Hadithi Ya 03: Nguzo Za Kiislamu Ni Tano


الحديث الثالث
"بني الإسلام على خمس"
 عن أبي عَبْدِ الرَّحْمنِ عَبْدِ اللهِ بنِ عُمَرَ بنِ الخَطابِ رَضيَ اللهُ عنهُما قال: سَمِعْتُ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم يقولُ: (( بُنَي الإسلامُ على خَمْسٍ : شهادَةِ أَنْ لا إلهَ إلا اللهُ وأَنَّ محمَّداً رسولُ اللهِ، وإقَامِ الصَّلاةِ، وإيتَاءِ الزَّكاةِ، وحَجِّ البَيْتِ، وصَوْمِ رَمَضَانَ )).

رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ



HADITHI YA 3
NGUZO ZA KIISLAMU NI TANO
Kutoka kwa Abu Abdur-Rahman Abdullah Ibn 'Umar Ibn  Al-Khattaab  رضي الله عنه   Ambaye alisema:   Nilimsikia Bwana Mtume صلى الله عليه وسلم  akisema: Uislamu umejengwa kwa nguzo tano:
Shahada kuwa hakuna Mola apasaye kuabudiwa isipokuwa Allaah na Muhammad ni Mjumbe wake, kuswali, kutoa Zaka, kuhiji           (Makka) na kufunga Ramadhan.
Imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim