الحديث التاسع والعشرون
"تعبد الله لا تشرك به شيئا"
عن معاذِ بن جبلٍ رضي الله عنه قال: قلت: يا رسول الله، أخْبِرني
بِعَمَلٍ يُدْخِلُني الجنَةَ ويُبَاعِدُني عَنِ النارِ. قال: ((لَقَدْ سألْتَ عَنْ
عَظيمٍ، وإنَهُ لَيَسيرٌ عَلى من يَسَّرَهُ اللهُ تعالى عَلَيْهِ : تَعْبُدُ اللهَ
لا تُشْرِكُ بِهِ شَيئاً، وتُقيمُ الصَّلاةَ ،وتُؤتي الزكاةَ، وتصومُ
رمضانَ، وتَحُجُّ البيتَ)) .ثم قال: (( ألا أَدُلُّكَ على أبْوَابِ الخيرِ؟:
الصَّومُ جُنَّةٌ، والصَّدقةُ تُطْفِىءُ الخَطِيئةَ كما يُطْفىءُ الماءُ النارَ،
وصَلاةَ الرَّجُلِ في جَوْفِ الَّليْلِ، ثم تلا: {تَتَجَافَى جُنُوبُهُمْ عَنْ
الْمَضَاجِعِ} - حتى بلغ - {يَعْمَلُونَ} السجدة: 16-17 .
ثم قال: ((ألا أُخْبِرُكَ بِرَأسِ الأمْرِ وَعَمودِهِ
وَذِرْوَةِ سَنَامِهِ؟)) قلتُ: بَلىَ يا رسول الله. قال: (( رَأْسُ الأمْرِ
الإسلامُ، وعَمُودُهُ الصَّلاةُ، وَذِرْوَةُ سَنَامِهِ الجِهادُ )).
ثم قال: (( ألا أخْبِرُكَ بِمِلاكَ ذَلِكَ كلِّهِ ؟)) فَقُلْتُ
بَلَى يا رَسول الله، فأخَذَ بِلِسانِهِ وقال: ((كُفَّ عَلَيْكَ هذا))
. قلت : يا نبيَّ الله، وإنَّا لمؤاخَذُونَ بِما نَتَكَلَّمُ بِه ؟)) فقال: ((
ثَكِلَتْكَ أمُّكَ يَا مُعَاذُ, وَهَلْ يَكُبُّ الناسَ في النارِ على
وُجُوهِهِمْ )) أو قال: ((على مناخِرِهِم - إلاَّ حَصَائدُ
ألسِنَتهم))
رَوَاهُ
التِّرْمِذِيُّ وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ.
HADITHI YA 29
MUABUDU ALLAAH NA USIMSHIRIKISHE NA CHOCHOTE
Kutoka kwa
Mu'aadh Ibn Jabal رضي الله عنه amesema:
Nilisema: Ewe Mtume صلى الله عليه وسلم , niambie kitendo ambacho
kitanipeleka peponi na kitaniokoa na moto. Akasema : Umeniuliza jambo
kubwa lakini ni rahisi kwa yule ambae Mola anaemsahilishia. Muabudu
Allaah wala usimshirikishe na chochote, Swali, toa Zaka, funga
Ramadhani,
nenda kuhiji (Makka). Kisha akasema: Je? Nikuonyeshe milango
ya kheri? Saumu ni ngao, sadaka inazima dhambi kama vile maji yanavyozima
moto, na kuswali katikati ya usiku: Kisha akasoma {Mbavu zao zinaachana na vitanda kwa kumwomba Mola wao Mlezi kwa
khofu na kutumaini, na hutoa kutokana na tulivyo waruzuku. Nafsi yoyote haijui
waliyo fichiwa katika hayo yanayo furahisha macho - ni malipo ya yale waliyo
kuwa wakiyatenda}
Sura As-Sajda 32: 16 na 17
Tena akasema: Je, nikwambie kilele cha
hilo jambo; nguzo yake na sehemu yake ya juu kabisa? Nikasema : Ndio ewe
Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu. Akasema: kilele chake ni Uislamu, nguzo
yake ni Swala na sehemu yake ya juu kabisa ni Jihaad. Kisha akasema
: Je, nikwambie muhimili wa yote haya? Nikasema: Ndio ewe
Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu. Akaukamata ulimi wake na
akasema; Uzuie huu. Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu; yale tunayoyasema
tutahukumiwa kwayo? Akasema: mama yako akuhurumie ewe
Mu'aadh! Kuna kitu zaidi kinachowaangusha watu kifudifudi motoni kama si
mavuno ya ndimi zao?
Imesimuliwa
na At-Tirmidhi na ni hadithi Hasan.