Hadiyth Ya 30 - Mtume صلى الله عليه وسلم Pekee Ataweza Kutuombea Siku Ya Qiyaamah


  
عَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:  يَجْتَمِعُ الْمُؤْمِنُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَيَقُولُونَ لَوْ اسْتَشْفَعْنَا إِلَى رَبِّنَا فَيَأْتُونَ آدَمَ فَيَقُولُونَ: أَنْتَ أَبُو النَّاسِ خَلَقَكَ اللَّهُ بِيَدِهِ وَأَسْجَدَ لَكَ مَلَائِكَتَهُ وَعَلَّمَكَ أَسْمَاءَ كُلِّ شَيْءٍ فَاشْفَعْ لَنَا عِنْدَ رَبِّكَ حَتَّى يُرِيحَنَا مِنْ مَكَانِنَا هَذَا.  فَيَقُولُ لَسْتُ هُنَاكُمْ وَيَذْكُرُ ذَنْبَهُ فَيَسْتَحِي - ائْتُوا نُوحًا فَإِنَّهُ أَوَّلُ رَسُولٍ بَعَثَهُ اللَّهُ إِلَى أَهْلِ الْأَرْضِ.  فَيَأْتُونَهُ فَيَقُولُ لَسْتُ هُنَاكُمْ وَيَذْكُرُ سُؤَالَهُ رَبَّهُ مَا لَيْسَ لَهُ بِهِ عِلْمٌ. فَيَسْتَحِي فَيَقُولُ: ائْتُوا خَلِيلَ الرَّحْمَنِ فَيَأْتُونَهُ فَيَقُولُ: لَسْتُ هُنَاكُمْ.  ائْتُوا مُوسَى عَبْدًا كَلَّمَهُ اللَّهُ وَأَعْطَاهُ التَّوْرَاةَ.  فَيَأْتُونَهُ فَيَقُولُ. لَسْتُ هُنَاكُمْ وَيَذْكُرُ قَتْلَ النَّفْسِ بِغَيْرِ نَفْسٍ فَيَسْتَحِي مِنْ رَبِّهِ فَيَقُولُ: ائْتُوا عِيسَى عَبْدَ اللَّهِ وَرَسُولَهُ وَكَلِمَةَ اللَّهِ وَرُوحَهُ فَيَقُولُ: لَسْتُ هُنَاكُمْ ائْتُوا مُحَمَّدًا صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَبْدًا غَفَرَ اللَّهُ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ وَمَا تَأَخَّرَ. فَيَأْتُونِي. فَأَنْطَلِقُ حَتَّى أَسْتَأْذِنَ عَلَى رَبِّي فَيُؤْذَنَ لِي فَإِذَا رَأَيْتُ رَبِّي وَقَعْتُ سَاجِدًا فَيَدَعُنِي مَا شَاءَ اللَّهُ ثُمَّ يُقَالُ: ارْفَعْ رَأْسَكَ وَسَلْ تُعْطَهْ وَقُلْ يُسْمَعْ وَاشْفَعْ تُشَفَّعْ.  فَأَرْفَعُ رَأْسِي فَأَحْمَدُهُ بِتَحْمِيدٍ يُعَلِّمُنِيهِ ثُمَّ أَشْفَعُ فَيَحُدُّ لِي حَدًّا فَأُدْخِلُهُمْ الْجَنَّةَ.  ثُمَّ أَعُودُ إِلَيْهِ فَإِذَا رَأَيْتُ رَبِّي مِثْلَهُ ثُمَّ أَشْفَعُ فَيَحُدُّ لِي حَدًّا فَأُدْخِلُهُمْ الْجَنَّةَ.  ثُمَّ أَعُودُ الرَّابِعَةَ فَأَقُولُ مَا بَقِيَ فِي النَّارِ إِلَّا مَنْ حَبَسَهُ الْقُرْآنُ وَوَجَبَ عَلَيْهِ الْخُلُودُ)) البخاري, مسلم , مالك, الترمذي وابن ماجه

Kutoka kwa Anasرضي الله عنه  kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم ambaye amesema: ((Waumini watajumuika siku ya Qiyaamah watasema: Hatupati mtu wa kutuombea kwa Mola wetu? Kwa hivyo watakwenda kwa (Nabii) Aadam watasema: Wewe ndie baba wa wana wa Aadam wote, Allaah Kakuumba kwa mkono Wake na Aliwaamrisha Malaika wakusujudie na Alikufundisha majina ya vitu vyote, kwa hivyo tuombee  kwa Mola wako ili tupate afueni kutoka na adhabu za hapa tulipo. Atasema: Siwezi. Atataja makosa yake na ataona hayaa na atasema: Nendeni kwa Nuuh kwani yeye ndiye Mjumbe wa kwanza Allaah Aliyempeleka kwa watu wa duniani. Kwa hivyo watakwenda kwake na atasema: Siwezi. Atataja kuwa alimuomba Allaah kile ambacho alikuwa hana ujuzi nacho, ataona hayaa na atawaambia: Nendeni kwa Khaliylur-Rahmaan Watakwenda (kwa Nabii Ibraahiym) na atasema: Siwezi, nendeni kwa Muusa, Mja ambaye Allaah Alizungumza naye na alimpa Tawraat. Watakwenda atasema: Siwezi. Atataja kuhusu kuua mtu bila ya kulipiza kifo (nafsi kwa nafsi) ataona hayaa (kumwendea) Bwana wake. Atasema: Nendeni kwa ‘Iysa Mja wa Allaah na Mjumbe Wake na neno Lake na roho Yake. Watakwenda na atasema, siwezi, nendeni kwa Muhammad صلى الله عليه وسلم Mja ambaye Allaah Kamsamehe dhambi zake zote zilizopita na zijazo. Watakuja kwangu na nitaondoka kutaka ruhusa ya kuonana na Mola wangu, ruhusa itatolewa, na nitakapomuona, nitasujudu. Ataniacha hivyo hivyo kwa muda atakaopenda, tena nitaambiwa: Nyanyua kichwa chako, omba na utakubaliwa. Sema na utasikizwa. Ombea (watu) shafa’a na shafa’a yako itakubaliwa. Nitanyanyua kichwa changu na nitamshukuru Allaah kwa maneno Atakayonielimisha. Kisha nitawaombea na Ataniwekea kiwango (cha wale watakaokubaliwa kuingia Peponi), nitawaingiza peponi. Kisha nitarejea (tena) kwa Allaah na nitakapomuona nitasujudu kama mwanzo. Nitaomba shafa’a (uombolezi) na Ataniwekea kiwango. Nitawaingiza Peponi. Nitarejea kwa mara ya tatu, tena mara ya nne na nitasema: Wamebaki motoni wale ambao Qur-aan imewafunga peke yao na watakuwa humo milele)) [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik, At-Tirmidhiy na Ibn Maajah]