Hadiyth Ya 37
  Ewe Mwanaadamu Sitojali Dhambi Zako Madamu Utanikaribia Kuomba Msamaha



عن أَنَسُ بْنُ مَالِكٍ قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((قَالَ اللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى يَا ابْنَ آدَمَ.  إِنَّكَ مَا دَعَوْتَنِي وَرَجَوْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ عَلَى مَا كَانَ فِيكَ وَلَا أُبَالِي.  يَا ابْنَ آدَمَ لَوْ بَلَغَتْ ذُنُوبُكَ عَنَانَ السَّمَاءِ ثُمَّ اسْتَغْفَرْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ وَلَا أُبَالِي. يَا ابْنَ آدَمَ إِنَّكَ لَوْ أَتَيْتَنِي بِقُرَابِ الْأَرْضِ خَطَايَا ثُمَّ لَقِيتَنِي لَا تُشْرِكُ بِي شَيْئًا لَأَتَيْتُكَ بِقُرَابِهَا مَغْفِرَةً)) الترمذي وأحمد  


Kutoka kwa Anas رضي الله عنه   ambaye alisema: Nilimsikia Mtume صلى الله عليه وسلم akisema: ((Allaah تَبَارَكَ وَتَعَالَى Amesema: Ewe Mwana wa Aadam utakaponiomba na kuweka matumaini kwangu, basi Nitakusamehe makosa uliyoyafanya na sitojali. Ewe Mwana wa Aadam kama dhambi zako zingefika mawingu ya mbingu na wewe ukaomba msamaha Kwangu, Ningekusamehe.  Ewe Mwana Wa Aadam kama ungelinijia na dhambi kubwa kama dunia na ukanikabili bila ya Kunishirikisha Nitakupa maghfira)) [At-Tirmidhy na Ahmad)