Hadiyth ya 32 Mja Aliyejiua Akaharamishiwa Pepo
عَنْ جُنْدَبُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ
قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: (( كَانَ
فِيمَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ رَجُلٌ بِهِ جُرْحٌ فَجَزِعَ فَأَخَذَ سِكِّينًا فَحَزَّ
بِهَا يَدَهُ فَمَا رَقَأَ الدَّمُ حَتَّى مَاتَ قَالَ اللَّهُ تَعَالَى
بَادَرَنِي عَبْدِي بِنَفْسِهِ حَرَّمْتُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ)) البخاري
Kutoka kwa
Jundub bin Abdillaahرضي الله عنه ambaye
amesema kwamba: Mtume صلى الله عليه وسلم amesema: ((Alikuweko miongoni wa wale waliokutangulieni mtu ambaye
alijeruhiwa. Alikuwa na maumivu makubwa kwa hivyo alichukua kisu akajikata
mkononi mwake, damu haikusita kutoka mpaka akafa. Allaah سبحان وتعالى Akasema: Mja wangu kaniwahi kwa (kuitoa) nafsi yake;
nimemuharamishia yeye pepo)) [Al-Bukhaariy]