Hadiyth Ya 10
Mwenye Kufanya Amali Isiyokuwa Kwa Ajili Yangu Nitaikanusha
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ
رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ (( قَالَ اللَّهُ تَبَارَكَ
وَتَعَالَى أَنَا أَغْنَى الشُّرَكَاءِ عَنْ الشِّرْكِ مَنْ عَمِلَ عَمَلًا
أَشْرَكَ فِيهِ مَعِي غَيْرِي تَرَكْتُهُ وَشِرْكَهُ)) مسلم و ابن ماجه
Kutoka kwa Abu Huraryah رضي
الله عنه ambaye amesema: Mtume صلى
الله عليه وسلم amesema: ((Allaah تَبَارَكَ وَتَعَالَىAmesema: Mimi mkamilifu [kabisa kabisa mwenye
kukamilika kwa kila kitu] Sihitaji mshirika. Kwa hiyo, yule anayefanya amali
kwa ajili ya mwengine isiyokuwa kwa ajili Yangu, Nitaikanusha pamoja mshirika
wake)) [Muslim na Ibn Maajah]