Hadithi Ya 04: Hakika Umbo La Kila Mmoja Wenu Linakusanywa Katika Tumbo La Mama Yake
الحديث الرابع
"إن أحدكم يجمع في بطن أمه"
عن
أبي عبْدِ الرَّحْمن عبدِ الله بنِ مسعودٍ رضي الله عنه قال: حدَّثَنا
رسولُ الله صلى الله عليه وسلم وهُوَ الصَّادقُ المَصْدوق: (( إنَّ
أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ في بَطْنِ أُمِّه أرْبعينَ يوْماً نُطْفَةً،
ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذلك، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذلك،
ثُمَّ يُرْسَلُ إليه المَلكُ فَيَنْفخُ فيه الرُّوحَ ويُؤمَرُ بأرْبَعِ
كلماتٍ: بِكَتْبِ رِزْقِهِ وأَجَلِهِ وعَمَلِهِ وشَقيٌّ أو سَعيدٌ،
فَوَاللهِ الَّذي لا إله غَيْرُهُ إنَّ أَحَدَكُمْ ليَعْمَلُ بعَمَلِ أهْلِ
الجَنَّةِ حتى ما يكُونَ بَيْنَهُ وبَيْنَها إلا ذِرَاعٌ، فَيَسْبِقُ
عَليْه الكِتابُ فَيَعْمَلُ بعَملِ أَهْلِ النَّارِ فَيَدْخُلُها. وإنَّ
أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهل النَّارِ حتى ما يَكُونَ بَيْنَهُ
وبَيْنَها إلا ذِرَاعٌ، فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الكتابُ، فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ
أهل الجنَّةِ فَيَدْخُلُها))
رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ
HADITHI YA 4
HAKIKA UMBO LA KILA MMOJA WENU LINAKUSANYWA KATIKA TUMBO LA MAMA YAKE.
Kutoka kwa Abu Abdur-Rahman Abdullaah Ibn Masu'ud رضي الله عنه ambaye alisema: Mtume صلى الله عليه وسلم naye ndie mkweli, anaesadikiwa alitueleza haya:
Hakika
umbo la kila mmoja wenu linakusanywa pamoja katika tumbo la mama
yake kwa muda wa siku arubaini, ikiwa katika hali ya mbegu, baadaye tone
la damu kwa muda kama huo, tena huwa ni kipande cha nyama kwa muda kama
huo, tena hupelekwa Malaika anaempulizia pumzi za uhai na
anaamrishwa mambo manne: kuandika rizki yake, maisha yake, amali
yake na akiwa atakuwa (mtu) mbaya au mwema. Kwa Allaah ambaye hakuna
Mungu isipokuwa Yeye, mmoja katika nyinyi hufanya vitendo vya watu
wa peponi mpaka baina yake na pepo ikawa dhiraa na kile kilichoandikwa
kikathibiti akafanya amali ya watu wa motoni akaingia motoni. Na
mmoja katika nyinyi hufanya amali ya watu wa motoni mpaka baina
yake na moto ikawa dhiraa, na hapo kile kilichoandikwa kikathibiti
akafanya amali ya watu wa peponi akaingia peponi.
Imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim.