HADITHI YA 34

الحديث الرابع والثلاثون
"من رأى منكم منكرا فليغيره بيده"

عن أبي سعيدٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه قال: سمعتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يقوُل :
((مَنْ رَأَى مِنْكُمْ مُنْكَراً فَلْيُغَيِّرْهُ بِيَدِهِ، فَإنْ لمَْ يَسْتَطِعْ فَبلِسانِهِ، فَإنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبقَلْبِهِ، وَذَلِكَ أضْعَفُ
اْلإِيمَانِ))
رَوَاهُ مُسْلِمٌ  
HADITHI  YA  34
YEYOTE ATAKAYEONA KITENDO KIOVU AKIONDOE
 KWA MKONO WAKE

Kutoka kwa Abu Sa'iid Al-Khudhriy  رضي الله عنه  ambaye amesema : Nilimsikia Mtume صلى الله عليه وسلم  akisema:
Yeyote yule atakayeona kitendo kiovu mwache akiondoe (abadilishe) kwa mkono wake, ikiwa hawezi basi kwa ulimi wake (alikemee au kukataza), na ikiwa hawezi basi kwa moyo wake (achukie) na huo (yaani kuona baya na kunyamaza) ni udhaifu wa Imani.

Imesimuliwa na Muslim