Hadithi Ya 01: Kila Kitendo Kwa Nia Yake
الحديث الأول
" إنما الأعمال بالنيات "
عن
أَمِيرِ المُؤمِنِينَ أَبي حَفْصٍ عُمَرَ بنِ الخطَّابِ رَضِيَ اللهُ
عَنْهُ قَالَ : سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم
يَقُولُ: ((إِنَّما الأَعْمَالُ بالنِّيَّاتِ وإنَّما لكُلِّ
امْرِىءٍ ما نَوَى، فَمَنْ كانَتْ هِجْرَتُهُ إلى اللهِ ورَسُولِهِ
فَهِجْرَتُهُ إلى اللهِ ورَسُولِهِ، ومَنْ كانَتْ هِجْرَتُهُ لِدُنْيا
يُصِيبُها أو امْرأةٍ يَنْكِحُها فَهِجْرَتُهُ إلى ما هَاجَرَ إليه)).
رَوَاهُ
إِمَامَا الْمُحَدِّثِينَ أَبُو عَبْدِ اللهِ مُحَمَّدُ بنُ إِسْمَاعِيل
بن إِبْرَاهِيم بن الْمُغِيرَة بن بَرْدِزبَه الْبُخَارِيُّ
وَأَبُو الْحُسَيْنِ مُسْلِمٌ بنُ الْحَجَّاج بن مُسْلِم
الْقُشَيْرِيُّ النَّيْسَابُورِيُّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا فِي
"صَحِيحَيْهِمَا" اللذينِ هُمَا أَصَحُّ الْكُتُبِ الْمُصَنَّفَةِ.
HADITHI YA 1
KILA KITENDO KWA NIA YAKE
Kutoka kwa Amiri wa Waumuni, Abu Hafs 'Umar Ibn Al Khattaab رضى الله عنه ambaye alisema : Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu صلى الله
عليه وسلم akisema:
Vitendo
vinategemea (vinalipwa kwa) nia na kila mtu atapata kwa mujibu wa kile
alichokusudia. Kwa hivyo yule aliyehama kwa ajili ya Allaah
na Mtume wake, uhamaji wake ni kwa ajili ya Allaah na Mtume wake,
na yule ambae uhamaji wake ulikuwa ni kwa ajili ya manufaa ya
kidunia au kwa ajili ya kumuoa mwanamke (Fulani) uhamaji wake ulikuwa kwa kile kilichomuhamisha.
Imesimuliwa
na Maimam wawili mabingwa wa hadithi Abu Abdalla Muhammad Ibn
Ismail Ibn Ibrahim Ibn Mughiyra Ibn Bardizbah Al Bukhari na Abu Al
Husayn Muslim Ibn Al-Hajjaj Ibn Muslim Al Qushayri An-Naysaburi, katika
sahihi zao mbili ambavyo ni vitabu vya kutegemewa.