Quraysh (106)


سُورَةُ  قُرَيْش
Quraysh (106)

(Imeteremka Makka)

 
Mwenyezi Mungu katika Sura hii anataja neema alizo wafanyia Maqureshi kwa Nyumba yake takatifu ambayo ameilinda na maadui wake, naye akawapa maskani karibu yake wakapata utukufu na amani, na wakawa wanasafiri siku za baridi kwenda Yaman, na siku za joto wakenda Shamu, kwa ajili ya biashara bila ya mtu yeyote kuwaletea maovu, na hali watu jirani zao siku zote wakinyakuliwa. Na neema hizo zinawajibikia kumuabudu huyo aliye kuwa anawalisha wasipate njaa, na akawalinda na khofu.

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

لِإِيلَافِ قُرَيْشٍ ﴿١﴾

1. Kwa ada ya Maquraysh.

إِيلَافِهِمْ رِحْلَةَ الشِّتَاءِ وَالصَّيْفِ ﴿٢﴾

2. Ada yao ya misafara ya majira ya baridi na majira ya joto.

فَلْيَعْبُدُوا رَبَّ هَـٰذَا الْبَيْتِ ﴿٣﴾

3. Basi wamuabudu Rabb (Mola) wa nyumba hii (Ka’bah).

الَّذِي أَطْعَمَهُم مِّن جُوعٍ وَآمَنَهُم مِّنْ خَوْفٍ ﴿٤﴾

4. Ambaye Anawalisha (wakati waliowazunguka wakiwa kwenye) njaa, na Akawapa amani (wakati waliowazunguka wakiwa kwenye) khofu.





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com