An-Naazi’aat (79)


سُورَةُ  النَّازِعَات
An-Naazi’aat (79)

(Imeteremka Makka)

 
Imeanza Sura hii kwa kiapo juu ya kumkinika kufufuliwa na kutokea kwake, na ikafuatia hayo hadithi ya Musa na Firauni kumliwaza Mtume s.a.w., na ikataja khabari za binaadamu na juhudi zake, na ikadhihirisha yanayo wangojea majabari, na yanayo wangojea makhaini. Na Sura ikakhitimisha kwa kuuliza kwao washirikina lini itakuwa hiyo Saa ya Kiyama, na ikabainisha kwamba kazi ya Mtume ni kuwaonya wenye kukiogopa Kiyama, sio kujua wakati wake.


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

وَالنَّازِعَاتِ غَرْقًا ﴿١﴾

1. Naapa kwa wanaong’oa kwa nguvu.


وَالنَّاشِطَاتِ نَشْطًا ﴿٢﴾

2. Na (Naapa kwa) wanaotoa kwa upole.


وَالسَّابِحَاتِ سَبْحًا ﴿٣﴾

3. Na (Naapa kwa) wanaoogelea kuogelea (katika anga).

فَالسَّابِقَاتِ سَبْقًا ﴿٤﴾

4. Kisha (Naapa kwa) wenye kutangulia mbele kwa kushidana.

فَالْمُدَبِّرَاتِ أَمْرًا ﴿٥﴾

5. Kisha (Naapa kwa) wenye kudabiri (kila) jambo.

يَوْمَ تَرْجُفُ الرَّاجِفَةُ ﴿٦﴾

6. Siku itakapotetemeka tetemeko.


تَتْبَعُهَا الرَّادِفَةُ ﴿٧﴾

7.   Itaifuata ar-raadifah (inayofuatia).


قُلُوبٌ يَوْمَئِذٍ وَاجِفَةٌ ﴿٨﴾

8. Nyoyo siku hiyo zitatikisika (kwa nguvu).

أَبْصَارُهَا خَاشِعَةٌ ﴿٩﴾

9. Macho yake yatainama (kwa udhalilifu, khofu, majuto).

يَقُولُونَ أَإِنَّا لَمَرْدُودُونَ فِي الْحَافِرَةِ ﴿١٠﴾

10. Watasema: “Je, hivi sisi tutarudishwa katika hali ya asili (ya uhai)?

أَإِذَا كُنَّا عِظَامًا نَّخِرَةً ﴿١١﴾

11. “Je, (hata) tukiwa ni mifupa iliyovurugika?”

قَالُوا تِلْكَ إِذًا كَرَّةٌ خَاسِرَةٌ ﴿١٢﴾

12. Watasema: “Hiyo basi ni marejeo (yenye) khasara.”

فَإِنَّمَا هِيَ زَجْرَةٌ وَاحِدَةٌ ﴿١٣﴾

13. Basi hakika hicho (Qiyaamah) ni zajratun (ukelele wa baragumu) mmoja tu!

فَإِذَا هُم بِالسَّاهِرَةِ ﴿١٤﴾

14. Tahamaki hao uwandani.

هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ مُوسَىٰ ﴿١٥﴾

15. Je, imekufikia hadiyth ya Muwsaa?

إِذْ نَادَاهُ رَبُّهُ بِالْوَادِ الْمُقَدَّسِ طُوًى ﴿١٦﴾

16. (Pale) Rabb (Mola) wake Alipomuita kwenye bonde takatifu la Twuwaa.

اذْهَبْ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ إِنَّهُ طَغَىٰ ﴿١٧﴾

17. (Akamwambia): “Nenda kwa Fir-’awn, hakika yeye amepindukia mipaka.”

فَقُلْ هَل لَّكَ إِلَىٰ أَن تَزَكَّىٰ ﴿١٨﴾

18. Umwambie: “Je, unataka kujitakasa?

وَأَهْدِيَكَ إِلَىٰ رَبِّكَ فَتَخْشَىٰ ﴿١٩﴾

19. “Na nikuongoze kwa Rabb (Mola) wako umuogope?”

فَأَرَاهُ الْآيَةَ الْكُبْرَىٰ ﴿٢٠﴾

20. Basi akamuonyesha Aayah (ishara, dalili, hoja) kubwa kabisa.

فَكَذَّبَ وَعَصَىٰ ﴿٢١﴾

21. Lakini akakadhibisha, na akaasi.

ثُمَّ أَدْبَرَ يَسْعَىٰ ﴿٢٢﴾

22. Kisha akageuka nyuma na kufanya juhudi (dhidi ya Muwsaa na ujumbe aliokuja nao). 

فَحَشَرَ فَنَادَىٰ ﴿٢٣﴾

23. Akakusanya (watu), kisha akanadi.

فَقَالَ أَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَىٰ ﴿٢٤﴾

24. Akasema: “Mimi ni mola wenu mkuu.”

فَأَخَذَهُ اللَّـهُ نَكَالَ الْآخِرَةِ وَالْأُولَىٰ ﴿٢٥﴾

25. Basi Allaah Alimchukuwa kwa adhabu ya mfano wa pekee mwisho na mwanzo. 

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبْرَةً لِّمَن يَخْشَىٰ ﴿٢٦﴾

26. Hakika katika hayo bila shaka (kuna) zingatio kwa yule anayeogopa.

أَأَنتُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَمِ السَّمَاءُ ۚ بَنَاهَا ﴿٢٧﴾

27. Je, nyinyi ndio wenye umbo la nguvu zaidi, au mbingu? Alizozijenga.

رَفَعَ سَمْكَهَا فَسَوَّاهَا ﴿٢٨﴾

28. Amenyanyua kimo chake, kisha Akazisawazisha.

وَأَغْطَشَ لَيْلَهَا وَأَخْرَجَ ضُحَاهَا ﴿٢٩﴾

29. Na Akaufunika (giza) usiku wake, na Akautoa mchana wake (kwenye mwanga).

وَالْأَرْضَ بَعْدَ ذَٰلِكَ دَحَاهَا ﴿٣٠﴾

30. Na ardhi baada ya hayo Akaitandaza.


أَخْرَجَ مِنْهَا مَاءَهَا وَمَرْعَاهَا ﴿٣١﴾

31. Akatoa humo maji yake na malisho yake.

وَالْجِبَالَ أَرْسَاهَا ﴿٣٢﴾

32. Na majabali Akayathibitisha imara.


مَتَاعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ ﴿٣٣﴾

33. (Kuwa ni) Manufaa kwenu na kwa wanyama wenu wa mifugo.

فَإِذَا جَاءَتِ الطَّامَّةُ الْكُبْرَىٰ ﴿٣٤﴾
34. Basi itakapokuja atw-Twaammah (balaa) kubwa (Qiyaamah).


يَوْمَ يَتَذَكَّرُ الْإِنسَانُ مَا سَعَىٰ ﴿٣٥﴾

35. Siku insani atakapokumbuka yale (yote) aliyoyakimbilia kwa kuyafanyia juhudi.

وَبُرِّزَتِ الْجَحِيمُ لِمَن يَرَىٰ ﴿٣٦﴾

36. Na (Moto wa) Al-Jahiym utakapoonyeshwa wazi kwa aonaye.

فَأَمَّا مَن طَغَىٰ ﴿٣٧﴾

37. Basi yule aliyevuka mipaka kuasi.

وَآثَرَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا ﴿٣٨﴾

38. Na akapendelea uhai wa dunia.

فَإِنَّ الْجَحِيمَ هِيَ الْمَأْوَىٰ ﴿٣٩﴾

39. Basi hakika (Moto wa) Al-Jahiym (utakuwa) ndio mahali pa makaazi (yake).

وَأَمَّا مَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ وَنَهَى النَّفْسَ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٤٠﴾

40. Ama yule aliyekhofu kisimamo cha Rabb (Mola) wake, na akaikataza nafsi yake na matamanio.

فَإِنَّ الْجَنَّةَ هِيَ الْمَأْوَىٰ ﴿٤١﴾

41. Basi hakika Jannah (itakuwa) ndio mahali pa makaazi (yake).

يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا ﴿٤٢﴾

42. Wanakuuliza (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Saa (Qiyaamah) lini kutokea kwake?

فِيمَ أَنتَ مِن ذِكْرَاهَا ﴿٤٣﴾

43. Uko wapi wewe (una elimu gani) uweze kukitaja?

إِلَىٰ رَبِّكَ مُنتَهَاهَا ﴿٤٤﴾

44. Kwa Rabb (Mola) wako ndio kuishia kwake.


إِنَّمَا أَنتَ مُنذِرُ مَن يَخْشَاهَا ﴿٤٥﴾

45. Hakika wewe ni muonyaji wa yule anayekiogopa.

كَأَنَّهُمْ يَوْمَ يَرَوْنَهَا لَمْ يَلْبَثُوا إِلَّا عَشِيَّةً أَوْ ضُحَاهَا ﴿٤٦﴾

46. Siku watakapokiona, watakuwa kama kwamba hawakukaa (duniani) isipokuwa jioni moja au mchana wake.





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com