Hadiyth Ya 40Mambo Yaliyozungushiwa Pepo Na Moto
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ رَسُولِ
اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((لَمَّا خَلَقَ اللَّهُ
الْجَنَّةَ وَالنَّارَ أَرْسَلَ جِبْرِيلَ إِلَى الْجَنَّةِ فَقَال: انْظُرْ
إِلَيْهَا وَإِلَى مَا أَعْدَدْتُ لِأَهْلِهَا فِيهَاز قَالَ:
فَجَاءَهَا وَنَظَرَ إِلَيْهَا وَإِلَى مَا أَعَدَّ اللَّهُ لِأَهْلِهَا
فِيهَا. قَالَ: فَرَجَعَ إِلَيْهِ قَالَ: فَوَعِزَّتِكَ لَا
يَسْمَعُ بِهَا أَحَدٌ إِلَّا دَخَلَهَا. فَأَمَرَ بِهَا فَحُفَّتْ
بِالْمَكَارِهِ. فَقَالَ: ارْجِعْ إِلَيْهَا فَانْظُرْ إِلَى مَا أَعْدَدْتُ
لِأَهْلِهَا فِيهَاز قَالَ: فَرَجَعَ
إِلَيْهَا فَإِذَا هِيَ قَدْ حُفَّتْ بِالْمَكَارِهِز فَرَجَعَ إِلَيْهِ فَقَالَ: وَعِزَّتِكَ لَقَدْ
خِفْتُ أَنْ لَا يَدْخُلَهَا أَحَدٌ. قَالَ: اذْهَبْ إِلَى النَّارِ فَانْظُرْ
إِلَيْهَا وَإِلَى مَا أَعْدَدْتُ لِأَهْلِهَا فِيهَا. فَإِذَا هِيَ يَرْكَبُ بَعْضُهَا بَعْضًا. فَرَجَعَ إِلَيْهِ فَقَالَ: وَعِزَّتِكَ لَا
يَسْمَعُ بِهَا أَحَدٌ فَيَدْخُلَهَا. فَأَمَرَ بِهَا فَحُفَّتْ بِالشَّهَوَاتِ
فَقَالَ: ارْجِعْ إِلَيْهَا فَرَجَعَ إِلَيْهَا فَقَالَ: وَعِزَّتِكَ لَقَدْ
خَشِيتُ أَنْ لَا يَنْجُوَ مِنْهَا أَحَدٌ إِلَّا دَخَلَهَا)) الترمذي و قال حديث حسن صحيح – ابو داود
والنسائي
Kutoka kwa
Abu Hurayrahرضي الله عنه kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم amesema: ((Allaah Alipoumba Pepo na moto, Alimtuma Jibriyl Peponi
Akimwambia: Iangalie na angalia matayarisho Nliyoyatayarisha kwa ajili ya
wakaazi wake. Akasema (Mtume صلى الله عليه وسلم) Kwa
hivyo alikuja kuiangalia na kuangalia matayarisho Allaah Aliyofanya kwa ajili
ya wakaazi wake. Akasema: Akarejea kwa Allaah na kusema: Kwa Utukufu Wako,
hakuna atakayesikia (habari yake) ila tu ataingia (Peponi). Kisha Akaamrisha
izungushwe (ihusishwe) mambo magumu watu wasiyoyapenda, Akasema: Rejea na
angalia yale Niliyoyatayarisha kwa ajili ya wakaazi wake. Akasema: Kisha
akarejea na akakuta imezungukwa na mambo magumu watu wasiyoyapenda. Hapo
alirejea kwa Allaah na akasema: Kwa utukufu Wako, nina khofu hakuna hata mtu
mmoja atakayeingia. Akasema: Nenda motoni ukauangalie na uangalie matayarisho
Yangu kwa ajili ya wakaazi wake. Akaona ulikuwa na matabaka moja juu ya tabaka
jengine. Akarejea kwa Allaah na akamuambia: Kwa Utukufu Wako hakuna hata mmoja
ausikiae (sifa zake) atakayeingia. Kisha Allaah Aliamrisha Uhusishwe na shahawa
(matamanio ya nafsi). Kisha Allaah Akamuambia: Rejea tena (motoni). Alirejea
tena na akasema: Kwa Utukufu, wako nakhofia kuwa hapatakuwa na yeyote
atakayenusurika nao)) [At-Tirmidhiy
akasema ni Hadiyth hasan, na Abu Daawuud na An-Nasaaiy]