Hadiyth ya 13
Mja Hakuonekana Na Jema Isipokuwa Kuamrisha Watu Wasamehe Wenzie
عَنْ أَبِي مَسْعُودٍ الأنصاري رضي
الله عنه قال: قال رسول اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ((حُوسِبَ
رَجُلٌ مِمَّنْ كَانَ قَبْلَكُمْ فَلَمْ يُوجَدْ لَهُ مِنْ الْخَيْرِ شَيْءٌ
إِلاَّ أَنَّهُ كَانَ يُخَالِطُ النَّاسَ وَكَانَ مُوسِرًا فَكَانَ يَأْمُرُ
غِلْمَانَهُ أَنْ يَتَجَاوَزُوا عَنْ الْمُعْسِرِ قَالَ: قَالَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ : نَحْنُ أَحَقُّ
بِذَلِكَ مِنْهُ تَجَاوَزُوا عَنْهُ)) البخاري, مسلم والنسائي
Kutoka
kwa Abu Mas’uud Al Answaariyرضي الله
عنه ambaye
alisema: Mjumbe wa Allaah صلى الله عليه
وسلم amesema: ((Mtu
mmoja katika wale waliokutangulieni alitakiwa ajieleze. Hakuonekana na jema
lolote isipokuwa alikuwa akiamiliana na watu, na alivyokuwa ni tajiri
akiwaamrisha wafanyakazi wake wamuachie (wamsamehe) mtu aliyekuwa katika hali
mbaya ya pesa (asilipe deni lake). (Akasema Mtume) Allaah عَزَّ
وَجَلَّ Akasema: Sisi Tuna
haki zaidi kuliko yeye kumsamehe)) [Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nasaaiy]