HADITHI YA 38

الحديث الثامن والثلاثون
"من عادى لي وليا فقد آذنته بالحرب"
عن أبي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قال: قال رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : ((إنَّ الله تَعالَى قَال : مَنْ عَادَى لي وَلِيّاً فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالْحَرْبِ، وَمَا تَقَرَّبَ إلَيَّ عَبْدِي بِشَيْءٍ أَحَبَّ إلَيَّ مِمَّا افْتَرَضْتُهُ عَلَيْهِ، وَلا يَزَالُ عَبْدِي يَتَقَرَّبُ إلَيَّ بِالنَّوَافِلٍ حَتَّى أُحِبَّهُ، فإذَا أَحْبَبْتُهُ كُنْتُ سَمْعَهُ الَّذِي يَسْمَعُ بهِ، وَبَصَرَهُ الَّذِي يُبْصِرُ بهِ، وَيَدَهُ الّتي يَبْطِشُ بهَا، وَرِجْلَهُ الّتي يَمْشي بِهَا، وَلَئِنْ سَأَلِني لأعْطِيَنَّهُ، ولَئِن اسْتَعَاذَنِي لأُعِيذَنَّهُ ))

رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ     
HADITHI YA   38
ANAYEONYESHA UADUI KWA RAFIKI YANGU MTIIFU
NINATANGAZA VITA DHIDI YAKE

Kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه  ambaye amesema  kuwa Mtume صلى الله عليه وسلم  kasema: Allaah سبحانه وتعالى  kasema:  Anayeonyesha uadui kwa Walii Wangu (rafiki wa karibu, yaani mja mtiifu aliye karibu naye) , nitatangaza vita dhidi yake.  Mja Wangu hanikaribii  na kitu chochote ninachokipenda zaidi kama zile amali nilizomuwajibisha, na mja Wangu anazidi kukaribia Kwangu kwa amali njema zisizokuwa wajibu ili nimpende. Ninapompenda, Ninakuwa masikio yake anayosikilizia (yaani Allah atamjaalia asikie mazuri kama Qur’an, Dhikr, Mawaidha n.k. Na sio Muziki, Masengenyo, na Machafu mengine), macho yake anayoonea (yaani Allah atamfanya macho yake yawe yanatazama yale ya kheri), mikono yake ambayo anakamatia (Allah atafanya mikono yake ikamate vile vya halali na kufanya yale yanayomridhisha Allah), miguu yake anayoendea (na Allah ataifanya miguu yake isitembee kuyaendea ila yale mema, ya kheri na Atakayoridhika nayo Yeye Allah).  Anaponiomba (kitu) bila shaka Ninampa, na anaponiomba ulinzi bila shaka Nitamlinda.

Imesimuliwa na Al-Bukhari