waliofanya mazuri watapata (jazaa) nzuri kabisa na ziada (kumuona Allaah Jannah). Na wala vumbi halitowafunika nyuso zao na wala (hawatopatikana na) udhalilifu. Hao ni watu wa Jannah. Wao humo ni wenye kudumu.


وَالَّذِينَ كَسَبُوا السَّيِّئَاتِ جَزَاءُ سَيِّئَةٍ بِمِثْلِهَا وَتَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۖ مَّا لَهُم مِّنَ اللَّـهِ مِنْ عَاصِمٍ ۖ كَأَنَّمَا أُغْشِيَتْ وُجُوهُهُمْ قِطَعًا مِّنَ اللَّيْلِ مُظْلِمًا ۚ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴿٢٧﴾
27. Na wale waliochuma maovu, jazaa ya uovu ni mfano wake vile vile, na udhalilifu utawafunika. Hawatopata atakayewaepusha na (adhabu ya) Allaah. Zitakuwa nyuso zao kama kwamba zimefunikwa na vipande vya usiku wenye giza kubwa. Hao ni watu wa Motoni, wao humo ni wenye kudumu.


وَيَوْمَ نَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشْرَكُوا مَكَانَكُمْ أَنتُمْ وَشُرَكَاؤُكُمْ ۚ فَزَيَّلْنَا بَيْنَهُمْ ۖ وَقَالَ شُرَكَاؤُهُم مَّا كُنتُمْ إِيَّانَا تَعْبُدُونَ﴿٢٨﴾
28. Na (wakumbushe): Siku Tutakayowakusanya wote, kisha Tutawaambia wale walioshirikisha: “(Bakieni) mahali penu nyinyi na washirika wenu (mliowashirikisha na Allaah duniani).” Kisha Tutawatenganisha baina yao. Na washirika wao watasema: “Hamkuwa mkituabudu sisi.”


فَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ إِن كُنَّا عَنْ عِبَادَتِكُمْ لَغَافِلِينَ﴿٢٩﴾
29. “Basi Allaah Anatosheleza kuwa Shahiydaa (Mwenye kushuhudia yote) baina yetu na baina yenu kwamba sisi tulikuwa hatuna habari na ‘ibaadah zenu.” 


هُنَالِكَ تَبْلُو كُلُّ نَفْسٍ مَّا أَسْلَفَتْ ۚ وَرُدُّوا إِلَى اللَّـهِ مَوْلَاهُمُ الْحَقِّ ۖ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ﴿٣٠﴾
30. Huko (Siku ya Qiyaamah) kila nafsi itatiwa mtihanini kwa iliyoyatanguliza. Na watarudishwa kwa Allaah, Mawlaa (Mola) wao wa haki. Na yatawapotea yale yote waliyokuwa wakiyatunga. 


قُلْ مَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ أَمَّن يَمْلِكُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَمَن يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَمَن يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۚ فَسَيَقُولُونَ اللَّـهُ ۚ فَقُلْ أَفَلَا تَتَّقُونَ﴿٣١﴾
31. Sema: (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) “Nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni na ardhini. Au nani anayemiliki kusikia na kuona; na nani anayemtoa (aliye) hai kutoka mfu, na anayemtoa mfu kutoka (aliye) uhai; na nani anayedabiri mambo (yote)?   Watasema: “Ni Allaah”; basi sema: “Je basi hamwogopi (Allaah)?” 


فَذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمُ الْحَقُّ ۖ فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ إِلَّا الضَّلَالُ ۖ فَأَنَّىٰ تُصْرَفُونَ﴿٣٢﴾
32. Basi Huyo Ndiye Allaah, Rabb (Mola) wenu wa haki. Na kuna nini baada ya haki ila upotofu? Basi mnageuzwa wapi?


كَذَٰلِكَ حَقَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ عَلَى الَّذِينَ فَسَقُوا أَنَّهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ﴿٣٣﴾
33. Hivyo ndivyo Neno la Rabb (Mola) wako lilivyothibiti juu ya wale waliofanya ufasiki kwamba hawatoamini.


قُلْ هَلْ مِن شُرَكَائِكُم مَّن يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ ۚ قُلِ اللَّـهُ يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ﴿٣٤﴾
34. Sema: “Je, yuko kati ya washirika wenu anayeanzisha uumbaji kisha anaurudisha?” Sema: “Allaah Anaanzisha uumbaji kisha Anaurudisha. Basi vipi mnaghilibiwa (mbali na haki?)


قُلْ هَلْ مِن شُرَكَائِكُم مَّن يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ ۚ قُلِ اللَّـهُ يَهْدِي لِلْحَقِّ ۗ أَفَمَن يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ أَحَقُّ أَن يُتَّبَعَ أَمَّن لَّا يَهِدِّي إِلَّا أَن يُهْدَىٰ ۖ فَمَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ﴿٣٥﴾
35. Sema: “Je, yuko kati ya (hao) washirika wenu anayeongoza kwenye haki?” Sema: “Allaah Anaongoza kwenye haki.  Je, basi anayeongoza kwenye haki anastahiki zaidi kufuatwa au (anastahiki) ambaye asiyeongoza isipokuwa tu yeye (mwenyewe) aongozwe?  Basi mna nini, mnvyohukumu?”


وَمَا يَتَّبِعُ أَكْثَرُهُمْ إِلَّا ظَنًّا ۚ إِنَّ الظَّنَّ لَا يُغْنِي مِنَ الْحَقِّ شَيْئًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِمَا يَفْعَلُونَ﴿٣٦﴾
36. Na wengi wao hawafuati ila dhana tu. Hakika dhana haifai kitu (chochote) mbele ya haki. Hakika Allaah ni ‘Aliym (Mjuzi) kwa yale yote wayatendayo.


وَمَا كَانَ هَـٰذَا الْقُرْآنُ أَن يُفْتَرَىٰ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَـٰكِن تَصْدِيقَ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ وَتَفْصِيلَ الْكِتَابِ لَا رَيْبَ فِيهِ مِن رَّبِّ الْعَالَمِينَ﴿٣٧﴾
37. Na haiwezekani hii Qur-aan kuwa imetungwa pasi na Allaah, lakini inasadikisha yale yaliyokuja kabla yake (Tawraat, Injiyl, Zabuwr), na ni tafsili ya Kitabu ambayo haina shaka ndani yake imetoka kwa Rabb (Mola) wa walimwengu.


أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۖ قُلْ فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِّثْلِهِ وَادْعُوا مَنِ اسْتَطَعْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿٣٨﴾
38. Je, (ndio) wanasema (kuwa Qur-aan) ameitunga (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)?  Sema: “Hebu basi leteni Suwrah (yoyote ile) ya mfano wake, na waiteni mnaoweza (wakusaidieni) pasi na Allaah mkiwa ni wakweli.”


بَلْ كَذَّبُوا بِمَا لَمْ يُحِيطُوا بِعِلْمِهِ وَلَمَّا يَأْتِهِمْ تَأْوِيلُهُ ۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الظَّالِمِينَ﴿٣٩﴾
39. Bali wamekadhibisha yale wasiyoyaelewa vyema elimu yake, na wala uhakika wake halisi haujawafikia. Hivyo ndivyo walivyokadhibisha wale wa kabla yao. Basi tazama vipi ilikuwa hatima ya madhalimu.


وَمِنْهُم مَّن يُؤْمِنُ بِهِ وَمِنْهُم مَّن لَّا يُؤْمِنُ بِهِ ۚ وَرَبُّكَ أَعْلَمُ بِالْمُفْسِدِينَ﴿٤٠﴾
40. Na miongoni mwao wako wanaoiamini, na miongoni mwao wako wasioiamini. Na Rabb (Mola) wako Anawajua zaidi mafisadi.


وَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل لِّي عَمَلِي وَلَكُمْ عَمَلُكُمْ ۖ أَنتُم بَرِيئُونَ مِمَّا أَعْمَلُ وَأَنَا بَرِيءٌ مِّمَّا تَعْمَلُونَ﴿٤١﴾
41. Na wakikukadhibisha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi sema: “Mimi nina ‘amali zangu, nanyi mna ‘amali zenu. Nyinyi hamna dhima na yale niyatendayo, na wala mimi sina dhima na yale myatendayo.


وَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُونَ إِلَيْكَ ۚ أَفَأَنتَ تُسْمِعُ الصُّمَّ وَلَوْ كَانُوا لَا يَعْقِلُونَ﴿٤٢﴾
42. Na miongoni mwao (wako) wanaokusikiliza. Je, kwani wewe unasikilizisha viziwi japokuwa hawatii akilini?


وَمِنْهُم مَّن يَنظُرُ إِلَيْكَ ۚ أَفَأَنتَ تَهْدِي الْعُمْيَ وَلَوْ كَانُوا لَا يُبْصِرُونَ﴿٤٣﴾
43. Na miongoni mwao (wako) wanaokutazama. Je, kwani wewe unaongoza kipofu japokuwa hawaoni?


إِنَّ اللَّـهَ لَا يَظْلِمُ النَّاسَ شَيْئًا وَلَـٰكِنَّ النَّاسَ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ﴿٤٤﴾
44. Hakika Allaah Hadhulumu watu chochote, lakini watu nafsi zao wenyewe (ndio) wenye kujidhulumu.


وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ كَأَن لَّمْ يَلْبَثُوا إِلَّا سَاعَةً مِّنَ النَّهَارِ يَتَعَارَفُونَ بَيْنَهُمْ ۚ قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِلِقَاءِ اللَّـهِ وَمَا كَانُوا مُهْتَدِينَ﴿٤٥﴾
45. Na (wakumbushe) Siku Atakayowakusanya (wataona) kama kwamba hawakuishi (duniani) isipokuwa saa moja ya mchana, watatambuana. Kwa yakini wamekhasirika wale waliokadhibisha kukutana na Allaah, na hawakuwa wenye kuongoka.


وَإِمَّا نُرِيَنَّكَ بَعْضَ الَّذِي نَعِدُهُمْ أَوْ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِلَيْنَا مَرْجِعُهُمْ ثُمَّ اللَّـهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا يَفْعَلُونَ﴿٤٦﴾
46. Na kama Tutakuonyesha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) baadhi ya yale Tunayowaahidi (ya adhabu) au Tukikufisha, basi Kwetu (ndio) marejeo yao; kisha Allaah ni Shahiyd (Mwenye kushuhudia yote) juu ya yale wanayoyatenda.


وَلِكُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولٌ ۖ فَإِذَا جَاءَ رَسُولُهُمْ قُضِيَ بَيْنَهُم بِالْقِسْطِ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ﴿٤٧﴾
47. Na kila ummah kuna Rasuli. Basi anapokuja Rasuli wao (wakimkanusha) inahukumiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawatodhulumiwa.


وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿٤٨﴾
48. Na wanasema: “Lini (itafika) hiyo ahadi mkiwa ni wakweli?”


قُل لَّا أَمْلِكُ لِنَفْسِي ضَرًّا وَلَا نَفْعًا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ ۗ لِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٌ ۚ إِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ فَلَا يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً ۖ وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ﴿٤٩﴾
49. Sema: “Siimilikii kwa ajili ya nafsi yangu dhara na wala manufaa isipokuwa Aliyotaka Allaah. Kwa kila Ummah una muda (wake) maalumu. Utakapofika muda wao, basi hawatoweza kuakhirisha saa moja wala hawatoweza kutanguliza.”


قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَتَاكُمْ عَذَابُهُ بَيَاتًا أَوْ نَهَارًا مَّاذَا يَسْتَعْجِلُ مِنْهُ الْمُجْرِمُونَ﴿٥٠﴾
50. Sema: “Mnaonaje ikikufikieni adhabu Yake usiku au mchana, (sehemu) ipi wanaihimiza wahalifu?”


أَثُمَّ إِذَا مَا وَقَعَ آمَنتُم بِهِ ۚ آلْآنَ وَقَدْ كُنتُم بِهِ تَسْتَعْجِلُونَ﴿٥١﴾
51. Kisha tena! Itakapotokea ndio mtaiamini? (Wataambiwa): “Je, sasa? (Ndio mnaamini)? Na hali mlikuwa mnaihimiza?”


ثُمَّ قِيلَ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا ذُوقُوا عَذَابَ الْخُلْدِ هَلْ تُجْزَوْنَ إِلَّا بِمَا كُنتُمْ تَكْسِبُونَ﴿٥٢﴾
52. Kisha wataambiwa wale waliodhulumu: “Onjeni adhabu yenye kudumu. Kwani je, mtalipwa (vingine) isipokuwa kwa yale mliyokuwa mkiyachuma?”


وَيَسْتَنبِئُونَكَ أَحَقٌّ هُوَ ۖ قُلْ إِي وَرَبِّي إِنَّهُ لَحَقٌّ ۖ وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ﴿٥٣﴾
53. Na wanakuuliza je, hiyo (adhabu ya Qiyaamah) ni kweli?  Sema: “Ndio! Naapa kwa Rabb (Mola) wangu! Hakika hiyo bila shaka ni kweli! Nanyi si wenye kushinda kuikwepa.”


وَلَوْ أَنَّ لِكُلِّ نَفْسٍ ظَلَمَتْ مَا فِي الْأَرْضِ لَافْتَدَتْ بِهِ ۗ وَأَسَرُّوا النَّدَامَةَ لَمَّا رَأَوُا الْعَذَابَ ۖ وَقُضِيَ بَيْنَهُم بِالْقِسْطِ ۚ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ﴿٥٤﴾
54. Na kama ingelikuwa kila nafsi iliyodhulumu, inamiliki yote yaliyomo katika ardhi, bila shaka ingeliyatolea fidia kwayo (lakini haitopokelewa), na wataficha (au watadhihirisha) majuto watakapoona adhabu. Na itahukumiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawatodhulumiwa. 


أَلَا إِنَّ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ أَلَا إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿٥٥﴾
55. Tanabahi!  Hakika ni vya Allaah (Pekee) vilivyomo katika mbingu na ardhi. Tanabahi! Hakika ahadi ya Allaah ni kweli, lakini wengi wao hawajui.


هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ﴿٥٦﴾
56. Yeye Ndiye Anayehuisha na Anayefisha, na Kwake (Yeye Pekee) mtarejeshwa.


يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَتْكُم مَّوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَشِفَاءٌ لِّمَا فِي الصُّدُورِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ﴿٥٧﴾
57. Enyi watu! Kwa yakini yamekujieni mawaidha kutoka kwaRabb (Mola) wenu, na shifaa (poza) ya yale (maradhi) yote yaliyomo vifuani, na Mwongozo na Rahmah kwa Waumini.


قُلْ بِفَضْلِ اللَّـهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَبِذَٰلِكَ فَلْيَفْرَحُوا هُوَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ﴿٥٨﴾
58. Sema: “Kwa fadhila za Allaah na kwa Rahmah Yake basi kwa hayo wafurahi.” Hayo ni kheri kuliko wanayoyakusanya.


قُلْ أَرَأَيْتُم مَّا أَنزَلَ اللَّـهُ لَكُم مِّن رِّزْقٍ فَجَعَلْتُم مِّنْهُ حَرَامًا وَحَلَالًا قُلْ آللَّـهُ أَذِنَ لَكُمْ ۖ أَمْ عَلَى اللَّـهِ تَفْتَرُونَ﴿٥٩﴾
59. Sema: (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) “Mnaonaje zile riziki Alizokuteremshieni Allaah, kisha mkazifanya katika hizo (nyingine kuwa) ni haraam na halaal.” Sema: “Je, Allaah Amekupeni idhini (kuzifanya hivyo?) Au mnamtungia (uongo) Allaah?”


وَمَا ظَنُّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَشْكُرُونَ﴿٦٠﴾
60. Na nini dhana ya wale wanaomtungia Allaah uongo Siku ya Qiyaamah? (wanadhani hawatoadhibiwa?) Hakika Allaah Ana fadhila (nyingi) juu ya watu, lakini wengi wao hawashukuru.


وَمَا تَكُونُ فِي شَأْنٍ وَمَا تَتْلُو مِنْهُ مِن قُرْآنٍ وَلَا تَعْمَلُونَ مِنْ عَمَلٍ إِلَّا كُنَّا عَلَيْكُمْ شُهُودًا إِذْ تُفِيضُونَ فِيهِ ۚ وَمَا يَعْزُبُ عَن رَّبِّكَ مِن مِّثْقَالِ ذَرَّةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ وَلَا أَصْغَرَ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْبَرَ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ﴿٦١﴾
61. Na hushughuliki katika jambo lolote, na wala husomi humo (chochote) katika Qur-aan, na wala hamtendi ‘amali yoyote isipokuwa Tunakuwa Mashahidi juu yenu mnaposhughulika nayo. Na hakifichiki kwa Rabb (Mola) wako (chochote hata) cha uzito wa atomu (au sisimizi) katika ardhi wala mbinguni na (hata) kidogo kuliko hicho na (hata) kikubwa zaidi ya hicho isipokuwa kimo katika Kitabu kilicho bayana.


أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّـهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴿٦٢﴾
62. Tanabahi!  Hakika vipenzi wa Allaah hawana khofu juu yao, na wala hawatohuzunika.


الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ﴿٦٣﴾
63. Ambao wameamini na wakawa wana taqwa.


لَهُمُ الْبُشْرَىٰ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۚ لَا تَبْدِيلَ لِكَلِمَاتِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿٦٤﴾
64. Watapata bishara katika uhai wa dunia na ya Aakhirah. Hakuna mabadiliko katika Maneno ya Allaah. Huko ndiko kufuzu adhimu.


وَلَا يَحْزُنكَ قَوْلُهُمْ ۘ إِنَّ الْعِزَّةَ لِلَّـهِ جَمِيعًا ۚ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ﴿٦٥﴾
65. Na wala isikuhuzunishe kauli yao. Hakika taadhima zote ni za Allaah Pekee. Yeye Ndiye As-Samiy’ul-‘Aliym (Mwenye kusikia yote – Mjuzi wa yote).


أَلَا إِنَّ لِلَّـهِ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ ۗ وَمَا يَتَّبِعُ الَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ شُرَكَاءَ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ﴿٦٦﴾
66. Tanabahi!  Ni vya Allaah Pekee vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na wale wanaoomba asiyekuwa Allaah, hawafuati washirika (wanaodaiwa kuwa ni wa Allaah). Hawafuati isipokuwa dhana, nao hawana isipokuwa wanabuni uongo.


هُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ اللَّيْلَ لِتَسْكُنُوا فِيهِ وَالنَّهَارَ مُبْصِرًا ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ﴿٦٧﴾
67. Yeye Ndiye Aliyekufanyieni usiku ili mpate utulivu humo, na mchana ung’aao (mpate kuonea). Hakika katika hayo ni Aayaat (ishara, hoja, dalili n.k) kwa watu wanaosikia (wakazingatia).


قَالُوا اتَّخَذَ اللَّـهُ وَلَدًا ۗ سُبْحَانَهُ ۖ هُوَ الْغَنِيُّ ۖ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ إِنْ عِندَكُم مِّن سُلْطَانٍ بِهَـٰذَا ۚ أَتَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ﴿٦٨﴾
68. (Mayahudi na Manaswara) Wanasema: “(Allaah) Amejifanyia waladi.” Subhaanah! (Utakasifu ni Wake). Yeye Ni Al-Ghaniyyu (Mkwasi) Ni Vyake vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Hamna nyinyi dalili kwa hayo (mnayodai). Je, mnasema juu ya Allaah msiyoyajua?


قُلْ إِنَّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ لَا يُفْلِحُونَ﴿٦٩﴾
69. Sema: “Hakika wale wanaomtungia uongo Allaah hawatofaulu.”


مَتَاعٌ فِي الدُّنْيَا ثُمَّ إِلَيْنَا مَرْجِعُهُمْ ثُمَّ نُذِيقُهُمُ الْعَذَابَ الشَّدِيدَ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ﴿٧٠﴾
70. (Watapata) Starehe (chache tu) katika dunia, kisha Kwetu ndio marejeo yao, kisha Tutawaonjesha adhabu kali kwa yale waliyokuwa wakiyakufuru.


وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ نُوحٍ إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ إِن كَانَ كَبُرَ عَلَيْكُم مَّقَامِي وَتَذْكِيرِي بِآيَاتِ اللَّـهِ فَعَلَى اللَّـهِ تَوَكَّلْتُ فَأَجْمِعُوا أَمْرَكُمْ وَشُرَكَاءَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُنْ أَمْرُكُمْ عَلَيْكُمْ غُمَّةً ثُمَّ اقْضُوا إِلَيَّ وَلَا تُنظِرُونِ﴿٧١﴾
71. Na wasomee habari ya Nuwh, alipoiambia kaumu yake: “Enyi kaumu yangu! Ikiwa kukaa kwangu na kukumbusha kwangu Aayaat (ishara, hoja n.k) za Allaah kumekuwa ni taklifu (na udhia) juu yenu   basi kwa Allaah nategemea. Basi pangeni mambo yenu na washirika wenu (mnidhuru), kisha mpango wenu usifichike kwenu; kisha mpitishe kwangu wala msinipe muda wa kungojea.”


فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَمَا سَأَلْتُكُم مِّنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى اللَّـهِ ۖ وَأُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْمُسْلِمِينَ﴿٧٢﴾
72. “Mkikengeuka, (wito wangu khiari yenu) kwani mimi sikukuombeni ujira wowote. Sitaki ujira isipokuwa kwa Allaah na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waislamu.”


فَكَذَّبُوهُ فَنَجَّيْنَاهُ وَمَن مَّعَهُ فِي الْفُلْكِ وَجَعَلْنَاهُمْ خَلَائِفَ وَأَغْرَقْنَا الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُنذَرِينَ﴿٧٣﴾
73. Lakini walimkadhibisha; Tukamuokoa (Nuwh) pamoja na waliokuwa naye katika jahazi, na Tukawafanya makhalifa, na Tukawagharikisha wale waliokadhibisha Aayaat (ishara) Zetu. Basi tazama vipi ilikuwa hatima ya walioonywa.


ثُمَّ بَعَثْنَا مِن بَعْدِهِ رُسُلًا إِلَىٰ قَوْمِهِمْ فَجَاءُوهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَمَا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا بِمَا كَذَّبُوا بِهِ مِن قَبْلُ ۚ كَذَٰلِكَ نَطْبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِ الْمُعْتَدِينَ﴿٧٤﴾
74. Kisha Tukapeleka baada yake, Rasuli kwa kaumu zao, wakawajia kwa hoja bayana; lakini hawakuwa wenye kuyaaamini yale waliyoyakadhibisha zamani.  Hivyo ndivyo Tunavyopiga chapa juu ya nyoyo za wenye kutaadi.


ثُمَّ بَعَثْنَا مِن بَعْدِهِم مُّوسَىٰ وَهَارُونَ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ بِآيَاتِنَا فَاسْتَكْبَرُوا وَكَانُوا قَوْمًا مُّجْرِمِينَ﴿٧٥﴾
75. Kisha baada ya hao, Tukamtuma Muwsaa na Haaruwn kwa Fir’awn na wakuu wake kwa Aayaat (miujiza, ishara) Zetu walitakabari na wakawa watu wahalifu.


فَلَمَّا جَاءَهُمُ الْحَقُّ مِنْ عِندِنَا قَالُوا إِنَّ هَـٰذَا لَسِحْرٌ مُّبِينٌ﴿٧٦﴾
76. Ilipowajia haki kutoka Kwetu, walisema: “Hii bila shaka ni sihiri bayana.”


قَالَ مُوسَىٰ أَتَقُولُونَ لِلْحَقِّ لَمَّا جَاءَكُمْ ۖ أَسِحْرٌ هَـٰذَا وَلَا يُفْلِحُ السَّاحِرُونَ﴿٧٧﴾
77. Muwsaa akasema: “Je, mnasema (hivyo) kuhusu haki ilipokujeni? Hii ni sihiri?  Na wachawi hawafaulu.”


قَالُوا أَجِئْتَنَا لِتَلْفِتَنَا عَمَّا وَجَدْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا وَتَكُونَ لَكُمَا الْكِبْرِيَاءُ فِي الْأَرْضِ وَمَا نَحْنُ لَكُمَا بِمُؤْمِنِينَ﴿٧٨﴾
78. Wakasema: “Je, umetujia ili utugeuze kutokana na yale tuliyowakuta nayo baba zetu, na ili muwe na kiburi (nyinyi wawili) katika ardhi? Na sisi hatutawaamini nyinyi.”


وَقَالَ فِرْعَوْنُ ائْتُونِي بِكُلِّ سَاحِرٍ عَلِيمٍ﴿٧٩﴾
79. Na Fir’awn akasema: “Nileteeni kila mchawi mjuzi.”


فَلَمَّا جَاءَ السَّحَرَةُ قَالَ لَهُم مُّوسَىٰ أَلْقُوا مَا أَنتُم مُّلْقُونَ﴿٨٠﴾
80. Basi walipokuja wachawi, Muwsaa akawaambia: “Tupeni mnavyotaka kuvitupa.”


فَلَمَّا أَلْقَوْا قَالَ مُوسَىٰ مَا جِئْتُم بِهِ السِّحْرُ ۖ إِنَّ اللَّـهَ سَيُبْطِلُهُ ۖ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُصْلِحُ عَمَلَ الْمُفْسِدِينَ﴿٨١﴾
81. Basi walipotupa, Muwsaa alisema: “Mliyokuja nayo ni sihiri.  Hakika Allaah Atayabatilisha. Hakika Allaah Hatengenezi ‘amali za mafisadi.”


وَيُحِقُّ اللَّـهُ الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُجْرِمُونَ﴿٨٢﴾
82. “Na Allaah Atathibitisha haki kwa maneno Yake; japokuwa watakirihika wahalifu.”



فَمَا آمَنَ لِمُوسَىٰ إِلَّا ذُرِّيَّةٌ مِّن قَوْمِهِ عَلَىٰ خَوْفٍ مِّن فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِمْ أَن يَفْتِنَهُمْ ۚ وَإِنَّ فِرْعَوْنَ لَعَالٍ فِي الْأَرْضِ وَإِنَّهُ لَمِنَ الْمُسْرِفِينَ﴿٨٣﴾
83. Basi hawakumwamini Muwsaa isipokuwa (baadhi tu ya) vizazi katika kaumu yake kwa kumkhofu Fir’awn na wakuu wao wasiwafitinishe (kuwatesa). Na hakika Fir’awn ni jeuri katika ardhi, na hakika yeye bila shaka ni miongoni mwa wapindukao mipaka.


وَقَالَ مُوسَىٰ يَا قَوْمِ إِن كُنتُمْ آمَنتُم بِاللَّـهِ فَعَلَيْهِ تَوَكَّلُوا إِن كُنتُم مُّسْلِمِينَ﴿٨٤﴾
84. Na Muwsaa akasema: “Enyi watu wangu! Ikiwa mmemwamini Allaah; basi Kwake mtawakali, mkiwa ni Waislamu.”


فَقَالُوا عَلَى اللَّـهِ تَوَكَّلْنَا رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِّلْقَوْمِ الظَّالِمِينَ﴿٨٥﴾
85. Wakasema: “Tumetawakali kwa Allaah. Ee Rabb (Mola) wetu! Usitujaalie kuwa ni mtihani kwa watu madhalimu.”


وَنَجِّنَا بِرَحْمَتِكَ مِنَ الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ﴿٨٦﴾
86. “Na Tuokoe kwa Rahmah Yako dhidi ya watu makafiri.


وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ وَأَخِيهِ أَن تَبَوَّآ لِقَوْمِكُمَا بِمِصْرَ بُيُوتًا وَاجْعَلُوا بُيُوتَكُمْ قِبْلَةً وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ ۗ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ﴿٨٧﴾
87. Na Tukamfunulia Wahy Muwsaa na kaka yake kwamba: “Watengenezeeni watu wenu katika mji nyumba na zifanyeni nyumba zenu sehemu za ‘ibaadah na simamisheni Swalaah. Na wabashirie Waumini.


وَقَالَ مُوسَىٰ رَبَّنَا إِنَّكَ آتَيْتَ فِرْعَوْنَ وَمَلَأَهُ زِينَةً وَأَمْوَالًا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا رَبَّنَا لِيُضِلُّوا عَن سَبِيلِكَ ۖ رَبَّنَا اطْمِسْ عَلَىٰ أَمْوَالِهِمْ وَاشْدُدْ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَلَا يُؤْمِنُوا حَتَّىٰ يَرَوُا الْعَذَابَ الْأَلِيمَ﴿٨٨﴾
88. Na Muwsaa akasema: “Ee Rabb (Mola) Wetu! Hakika Wewe Umempa Fir’awn na wakuu wake mapambo na mali katika uhai wa dunia. Ee Rabb wetu, ili wapoteze (watu) njia Yako. Rabb wetu! Ziangamize mali zao na fanya nyoyo zao ziwe ngumu kwani hawatoamini mpaka waone adhabu iumizayo.”


قَالَ قَدْ أُجِيبَت دَّعْوَتُكُمَا فَاسْتَقِيمَا وَلَا تَتَّبِعَانِّ سَبِيلَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ﴿٨٩﴾
89. (Allaah) Akasema: “Imekwishaitikiwa du’aa yenu nyinyi wawili, basi nyookeni (katika Dini na kulingania) na wala msifuate njia ya wale wasiojua (haki).”


وَجَاوَزْنَا بِبَنِي إِسْرَائِيلَ الْبَحْرَ فَأَتْبَعَهُمْ فِرْعَوْنُ وَجُنُودُهُ بَغْيًا وَعَدْوًا ۖ حَتَّىٰ إِذَا أَدْرَكَهُ الْغَرَقُ قَالَ آمَنتُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا الَّذِي آمَنَتْ بِهِ بَنُو إِسْرَائِيلَ وَأَنَا مِنَ الْمُسْلِمِينَ﴿٩٠﴾
90. Na Tukawavukisha wana wa Israaiyl bahari, basi Fir’awn akawafuata (pamoja) na jeshi lake kwa ukandamizaji na uadui; mpaka ilipomfikia (Fir’awn) gharka akasema: “Nimeamini kwamba hapana ilaah (muabudiwa wa haki) isipokuwa Yule waliyemwamini wana wa Israaiyl, na mimi ni miongoni mwa Waislamu.”


آلْآنَ وَقَدْ عَصَيْتَ قَبْلُ وَكُنتَ مِنَ الْمُفْسِدِينَ﴿٩١﴾
91. (Malaika wakamwambia): “Sasa (ndio unaamini) na hali umeasi kabla, na ulikuwa miongoni mwa mafisadi!?”


فَالْيَوْمَ نُنَجِّيكَ بِبَدَنِكَ لِتَكُونَ لِمَنْ خَلْفَكَ آيَةً ۚ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ عَنْ آيَاتِنَا لَغَافِلُونَ﴿٩٢﴾
92. Basi leo Tunakuokoa kwa (kuuweka) mwili wako ili uwe Aayah (zingatio, ishara) kwa watakaokuja nyuma yako. Na hakika watu wengi wameghafilika na Aayaat (ishara, hoja) Zetu.  


وَلَقَدْ بَوَّأْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ مُبَوَّأَ صِدْقٍ وَرَزَقْنَاهُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ فَمَا اخْتَلَفُوا حَتَّىٰ جَاءَهُمُ الْعِلْمُ ۚ إِنَّ رَبَّكَ يَقْضِي بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ﴿٩٣﴾
93. Na kwa yakini Tuliwapa makazi wana wa Israaiyl; makazi mazuri, na Tukawaruzuku katika vizuri; na hawakukhitilafiana mpaka ilipowajia elimu. Hakika Rabb (Mola) wako Atahukumu baina yao Siku ya Qiyaamah katika yale yote waliyokuwa wakikhitilafiana.


فَإِن كُنتَ فِي شَكٍّ مِّمَّا أَنزَلْنَا إِلَيْكَ فَاسْأَلِ الَّذِينَ يَقْرَءُونَ الْكِتَابَ مِن قَبْلِكَ ۚ لَقَدْ جَاءَكَ الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُمْتَرِينَ﴿٩٤﴾
94. Na ukiwa una shaka (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika yale Tuliyokuteremshia, basi waulize wale wanaosoma Kitabu (cha Injiyl na Tawraat) kabla yako. Kwa yakini imekujia haki kutoka kwa Rabb (Mola) wako, basi usijekuwa miongoni mwa wanaoshuku.


وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ فَتَكُونَ مِنَ الْخَاسِرِينَ﴿٩٥﴾
95. Wala usijekuwa miongoni mwa wale waliokadhibisha Aayaat (na ishara, hoja n.k) za Allaah ukawa miongoni mwa waliokhasirika.


إِنَّ الَّذِينَ حَقَّتْ عَلَيْهِمْ كَلِمَتُ رَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ﴿٩٦﴾
96. Hakika wale ambao neno la (ghadhabu la) Rabb (Mola) wako limethibiti juu yao, hawataamini.


وَلَوْ جَاءَتْهُمْ كُلُّ آيَةٍ حَتَّىٰ يَرَوُا الْعَذَابَ الْأَلِيمَ﴿٩٧﴾
97. Japokuwa itawajia kila Aayah (mawaidha, zingatio) mpaka waone adhabu iumizayo.


فَلَوْلَا كَانَتْ قَرْيَةٌ آمَنَتْ فَنَفَعَهَا إِيمَانُهَا إِلَّا قَوْمَ يُونُسَ لَمَّا آمَنُوا كَشَفْنَا عَنْهُمْ عَذَابَ الْخِزْيِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَمَتَّعْنَاهُمْ إِلَىٰ حِينٍ﴿٩٨﴾
98. Basi kwa nini usiweko mji mmoja ukaamini (kabla ya adhabu) na iymaan yake ikawafaa (kujikinga na adhabu? Hukukutokea katika tarehe) isipokuwa kaumu ya Yuwnus. Walipoamini, Tuliwaondoshea adhabu ya hizaya duniani, na Tukawasterehesha mpaka wakati (tulioutaka).


وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ لَآمَنَ مَن فِي الْأَرْضِ كُلُّهُمْ جَمِيعًا ۚ أَفَأَنتَ تُكْرِهُ النَّاسَ حَتَّىٰ يَكُونُوا مُؤْمِنِينَ﴿٩٩﴾
99. Na kama Angetaka Rabb (Mola) wako, basi wangeliamini wote pamoja walioko katika ardhi. Je, basi wewe (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) utashurutisha watu mpaka wawe Waumini?


وَمَا كَانَ لِنَفْسٍ أَن تُؤْمِنَ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَيَجْعَلُ الرِّجْسَ عَلَى الَّذِينَ لَا يَعْقِلُونَ﴿١٠٠﴾
100. Na hakuna nafsi yoyote iamini isipokuwa kwa idhini ya Allaah. Naye Hujaalia ar-rijsa (shari, upotofu, hizaaya) kwa wale ambao wasiotia akilini.


قُلِ انظُرُوا مَاذَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَمَا تُغْنِي الْآيَاتُ وَالنُّذُرُ عَن قَوْمٍ لَّا يُؤْمِنُونَ﴿١٠١﴾
101. Sema: “Tazameni nini yaliyoko mbinguni na ardhini.” Lakini Aayaat (ishara, zingatio) zote na maonyo haiwafai kitu watu wasioamini.


فَهَلْ يَنتَظِرُونَ إِلَّا مِثْلَ أَيَّامِ الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلِهِمْ ۚ قُلْ فَانتَظِرُوا إِنِّي مَعَكُم مِّنَ الْمُنتَظِرِينَ﴿١٠٢﴾
102. Je, wanangojea jingine (la maangamizi) isipokuwa mfano wa siku (za) wale waliopita kabla yao?  Sema: “Basi ngojeeni, hakika mimi (pia) ni pamoja nanyi miongoni mwa wanaongojea.”


ثُمَّ نُنَجِّي رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا ۚ كَذَٰلِكَ حَقًّا عَلَيْنَا نُنجِ الْمُؤْمِنِينَ﴿١٠٣﴾
103. Kisha (mwishowe) Tunawaokoa Rasuli Wetu na wale walioamini. Hivyo ndivyo haki Kwetu kuwaokoa Waumini.


قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِن كُنتُمْ فِي شَكٍّ مِّن دِينِي فَلَا أَعْبُدُ الَّذِينَ تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَـٰكِنْ أَعْبُدُ اللَّـهَ الَّذِي يَتَوَفَّاكُمْ ۖ وَأُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ﴿١٠٤﴾
104. Sema: (Ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) “Enyi watu! Ikiwa mna shaka kutokana na Dini yangu, basi (mimi) siabudu ambavyo mnaviabudu badala ya Allaah; lakini namwabudu Allaah Ambaye Anakufisheni. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waumini.”


وَأَنْ أَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُشْرِكِينَ﴿١٠٥﴾
105. “Na (nimeamrishwa kwamba): Elekeza uso wako kwa Dini Haniyfaa (ya Tawhiyd - kumpwekesha Allaah), na wala usijekuwa miongoni mwa washirikina.



وَلَا تَدْعُ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُكَ وَلَا يَضُرُّكَ ۖ فَإِن فَعَلْتَ فَإِنَّكَ إِذًا مِّنَ الظَّالِمِينَ﴿١٠٦﴾
106. “Na (nimeamrishwa pia): Wala usiombe badala ya Allaah asiyekufaa (ukimwabudu) na wala asiyekudhuru (usipomwabudu). Na ukifanya (hivyo), basi hakika utakuwa miongoni mwa madhalimu.”


وَإِن يَمْسَسْكَ اللَّـهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ ۖ وَإِن يُرِدْكَ بِخَيْرٍ فَلَا رَادَّ لِفَضْلِهِ ۚ يُصِيبُ بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۚ وَهُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿١٠٧﴾
107. Na Allaah Akikugusisha dhara, basi hakuna wa kuiondosha isipokuwa Yeye. Na (Allaah) Akikutakia kheri, basi hakuna wa kurudisha fadhila Zake, Anasababisha kumfikia kwayo (fadhila Yake) Amtakaye katika waja Wake. Naye ni Al-Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).


قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَكُمُ الْحَقُّ مِن رَّبِّكُمْ ۖ فَمَنِ اهْتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهْتَدِي لِنَفْسِهِ ۖ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيْهَا ۖ وَمَا أَنَا عَلَيْكُم بِوَكِيلٍ﴿١٠٨﴾
108. Sema: “Enyi watu!  Kwa yakini imekujieni haki kutoka kwaRabb (Mola) wenu. Basi atakayeongoka, hakika anaongoka kwa ajili ya (manufaa ya) nafsi yake. Na atakayepotoka, hakika anapotoka kwa (hasara) ya nafsi yake. Nami si msimamizi wenu.” (wa kukuongoeni).


وَاتَّبِعْ مَا يُوحَىٰ إِلَيْكَ وَاصْبِرْ حَتَّىٰ يَحْكُمَ اللَّـهُ ۚ وَهُوَ خَيْرُ الْحَاكِمِينَ﴿١٠٩﴾
109. Na fuata (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) yale ulofunuliwa Wahy na subiri mpaka Allaah Ahukumu. Naye ni Mbora wa wanaohukumu. 


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com