Hadiyth Ya 43 Nani Aapaye Kwa Jina Langu Kuwa Sitamsamehe Fulani?



  عَنْ جُنْدَبٍ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَدَّثَ ((أَنَّ رَجُلًا قَالَ وَاللَّهِ لَا يَغْفِرُ اللَّهُ لِفُلَانٍ وَإِنَّ اللَّهَ تَعَالَى قَالَ مَنْ ذَا الَّذِي يَتَأَلَّى عَلَيَّ أَنْ لَا أَغْفِرَ لِفُلَانٍ فَإِنِّي قَدْ غَفَرْتُ لِفُلَانٍ وَأَحْبَطْتُ عَمَلَكَ))  أَوْ كَمَا قَالَمسلم


Kutoka kwa Jundub رضي الله عنه    ambaye alisema kuwa  Mtume صلى الله عليه وسلم  alihadithia:((Mtu alisema: WaLLaahi, Allaah Hatomsamehe fulani kwa haya, Allaah سبحانه وتعالى Akasema, ni nani huyo aapaye kwa Jina Langu kuwa Sitamsamehe fulani? Basi kwa yakini Nimemsamehe (huyo) fulani na Nimeporomosha 'amali zako.)) [au kama alivyosema]. [Muslim]