Hadiyth Ya 4 Binaadamu Amenikana Na Amenitukana



Hadiyth Ya 4



Binaadamu Amenikana Na Amenitukana


عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ ((قَالَ اللَّهُ كَذَّبَنِي ابْنُ آدَمَ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ ذَلِكَ وَشَتَمَنِي وَلَمْ يَكُنْ لَهُ ذَلِكَ فَأَمَّا تَكْذِيبُهُ إِيَّايَ فَقَوْلُهُ لَنْ يُعِيدَنِي كَمَا بَدَأَنِي وَلَيْسَ أَوَّلُ الْخَلْقِ بِأَهْوَنَ عَلَيَّ مِنْ إِعَادَتِهِ وَأَمَّا شَتْمُهُ إِيَّايَ فَقَوْلُهُ اتَّخَذَ اللَّهُ وَلَدًا وَأَنَا الْأَحَدُ الصَّمَدُ لَمْ أَلِدْ وَلَمْ أُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لِي كُفْئًا أَحَدٌ)) البخاري والنسائ
  
Kutoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه   kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم amesema: ((Allaah Amesema: Binaadamu amenikana na hana haki ya kufanya hivyo, na amenitukana na hana haki ya kufanya hivyo. Ama kunikana kwake ni kusema: Hatonirejesha (tena) kama Alivyoniumba (Hatonifufua kama vile Alivyoniumba). Na kuumba hakukuwa rahisi Kwangu kuliko kumfufua. Ama kunitukana kwake ni kule kusema: Allaah Ana mtoto wakati Mimi ni Pweke, Mwenye kubaki Sikuzaa wala Sikuzaliwa na hakuna chochote kinacholingana Nami)) [Al-Bukhaariy na An-Nasaaiy]