Hadiyth Ya 6
Mmoja Katika Waja Wangu Ameamini Na Mmoja Amekufuru
عَنْ زَيْدِ بْنِ خَالِدٍ الْجُهَنِيِّ
قَالَ صَلَّى لَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ صَلَاةَ
الصُّبْحِ بِالْحُدَيْبِيَةِ عَلَى أَثَرِ سَمَاءٍ كَانَتْ مِنْ اللَّيْلِ
فَلَمَّا انْصَرَفَ أَقْبَلَ عَلَى النَّاسِ قَالَ: ((هَلْ تَدْرُونَ مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ؟))
قَالُوا اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ قَالَ(( أَصْبَحَ مِنْ عِبَادِي مُؤْمِنٌ
بِي وكَافِرٌ, فَأَمَّا مَنْ قَالَ
مُطِرْنَا بِفَضْلِ اللَّهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَذَلِكَ مُؤْمِنٌ بِي كَافِرٌ
بِالْكَوْكَبِ وَأَمَّا مَنْ قَالَ مُطِرْنَا بِنَوْءِ كَذَا وَكَذَا فَذَلِكَ
كَافِرٌ بِي مُؤْمِنٌ بِالْكَوْكَبِ)) البخاري والنسائي
Kutoka
kwa Zayd bin Khaalid Al-Juhaniyy رضي الله
عنه ambaye amesema: Mtume صلى الله عليه وسلم alituswalisha
Swalah ya Alfajiri (huko) Al-Hudaybiyah baada ya kunyesha mvua usiku. ِAlipomaliza
aliwaelekea watu akasema: ((Je, mnajua Mola wetu kasema nini?)) Watu wakasema
Allaah na Mjumbe Wake ni wajuzi bora. Akasema: ((Mmoja katika waja Wangu
ameamka asubuhi akiwa ameniamini na mmoja amenikufuru. Ama aliyesema: tumepewa
mvua kwa fadhila za Allaah na Rehma Zake, huyo ameniamini Mimi na amezikana
nyota; ama aliyesema: tumepewa mvua kwa nyota kadhaa wa kadhaa huyu amenikufuru
Mimi na ameamini nyota)) [Al-Bukhaariy na An-Nasaaiy]