Hadiyth Ya 42 Waja Peponi Watapata Ridhaa Ya Allaah
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ
قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ اللَّهَ
تَبَارَكَ وَتَعَالَى يَقُولُ لِأَهْلِ الْجَنَّةِ: يَا أَهْلَ الْجَنَّةِ. فَيَقُولُونَ لَبَّيْكَ رَبَّنَا
وَسَعْدَيْكَ. فَيَقُولُ هَلْ رَضِيتُمْ؟ فَيَقُولُونَ وَمَا لَنَا لَا نَرْضَى وَقَدْ
أَعْطَيْتَنَا مَا لَمْ تُعْطِ أَحَدًا مِنْ خَلْقِكَز فَيَقُولُ:
أَنَا أُعْطِيكُمْ أَفْضَلَ مِنْ ذَلِكَ.
قَالُوا: يَا رَبِّ وَأَيُّ شَيْءٍ أَفْضَلُ مِنْ ذَلِكَ؟ فَيَقُولُ: أُحِلُّ عَلَيْكُمْ رِضْوَانِي
فَلَا أَسْخَطُ عَلَيْكُمْ بَعْدَهُ أَبَدًا)) البخاري, مسلم و الترمذي
Kutoka kwa
Abu Sa’iyd Al-Khudriyyرضي الله عنه ambaye kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم amesema: ((Allaah تَبَارَكَ وَتَعَالَى Atawaambia watu wa peponi: Enyi watu wa
Peponi! Watasema: Labeka Mola wetu tuko kwa ajili ya amri Yako. Kheri yote imo
katika mikono Yako. Kisha Atasema: Je,
mmeridhika? Watasema: Vipi tusiridhike
na hali Umetupa ambayo Hukumpa yeyote mwengine katika viumbe Vyako? Kisha
Atasema: Nitakupeni kilicho bora kuliko
hayo. Watasema: Ee Mola, ni kipi kilicho bora kuliko haya? Atasema: Nitafanya
ridhaa (mapenzi) Yangu iwateremkie na baada ya hapo Sitokasirika nanyi tena
abadan)) [Al-Bukhaariy,
Muslim na At-Tirmidhy]