Hadiyth Ya 31
 Mashahidi Wako Hai Peponi Wanatamani Kurudi Kupigana Tena Fiy Sabili Allaah

  
عَنْ مَسْرُوقٍ قَالَ سَأَلْنَا عَبْدَ اللَّهِ عَنْ هَذِهِ الْآيَةِ:  ((وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ أَمْوَاتًا بَلْ أَحْيَاءٌ عِنْدَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ))  قَالَ أَمَا إِنَّا قَدْ سَأَلْنَا عَنْ ذَلِكَ فَقَالَ:  ((أَرْوَاحُهُمْ فِي جَوْفِ طَيْرٍ خُضْرٍ لَهَا قَنَادِيلُ مُعَلَّقَةٌ بِالْعَرْشِ تَسْرَحُ مِنْ الْجَنَّةِ حَيْثُ شَاءَتْ ثُمَّ تَأْوِي إِلَى تِلْكَ الْقَنَادِيلِ فَاطَّلَعَ إِلَيْهِمْ رَبُّهُمْ اطِّلَاعَةً فَقَالَ: هَلْ تَشْتَهُونَ شَيْئًا:  قَالُوا أَيَّ شَيْءٍ نَشْتَهِي وَنَحْنُ نَسْرَحُ مِنْ الْجَنَّةِ حَيْثُ شِئْنَا؟ فَفَعَلَ ذَلِكَ بِهِمْ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ. فَلَمَّا رَأَوْا أَنَّهُمْ لَنْ يُتْرَكُوا مِنْ أَنْ يُسْأَلُوا قَالُوا يَا رَبِّ نُرِيدُ أَنْ تَرُدَّ أَرْوَاحَنَا فِي أَجْسَادِنَا حَتَّى نُقْتَلَ فِي سَبِيلِكَ مَرَّةً أُخْرَى فَلَمَّا رَأَى أَنْ لَيْسَ لَهُمْ حَاجَةٌ تُرِكُوا)) مسلم, الترمذي, النسائي وابن ماجه


Kutoka kwa Masruuq ambaye amesema: Tulimuuliza ‘Abdullaah kuhusu Aayah hii ((Wala usiwadhani wale waliouwawa katika njia ya Allaah kuwa ni wafu (maiti) bali wahai, wanaruzukiwa kwa Mola wao)) [Al-‘Imraan 3:169] Akasema: Ama tuliuliza kuhusu Aayah hiyo akasema (Mtume صلى الله عليه وسلم) ((Roho zao zimo ndani ya ndege wa kijani wenye kandili zinazoning’inia kutoka kwenye ‘Arsh wanatembea huria Peponi popote wapendapo, tena hujibanza kwenye hizo kandili. Mola wao aliwatupia jicho na Akasema: Je, Mnataka chochote? Wakasema: Tutake nini tena na tunajifaragua tutakavyo Peponi? Alifanya hivyo (Mola) mara tatu. Walipoona hawataachiwa kuulizwa (tena) walisema: Ewe Mola; tungependa roho zetu uzirejeshe katika viwiliwili vyetu ili tuweze tena kupigana kwa ajili yako. Tena alipoona (Mola) hawahitaji chochote waliachiwa)) [Muslim, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah]