HADITHI YA 35

الحديث الخامس والثلاثون
"لا تحاسدوا ولا تناجشوا ولا تباغضوا"
 عن أبي هُريرةَ رضي اللهُ عنه قال: قال رسوُل الله صلى الله عليه وسلم : ((لا تَحَاسَدُوا، ولا تَنَاجَشُوا، ولا تَباغَضُوا، ولا تَدَابَرُوا، ولا يَبعْ بَعْضُكُمْ على بَيْعِ بَعْضٍ، وكُونُوا عِبادَ اللهِ إخْوَاناً، المُسْلمُ أَخُو المُسْلمِ: لا يَظْلِمُهُ، ولا يَكْذِبُهُ، ولا يَحْقِرُهُ، التَّقْوَى هاهُنا - ويُشِيرُ إلى صَدْرِه ثَلاثَ مَرَّاتٍ , بِحَسْبِ امْرِىءٍ مِنَ الشَّرِّ أن يَحْقِرَ أخاهُ المُسْلِمَ، كُلُّ المُسْلِمِ على الْمسْلِم حَرَامٌ: دَمُهُ ومالُهُ وعِرْضُهُ))

رَوَاهُ مُسْلِمٌ  
HADITHI YA 35
MSIONEANE CHOYO, MSIZIDISHIANE BEI, MSICHUKIANE

Kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه   ambae amesema: Mtume صلى الله عليه وسلم   kasema:
Msioneane choyo, wala msizidishiane bei (za vitu), wala msichukiane, wala msipigane mapande (msitengane), wala msishindane kwa kupunguza bei.  Lakini kuweni ndugu, enyi  waja wa Mwenyeezi Mungu, Muislamu ni ndugu wa Muislamu mwenzake, hamdhulumu wala hamvunji, hamwambii uongo wala hamdharau.  Ucha Mungu  uko hapa (huku akiashiria kifuani kwake kwa vidole vyake) mara tatu.  Ni uovu wa kutosha kwa mtu kumdharau ndugu yake Muislamu.  Muislamu ameharamishiwa kwa Muislamu mwenzake: damu yake,mali yake na heshima yake (Yaani haramu kuchukua mali ya mwenzako, kumuua na kumdhalilisha).

Imesimuliwa na Muslim