Al-A’raaf: 7

ألأَعْرَاف
Al-A’raaf: 7

(Imeteremka Makka)


Sura hii imeteremka Makka isipo kuwa Aya nane, nazo ni 163 mpaka 170. Na idadi za Aya zake ni 206.
Mwanzo wa Sura hii ni kuendeleza yaliyo kuja mwisho wa Sura ya Al-Ana'm, na baada ya hayo imeingia kueleza khulka ya kibinaadamu. Ikataja kisa cha Adam na Hawa, na walivyo toka kwenye Bustani kwa kutiwa wasiwasi na Shet'ani, na ikaeleza huo wasiwasi unaoendelea kwa watu katika mavazi na chakula. Kisha Aya za Sura hii tukufu, kama sura nyengine za Qur'ani zikaingia kutupia jicho kwenye mbingu na ardhi na viliomo ndani yao, na kuzingatia uumbaji wake wa ajabu.
Kadhaalika Sura hii imeeleza hadithi za Manabii kama Nuhu na Hud na kaumu yake kina A'ad. Kisha hadithi ya Saleh na kaumu yake, Thamud, walio sifika kwa nguvu zao na wakapewa utajiri; na hadithi ya Lut' na kaumu yake, na ikataja maovu waliyo kuwa wakiyafanya; na hadithi ya Shua'ib na watu wa Madyana. Na baada ya hadithi hizo za kweli Sura imeeleza mafunzo na mazingatio yaliyomo. Naye Subhanahu wa Ta'ala amefuatilizia hayo kwa kisa cha Musa na yaliyo tokea katika mambo ya Firauni.
Na Sura ikakhitimishia kwa kumathilisha nini hali ya mwenye kupewa hidaya khalafu akabanduka kwenye uwongofu akaingia kwenye upotovu kwa kumfwata Shet'ani, na Sura pia ikamalizia kueleza Wito wa kuendea Haki alio kuja nao Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.



بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


المص ﴿١﴾
1. Alif Laam Miym Swaad.



كِتَابٌ أُنزِلَ إِلَيْكَ فَلَا يَكُن فِي صَدْرِكَ حَرَجٌ مِّنْهُ لِتُنذِرَ بِهِ وَذِكْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ ﴿٢﴾
2. (Hii Qur-aan ni) Kitabu kimeteremshwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) basi isiwe katika kifua chako dhiki kwa ajili yake, (kwani umeteremshiwa) ili uwaonye kwacho na (kiwe ni) ukumbusho (mawaidha na zingatio) kwa Waumini.


اتَّبِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلَا تَتَّبِعُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ ۗ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ ﴿٣﴾
3. Fuateni yale mliyoteremshiwa kutoka kwa Rabb (Mola) wenu (Qur-aan na Sunnah) na wala msifuate badala Yake walinzi na wasaidizi. Ni machache mnayoyakumbuka.


وَكَم مِّن قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَاهَا فَجَاءَهَا بَأْسُنَا بَيَاتًا أَوْ هُمْ قَائِلُونَ ﴿٤﴾
4. Na miji mingapi Tumeiangamiza ikaifikia adhabu Yetu usiku au walipokuwa katika qayluwlah (usingizi wa mchana).


فَمَا كَانَ دَعْوَاهُمْ إِذْ جَاءَهُم بَأْسُنَا إِلَّا أَن قَالُوا إِنَّا كُنَّا ظَالِمِينَ ﴿٥﴾
5. Basi haikuwa kilio chao ilipowajia adhabu Yetu isipokuwa walisema:  “Hakika sisi tulikuwa madhalimu.”


فَلَنَسْأَلَنَّ الَّذِينَ أُرْسِلَ إِلَيْهِمْ وَلَنَسْأَلَنَّ الْمُرْسَلِينَ ﴿٦﴾
6. Basi bila ya shaka Tutawauliza wale waliopelekewa (Rasuli) na bila shaka Tutawauliza Rasuli (pia).


فَلَنَقُصَّنَّ عَلَيْهِم بِعِلْمٍ ۖ وَمَا كُنَّا غَائِبِينَ ﴿٧﴾
7. Kisha Tutawasimulia kwao kwa ujuzi (kila walichokitenda), na hatukuwa wenye kukosekana.


وَالْوَزْنُ يَوْمَئِذٍ الْحَقُّ ۚ فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٨﴾
8. Na mizani (ya ‘amali) Siku hiyo (ya Qiyaamah) itakuwa ni haki. Basi ambao mizani yao itakuwa nzito, hao ndio watakaofaulu.


وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُم بِمَا كَانُوا بِآيَاتِنَا يَظْلِمُونَ ﴿٩﴾
9. Na ambao mizani yao itakuwa khafifu, basi hao ni wale waliokhasirika nafsi zao kwa yale waliyokuwa wakizifanyia dhulma Aayaat Zetu.


وَلَقَدْ مَكَّنَّاكُمْ فِي الْأَرْضِ وَجَعَلْنَا لَكُمْ فِيهَا مَعَايِشَ ۗ قَلِيلًا مَّا تَشْكُرُونَ ﴿١٠﴾
10. Kwa yakini Tumekumakinisheni katika ardhi na Tukawaekea humo (mimea, madini, tijara n.k. kama njia za) maisha. Kidogo sana mnayoshukuru. 


وَلَقَدْ خَلَقْنَاكُمْ ثُمَّ صَوَّرْنَاكُمْ ثُمَّ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ لَمْ يَكُن مِّنَ السَّاجِدِينَ ﴿١١﴾
11. Na kwa yakini Tumekuumbeni kisha Tukakutieni sura; kisha Tukawaambia Malaika: “Msujudieni Aadam.” Wakasujudu (wote) isipokuwa Ibliys hakuwa miongoni mwa waliosujudu.


قَالَ مَا مَنَعَكَ أَلَّا تَسْجُدَ إِذْ أَمَرْتُكَ ۖ قَالَ أَنَا خَيْرٌ مِّنْهُ خَلَقْتَنِي مِن نَّارٍ وَخَلَقْتَهُ مِن طِينٍ ﴿١٢﴾
12. (Allaah) Akasema “Nini kilichokuzuia usisujudu Nilipokuamrisha?” (Ibliys) Akasema: “Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, na yeye Umemuumba kwa udongo.”


قَالَ فَاهْبِطْ مِنْهَا فَمَا يَكُونُ لَكَ أَن تَتَكَبَّرَ فِيهَا فَاخْرُجْ إِنَّكَ مِنَ الصَّاغِرِينَ ﴿١٣﴾
13. (Allaah) Akasema: “Basi shuka humo, kwani haikupasa kwako utakabari humo. Hivyo toka hakika wewe ni miongoni mwa walio duni (na dhalili).”

قَالَ أَنظِرْنِي إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ ﴿١٤﴾
14. (Ibliys) Akasema: “Nipe muhula hadi Siku watakapofufuliwa (viumbe).”


قَالَ إِنَّكَ مِنَ الْمُنظَرِينَ ﴿١٥﴾
15. (Allaah) Akasema: “Hakika wewe ni miongoni mwa waliopewa muhula.”


قَالَ فَبِمَا أَغْوَيْتَنِي لَأَقْعُدَنَّ لَهُمْ صِرَاطَكَ الْمُسْتَقِيمَ ﴿١٦﴾
16. (Ibliys) Akasema: “Basi kwa kuwa Umenihukumia kupotoka, nitawakalia (waja Wako) katika njia Yako iliyonyooka.”



ثُمَّ لَآتِيَنَّهُم مِّن بَيْنِ أَيْدِيهِمْ وَمِنْ خَلْفِهِمْ وَعَنْ أَيْمَانِهِمْ وَعَن شَمَائِلِهِمْ ۖ وَلَا تَجِدُ أَكْثَرَهُمْ شَاكِرِينَ ﴿١٧﴾
17. Kisha nitawaendea mbele yao na nyuma na kuliani kwao na kushotoni kwao, na wala Hutopata wengi wao wenye kushukuru.


قَالَ اخْرُجْ مِنْهَا مَذْءُومًا مَّدْحُورًا ۖ لَّمَن تَبِعَكَ مِنْهُمْ لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنكُمْ أَجْمَعِينَ ﴿١٨﴾
18. (Allaah) Akasema: “Toka humo ukiwa umeshutumiwa na umefukuzwa. Atakayekufuata miongoni mwao, bila shaka Nitajaza (Moto wa) Jahannam kwa nyinyi nyote.”


وَيَا آدَمُ اسْكُنْ أَنتَ وَزَوْجُكَ الْجَنَّةَ فَكُلَا مِنْ حَيْثُ شِئْتُمَا وَلَا تَقْرَبَا هَـٰذِهِ الشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿١٩﴾
19. (Allaah Akasema): “Na ee Aadam, ishi wewe na mkeo Jannah na mle humo popote mpendapo; na wala msikaribie huu mti, msijekuwa miongoni mwa madhalimu.”


فَوَسْوَسَ لَهُمَا الشَّيْطَانُ لِيُبْدِيَ لَهُمَا مَا وُورِيَ عَنْهُمَا مِن سَوْآتِهِمَا وَقَالَ مَا نَهَاكُمَا رَبُّكُمَا عَنْ هَـٰذِهِ الشَّجَرَةِ إِلَّا أَن تَكُونَا مَلَكَيْنِ أَوْ تَكُونَا مِنَ الْخَالِدِينَ ﴿٢٠﴾
20. Basi shaytwaan (naye ni Ibliys) akawatia wasiwasi ili awafichulie yaliyofichwa kwao ya sehemu zao za siri. Na akasema (kuwaambia Aadam na mkewe): “Rabb (Mola) wenu Hakukukatazeni (nyote wawili) huu mti isipokuwa msijekuwa Malaika au kuwa miongoni mwa wenye kudumu.”


وَقَاسَمَهُمَا إِنِّي لَكُمَا لَمِنَ النَّاصِحِينَ ﴿٢١﴾
21. Naye akawaapia (kwa kuwaambai): “Hakika mimi kwenu (nyote wawili) ni mwenye kukunasihini kidhati.”


فَدَلَّاهُمَا بِغُرُورٍ ۚ فَلَمَّا ذَاقَا الشَّجَرَةَ بَدَتْ لَهُمَا سَوْآتُهُمَا وَطَفِقَا يَخْصِفَانِ عَلَيْهِمَا مِن وَرَقِ الْجَنَّةِ ۖ وَنَادَاهُمَا رَبُّهُمَا أَلَمْ أَنْهَكُمَا عَن تِلْكُمَا الشَّجَرَةِ وَأَقُل لَّكُمَا إِنَّ الشَّيْطَانَ لَكُمَا عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿٢٢﴾
22. Basi akawachota (wote wawili) kwa ghururi. Basi (wote wawili) walipoonja mti ule (waliokatazwa) zikawafichukia (wote wawili) sehemu zao za siri; na wakaanza kujibandika majani ya Jannah. Na Rabb (Mola) wao Akawaita (wote wawili na kuwaambia): “Je, kwani Mimi Sikukukatazeni (nyote wawili) mti huo na kukuambieni kwamba shaytwaan ni adui bayana kwenu?”


قَالَا رَبَّنَا ظَلَمْنَا أَنفُسَنَا وَإِن لَّمْ تَغْفِرْ لَنَا وَتَرْحَمْنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٢٣﴾
23. (Wote wawili) Wakasema: “Rabb (Mola) wetu! Tumedhulumu nafsi zetu, na basi Usipotughufuria na Ukaturehemu; bila shaka tutakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”


قَالَ اهْبِطُوا بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖ وَلَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُسْتَقَرٌّ وَمَتَاعٌ إِلَىٰ حِينٍ ﴿٢٤﴾
24. (Allaah) Akasema: “Shukeni! Nyinyi kwa nyinyi ni maadui. Na kwenye ardhi ndio itakuwa mastakimu na starehe mpaka muda (maalumu tu).”


قَالَ فِيهَا تَحْيَوْنَ وَفِيهَا تَمُوتُونَ وَمِنْهَا تُخْرَجُونَ ﴿٢٥﴾
25. (Allaah) Akasema: “Humo mtaishi, na humo mtakufa na kutoka humo mtatolewa (mfufuliwe).”


يَا بَنِي آدَمَ قَدْ أَنزَلْنَا عَلَيْكُمْ لِبَاسًا يُوَارِي سَوْآتِكُمْ وَرِيشًا ۖ وَلِبَاسُ التَّقْوَىٰ ذَٰلِكَ خَيْرٌ ۚ ذَٰلِكَ مِنْ آيَاتِ اللَّـهِ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ ﴿٢٦﴾
26. “Enyi wana wa Aadam! Kwa yakini Tumekuteremshieni libasi (vazi) linaficha sehemu zenu za siri na (nguo) kama pambo. Na libasi la taqwa ndiyo bora zaidi. Hizo ni katika Aayaat (ishara, dalili) za Allaah wapate kukumbuka (na kuwaidhika).”


يَا بَنِي آدَمَ لَا يَفْتِنَنَّكُمُ الشَّيْطَانُ كَمَا أَخْرَجَ أَبَوَيْكُم مِّنَ الْجَنَّةِ يَنزِعُ عَنْهُمَا لِبَاسَهُمَا لِيُرِيَهُمَا سَوْآتِهِمَا ۗ إِنَّهُ يَرَاكُمْ هُوَ وَقَبِيلُهُ مِنْ حَيْثُ لَا تَرَوْنَهُمْ ۗ إِنَّا جَعَلْنَا الشَّيَاطِينَ أَوْلِيَاءَ لِلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٢٧﴾
27. “Enyi wana wa Aadam! Asikukufitinini shaytwaan (Ibliys) kama alivyowatoa wazazi wenu (wawili) katika Jannah; akiwavua nguo zao ili awafichulie sehemu zao za siri. Hakika yeye (Ibliys) anakuoneni, yeye na kabila lake (la mashaytwaan wa majini) na hali ya kuwa nyinyi hamuwaoni. Hakika Sisi Tumejaaliya mashaytwaan kuwa ni marafiki, wandani kwa wale wasioamini.”


وَإِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً قَالُوا وَجَدْنَا عَلَيْهَا آبَاءَنَا وَاللَّـهُ أَمَرَنَا بِهَا ۗ قُلْ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَأْمُرُ بِالْفَحْشَاءِ ۖ أَتَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٢٨﴾
28. Na wanapofanya uchafu (wa aina yoyote ule) husema: “Tumewakuta nayo baba zetu, na Allaah (pia) Ametuamrisha kwayo.” Sema: “Hakika Allaah Haamrishi machafu. Je mnasema juu ya Allaah msiyoyajua?”


قُلْ أَمَرَ رَبِّي بِالْقِسْطِ ۖ وَأَقِيمُوا وُجُوهَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَادْعُوهُ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ ۚ كَمَا بَدَأَكُمْ تَعُودُونَ ﴿٢٩﴾
29. Sema: “Rabb (Mola) wangu Ameniamrisha uadilifu; na muelekeze nyuso zenu (kumwabudu Yeye Pekee na kuelekea Al-Ka’bah) kwenye kila mahali pa kusujudu na mumuombe (Yeye Pekee) mukhliswiyn (wenye kumtakasia) Dini. Kama Alivyokuanzisheni (kukuumbeni) mtarudi (tena Kwake).


فَرِيقًا هَدَىٰ وَفَرِيقًا حَقَّ عَلَيْهِمُ الضَّلَالَةُ ۗ إِنَّهُمُ اتَّخَذُوا الشَّيَاطِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ اللَّـهِ وَيَحْسَبُونَ أَنَّهُم مُّهْتَدُونَ ﴿٣٠﴾
30. Kundi Ameliongoa, na kundi (jingine) imethibiti juu yao upotofu. Hakika wao wamefanya mashaytwaan kuwa marafiki wandani na walinzi badala ya Allaah na wanadhani kwamba wao wameongoka.


يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ ﴿٣١﴾
31. Enyi wana wa Aadam! Chukueni mapambo yenu katika kila Masjid; na kuleni na kunyweni; na wala msifanye israfu. Hakika Yeye (Allaah) Hapendi wanaofanya israfu.


قُلْ مَنْ حَرَّمَ زِينَةَ اللَّـهِ الَّتِي أَخْرَجَ لِعِبَادِهِ وَالطَّيِّبَاتِ مِنَ الرِّزْقِ ۚ قُلْ هِيَ لِلَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا خَالِصَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٣٢﴾
32. Sema: “Nani aliyeharamisha mapambo ya Allaah ambayo Amewatolea waja Wake na, vizuri katika riziki?” Sema: “Hivyo ni kwa ajili ya wale walioamini katika uhai wa dunia (na vitakuwa) makhsusi (kwa Waumini pekee) Siku ya Qiyaamah. Hivyo ndivyo Tunavyofasili Aayaat kwa watu wanaojua.”


قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَالْإِثْمَ وَالْبَغْيَ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَأَن تُشْرِكُوا بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٣٣﴾
33. Sema: “Hakika Rabb (Mola) wangu Ameharamisha machafu (ya aina yoyote) yaliyodhihirika na yaliyofichika na dhambi (za kila aina), na ukandamizaji bila ya haki, na (Ameharamisha) kumshirikisha Allaah kwa (chochote kile) ambayo Hakukiteremshia mamlaka na kusema juu ya Allaah yale ambayo hamyajui.” 


وَلِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٌ ۖ فَإِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ لَا يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً ۖ وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ ﴿٣٤﴾
34. Na kwa kila ummah una muda wao (maalumu uliokadiriwa). Basi utakapofika muda wao huo, hawatakawia (hata) saa na wala hawatatangulia (kabla haujafika).


يَا بَنِي آدَمَ إِمَّا يَأْتِيَنَّكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ يَقُصُّونَ عَلَيْكُمْ آيَاتِي ۙ فَمَنِ اتَّقَىٰ وَأَصْلَحَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٣٥﴾
35. Enyi wana wa Aadam! Watakapokufikieni Rasuli miongoni mwenu wanakusimulieni Aayaat Zangu; basi atakayekuwa na taqwa na akatengenea, haitakuwa khofu juu yao na wala hawatahuzunika.


وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَاسْتَكْبَرُوا عَنْهَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٣٦﴾
36. Na wale waliokadhibisha Aayaat (ishara, dalili) Zetu na wakatakabari nazo, hao ni watu wa Motoni, wao humo ni wenye kudumu.


فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ ۚ أُولَـٰئِكَ يَنَالُهُمْ نَصِيبُهُم مِّنَ الْكِتَابِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا جَاءَتْهُمْ رُسُلُنَا يَتَوَفَّوْنَهُمْ قَالُوا أَيْنَ مَا كُنتُمْ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ قَالُوا ضَلُّوا عَنَّا وَشَهِدُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ أَنَّهُمْ كَانُوا كَافِرِينَ ﴿٣٧﴾
37. Basi nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyemtungia Allaah uongo au aliyekadhibisha Aayaat (na ishara) Zake. Hao itawafikia sehemu yao ya Kitabu (waliyokidhiwa); mpaka watakapowajia Wajumbe Wetu kuwafisha watawaambia: “Wako wapi wale mliokuwa mkiwaomba pasi na Allaah?” Watasema: “Wametupotea.” Na watajishuhudia nafsi zao wenyewe kwamba walikuwa makafiri.


قَالَ ادْخُلُوا فِي أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِكُم مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ فِي النَّارِ ۖ كُلَّمَا دَخَلَتْ أُمَّةٌ لَّعَنَتْ أُخْتَهَا ۖ حَتَّىٰ إِذَا ادَّارَكُوا فِيهَا جَمِيعًا قَالَتْ أُخْرَاهُمْ لِأُولَاهُمْ رَبَّنَا هَـٰؤُلَاءِ أَضَلُّونَا فَآتِهِمْ عَذَابًا ضِعْفًا مِّنَ النَّارِ ۖ قَالَ لِكُلٍّ ضِعْفٌ وَلَـٰكِن لَّا تَعْلَمُونَ ﴿٣٨﴾
38. (Allaah) Atasema (Siku ya Qiyaamah): “Ingieni Motoni pamoja na ummah zilokwishapita kabla yenu miongoni mwa majini na wanadamu.  Kila utakapoingia ummah utalaani nduguye. Mpaka watakapokusanyika (mrundo) wote pamoja; watasema wa mwisho wao (waliofuata wakuu) kwa wa mwanzo wao (wakuu wao): “Rabb (Mola) wetu! Hawa wametupoteza; basi Wape adhabu maradufu ya Moto.” (Allaah) Atasema: “Kila mmoja atapata (adhabu ya) maradufu lakini hamjui.”


وَقَالَتْ أُولَاهُمْ لِأُخْرَاهُمْ فَمَا كَانَ لَكُمْ عَلَيْنَا مِن فَضْلٍ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْسِبُونَ ﴿٣٩﴾
39. Na wa kwanza wao watawaambia wa mwisho wao: “Basi hamkuwa na fadhila juu yetu.  Hivyo onjeni adhabu kwa yale mliyokuwa mkiyachuma.”


إِنَّ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَاسْتَكْبَرُوا عَنْهَا لَا تُفَتَّحُ لَهُمْ أَبْوَابُ السَّمَاءِ وَلَا يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ حَتَّىٰ يَلِجَ الْجَمَلُ فِي سَمِّ الْخِيَاطِ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُجْرِمِينَ ﴿٤٠﴾
40. Hakika wale waliokadhibisha Aayaat (na ishara) Zetu na wakatakabari nazo, hawatofunguliwa milango ya mbingu na wala hawatoingia Jannah mpaka ngamia aingie katika tundu ya sindano (na hili haliwezekani kamwe!). Na hivyo ndivyo Tunavyowalipa wahalifu.


لَهُم مِّن جَهَنَّمَ مِهَادٌ وَمِن فَوْقِهِمْ غَوَاشٍ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الظَّالِمِينَ ﴿٤١﴾
41. Watapata vitanda vya (Moto wa) Jahannam na juu yao vifuniko (vya nguo za Moto) na hivyo ndivyo Tunavyowalipa madhalimu.


وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٤٢﴾
42. Na wale walioamini na wakatenda mema, Hatuikalifishi nafsi ila kadiri ya uwezo wake. Hao ni watu wa Jannah, wao humo ni wenye kudumu.


وَنَزَعْنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنْ غِلٍّ تَجْرِي مِن تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ ۖ وَقَالُوا الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي هَدَانَا لِهَـٰذَا وَمَا كُنَّا لِنَهْتَدِيَ لَوْلَا أَنْ هَدَانَا اللَّـهُ ۖ لَقَدْ جَاءَتْ رُسُلُ رَبِّنَا بِالْحَقِّ ۖ وَنُودُوا أَن تِلْكُمُ الْجَنَّةُ أُورِثْتُمُوهَا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٤٣﴾
43. Na Tutaondoa yale ya mafundo (kinyongo, chuki n.k.) yaliyomo vifuani mwao, zitapita chini yao mito. Na watasema: “AlhamduliLLaahi (Himidi zote Anastahiki Allaah) Ambaye Ametuongoza kwa haya; na hatukuwa wenye kuongoka kama Allaah Asingetuongoza. Kwa yakini wamekuja Rasuli wa Rabb (Mola) wetu kwa haki.” Na wataitwa (kuambiwa): “Hii ndiyo Jannah mliyorithishwa kwa yale mliyokuwa mnayatenda.”


وَنَادَىٰ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ أَصْحَابَ النَّارِ أَن قَدْ وَجَدْنَا مَا وَعَدَنَا رَبُّنَا حَقًّا فَهَلْ وَجَدتُّم مَّا وَعَدَ رَبُّكُمْ حَقًّا ۖ قَالُوا نَعَمْ ۚ فَأَذَّنَ مُؤَذِّنٌ بَيْنَهُمْ أَن لَّعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الظَّالِمِينَ ﴿٤٤﴾
44. Na watu wa Jannah watawaita watu wa Motoni (kuwaambia) kwamba: “Kwa yakini tumekwishayapata Aliyotuahidi Rabb (Mola) wetu kuwa ni haki. Je, basi nyinyi (vipi) mmekwishapata Aliyokuahidini Rabb wenu kuwa ni haki?”  Watasema: (watu wa Motoni) “Naam!” Basi mtangazaji atatangaza baina yao kwamba: “Laana ya Allaah iwe juu ya madhalimu”. 


الَّذِينَ يَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجًا وَهُم بِالْآخِرَةِ كَافِرُونَ ﴿٤٥﴾
45. Ambao wanazuia (watu) njia ya Allaah na wanaitafutia kosa; na wao kwa Aakhirah ni wenye kuikanusha.


وَبَيْنَهُمَا حِجَابٌ ۚ وَعَلَى الْأَعْرَافِ رِجَالٌ يَعْرِفُونَ كُلًّا بِسِيمَاهُمْ ۚ وَنَادَوْا أَصْحَابَ الْجَنَّةِ أَن سَلَامٌ عَلَيْكُمْ ۚ لَمْ يَدْخُلُوهَا وَهُمْ يَطْمَعُونَ ﴿٤٦﴾
46. Na baina yao ni kizuizi (kama ukuta). Na kwenye Al-A’raaf (mnyanyuko baina ya Jannah na Moto) patakuweko watu (hawako Jannah wala Motoni) wanaowatambua wote (wa Jannah na wa Motoni) kwa alama zao. Na watawaita watu wa Jannah (kwa kusema): “Salaamun ‘Alaykum” (amani iwe juu yenu). Hawakuingia humo lakini huku wao wanatumaini (kuingia Jannah).  


وَإِذَا صُرِفَتْ أَبْصَارُهُمْ تِلْقَاءَ أَصْحَابِ النَّارِ قَالُوا رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٤٧﴾
47. Na yatakapogeuzwa macho yao (watu wa Al-A’raaf) kuelekea watu wa Motoni watasema: “Rabb (Mola) wetu! Usitujaalie kuwa pamoja na watu madhalimu.”


وَنَادَىٰ أَصْحَابُ الْأَعْرَافِ رِجَالًا يَعْرِفُونَهُم بِسِيمَاهُمْ قَالُوا مَا أَغْنَىٰ عَنكُمْ جَمْعُكُمْ وَمَا كُنتُمْ تَسْتَكْبِرُونَ ﴿٤٨﴾
48. Na watu wa Al-A’raaf watawaita watu (wa Motoni) wanaowatambua kwa alama zao, watasema: “Hakukufaeni kujumuika kwenu (duniani na wingi wenu) na vile mlivyokuwa mkitakabari.”



أَهَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ أَقْسَمْتُمْ لَا يَنَالُهُمُ اللَّـهُ بِرَحْمَةٍ ۚ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ لَا خَوْفٌ عَلَيْكُمْ وَلَا أَنتُمْ تَحْزَنُونَ ﴿٤٩﴾
49. (Allaah Atasema): “Je, hawa si wale ambao (nyinyi watu wa Motoni) mliapa kwamba Allaah hatowafikishia kwa Rahmah yoyote ile?” (Leo wanaambiwa)  “Ingieni Jannah! Hakuna khofu juu yenu na wala nyinyi hamtohuzunika.” 


وَنَادَىٰ أَصْحَابُ النَّارِ أَصْحَابَ الْجَنَّةِ أَنْ أَفِيضُوا عَلَيْنَا مِنَ الْمَاءِ أَوْ مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّـهُ ۚ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ حَرَّمَهُمَا عَلَى الْكَافِرِينَ ﴿٥٠﴾
50. Na watu wa Motoni watawaita watu wa Jannah (kuwaambia): “Tumiminieni maji au (chochote) katika Alivyokuruzukuni Allaah.”  Watasema: “Hakika Allaah Ameviharamisha kwa makafiri.”


الَّذِينَ اتَّخَذُوا دِينَهُمْ لَهْوًا وَلَعِبًا وَغَرَّتْهُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا ۚ فَالْيَوْمَ نَنسَاهُمْ كَمَا نَسُوا لِقَاءَ يَوْمِهِمْ هَـٰذَا وَمَا كَانُوا بِآيَاتِنَا يَجْحَدُونَ ﴿٥١﴾
51. Wale ambao wameifanya dini yao pumbao na mchezo, na ukawaghururi uhai wa dunia. Basi leo Tunawasahau kama walivyosahau kukutana na Siku yao hii; na kwa yale waliyokuwa wakizikanusha kwa jeuri Aayaat (na ishara, dalili) Zetu.


وَلَقَدْ جِئْنَاهُم بِكِتَابٍ فَصَّلْنَاهُ عَلَىٰ عِلْمٍ هُدًى وَرَحْمَةً لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٥٢﴾
52. Kwa yakini Tumewaletea Kitabu Tulichokifasili kwa ujuzi (ambacho) ni Mwongozo na Rahmah kwa watu wanaoamini.


هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا تَأْوِيلَهُ ۚ يَوْمَ يَأْتِي تَأْوِيلُهُ يَقُولُ الَّذِينَ نَسُوهُ مِن قَبْلُ قَدْ جَاءَتْ رُسُلُ رَبِّنَا بِالْحَقِّ فَهَل لَّنَا مِن شُفَعَاءَ فَيَشْفَعُوا لَنَا أَوْ نُرَدُّ فَنَعْمَلَ غَيْرَ الَّذِي كُنَّا نَعْمَلُ ۚ قَدْ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿٥٣﴾
53. Je, wanangojea (nini) isipokuwa matokeo yake? Siku itakapofika matokeo yake watasema wale walioisahau kabla: “Kwa yakini wamekuja Rasuli wa Rabb (Mola) wetu kwa haki (tunakubali sasa). Je, tuna waombezi wowote watuombee, au turudishwe (duniani) ili tufanye ghairi ya yale tuliyokuwa tunafanya.” Kwa yakini wamekhasiri nafsi zao na imewapotea yale waliyokuwa wakiyatunga.


إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ يَطْلُبُهُ حَثِيثًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ وَالنُّجُومَ مُسَخَّرَاتٍ بِأَمْرِهِ ۗ أَلَا لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ ۗ تَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٥٤﴾
54. Hakika Rabb (Mola) wenu ni Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha Istawaa juu ya ‘Arshi; (Yuko juu kabisa kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah). Anafunika usiku kwa mchana, unaufuatia upesi upesi na (Ameumba) jua na mwezi na nyota (vyote) vimetiishwa kwa amri Yake. Tanabahi! Ni Vyake Pekee uumbaji na amri. Amebarikika Allaah Rabb wa walimwengu.


ادْعُوا رَبَّكُمْ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ ﴿٥٥﴾
55. Muombeni Rabb (Mola) wenu kwa unyenyekevu na kwa siri, hakika Yeye Hapendi wenye kutaadi.


وَلَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ بَعْدَ إِصْلَاحِهَا وَادْعُوهُ خَوْفًا وَطَمَعًا ۚ إِنَّ رَحْمَتَ اللَّـهِ قَرِيبٌ مِّنَ الْمُحْسِنِينَ ﴿٥٦﴾
56. Na wala msifanye ufisadi katika ardhi baada ya kutengenea kwake; na muombeni kwa khofu na matumaini. Hakika Rahmah ya Allaah iko karibu na wafanyao ihsaan.


وَهُوَ الَّذِي يُرْسِلُ الرِّيَاحَ بُشْرًا بَيْنَ يَدَيْ رَحْمَتِهِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا أَقَلَّتْ سَحَابًا ثِقَالًا سُقْنَاهُ لِبَلَدٍ مَّيِّتٍ فَأَنزَلْنَا بِهِ الْمَاءَ فَأَخْرَجْنَا بِهِ مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ ۚ كَذَٰلِكَ نُخْرِجُ الْمَوْتَىٰ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ ﴿٥٧﴾
57. Naye Ndiye Anayetuma upepo mzuri kuwa bishara kabla ya Rahmah Yake; hata unapobeba mawingu mazito Tunayasukuma kwenye nchi iliyokufa. Kisha Tunateremsha kwayo maji na kisha Tunatoa kwayo kila (aina ya) mazao. Hivyo ndivyo Tunavyotoa wafu, ili mpate kukumbuka (na kuwaidhika).


وَالْبَلَدُ الطَّيِّبُ يَخْرُجُ نَبَاتُهُ بِإِذْنِ رَبِّهِ ۖ وَالَّذِي خَبُثَ لَا يَخْرُجُ إِلَّا نَكِدًا ۚ كَذَٰلِكَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَشْكُرُونَ ﴿٥٨﴾
58. Na nchi nzuri hutoa mimea yake kwa idhini ya Rabb (Mola) wake. Na (nchi) ile ambayo ni mbaya haitoi ila haba. Hivyo ndivyo Tunavyosarifu Aayaat kwa watu wanaoshukuru.


لَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ فَقَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿٥٩﴾
59. Kwa yakini Tulimpeleka Nuwh kwa kaumu yake akasema: “Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah (kwani nyinyi) hamna ilaah (muabudiwa wa haki) ghairi Yake. Hakika mimi nakukhofieni adhabu Siku kubwa mno.


قَالَ الْمَلَأُ مِن قَوْمِهِ إِنَّا لَنَرَاكَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٦٠﴾
60. Wakasema wakuu katika kaumu yake: “Hakika sisi tunakuona umo katika upotofu bayana.”


قَالَ يَا قَوْمِ لَيْسَ بِي ضَلَالَةٌ وَلَـٰكِنِّي رَسُولٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٦١﴾
61. (Nuwh) Akasema: “Enyi kaumu yangu! Mimi sina upotofu lakini mimi ni Rasuli kutoka kwa Rabb (Mola) wa walimwengu.”


أُبَلِّغُكُمْ رِسَالَاتِ رَبِّي وَأَنصَحُ لَكُمْ وَأَعْلَمُ مِنَ اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٦٢﴾
62. “Nakubalighishieni ujumbe wa Rabb (Mola) wangu na nakunasihini, na ninajua kutoka kwa Allaah msiyoyajua.”


أَوَعَجِبْتُمْ أَن جَاءَكُمْ ذِكْرٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَلَىٰ رَجُلٍ مِّنكُمْ لِيُنذِرَكُمْ وَلِتَتَّقُوا وَلَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٦٣﴾
63. “Je, mmestaajabu kwamba imekujieni ukumbusho (na mawaidha) kutoka kwa Rabb (Mola) wenu kupitia kwa mtu miongoni mwenu ili akuonyeni na ili muwe na taqwa na mpate kurehemewa?”


فَكَذَّبُوهُ فَأَنجَيْنَاهُ وَالَّذِينَ مَعَهُ فِي الْفُلْكِ وَأَغْرَقْنَا الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا عَمِينَ ﴿٦٤﴾
64. Basi walimkadhibisha na Tukamuokoa pamoja na wale waliokuwa naye katika jahazi; na Tukawagharikisha wale waliokadhibisha Aayaat (ishara, dalili) Zetu. Hakika wao walikuwa watu vipofu.



وَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمْ هُودًا ۗ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۚ أَفَلَا تَتَّقُونَ ﴿٦٥﴾
65. Na kwa ‘Aad (Tuliwapelekea) kaka yao Huwd.  Akasema: “Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah (kwani nyinyi) hamna ilaah (muabudiwa wa haki) ghairi Yake. Je hamwogopi (Allaah)?” 


قَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَوْمِهِ إِنَّا لَنَرَاكَ فِي سَفَاهَةٍ وَإِنَّا لَنَظُنُّكَ مِنَ الْكَاذِبِينَ ﴿٦٦﴾
66. Wakasema wakuu waliokufuru katika kaumu yake: “Hakika sisi tunakuona umo katika usafihi, na hakiki sisi tunadhani (wewe ni) miongoni mwa waongo.”


قَالَ يَا قَوْمِ لَيْسَ بِي سَفَاهَةٌ وَلَـٰكِنِّي رَسُولٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٦٧﴾
67. (Huwd) Akasema: “Enyi kaumu yangu! Mimi siko katika usafihi lakini mimi ni Rasuli kutoka kwa Rabb (Mola) wa walimwengu.”


أُبَلِّغُكُمْ رِسَالَاتِ رَبِّي وَأَنَا لَكُمْ نَاصِحٌ أَمِينٌ ﴿٦٨﴾
68. Nakubalighishieni ujumbe wa Rabb (Mola) wangu, nami kwenu ni mtoaji nasiha mwaminifu.


أَوَعَجِبْتُمْ أَن جَاءَكُمْ ذِكْرٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَلَىٰ رَجُلٍ مِّنكُمْ لِيُنذِرَكُمْ ۚ وَاذْكُرُوا إِذْ جَعَلَكُمْ خُلَفَاءَ مِن بَعْدِ قَوْمِ نُوحٍ وَزَادَكُمْ فِي الْخَلْقِ بَسْطَةً ۖ فَاذْكُرُوا آلَاءَ اللَّـهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٦٩﴾
69. “Je, mmestaajabu kwamba imekujieni ukumbusho (na mawaidha) kutoka kwa Rabb (Mola) wenu kupitia kwa mtu miongoni mwenu ili akuonyeni. Na kumbukeni Alipokufanyeni makhalifa (mkashika mahala pao) baada ya kaumu ya Nuwh, na Akakuzidisheni kwa ukunjufu katika umbo (kimo kwa urefu, nguvu, akili). Basi kumbukeni neema nyingi za Allaah mpate kufaulu.”


قَالُوا أَجِئْتَنَا لِنَعْبُدَ اللَّـهَ وَحْدَهُ وَنَذَرَ مَا كَانَ يَعْبُدُ آبَاؤُنَا ۖ فَأْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٧٠﴾
70. Wakasema: “Je, umetujia ili tumwambudu Allaah Pekee na tuache yale waliyokuwa wakiabudu baba zetu? Basi tuletee hayo unayotuahidi ukiwa ni miongoni mwa wakweli.”



قَالَ قَدْ وَقَعَ عَلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ رِجْسٌ وَغَضَبٌ ۖ أَتُجَادِلُونَنِي فِي أَسْمَاءٍ سَمَّيْتُمُوهَا أَنتُمْ وَآبَاؤُكُم مَّا نَزَّلَ اللَّـهُ بِهَا مِن سُلْطَانٍ ۚ فَانتَظِرُوا إِنِّي مَعَكُم مِّنَ الْمُنتَظِرِينَ ﴿٧١﴾
71. (Huwd) Akasema: “Kwa yakini imekwishakuangukieni rijsun (laana, adhabu) na ghadhabu kutoka kwa Rabb (Mola) wenu. Je, mnanijadili katika majina mliyoyaita (masanamu) nyinyi na baba zenu (ambayo) Allaah Hakuyateremshia kwayo mamlaka?  Basi ngojeeni, hakika mimi (pia) niko pamoja nanyi katika wanaongojea.”


فَأَنجَيْنَاهُ وَالَّذِينَ مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَقَطَعْنَا دَابِرَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۖ وَمَا كَانُوا مُؤْمِنِينَ ﴿٧٢﴾
72. Basi Tukamuokoa (Huwd) na wale waliokuwa pamoja naye kwa Rahmah kutoka Kwetu na Tukakata mizizi ya wale waliokadhibisha Aayaat (ishara, dalili) Zetu na hawakuwa wenye kuamini.


وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا ۗ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ قَدْ جَاءَتْكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ ۖ هَـٰذِهِ نَاقَةُ اللَّـهِ لَكُمْ آيَةً ۖ فَذَرُوهَا تَأْكُلْ فِي أَرْضِ اللَّـهِ ۖ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٣﴾
73. Na kwa Thamuwd (Tuliwapelekea) kaka yao Swaalih. Akasema: “Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah (kwani nyinyi) hamna ilaah (muabudiwa wa haki) ghairi Yake. Kwa yakini imekujieni hoja bayana kutoka kwa Rabb (Mola) wenu. Huyu ngamia jike wa Allaah kwenu ni Aayah! (ishara, dalili) Basi muacheni ale katika ardhi ya Allaah, na wala msimguse kwa uovu (wowote ule), isije ikakuchukueni adhabu iumizayo.”


وَاذْكُرُوا إِذْ جَعَلَكُمْ خُلَفَاءَ مِن بَعْدِ عَادٍ وَبَوَّأَكُمْ فِي الْأَرْضِ تَتَّخِذُونَ مِن سُهُولِهَا قُصُورًا وَتَنْحِتُونَ الْجِبَالَ بُيُوتًا ۖ فَاذْكُرُوا آلَاءَ اللَّـهِ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ ﴿٧٤﴾
74. “Na kumbukeni Alipokujaalieni makhalifa baada ya ‘Aad, Akakufanyieni makaazi katika ardhi mnachukua katika nyanda zake tambarare maqasri (majumba ya fakhari) na mnachonga majumba kutokana na majabali (yake). Basi kumbukeni neema nyingi za Allaah na wala msifanye vitendo vya hujuma katika ardhi (mkawa) mafisadi.”


قَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا مِن قَوْمِهِ لِلَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا لِمَنْ آمَنَ مِنْهُمْ أَتَعْلَمُونَ أَنَّ صَالِحًا مُّرْسَلٌ مِّن رَّبِّهِ ۚ قَالُوا إِنَّا بِمَا أُرْسِلَ بِهِ مُؤْمِنُونَ ﴿٧٥﴾
75. Wakasema wakuu waliotakabari katika kaumu yake kuwaambia wale waliokandamizwa ambao walioamini miongoni mwao: “Je, mnajua kwamba Swaalih ametumwa kutoka kwa Rabb (Mola) wake?”   Wakasema: “Hakika sisi kwa yale aliyotumwa nayo ni wenye kuyaamini.” 


قَالَ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا إِنَّا بِالَّذِي آمَنتُم بِهِ كَافِرُونَ ﴿٧٦﴾
76. Wakasema wale waliotakabari: “Hakika sisi kwa yale mliyoyaamini ni wenye kuyakanusha.”


فَعَقَرُوا النَّاقَةَ وَعَتَوْا عَنْ أَمْرِ رَبِّهِمْ وَقَالُوا يَا صَالِحُ ائْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِن كُنتَ مِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٧٧﴾
77. Basi wakamkata ukano wa mvungu wa goti (wakamchinja) yule ngamia na wakaasi amri ya Rabb (Mola) wao; na wakasema: “Ee Swaalih, tuletee hayo unayotuahidi ukiwa ni miongoni mwa Rasuli.”


فَأَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دَارِهِمْ جَاثِمِينَ ﴿٧٨﴾
78. Basi ikawachukuwa tetemeko la ardhi wakawa majumbani mwao wenye kuanguka kifudifudi (wamekufa).


فَتَوَلَّىٰ عَنْهُمْ وَقَالَ يَا قَوْمِ لَقَدْ أَبْلَغْتُكُمْ رِسَالَةَ رَبِّي وَنَصَحْتُ لَكُمْ وَلَـٰكِن لَّا تُحِبُّونَ النَّاصِحِينَ ﴿٧٩﴾
79. Basi (Swaalih) akajitenga nao na akasema: “Enyi kaumu yangu! Kwa yakini nilishakubalighishieni ujumbe wa Rabb (Mola) wangu na nilikunasihini, lakini nyinyi hamuwapendi wenye kunasihi.”


وَلُوطًا إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ أَتَأْتُونَ الْفَاحِشَةَ مَا سَبَقَكُم بِهَا مِنْ أَحَدٍ مِّنَ الْعَالَمِينَ ﴿٨٠﴾
80.  Na (Tulimtuma) Luwtw, alipowaambia kaumu yake: “Je, mnafanya uchafu (wa liwati) ambao hajakutangulieni nao yeyote katika walimwengu?”


إِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ الرِّجَالَ شَهْوَةً مِّن دُونِ النِّسَاءِ ۚ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ مُّسْرِفُونَ ﴿٨١﴾
81. “Hakika nyinyi mnawaingilia wanaume kwa matamanio badala ya wanawake? Bali nyinyi ni watu wapindukiaji mipaka.”


وَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِ إِلَّا أَن قَالُوا أَخْرِجُوهُم مِّن قَرْيَتِكُمْ ۖ إِنَّهُمْ أُنَاسٌ يَتَطَهَّرُونَ ﴿٨٢﴾
82. Na halikuwa jibu la kaumu yake isipokuwa walisema: “Wafukuzeni kutoka mji wenu, kwani hakika wao ni watu wanaojitakasa.”


فَأَنجَيْنَاهُ وَأَهْلَهُ إِلَّا امْرَأَتَهُ كَانَتْ مِنَ الْغَابِرِينَ ﴿٨٣﴾
83. Basi Tukamuokoa (Luwtw) na ahli yake isipokuwa mkewe alikuwa miongoni mwa waliokuwa nyuma (na wafanya maasi).



وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِم مَّطَرًا ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُجْرِمِينَ ﴿٨٤﴾
84. Na Tukawateremshia mvua kubwa (ya mawe kuwa ni adhabu). Basi tazama vipi ilikuwa hatima ya wahalifu.


وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا ۗ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ قَدْ جَاءَتْكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ ۖ فَأَوْفُوا الْكَيْلَ وَالْمِيزَانَ وَلَا تَبْخَسُوا النَّاسَ أَشْيَاءَهُمْ وَلَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ بَعْدَ إِصْلَاحِهَا ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٨٥﴾
85. Na kwa (watu wa mji wa) Madyan (Tuliwapelekea) kaka yao Shu’ayb.  Akasema: “Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah (kwani) hamna ilaah (muabudiwa wa haki) ghairi Yake. Kwa yakini imekujieni hoja bayana kutoka kwa Rabb (Mola) wenu. Basi timizeni kipimo na mizani wala msipunje watu vitu vyao wala msifanye ufisadi ardhini baada ya kutengenea kwake. Hivyo ni bora kwenu ikiwa mmeamini.”


وَلَا تَقْعُدُوا بِكُلِّ صِرَاطٍ تُوعِدُونَ وَتَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ مَنْ آمَنَ بِهِ وَتَبْغُونَهَا عِوَجًا ۚ وَاذْكُرُوا إِذْ كُنتُمْ قَلِيلًا فَكَثَّرَكُمْ ۖ وَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُفْسِدِينَ ﴿٨٦﴾
86. “Na wala msikalie kila njia mkifanya vitisho kwa watu na kuwazuia njia ya Allaah (wale) wenye kuiamini na mkaitafutia upogo. Na kumbukeni mlipokuwa wachache Akakukithirisheni. Na tazameni vipi ilikuwa hatima ya mafisadi.”


وَإِن كَانَ طَائِفَةٌ مِّنكُمْ آمَنُوا بِالَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ وَطَائِفَةٌ لَّمْ يُؤْمِنُوا فَاصْبِرُوا حَتَّىٰ يَحْكُمَ اللَّـهُ بَيْنَنَا ۚ وَهُوَ خَيْرُ الْحَاكِمِينَ ﴿٨٧﴾
87. “Na kama liko kundi miongoni mwenu limeamini kwa yale niliyotumwa nayo na kundi halikuamini; basi subirini mpaka Allaah Ahukumu baina yetu. Naye ni Mbora wa wenye kuhukumu”.



قَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا مِن قَوْمِهِ لَنُخْرِجَنَّكَ يَا شُعَيْبُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَكَ مِن قَرْيَتِنَا أَوْ لَتَعُودُنَّ فِي مِلَّتِنَا ۚ قَالَ أَوَلَوْ كُنَّا كَارِهِينَ﴿٨٨﴾
88. Wakasema wakuu waliotakabari katika kaumu yake: “Tutakutoa ewe Shua’yb na wale walioamini pamoja nawe kutoka mji wetu, au mrejee katika millah yetu.” (Shu’ayb) Akasema: “Japokuwa tumekirihika?”


قَدِ افْتَرَيْنَا عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا إِنْ عُدْنَا فِي مِلَّتِكُم بَعْدَ إِذْ نَجَّانَا اللَّـهُ مِنْهَا ۚ وَمَا يَكُونُ لَنَا أَن نَّعُودَ فِيهَا إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ رَبُّنَا ۚ وَسِعَ رَبُّنَا كُلَّ شَيْءٍ عِلْمًا ۚ عَلَى اللَّـهِ تَوَكَّلْنَا ۚ رَبَّنَا افْتَحْ بَيْنَنَا وَبَيْنَ قَوْمِنَا بِالْحَقِّ وَأَنتَ خَيْرُ الْفَاتِحِينَ﴿٨٩﴾
89. “Kwa yakini (itakuwa) tumemtungia Allaah uongo ikiwa tutarudi katika millah yenu baada ya Allaah kutuokoa nayo. Na haiwi kwetu kurejea humo isipokuwa Akitaka Allaah Rabb (Mola) wetu. Rabb wetu Amekienea kila kitu kwa ujuzi. Kwa Allaah tunatawakali. Rabb wetu! Hukumu baina yetu na baina ya kaumu yetu kwa haki, Nawe ni Mbora wa wenye kuhukumu”. 


وَقَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَوْمِهِ لَئِنِ اتَّبَعْتُمْ شُعَيْبًا إِنَّكُمْ إِذًا لَّخَاسِرُونَ﴿٩٠﴾
90. Na wakasema wakuu waliokufuru katika kaumu yake: “Mkimfuata Shu’ayb hakika hapo mtakuwa bila shaka wenye kukhasirika.”


فَأَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دَارِهِمْ جَاثِمِينَ﴿٩١﴾
91. Basi ikawachukua ar-rajfah (tetemeko la ardhi) wakawa majumbani mwao wenye kuanguka kifudifudi (wamekufa).


الَّذِينَ كَذَّبُوا شُعَيْبًا كَأَن لَّمْ يَغْنَوْا فِيهَا ۚ الَّذِينَ كَذَّبُوا شُعَيْبًا كَانُوا هُمُ الْخَاسِرِينَ﴿٩٢﴾
92. Wale waliomkadhibisha Shu’ayb wakawa kama kwamba hawakuishi (wakanufaika) humo. Waliomkadhibisha Shu’ayb wakawa ndio wenye kukhasirika. 


فَتَوَلَّىٰ عَنْهُمْ وَقَالَ يَا قَوْمِ لَقَدْ أَبْلَغْتُكُمْ رِسَالَاتِ رَبِّي وَنَصَحْتُ لَكُمْ ۖ فَكَيْفَ آسَىٰ عَلَىٰ قَوْمٍ كَافِرِينَ﴿٩٣﴾
93. Basi (Shu’ayb) akajitenga nao akasema: “Enyi kaumu yangu!  Kwa yakini nimeshakubalighishieni ujumbe wa Rabb (Mola) wangu na nimekunasihini, basi vipi niwe na majonzi juu ya watu makafiri.”


وَمَا أَرْسَلْنَا فِي قَرْيَةٍ مِّن نَّبِيٍّ إِلَّا أَخَذْنَا أَهْلَهَا بِالْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ لَعَلَّهُمْ يَضَّرَّعُونَ﴿٩٤﴾
94. Na Hatukutuma katika mji wowote Nabiy yeyote (akakanushwa) isipokuwa Tunawashika (kuwatesa) watu wake, kwa mashaka (ufukara, dhiki ya maisha) na madhara (magonjwa, misiba n.k) ili wapate kunyenyekea (na kutubia kwa Allaah).


ثُمَّ بَدَّلْنَا مَكَانَ السَّيِّئَةِ الْحَسَنَةَ حَتَّىٰ عَفَوا وَّقَالُوا قَدْ مَسَّ آبَاءَنَا الضَّرَّاءُ وَالسَّرَّاءُ فَأَخَذْنَاهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ﴿٩٥﴾
95. Kisha Tukabadilisha mahali pa hali mbaya kwa nzuri hata wakazidi, (na wakaneemeka na kubarikiwa); na wakasema: “Kwa yakini iliwagusa baba zetu madhara na raha.” Basi Tukawachukuwa ghafla nao huku hawahisi. 


وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَىٰ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِم بَرَكَاتٍ مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ وَلَـٰكِن كَذَّبُوا فَأَخَذْنَاهُم بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿٩٦﴾
96. Na lau kama watu wa miji wangeliamimi na wakawa na taqwa, bila ya shaka Tungeliwafungulia baraka kutoka mbinguni na ardhini, lakini walikadhibisha, basi Tukawachukuwa kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.


أَفَأَمِنَ أَهْلُ الْقُرَىٰ أَن يَأْتِيَهُم بَأْسُنَا بَيَاتًا وَهُمْ نَائِمُونَ﴿٩٧﴾
97. Je, watu wa miji wameaminisha ya kuwa haitowafikia adhabu Yetu wakati wa usiku hali wao wamelala?


أَوَأَمِنَ أَهْلُ الْقُرَىٰ أَن يَأْتِيَهُم بَأْسُنَا ضُحًى وَهُمْ يَلْعَبُونَ﴿٩٨﴾
98. Au watu wa miji wameaminisha ya kuwa haitowafikia adhabu Yetu wakati wa dhwuhaa (asubuhi kabla ya mchana) hali wao wanacheza?


أَفَأَمِنُوا مَكْرَ اللَّـهِ ۚ فَلَا يَأْمَنُ مَكْرَ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْخَاسِرُونَ﴿٩٩﴾
99. Je, wameaminisha mipango ya Allaah? Basi hawaaminishi mipango ya Allaah isipokuwa watu wenye kukhasirika.


أَوَلَمْ يَهْدِ لِلَّذِينَ يَرِثُونَ الْأَرْضَ مِن بَعْدِ أَهْلِهَا أَن لَّوْ نَشَاءُ أَصَبْنَاهُم بِذُنُوبِهِمْ ۚ وَنَطْبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ﴿١٠٠﴾
100. Je, haikubainika kwa wale wanaorithi ardhi baada ya watu wake (wa zamani walioangamizwa) kwamba lau Tungelitaka Tungeliwasibu kwa dhambi zao. Na Tutapiga chapa juu ya nyoyo zao basi hawatosikia?


تِلْكَ الْقُرَىٰ نَقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنبَائِهَا ۚ وَلَقَدْ جَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَمَا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا بِمَا كَذَّبُوا مِن قَبْلُ ۚ كَذَٰلِكَ يَطْبَعُ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِ الْكَافِرِينَ﴿١٠١﴾
101. Hiyo ni miji Tunakusimulia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) baadhi ya habari zake. Na kwa yakini waliwajia Rasuli wao kwa hoja bayana, lakini hawakuwa wenye kuamini kwa yale waliyoyakadhibisha kabla. Hivyo ndivyo Allaah Anavopiga chapa juu ya nyoyo za makafiri.


وَمَا وَجَدْنَا لِأَكْثَرِهِم مِّنْ عَهْدٍ ۖ وَإِن وَجَدْنَا أَكْثَرَهُمْ لَفَاسِقِينَ﴿١٠٢﴾
102. Na Hatukuwakuta kwa wengi wao wenye (kutekeleza) ahadi yoyote. Bali kwa yakini Tumewakuta wengi wao ni mafasiki.


ثُمَّ بَعَثْنَا مِن بَعْدِهِم مُّوسَىٰ بِآيَاتِنَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَظَلَمُوا بِهَا ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُفْسِدِينَ﴿١٠٣﴾
103. Kisha Tukamtuma baada yao Muwsaa na Aayaat (miujiza, hoja) Zetu kwa Fir’awn na wakuu wake wakazifanyia dhulma. Basi tazama vipi ilikuwa hatima ya mafisadi. 


وَقَالَ مُوسَىٰ يَا فِرْعَوْنُ إِنِّي رَسُولٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ﴿١٠٤﴾
104. Na Muwsaa akasema: “Ee Fir’awn! Hakika mimi ni Rasuli kutoka kwa Rabb (Mola) wa walimwengu.”


حَقِيقٌ عَلَىٰ أَن لَّا أَقُولَ عَلَى اللَّـهِ إِلَّا الْحَقَّ ۚ قَدْ جِئْتُكُم بِبَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ فَأَرْسِلْ مَعِيَ بَنِي إِسْرَائِيلَ﴿١٠٥﴾
105. “Napaswa nisiseme juu ya Allaah isipokuwa ya haki. Kwa yakini nimekujieni kwa hoja bayana kutoka kwa Rabb (Mola) wenu; basi watume pamoja nami wana wa Israaiyl.” 


قَالَ إِن كُنتَ جِئْتَ بِآيَةٍ فَأْتِ بِهَا إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ﴿١٠٦﴾
106. (Fir’awn) Akasema: “Ikiwa umekuja na Aayah (ishara, hoja) basi ilete, ukiwa ni miongoni mwa wakweli.”


فَأَلْقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ ثُعْبَانٌ مُّبِينٌ﴿١٠٧﴾
107. Basi (Muwsaa) akaitupa fimbo yake, tahamaki (ikawa) joka bayana.


وَنَزَعَ يَدَهُ فَإِذَا هِيَ بَيْضَاءُ لِلنَّاظِرِينَ﴿١٠٨﴾
108. Na akatoa mkono wake; tahamaki (ukawa) mweupe (unang’ara) kwa watazamao.


قَالَ الْمَلَأُ مِن قَوْمِ فِرْعَوْنَ إِنَّ هَـٰذَا لَسَاحِرٌ عَلِيمٌ﴿١٠٩﴾
109. Wakasema wakuu katika kaumu ya Fir’awn: “Bila shaka huyu ni mchawi mjuzi.”


يُرِيدُ أَن يُخْرِجَكُم مِّنْ أَرْضِكُمْ ۖ فَمَاذَا تَأْمُرُونَ﴿١١٠﴾
110. “Anataka kukutoeni kutoka ardhini mwenu; basi mnaamrisha nini?”


قَالُوا أَرْجِهْ وَأَخَاهُ وَأَرْسِلْ فِي الْمَدَائِنِ حَاشِرِينَ﴿١١١﴾
111. Wakasema: (kumwambia Fir’awn): “Muahirishe kidogo na ndugu yake (Haaruwn) na tuma katika miji wenye kukusanya (wachawi).”


يَأْتُوكَ بِكُلِّ سَاحِرٍ عَلِيمٍ﴿١١٢﴾
112. “Wakujie kila mchawi mjuzi.”


وَجَاءَ السَّحَرَةُ فِرْعَوْنَ قَالُوا إِنَّ لَنَا لَأَجْرًا إِن كُنَّا نَحْنُ الْغَالِبِينَ﴿١١٣﴾
113. Wakaja wachawi wa Fir’awn; wakasema: “Je, tutapata ujira ikiwa sisi tutashinda?”


قَالَ نَعَمْ وَإِنَّكُمْ لَمِنَ الْمُقَرَّبِينَ﴿١١٤﴾
114. (Fir’awn) Akasema: “Naam! Bila shaka nanyi mtakuwa miongoni mwa waliokurubishwa (kwangu).”


قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِمَّا أَن تُلْقِيَ وَإِمَّا أَن نَّكُونَ نَحْنُ الْمُلْقِينَ﴿١١٥﴾
115. (Wachawi) Wakasema: “Ee Muwsaa, ima utupe (fimbo yako) au ima tuwe sisi wa (kwanza) kutupa.” 


قَالَ أَلْقُوا ۖ فَلَمَّا أَلْقَوْا سَحَرُوا أَعْيُنَ النَّاسِ وَاسْتَرْهَبُوهُمْ وَجَاءُوا بِسِحْرٍ عَظِيمٍ﴿١١٦﴾
116. (Muwsaa) Akasema: “Tupeni!” Basi walipotupa, waliyasihiri macho ya watu na wakawatia woga, na wakaja na sihiri kuu.


وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ أَنْ أَلْقِ عَصَاكَ ۖ فَإِذَا هِيَ تَلْقَفُ مَا يَأْفِكُونَ﴿١١٧﴾
117. Na Tukamtia ilhamu Muwsaa ya kwamba: “Tupa fimbo yako!” Tahamaki ikameza vyote walivovibuni.


فَوَقَعَ الْحَقُّ وَبَطَلَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١١٨﴾
118. Ukweli ukathibiti na yakabatilika yale waliyokuwa wakiyatenda.


فَغُلِبُوا هُنَالِكَ وَانقَلَبُوا صَاغِرِينَ﴿١١٩﴾
119. Wakashindwa hapo; na wakageuka kuwa wenye kudhalilika.


وَأُلْقِيَ السَّحَرَةُ سَاجِدِينَ﴿١٢٠﴾
120.  Na wachawi wakajiangusha wakisujdu.


قَالُوا آمَنَّا بِرَبِّ الْعَالَمِينَ﴿١٢١﴾
121. Wakasema: “Tumemwamini Rabb (Mola) wa walimwengu.”


رَبِّ مُوسَىٰ وَهَارُونَ﴿١٢٢﴾
122. “Rabb (Mola) wa Muwsaa na Haaruwn.”


قَالَ فِرْعَوْنُ آمَنتُم بِهِ قَبْلَ أَنْ آذَنَ لَكُمْ ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَمَكْرٌ مَّكَرْتُمُوهُ فِي الْمَدِينَةِ لِتُخْرِجُوا مِنْهَا أَهْلَهَا ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ﴿١٢٣﴾
123. Fir’awn akasema: “Je, mumemwamini kabla sijakupeni rukhsa? Hakika hii bila shaka ni njama mliyoipanga (nyinyi na Muwsaa) katika mji ili muwatoe watu wake humo. Mtakuja kujua (nini nitakufanyeni).”


لَأُقَطِّعَنَّ أَيْدِيَكُمْ وَأَرْجُلَكُم مِّنْ خِلَافٍ ثُمَّ لَأُصَلِّبَنَّكُمْ أَجْمَعِينَ﴿١٢٤﴾
124. “Bila shaka niitakata mikono yenu na miguu yenu kinyume (kulia kwa kushoto) kisha nitakusulubuni nyote.”


قَالُوا إِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا مُنقَلِبُونَ﴿١٢٥﴾
125. (Wachawi) Wakasema: “Hakika sisi kwa Rabb (Mola) wetu tutarudi.”


وَمَا تَنقِمُ مِنَّا إِلَّا أَنْ آمَنَّا بِآيَاتِ رَبِّنَا لَمَّا جَاءَتْنَا ۚ رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَتَوَفَّنَا مُسْلِمِينَ﴿١٢٦﴾
126. “Na huchukizwi nasi isipokuwa tu kwa kuwa tumeamini Aayaat (dalili, hoja) za Rabb (Mola) wetu zilipotujia. Ee Rabb wetu! Tumiminie subira na Tufishe (hali) tukiwa Waislamu (tunaojisilimisha Kwako).”


وَقَالَ الْمَلَأُ مِن قَوْمِ فِرْعَوْنَ أَتَذَرُ مُوسَىٰ وَقَوْمَهُ لِيُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَيَذَرَكَ وَآلِهَتَكَ ۚ قَالَ سَنُقَتِّلُ أَبْنَاءَهُمْ وَنَسْتَحْيِي نِسَاءَهُمْ وَإِنَّا فَوْقَهُمْ قَاهِرُونَ﴿١٢٧﴾
127. Na wakasema wakuu katika kaumu ya Fir’awn: “Je, unamwacha Muwsaa na kaumu yake wafisidi katika ardhi; na akuache (wewe) na miungu yako?”  (Fir’wan) Akasema: “Tutawaua watoto wao (wachanga) wa kiume na tutaacha hai wanawake wao; na hakika sisi ni wenye kushinda nguvu juu yao.”


قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ اسْتَعِينُوا بِاللَّـهِ وَاصْبِرُوا ۖ إِنَّ الْأَرْضَ لِلَّـهِ يُورِثُهَا مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۖ وَالْعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ﴿١٢٨﴾
128. Muwsaa akasema (kuwaambia) kaumu yake: “Ombeni msaada kwa Allaah na subirini. Hakika ardhi ni ya Allaah; Humrithisha Amtakaye katika wa waja Wake. Na mwisho (mzuri) ni kwa wenye taqwa.”


قَالُوا أُوذِينَا مِن قَبْلِ أَن تَأْتِيَنَا وَمِن بَعْدِ مَا جِئْتَنَا ۚ قَالَ عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يُهْلِكَ عَدُوَّكُمْ وَيَسْتَخْلِفَكُمْ فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرَ كَيْفَ تَعْمَلُونَ﴿١٢٩﴾
129. (Watu ya Muwsaa) Wakasema: “Tumeudhiwa kabla ya kutujia na baada ya kutujia.” (Muwsaa) akasema: “Huenda Rabb (Mola) wenu Akamuangamiza adui yenu na Akufanyeni watawala katika ardhi, Atazame mtakavyotenda.” 


وَلَقَدْ أَخَذْنَا آلَ فِرْعَوْنَ بِالسِّنِينَ وَنَقْصٍ مِّنَ الثَّمَرَاتِ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ﴿١٣٠﴾
130. Na kwa yakini Tuliwachukua (kwa kuwaadhibu) watu wa Fir’awn kwa miaka (mingi ya ukame) na upungufu wa mazao ili wapate kukumbuka (na wawaidhike). 


فَإِذَا جَاءَتْهُمُ الْحَسَنَةُ قَالُوا لَنَا هَـٰذِهِ ۖ وَإِن تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌ يَطَّيَّرُوا بِمُوسَىٰ وَمَن مَّعَهُ ۗ أَلَا إِنَّمَا طَائِرُهُمْ عِندَ اللَّـهِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿١٣١﴾
131. Basi ilipowajia zuri husema: “Hili letu.” Na likiwasibu ovu hunasibisha twiyarah (itikadi ya mkosi) kwa Muwsaa na walio pamoja naye. Tanabahi!  Hakika twiyarah (mkosi) wao uko kwa Allaah (kwa ajili ya ubaya wao), lakini wengi wao hawajui.


وَقَالُوا مَهْمَا تَأْتِنَا بِهِ مِنْ آيَةٍ لِّتَسْحَرَنَا بِهَا فَمَا نَحْنُ لَكَ بِمُؤْمِنِينَ﴿١٣٢﴾
132. Na wakasema (kumwambia Muwsaa): “Chochote utachotuletea kwacho katika Aayah (dalili, hoja) ili utusihiri nacho; basi sisi hatutokuamini.”


فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمُ الطُّوفَانَ وَالْجَرَادَ وَالْقُمَّلَ وَالضَّفَادِعَ وَالدَّمَ آيَاتٍ مُّفَصَّلَاتٍ فَاسْتَكْبَرُوا وَكَانُوا قَوْمًا مُّجْرِمِينَ﴿١٣٣﴾
133. Basi Tuliwapelekea tufani na nzige na chawa na vyura na damu Aayaat (ishara, hoja) zilizofasiliwa (kuwa wao ni waongo na madhalimu), lakini walitakabari wakawa watu mahalifu.


وَلَمَّا وَقَعَ عَلَيْهِمُ الرِّجْزُ قَالُوا يَا مُوسَى ادْعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِندَكَ ۖ لَئِن كَشَفْتَ عَنَّا الرِّجْزَ لَنُؤْمِنَنَّ لَكَ وَلَنُرْسِلَنَّ مَعَكَ بَنِي إِسْرَائِيلَ﴿١٣٤﴾
134. Na ilipowaangukia adhabu ya kufadhaika walisema: “Ee Muwsaa! Tuombee kwa Rabb (Mola) wako kwa yale Aliyokuahidi. Ukituondolea adhabu, bila shaka tutakuamini na bila shaka tutawapeleka pamoja nawe wana Israaiyl (mnakotaka). 


فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُمُ الرِّجْزَ إِلَىٰ أَجَلٍ هُم بَالِغُوهُ إِذَا هُمْ يَنكُثُونَ﴿١٣٥﴾
135.  Tulipowaondolea adhabu mpaka muda maalumu wao waufikie; tahamaki wao wanavunja ahadi.


فَانتَقَمْنَا مِنْهُمْ فَأَغْرَقْنَاهُمْ فِي الْيَمِّ بِأَنَّهُمْ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَكَانُوا عَنْهَا غَافِلِينَ﴿١٣٦﴾
136. Basi Tukawalipiza, Tukawagharikisha baharini kwa kuwa wao walikadhibisha Aayaat (ishara, hoja) Zetu na walikuwa ni wenye kughafilika nazo.


وَأَوْرَثْنَا الْقَوْمَ الَّذِينَ كَانُوا يُسْتَضْعَفُونَ مَشَارِقَ الْأَرْضِ وَمَغَارِبَهَا الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا ۖ وَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ الْحُسْنَىٰ عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ بِمَا صَبَرُوا ۖ وَدَمَّرْنَا مَا كَانَ يَصْنَعُ فِرْعَوْنُ وَقَوْمُهُ وَمَا كَانُوا يَعْرِشُونَ﴿١٣٧﴾
137. Na Tukawarithisha watu waliokuwa wakikandamizwa Mashariki ya ardhi na Magharibi yake ambayo Tumeibariki. Na likatimia neno zuri la Rabb (Mola) wako kwa wana wa Israaiyl kwa kule kusubiri kwao. Na Tukayadamirisha yale waliyokuwa wakitenda Fir’awn na kaumu yake na yale waliyokuwa wakiyajenga.


وَجَاوَزْنَا بِبَنِي إِسْرَائِيلَ الْبَحْرَ فَأَتَوْا عَلَىٰ قَوْمٍ يَعْكُفُونَ عَلَىٰ أَصْنَامٍ لَّهُمْ ۚ قَالُوا يَا مُوسَى اجْعَل لَّنَا إِلَـٰهًا كَمَا لَهُمْ آلِهَةٌ ۚ قَالَ إِنَّكُمْ قَوْمٌ تَجْهَلُونَ﴿١٣٨﴾
138. Na Tukawavusha wana wa Israaiyl bahari wakawafikia watu waliokuwa wanasabilia kwa utiifu masanamu yao. (Wana wa Israaiyl) Wakasema: “Ee Muwsaa! Tufanyie nasi mungu kama walivokuwa (hawa) wana miungu.  (Muwsaa) Akasema: “Hakika nyinyi ni watu mfanyao ujahili.”


إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ مُتَبَّرٌ مَّا هُمْ فِيهِ وَبَاطِلٌ مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١٣٩﴾
139. “Hakika hawa (wanaoabudu sanamu) yatateketezwa waliyo nayo, na ni yenye kubatilika yale waliyokuwa wakiyatenda.”


قَالَ أَغَيْرَ اللَّـهِ أَبْغِيكُمْ إِلَـٰهًا وَهُوَ فَضَّلَكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ﴿١٤٠﴾
140. (Muwsaa) Akasema: “Je, nikutafutieni mungu ghairi ya Allaah, na hali Yeye Amekufadhilisheni juu ya walimwengu?


وَإِذْ أَنجَيْنَاكُم مِّنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَسُومُونَكُمْ سُوءَ الْعَذَابِ ۖ يُقَتِّلُونَ أَبْنَاءَكُمْ وَيَسْتَحْيُونَ نِسَاءَكُمْ ۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَاءٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَظِيمٌ﴿١٤١﴾
141. Na (kumbukeni enyi wana wa Israaiyl), Tulipokuokoeni kutoka kwa watu wa Fir’awn walipokusibuni adhabu mbaya wakiwaua watoto wenu (wachanga wa kiume), na wakiacha hai wanawake wenu, na katika hayo kwenu ulikuwa ni mtihani mkuu kutoka kwa Rabb (Mola) wenu.


وَوَاعَدْنَا مُوسَىٰ ثَلَاثِينَ لَيْلَةً وَأَتْمَمْنَاهَا بِعَشْرٍ فَتَمَّ مِيقَاتُ رَبِّهِ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً ۚ وَقَالَ مُوسَىٰ لِأَخِيهِ هَارُونَ اخْلُفْنِي فِي قَوْمِي وَأَصْلِحْ وَلَا تَتَّبِعْ سَبِيلَ الْمُفْسِدِينَ﴿١٤٢﴾
142. Na Tukamuahidi Muwsaa misiku thelathini na Tukazitimiza kwa kumi; na ikatimia miyqaat (pahala pa miadi) ya Rabb (Mola) wake misiku arubaini. Muwsaa akasema (kumwambia) kaka yake Haaruwn: “Shika mahali pangu katika (kuwasimamia) watu wangu na tengeneza, na wala usifuate njia ya mafisadi.”


وَلَمَّا جَاءَ مُوسَىٰ لِمِيقَاتِنَا وَكَلَّمَهُ رَبُّهُ قَالَ رَبِّ أَرِنِي أَنظُرْ إِلَيْكَ ۚ قَالَ لَن تَرَانِي وَلَـٰكِنِ انظُرْ إِلَى الْجَبَلِ فَإِنِ اسْتَقَرَّ مَكَانَهُ فَسَوْفَ تَرَانِي ۚ فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُ لِلْجَبَلِ جَعَلَهُ دَكًّا وَخَرَّ مُوسَىٰ صَعِقًا ۚ فَلَمَّا أَفَاقَ قَالَ سُبْحَانَكَ تُبْتُ إِلَيْكَ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُؤْمِنِينَ﴿١٤٣﴾
143. Na alipokuja Muwsaa katika miyqaat (pahala pa miadi) Yetu, na Rabb (Mola) wake Akamsemesha, (Muwsaa) alisema: “Rabb wangu! Nionyeshe ili nikutazame.” (Allaah) Akasema: “Hutoniona! Lakini tazama jabali. Likitulia mahali pake, basi utaniona.” Basi Rabb wako Alipojidhihirisha katika jabali, Akalifanya livurugike kuwa vumbi; na Muwsaa akaanguka hali ya kuzimia. Alipozindukana akasema: “Subhaanak! (Utakasifu ni Wako!) Nimetubu Kwako, nami ni wa kwanza wa wanaoamini”


قَالَ يَا مُوسَىٰ إِنِّي اصْطَفَيْتُكَ عَلَى النَّاسِ بِرِسَالَاتِي وَبِكَلَامِي فَخُذْ مَا آتَيْتُكَ وَكُن مِّنَ الشَّاكِرِينَ﴿١٤٤﴾
144. (Allaah) Akasema: “Ee Muwsaa hakika Mimi Nimekuteua juu ya watu kwa ujumbe Wangu na maneno Yangu. Basi pokea Niliyokupa na kuwa miongoni mwa wanaoshukuru.


وَكَتَبْنَا لَهُ فِي الْأَلْوَاحِ مِن كُلِّ شَيْءٍ مَّوْعِظَةً وَتَفْصِيلًا لِّكُلِّ شَيْءٍ فَخُذْهَا بِقُوَّةٍ وَأْمُرْ قَوْمَكَ يَأْخُذُوا بِأَحْسَنِهَا ۚ سَأُرِيكُمْ دَارَ الْفَاسِقِينَ﴿١٤٥﴾
145. Na Tukamwandikia kwenye mbao kila kitu; mawaidha (ya kila namna) na tafsili ya kila kitu. (Tukamwambia): “Basi yashike kwa (azimio la) nguvuna uwaamrishe watu wako wayashike mazuri yake. Nitakuonyesheni miji (iliyoangamizwa) ya mafasiki.” 


سَأَصْرِفُ عَنْ آيَاتِيَ الَّذِينَ يَتَكَبَّرُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَإِن يَرَوْا كُلَّ آيَةٍ لَّا يُؤْمِنُوا بِهَا وَإِن يَرَوْا سَبِيلَ الرُّشْدِ لَا يَتَّخِذُوهُ سَبِيلًا وَإِن يَرَوْا سَبِيلَ الْغَيِّ يَتَّخِذُوهُ سَبِيلًا ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَكَانُوا عَنْهَا غَافِلِينَ﴿١٤٦﴾
146. “Nitawaepusha (wasifahamu) Aayaat (na hoja, dalili) Zangu wale waliotakabari katika ardhi bila ya haki. Na wanapoona kila Aayah hawaiamini. Na wanapoona njia ya uongofu hawaishiki kuwa ndio njia. Na wanapoona njia ya upotofu wanaishika kuwa ndio njia. Hivyo ni kwa kuwa wao walikadhibisha Aayaat Zetu na walikuwa wenye kughafilika nazo.”


وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَلِقَاءِ الْآخِرَةِ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ ۚ هَلْ يُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١٤٧﴾
147. Na wale waliokadhibisha Aayaat (na hoja, dalili) Zetu na makutano ya Aakhirah, zimebatilika ‘amali zao. Je, kwani watalipwa isipokuwa yale waliyokuwa wakiyatenda?


وَاتَّخَذَ قَوْمُ مُوسَىٰ مِن بَعْدِهِ مِنْ حُلِيِّهِمْ عِجْلًا جَسَدًا لَّهُ خُوَارٌ ۚ أَلَمْ يَرَوْا أَنَّهُ لَا يُكَلِّمُهُمْ وَلَا يَهْدِيهِمْ سَبِيلًا ۘ اتَّخَذُوهُ وَكَانُوا ظَالِمِينَ﴿١٤٨﴾
148. Na watu wa Muwsaa walijichukulia baada yake (alipokwenda kupokea Tawraat) katika mapambo yao (ya dhahabu wakayeyusha na kujitengenezea) ndama - kiwiliwili kilichokuwa na sauti kama ya ng’ombe (wakamwabudu). Je, hawakuona kwamba yeye (huyo ndama) hawasemeshi na wala hawaongozi njia? Walimchukuwa (kumfanya muabudiwa) na wakawa wenye kudhulumu (nafsi zao).


وَلَمَّا سُقِطَ فِي أَيْدِيهِمْ وَرَأَوْا أَنَّهُمْ قَدْ ضَلُّوا قَالُوا لَئِن لَّمْ يَرْحَمْنَا رَبُّنَا وَيَغْفِرْ لَنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ﴿١٤٩﴾
149. Na walipojuta na wakaona kwamba kwa yakini wamepotoka; walisema: “Asipoturehemu Rabb (Mola) wetu na Akatughufuria, bila shaka tutakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”


وَلَمَّا رَجَعَ مُوسَىٰ إِلَىٰ قَوْمِهِ غَضْبَانَ أَسِفًا قَالَ بِئْسَمَا خَلَفْتُمُونِي مِن بَعْدِي ۖ أَعَجِلْتُمْ أَمْرَ رَبِّكُمْ ۖ وَأَلْقَى الْأَلْوَاحَ وَأَخَذَ بِرَأْسِ أَخِيهِ يَجُرُّهُ إِلَيْهِ ۚ قَالَ ابْنَ أُمَّ إِنَّ الْقَوْمَ اسْتَضْعَفُونِي وَكَادُوا يَقْتُلُونَنِي فَلَا تُشْمِتْ بِيَ الْأَعْدَاءَ وَلَا تَجْعَلْنِي مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ﴿١٥٠﴾
150. “Na Muwsaa aliporejea kwa kaumu yake hali ya kuwa ameghadhibika na kusikitika, alisema: “Ubaya ulioje mmeniwakilisha baada yangu. Je, mmeharakiza (hamkuwa na subira juu ya) amri ya Rabb (Mola) wenu?” (Muwsaa) Akatupa zile mbao na akakamata kichwa cha kaka yake (Haaruwn) akimvuta kwake. (Haaruwn) Akasema (kumwambia Muwsaa): “Ee mwana wa mama yangu! Hakika watu (hawa) wamenikandamiza na walikaribia kuniua, basi usinifanye kifurahisho cha maadui, na wala usiniweke pamoja na watu madhalimu.”


قَالَ رَبِّ اغْفِرْ لِي وَلِأَخِي وَأَدْخِلْنَا فِي رَحْمَتِكَ ۖ وَأَنتَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ﴿١٥١﴾
151. (Muwsaa) Akasema: “Rabb (Mola) wangu! Nighufurie na ndugu yangu, na Utuingize katika Rahmah Yako. Nawe ni Mbora zaidi wa kurehemu kuliko wengine wote wenye kurehemu”.


إِنَّ الَّذِينَ اتَّخَذُوا الْعِجْلَ سَيَنَالُهُمْ غَضَبٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَذِلَّةٌ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُفْتَرِينَ﴿١٥٢﴾
152. Hakika wale waliomchukuwa ndama (na kumfanya muabudiwa) itawafika ghadhabu kutoka kwa Rabb (Mola) wao na udhalilifu katika uhai wa dunia. Na hivyo ndivyo Tunavowalipa watungaji (ubatilifu).


وَالَّذِينَ عَمِلُوا السَّيِّئَاتِ ثُمَّ تَابُوا مِن بَعْدِهَا وَآمَنُوا إِنَّ رَبَّكَ مِن بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١٥٣﴾
153. Na wale waliotenda maovu kisha wakatubu baada yake na wakaamini; hakika Rabb (Mola) wako baada ya hayo bila shaka ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).


وَلَمَّا سَكَتَ عَن مُّوسَى الْغَضَبُ أَخَذَ الْأَلْوَاحَ ۖ وَفِي نُسْخَتِهَا هُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلَّذِينَ هُمْ لِرَبِّهِمْ يَرْهَبُونَ﴿١٥٤﴾
154. Na ghadhabu zilipomtulia Muwsaa, alizichukuwa zile mbao. Na katika maandiko yake (mna) mwongozo na Rahmah kwa ambao wao wanamkhofu Rabb (Mola) wao.


وَاخْتَارَ مُوسَىٰ قَوْمَهُ سَبْعِينَ رَجُلًا لِّمِيقَاتِنَا ۖ فَلَمَّا أَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ قَالَ رَبِّ لَوْ شِئْتَ أَهْلَكْتَهُم مِّن قَبْلُ وَإِيَّايَ ۖ أَتُهْلِكُنَا بِمَا فَعَلَ السُّفَهَاءُ مِنَّا ۖ إِنْ هِيَ إِلَّا فِتْنَتُكَ تُضِلُّ بِهَا مَن تَشَاءُ وَتَهْدِي مَن تَشَاءُ ۖ أَنتَ وَلِيُّنَا فَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا ۖ وَأَنتَ خَيْرُ الْغَافِرِينَ﴿١٥٥﴾
155. Na Muwsaa akachagua wanaume sabini (katika) kaumu yake kwa ajili ya miyqaat (pahala pa miadi) Yetu. Kisha ilipowachukuwa tetemeko la ardhi; Muwsaa alisema: “Rabb (Mola) wangu! Ungelitaka Ungeliwaangamiza wao na mimi kabla. Je, Unatuangamiza kwa yale waliyoyafanya masafihi miongoni mwetu?  Haya si chochote isipokuwa ni majaribio Yako. Unampotoa kwayo Umtakaye, na Unamuongoa Umtakaye. Wewe ni Waliyy (Mlinzi, Msaidizi) wetu, basi Tughufurie na Turehemu; Nawe ni Mbora wa wenye kughufuria.”


وَاكْتُبْ لَنَا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ إِنَّا هُدْنَا إِلَيْكَ ۚ قَالَ عَذَابِي أُصِيبُ بِهِ مَنْ أَشَاءُ ۖ وَرَحْمَتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ ۚ فَسَأَكْتُبُهَا لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَالَّذِينَ هُم بِآيَاتِنَا يُؤْمِنُونَ﴿١٥٦﴾
156. “Na Tuandikie katika dunia hii hasanah (mazuri) na katika Aakhirah (pia Tuandikie hasanah). Hakika sisi tumerudi kutubu Kwako.” (Allaah) Akasema: “Adhabu Yangu Nitamsibu nayo Nimtakaye. Na Rahmah Yangu imeenea kila kitu. Basi Nitawahukumia (khaswa) wale wenye taqwa na wanaotoa Zakaah na ambao wao wanaziamini Aayaat (na hoja, dalili) Zetu.”


الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الرَّسُولَ النَّبِيَّ الْأُمِّيَّ الَّذِي يَجِدُونَهُ مَكْتُوبًا عِندَهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ يَأْمُرُهُم بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَاهُمْ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ وَيَضَعُ عَنْهُمْ إِصْرَهُمْ وَالْأَغْلَالَ الَّتِي كَانَتْ عَلَيْهِمْ ۚ فَالَّذِينَ آمَنُوا بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُوا النُّورَ الَّذِي أُنزِلَ مَعَهُ ۙ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ﴿١٥٧﴾
157. Wale wanomfuata Rasuli, Nabiy al-Ummiyy (asiyejua kusoma wala kuandika) ambaye wanamkuta ameandikwa kwao katika Tawraat na Injiyl, anawaamrisha ma’-ruwf (mema) na anawakataza munkari (maovu), na anawahalalishia vizuri na anawaharamishia maovu, na anawaondoshea mizigo yao (shariy’ah ngumu) na minyororo (vikwazo, taklifu) ilokuwa juu yao. Basi wale waliomwamini na wakamtukuza, na wakamnusuru na wakafuata nuru (Qur-aan) ambayo imeteremshwa pamoja naye; hao ndio wenye kufaulu.


قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ النَّبِيِّ الْأُمِّيِّ الَّذِي يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَكَلِمَاتِهِ وَاتَّبِعُوهُ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ﴿١٥٨﴾
158. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi ni Rasuli wa Allaah kwenu nyinyi nyote. (Allaah) Ambaye Pekee Anao ufalme wa mbingu na ardhi. Hapana ilaah (muabudiwa wa haki) ila Yeye. Anahuisha na Anafisha. Basi mwaminini Allaah na Rasuli Wake, Nabiy al-Ummiyy ambaye anamwamini Allaah na maneno Yake, na mfuateni ili mpate kuongoka.”


وَمِن قَوْمِ مُوسَىٰ أُمَّةٌ يَهْدُونَ بِالْحَقِّ وَبِهِ يَعْدِلُونَ﴿١٥٩﴾
159. Na katika kaumu ya Muwsaa (walikuweko) ummah wanaongoza kwa haki na kwa (haki) hiyo wanafanya uadilifu.


وَقَطَّعْنَاهُمُ اثْنَتَيْ عَشْرَةَ أَسْبَاطًا أُمَمًا ۚ وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ إِذِ اسْتَسْقَاهُ قَوْمُهُ أَنِ اضْرِب بِّعَصَاكَ الْحَجَرَ ۖ فَانبَجَسَتْ مِنْهُ اثْنَتَا عَشْرَةَ عَيْنًا ۖ قَدْ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٍ مَّشْرَبَهُمْ ۚ وَظَلَّلْنَا عَلَيْهِمُ الْغَمَامَ وَأَنزَلْنَا عَلَيْهِمُ الْمَنَّ وَالسَّلْوَىٰ ۖ كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ ۚ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ﴿١٦٠﴾
160. Na Tukawagawanya makabila kumi na mbili; mataifa (mashuhuri). Na Tukamfunulia Wahy Muwsaa walipomuomba maji kaumu yake, kwamba: “Piga jiwe kwa fimbo yako.” Zikachimbuka humo chemchemu kumi na mbili. Kila kabila likajua mahali pa kinywaji chake. Na Tukawafunika kwa mawingu (hifadhi ya jua kali), na Tukawateremshia mannaa na salwaa. (Tukawaambia): “Kuleni katika vizuri Tuliyokuruzukuni.” Hawakutudhulumu Sisi lakini walikuwa wakizidhulumu nafsi zao.


وَإِذْ قِيلَ لَهُمُ اسْكُنُوا هَـٰذِهِ الْقَرْيَةَ وَكُلُوا مِنْهَا حَيْثُ شِئْتُمْ وَقُولُوا حِطَّةٌ وَادْخُلُوا الْبَابَ سُجَّدًا نَّغْفِرْ لَكُمْ خَطِيئَاتِكُمْ ۚ سَنَزِيدُ الْمُحْسِنِينَ﴿١٦١﴾
161. Na (taja ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) pale walipoambiwa: “Kaeni katika mji huu (Quds), na kuleni humo popote mpendapo, na semeni (wakati wa kuingia), “Hittwah (tuondolee mzigo wa madhambi yetu),” na ingieni katika mlango (wake) huku mmeinama kwa unyenyekevu. Tutakughufurieni makosa yenu, (na) Tutawazidishia (neema na thawabu) wafanyao ihsaan.


فَبَدَّلَ الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْهُمْ قَوْلًا غَيْرَ الَّذِي قِيلَ لَهُمْ فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِجْزًا مِّنَ السَّمَاءِ بِمَا كَانُوا يَظْلِمُونَ﴿١٦٢﴾
162. “Basi wale waliodhulumu walibadilisha kauli kwa (kusema kauli) isiyokuwa ile waliyoambiwa, Tukawapelekea rijzan (adhabu ya kufadhaika) kutoka mbinguni kwa yale waliyokuwa wakijidhulumu”.


وَاسْأَلْهُمْ عَنِ الْقَرْيَةِ الَّتِي كَانَتْ حَاضِرَةَ الْبَحْرِ إِذْ يَعْدُونَ فِي السَّبْتِ إِذْ تَأْتِيهِمْ حِيتَانُهُمْ يَوْمَ سَبْتِهِمْ شُرَّعًا وَيَوْمَ لَا يَسْبِتُونَ ۙ لَا تَأْتِيهِمْ ۚ كَذَٰلِكَ نَبْلُوهُم بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ﴿١٦٣﴾
163. Na waulize kuhusu mji ambao ulikuwa kando ya bahari, waliporuka mipaka ya As-Sabt (shariy’ah ya Jumamosi) walipowajia samaki wao waziwazi siku yao ya Sabt Na siku zisizokuwa za Sabt hawakuwajia. Hivyo ndivyo Tulivowajaribu kwa yale waliyokuwa wakifanya ufasiki.


وَإِذْ قَالَتْ أُمَّةٌ مِّنْهُمْ لِمَ تَعِظُونَ قَوْمًا ۙ اللَّـهُ مُهْلِكُهُمْ أَوْ مُعَذِّبُهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا ۖ قَالُوا مَعْذِرَةً إِلَىٰ رَبِّكُمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ﴿١٦٤﴾
164. Na (taja ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم); pale ummah miongoni mwao uliposema: “Kwa nini mnawawaidhi watu ambao Allaah Atawahiliki au Atawaadhibu adhabu kali?” Wakasema (watoaji mawaidha): “Tupate kuwa na udhuru mbele ya Rabb (Mola) wenu na huenda wakawa na taqwa.”


فَلَمَّا نَسُوا مَا ذُكِّرُوا بِهِ أَنجَيْنَا الَّذِينَ يَنْهَوْنَ عَنِ السُّوءِ وَأَخَذْنَا الَّذِينَ ظَلَمُوا بِعَذَابٍ بَئِيسٍ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ﴿١٦٥﴾
165. Basi waliposahau yale waliyokumbushwa nayo; Tuliwaokoa wale wanaokataza uovu, na Tukawachukuwa wale waliodhulumu kwa adhabu mbaya kabisa kwa yale waliyokuwa wakifanya ufasiki.


فَلَمَّا عَتَوْا عَن مَّا نُهُوا عَنْهُ قُلْنَا لَهُمْ كُونُوا قِرَدَةً خَاسِئِينَ﴿١٦٦﴾
166. Basi walipozidi kuasi kuhusu waliyokuwa wakikatazwa nayo, Tulisema (kuwaambia): “Kuweni manyani waliotezwa.


وَإِذْ تَأَذَّنَ رَبُّكَ لَيَبْعَثَنَّ عَلَيْهِمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَن يَسُومُهُمْ سُوءَ الْعَذَابِ ۗ إِنَّ رَبَّكَ لَسَرِيعُ الْعِقَابِ ۖ وَإِنَّهُ لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١٦٧﴾
167. Na (taja) pale Alipotangaza Rabb (Mola) wako (kwamba) bila shaka Atawaletea (Mayahudi) mpaka siku ya Qiyaamah (watu) watakaowasibu adhabu mbaya. Hakika Rabb wako ni Mwepesi wa kuakibu, na hakika Yeye bila shaka ni Ghafuwr-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).


وَقَطَّعْنَاهُمْ فِي الْأَرْضِ أُمَمًا ۖ مِّنْهُمُ الصَّالِحُونَ وَمِنْهُمْ دُونَ ذَٰلِكَ ۖ وَبَلَوْنَاهُم بِالْحَسَنَاتِ وَالسَّيِّئَاتِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ﴿١٦٨﴾
168. Na Tukawagawanya katika ardhi mataifa (mbali mbali); miongoni mwao ni wema na miongoni mwao kinyume chake. Na Tukawajaribu kwa mazuri na maovu ili wapate kurejea (katika utiifu).


فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ وَرِثُوا الْكِتَابَ يَأْخُذُونَ عَرَضَ هَـٰذَا الْأَدْنَىٰ وَيَقُولُونَ سَيُغْفَرُ لَنَا وَإِن يَأْتِهِمْ عَرَضٌ مِّثْلُهُ يَأْخُذُوهُ ۚ أَلَمْ يُؤْخَذْ عَلَيْهِم مِّيثَاقُ الْكِتَابِ أَن لَّا يَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ إِلَّا الْحَقَّ وَدَرَسُوا مَا فِيهِ ۗ وَالدَّارُ الْآخِرَةُ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ﴿١٦٩﴾
169. Basi wakafuatia baada yao wafuatiaji (waovu) waliorithi Kitabu (bila ya kukifuata), wanachukua anasa za hapa duniani na (huku) wanasema: “Tutaghufuriwa,” na inapowafikia (tena) anasa kama hizo wanazichukua. Je, haikuchukuliwa kwao fungamano la Kitabu kwamba wasiseme juu ya Allaah isipokuwa haki tu? Na wameshayasoma yaliyomo humo?  Na nyumba ya Aakhirah ni bora zaidi kwa wale wenye taqwa. Je, basi hamtii akilini?


وَالَّذِينَ يُمَسِّكُونَ بِالْكِتَابِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجْرَ الْمُصْلِحِينَ﴿١٧٠﴾
170. Na wale wanaoshikilia imara Kitabu na wakasimamisha Swalaah, hakika Sisi Hatupotezi ujira wa watengenezao mazuri.


وَإِذْ نَتَقْنَا الْجَبَلَ فَوْقَهُمْ كَأَنَّهُ ظُلَّةٌ وَظَنُّوا أَنَّهُ وَاقِعٌ بِهِمْ خُذُوا مَا آتَيْنَاكُم بِقُوَّةٍ وَاذْكُرُوا مَا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ﴿١٧١﴾
171. Na (taja) Tulipoling’oa jabali (Tukalinyanyua na kulining’iniza) juu yao, kama kwamba ni kiwingu kilichowafunika, na wakadhani kwamba litawaangukia. (Tukawaambia): “Chukueni Tuliyokupeni kwa (azimio la) nguvu, na kumbukeni yale yaliyomo humo ili mpate kuwa na taqwa.


وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِن بَنِي آدَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَأَشْهَدَهُمْ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ ۖ قَالُوا بَلَىٰ ۛ شَهِدْنَا ۛ أَن تَقُولُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّا كُنَّا عَنْ هَـٰذَا غَافِلِينَ﴿١٧٢﴾
172. Na (taja) pale Rabb wako Alipochukua katika wana wa Aadam kutoka migongoni mwao, kizazi chao, na Akawashuhudisha juu ya nafsi zao, (Akawuliza): “Je, Mimi siye Rabb wenu?” Wakasema: “Ndiye, tunashuhudia!” (Allaah Akawaambia): “Msije kusema Siku ya Qiyaamah (kwamba) hakika sisi tulikuwa tumeghafilika nayo haya.”


أَوْ تَقُولُوا إِنَّمَا أَشْرَكَ آبَاؤُنَا مِن قَبْلُ وَكُنَّا ذُرِّيَّةً مِّن بَعْدِهِمْ ۖ أَفَتُهْلِكُنَا بِمَا فَعَلَ الْمُبْطِلُونَ﴿١٧٣﴾
173. Au mkasema: “Hakika baba zetu ndio walioshirikisha kabla, nasi tulikuwa kizazi baada yao. Basi Utatuangamiza kwa yale waliyoyafanya wabatilifu?”


وَكَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ وَلَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ﴿١٧٤﴾
174. Na hivyo ndivyo Tunavyofasili Aayaat na ili wapate kurejea (katika utiifu).


وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ الَّذِي آتَيْنَاهُ آيَاتِنَا فَانسَلَخَ مِنْهَا فَأَتْبَعَهُ الشَّيْطَانُ فَكَانَ مِنَ الْغَاوِينَ﴿١٧٥﴾
175. Na wasomee (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) habari za yule Tuliyempa (ujuzi wa) Aayaat (hoja, dalili) Zetu akajivua nazo (asizifuate), na shaytwaan akamfuata na akawa miongoni mwa waliopotoka.


وَلَوْ شِئْنَا لَرَفَعْنَاهُ بِهَا وَلَـٰكِنَّهُ أَخْلَدَ إِلَى الْأَرْضِ وَاتَّبَعَ هَوَاهُ ۚ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ الْكَلْبِ إِن تَحْمِلْ عَلَيْهِ يَلْهَثْ أَوْ تَتْرُكْهُ يَلْهَث ۚ ذَّٰلِكَ مَثَلُ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۚ فَاقْصُصِ الْقَصَصَ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ﴿١٧٦﴾
176. Na lau Tungelitaka Tungelimnyanyua kwazo (hizo Aayaat), lakini aligandamana na dunia na akafuata hawaa zake. Basi mfano wake ni kama mfano wa mbwa, ukimhujumu ananing’iniza ulimi nje na kuhema, na ukimwacha pia ananing’iniza ulimi nje na kuhema. Hivyo ndiyo mfano wa watu waliokadhibisha Aayaat (ishara, hoja) Zetu. Basi simulia visa huenda wakatafakari.


سَاءَ مَثَلًا الْقَوْمُ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَأَنفُسَهُمْ كَانُوا يَظْلِمُونَ﴿١٧٧﴾
177. Uovu ulioje mfano wa watu waliokadhibisha Aayaat (ishara, hoja) Zetu na wakawa wanajidhulumu nafsi zao.


مَن يَهْدِ اللَّـهُ فَهُوَ الْمُهْتَدِي ۖ وَمَن يُضْلِلْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ﴿١٧٨﴾
178. Atakaowaongoza Allaah, basi ndio watakaoongoka, na Atakaowaachia kupotoka, basi hao ndio wenye kukhasirika.


وَلَقَدْ ذَرَأْنَا لِجَهَنَّمَ كَثِيرًا مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ ۖ لَهُمْ قُلُوبٌ لَّا يَفْقَهُونَ بِهَا وَلَهُمْ أَعْيُنٌ لَّا يُبْصِرُونَ بِهَا وَلَهُمْ آذَانٌ لَّا يَسْمَعُونَ بِهَا ۚ أُولَـٰئِكَ كَالْأَنْعَامِ بَلْ هُمْ أَضَلُّ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْغَافِلُونَ﴿١٧٩﴾
179. Kwa yakini Tumeuumbia (Moto wa) Jahannam wengi katika majini na wanadamu. Wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo. Na wana macho, lakini hawaoni kwayo. Na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama, bali wao ni wapotovu zaidi. Hao ndio walioghafilika.


وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚ سَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١٨٠﴾
180. Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. Na waacheni wale wanaopotoa katika (kuharibu utukufu, kukanusha, kugeuza maana, kushabihisha) Majina Yake, watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda.


وَمِمَّنْ خَلَقْنَا أُمَّةٌ يَهْدُونَ بِالْحَقِّ وَبِهِ يَعْدِلُونَ﴿١٨١﴾
181. Na katika Tuliowaumba, wako ummah wanaoongoza kwa haki na kwayo wanafanya uadilifu.


وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا سَنَسْتَدْرِجُهُم مِّنْ حَيْثُ لَا يَعْلَمُونَ﴿١٨٢﴾
182. Na wale waliokadhibisha Aayaat (na, ishara, hoja, dalili) Zetu Tutawavuta pole pole (kuwangamiza) kwa namna wasiyoijua.


وَأُمْلِي لَهُمْ ۚ إِنَّ كَيْدِي مَتِينٌ﴿١٨٣﴾
183. Na Nitawapa muhula. Hakika mpango Wangu (wa kuwarudishia vitimbi vyao) ni madhubuti.



أَوَلَمْ يَتَفَكَّرُوا ۗ مَا بِصَاحِبِهِم مِّن جِنَّةٍ ۚ إِنْ هُوَ إِلَّا نَذِيرٌ مُّبِينٌ﴿١٨٤﴾
184. Je, hawatafakari? Swahibu yao (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) hana wazimu! Hakuwa yeye ila ni mwonyaji bayana.


أَوَلَمْ يَنظُرُوا فِي مَلَكُوتِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا خَلَقَ اللَّـهُ مِن شَيْءٍ وَأَنْ عَسَىٰ أَن يَكُونَ قَدِ اقْتَرَبَ أَجَلُهُمْ ۖ فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَهُ يُؤْمِنُونَ﴿١٨٥﴾
185. Je, hawatazami ufalme wa mbingu na ardhi na vitu Alivyoviumba Allaah, na huenda ukawa muda wao uliopangwa umeshakaribia? Basi hadiyth gani baada yake (hii Qur-aan) wataamini?


مَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَلَا هَادِيَ لَهُ ۚ وَيَذَرُهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ﴿١٨٦﴾
186. Ambao Allaah Amewapotoa (kwa kutaka wenyewe), basi hakuna wa kuwaongoa. Na Atawaacha katika upindukaji mipaka ya kuasi kwao, wakitangatanga kwa upofu.


يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا ۖ قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِندَ رَبِّي ۖ لَا يُجَلِّيهَا لِوَقْتِهَا إِلَّا هُوَ ۚ ثَقُلَتْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ لَا تَأْتِيكُمْ إِلَّا بَغْتَةً ۗ يَسْأَلُونَكَ كَأَنَّكَ حَفِيٌّ عَنْهَا ۖ قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِندَ اللَّـهِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴿١٨٧﴾
187. Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Saa (Qiyaamah), lini kutokea kwake? Sema: “Hakika ujuzi wake uko kwa Rabb (Mola) wangu. Hakuna wa kuidhihirisha wakati wake isipokuwa Yeye (Pekee). Ni nzito katika mbingu na ardhi. Haitokufikieni isipokuwa kwa ghafla.” Wanakuuliza kama kwamba wewe unaijua vyema. Sema: “Hakika ujuzi wake uko kwa Allaah (Pekee), lakini watu wengi hawajui.


قُل لَّا أَمْلِكُ لِنَفْسِي نَفْعًا وَلَا ضَرًّا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ ۚ وَلَوْ كُنتُ أَعْلَمُ الْغَيْبَ لَاسْتَكْثَرْتُ مِنَ الْخَيْرِ وَمَا مَسَّنِيَ السُّوءُ ۚ إِنْ أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ﴿١٨٨﴾
188. Sema: “Siimilikii nafsi yangu manufaa yoyote wala dhara yoyote isipokuwa Apendavyo Allaah. Na lau ningekuwa najua ya ghayb, bila shaka ningelijikithirishia ya kheri, na wala lisingelinigusa ovu. Mimi si chochote isipokuwa ni mwonyaji na mbashiriaji kwa watu wanaoamini.


هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَجَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا لِيَسْكُنَ إِلَيْهَا ۖ فَلَمَّا تَغَشَّاهَا حَمَلَتْ حَمْلًا خَفِيفًا فَمَرَّتْ بِهِ ۖ فَلَمَّا أَثْقَلَت دَّعَوَا اللَّـهَ رَبَّهُمَا لَئِنْ آتَيْتَنَا صَالِحًا لَّنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ﴿١٨٩﴾
189. Yeye (Allaah) Ndiye Aliyekuumbeni kutokana na nafsi moja na Akafanya humo (kuumbwa) mke wake ili apate utulivu. Basi anapomuingilia hubeba mimba hafifu anayotembea nayo. Kisha inapokuwa nzito (mimba pevu; wote wawili mke na mume) humwomba Allaah Rabb (Mola) wao: “Ukitupa swaalihaa (mtoto mzima); bila shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru.”


فَلَمَّا آتَاهُمَا صَالِحًا جَعَلَا لَهُ شُرَكَاءَ فِيمَا آتَاهُمَا ۚ فَتَعَالَى اللَّـهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿١٩٠﴾
190. Basi Anapowapa swaalihaa (mtoto mzima), wanamfanyia (Allaah) washirika katika kile Alichowapa. Basi Ametukuka Allaah kwa Uluwa kutokana na yale yote wanayoshirikisha.


أَيُشْرِكُونَ مَا لَا يَخْلُقُ شَيْئًا وَهُمْ يُخْلَقُونَ﴿١٩١﴾
191. Je, wanawashirikisha (na Allaah) wale ambao hawaumbi kitu na hali wao wameumbwa?


وَلَا يَسْتَطِيعُونَ لَهُمْ نَصْرًا وَلَا أَنفُسَهُمْ يَنصُرُونَ﴿١٩٢﴾
192. Na wala hawawezi kuwanusuru na wala hawawezi kujinusuru nafsi zao.


وَإِن تَدْعُوهُمْ إِلَى الْهُدَىٰ لَا يَتَّبِعُوكُمْ ۚ سَوَاءٌ عَلَيْكُمْ أَدَعَوْتُمُوهُمْ أَمْ أَنتُمْ صَامِتُونَ﴿١٩٣﴾
193. Na mkiwaita kwenye Uongofu hawatakufuateni. Ni sawasawa kwenu, mkiwaita au mkiwanyamazia.


إِنَّ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ عِبَادٌ أَمْثَالُكُمْ ۖ فَادْعُوهُمْ فَلْيَسْتَجِيبُوا لَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿١٩٤﴾
194. Hakika wale mnaowaomba badala ya Allaah ni waja kama nyinyi. Hebu waiteni wakuitikieni ikiwa nyinyi ni wakweli.


أَلَهُمْ أَرْجُلٌ يَمْشُونَ بِهَا ۖ أَمْ لَهُمْ أَيْدٍ يَبْطِشُونَ بِهَا ۖ أَمْ لَهُمْ أَعْيُنٌ يُبْصِرُونَ بِهَا ۖ أَمْ لَهُمْ آذَانٌ يَسْمَعُونَ بِهَا ۗ قُلِ ادْعُوا شُرَكَاءَكُمْ ثُمَّ كِيدُونِ فَلَا تُنظِرُونِ﴿١٩٥﴾
195. Je, kwani wana miguu wanayotembelea nayo? Au wana mikono wanayokamatia kwayo? Au wana macho wanayoonea kwayo? Au wana masikio wanayosikilizia kwayo? Sema: “Waiteni washirika wenu, kisha nifanyieni njama; wala msinipe muhula.


إِنَّ وَلِيِّيَ اللَّـهُ الَّذِي نَزَّلَ الْكِتَابَ ۖ وَهُوَ يَتَوَلَّى الصَّالِحِينَ﴿١٩٦﴾
196. Hakika Waliyy (Mlinzi, Msaidizi) wangu ni Allaah Ambaye Ameteremsha Kitabu, Naye Ndiye Anayewalinda na kuwasaidia Swalihina.


وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَكُمْ وَلَا أَنفُسَهُمْ يَنصُرُونَ﴿١٩٧﴾
197. Na wale mnaowaomba (na kuwaabudu) badala ya Allaah hawawezi kuwanusuru na wala hawawezi kujinusuru nafsi zao.


وَإِن تَدْعُوهُمْ إِلَى الْهُدَىٰ لَا يَسْمَعُوا ۖ وَتَرَاهُمْ يَنظُرُونَ إِلَيْكَ وَهُمْ لَا يُبْصِرُونَ﴿١٩٨﴾
198. Na ukiwaita katika Uongofu hawasikii; na utawaona wanakutazama na hali wao hawaoni.


خُذِ الْعَفْوَ وَأْمُرْ بِالْعُرْفِ وَأَعْرِضْ عَنِ الْجَاهِلِينَ﴿١٩٩﴾
199.   Shikamana na usamehevu, na amrisha al’urf (mema), na jiepushe na majahili.


وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ ۚ إِنَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿٢٠٠﴾
200. Na pindi utakapokuchochea uchochezi kutokana na shaytwaan; basi jikinge na Allaah (sema, A’uwdhu biLLaahi). Hakika Yeye ni Samiy’un-‘Aliym (Mwenye kusikia yote – Mjuzi wa yote).


إِنَّ الَّذِينَ اتَّقَوْا إِذَا مَسَّهُمْ طَائِفٌ مِّنَ الشَّيْطَانِ تَذَكَّرُوا فَإِذَا هُم مُّبْصِرُونَ﴿٢٠١﴾
201. Hakika wale waliokuwa na taqwa inapowagusa pepesi za shaytwaan hukumbuka (Allaah), basi mara wao huwa wenye kumaizi (kutambua haki).


وَإِخْوَانُهُمْ يَمُدُّونَهُمْ فِي الْغَيِّ ثُمَّ لَا يُقْصِرُونَ﴿٢٠٢﴾
202. Na ndugu zao wanawavutia katika upotofu, kisha hawakasiri (hawahuli).


وَإِذَا لَمْ تَأْتِهِم بِآيَةٍ قَالُوا لَوْلَا اجْتَبَيْتَهَا ۚ قُلْ إِنَّمَا أَتَّبِعُ مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ مِن رَّبِّي ۚ هَـٰذَا بَصَائِرُ مِن رَّبِّكُمْ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ﴿٢٠٣﴾
203. Na usipowaletea Aayah (wazitakazo ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) husema: “Kwanini hukuibuni?” Sema: “Hakika (mimi) nafuata yale nilofunuliwa Wahy kutoka kwa Rabb (Mola) wangu. Hii (Qur-aan) ni baswaair (busara, nuru za elimu, umaizi, dalili wazi) kutoka kwa Rabb wenu, na ni Mwongozo na Rahmah kwa watu wanaoamini.”


وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ﴿٢٠٤﴾
204. Na inaposomwa Qur-aan, basi isikilizeni kwa makini na mkae kimya (mzingatie) mpate kurehemewa.


وَاذْكُر رَّبَّكَ فِي نَفْسِكَ تَضَرُّعًا وَخِيفَةً وَدُونَ الْجَهْرِ مِنَ الْقَوْلِ بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ وَلَا تَكُن مِّنَ الْغَافِلِينَ﴿٢٠٥﴾
205. Na mdhukuru Rabb (Mola) wako katika nafsi yako kwa unyenyekevu na kwa khofu na si kwa jahara (kunyanyua sauti) katika kauli asubuhi na jioni; na wala usiwe miongoni mwa walioghafilika.


إِنَّ الَّذِينَ عِندَ رَبِّكَ لَا يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِهِ وَيُسَبِّحُونَهُ وَلَهُ يَسْجُدُونَ ۩﴿٢٠٦﴾
206. Hakika wale (Malaika) walioko kwa Rabb (Mola) wako hawatakabari kufanya ‘ibaadah Yake na wanamsabbih na Kwake Pekee wanasujudu.


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com