Hadiyth Ya 8
Nitamsibu Mja Wangu Kwa Homa Duniani Nimpunguzie Moto Wa Akhera
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ رَسُولِ
اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ عَادَ مَرِيضًا وَمَعَهُ أَبُو
هُرَيْرَةَ مِنْ وَعْكٍ كَانَ بِهِ فَقَالَ لَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ
عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((أَبْشِرْ. إِنَّ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ يَقُولُ: نَارِي
أُسَلِّطُهَا عَلَى عَبْدِي الْمُؤْمِنِ فِي الدُّنْيَا لِتَكُونَ حَظَّهُ مِنْ
النَّارِ فِي الْآخِرَةِ)) أحمد وابن ماجه
والترمذي – حديث حسن
Kutoka
kwa Abu Hurayrahرضي الله عنه kwamba Mtume صلى الله عليه
وسلم alimtembelea
mgonjwa aliyekuwa na homa pamoja naye akamwambia mgonjwa: ((Bishara njema
(Furahi) kutoka kwa Allaah Anasema: Nitamsibu mja Wangu duniani kwa kwa moto
(homa) Wangu ili aepukane na sehemu ya moto wa Akhera)) [Ahmad, Ibn
Maajah, At-Tirmidhiy- Hadiyth Hasan]