Hadiyth Ya 36 Mja Aliyerudia Kufanya Madhambi Allaah Akamghufuria


عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِيمَا يَحْكِي عَنْ رَبِّهِ عَزَّ وَجَلَّ قَالَ: ((أَذْنَبَ عَبْدٌ ذَنْبًا فَقَالَ: اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي ذَنْبِي.  فَقَالَ تَبَارَكَ وَتَعَالَى:  أَذْنَبَ عَبْدِي ذَنْبًا فَعَلِمَ أَنَّ لَهُ رَبًّا يَغْفِرُ الذَّنْبَ وَيَأْخُذُ بِالذَّنْبِ ثُمَّ عَادَ فَأَذْنَبَ فَقَالَ:  أَيْ رَبِّ اغْفِرْ لِي ذَنْبِي فَقَالَ تَبَارَكَ وَتَعَالَى: عَبْدِي أَذْنَبَ ذَنْبًا فَعَلِمَ أَنَّ لَهُ رَبًّا يَغْفِرُ الذَّنْبَ وَيَأْخُذُ بِالذَّنْبِ ثُمَّ عَادَ فَأَذْنَبَ فَقَالَ: أَيْ رَبِّ اغْفِرْ لِي ذَنْبِي فَقَالَ تَبَارَكَ وَتَعَالَى: أَذْنَبَ عَبْدِي ذَنْبًا فَعَلِمَ أَنَّ لَهُ رَبًّا يَغْفِرُ الذَّنْبَ وَيَأْخُذُ بِالذَّنْبِ. اعْمَلْ مَا شِئْتَ فَقَدْ غَفَرْتُ لَكَ)) البخاري و مسلم



Kutoka kwa Abu Hurayrahرضي الله عنه  ambaye amesema kwamba mambo aliyohadithia Mtume صلى الله عليه وسلم  kutoka kwa Allaah عَزَّ وَجَلَّ ni kuwa Alisema: ((Mja wa Allaah alifanya maasi na akasema: Ewe Mola, nisamehe dhambi zangu. Na yeye Allaah تَبَارَكَ وَتَعَالَى Akasema: Mja wangu kafanya dhambi kisha kajua kwamba anaye Mola Ambaye Anasemehe madhambi na Anayeadhibu kwa kufanya dhambi. Kisha akarudi tena kufanya dhambi akasema: Ewe Mola, nisamehe dhambi zangu. Na Allaah تَبَارَكَ وَتَعَالَى Akasema: Mja wangu amefanya dhambi kisha kajua kwamba anaye Mola Ambaye Anasamehe dhambi na Anayeadhibu kwa kufanya dhambi. Kisha akarudia tena dhambi na akasema: Ee Mola, nisamehe dhambi zangu. Akasema تَبَارَكَ وَتَعَالَى: Mja wangu kafanya dhambi kisha akajua kwamba anaye Mola Anayesamehe dhambi na Anayeadhibu kwa kufanya dhambi. Fanya utakavyo, kwani Nimekusamehe)) [Al-Bukhaariy na Muslim]