Hadiyth Ya 35
 Mja Aliyewausia Wanawe Wamuunguze Kwa kukhofu Adhabu Ya Allaah


عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((كَانَ رَجُلٌ يُسْرِفُ عَلَى نَفْسِهِ فَلَمَّا حَضَرَهُ الْمَوْتُ قَالَ لِبَنِيهِ إِذَا أَنَا مُتُّ فَأَحْرِقُونِي ثُمَّ اطْحَنُونِي ثُمَّ ذَرُّونِي فِي الرِّيحِ فَوَاللَّهِ لَئِنْ قَدَرَ عَلَيَّ رَبِّي لَيُعَذِّبَنِّي عَذَابًا مَا عَذَّبَهُ أَحَدًا فَلَمَّا مَاتَ فُعِلَ بِهِ ذَلِكَ فَأَمَرَ اللَّهُ الْأَرْضَ فَقَالَ اجْمَعِي مَا فِيكِ مِنْهُ فَفَعَلَتْ فَإِذَا هُوَ قَائِمٌ فَقَالَ مَا حَمَلَكَ عَلَى مَا صَنَعْتَ قَالَ يَا رَبِّ خَشْيَتُكَ.  فَغَفَرَ لَهُ)) البخاري, مسلم, النسائي و ابن ماجه



Kutoka kwa Abu Hurayrahرضي الله عنه  kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وسلم kwamba amesema: ((Mtu alifanya maasi makubwa na wakati mauti yalipomfikia aliwausia wanawe akiwaambia: Nitapokufa, nichomeni, munisage na mulitawanye jivu langu baharini kwani, WaLLaahi, Allaah Atakaponipata, Ataniadhibu adhabu ambayo hajapata kuadhibiwa mtu mwingine. (Wanawe) walifanya walivyousiwa. Kisha (Mola) Aliiambia ardhi: Toa kile ulichokichukua. Hapo tena akazuka!  Na (Mola) akamuambia: Kitu gani kilichokufanya ufanye hayo uliyofanya? (Yule mtu) akasema: Ni kukuogopa Wewe Ee Mola wangu (au alisema: Ni kukukhofu wewe) na kwa sababu hiyo Mola Alimsamehe)) [Al-Bukhaariy, Muslim, An-Nasaaiy na Ibn Maajah]