Al-Jumu’ah (62)


سُورَةُ  الْجُمُعَة
Al-Jumu’ah (62)

(Imeteremka Madina)


Imefunguka Sura hii kwa kutoa khabari yake Mtukufu kwamba viliomo katika mbingu na ardhi vyote vinamsabihi Yeye. Na Mwenyezi Mungu aliye tukuka shani yake amesema kwamba ameineemesha kaumu isio jua kuandika wala kusoma kwa kuwaletea Mtume miongoni mwao, ambaye anawafundisha Kitabu, na hikima, na anawatakasa. Na hakika hii ni fadhila ya Mwenyezi Mungu humpa amtakaye.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amewakemea Mayahudi kwa kuacha kwao kutenda yaliyo amrishwa katika Taurati, na hali wao wanajua yaliomo humo. Na amepinga madai yao kwamba wao peke yao ndio vipenzi vya Mwenyezi Mungu, si watu wenginewe. Na amebariziana nao kwa kuwataka watamani kufa ikiwa wao wanasema kweli! Na Sura imekhitimisha kwa kuwaamrisha Waumini wakimbilie kwenda sali Sala ya Ijumaa pindi wakisikia adhana, na waache biashara. Na Sala ikisha malizika watawanyike katika nchi wende kutafuta fadhila za Mwenyezi Mungu. Na kawakataza wasiache biashara au jambo la pumbao lolote kuwashughulisha wasiisikilize khutba ya Ijumaa. Na Mwenyezi Mungu amewadhamini kuwaruzuku, na Yeye ndiye mbora wa kuruzuku.

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

يُسَبِّحُ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ الْمَلِكِ الْقُدُّوسِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ ﴿١﴾

1. Kinamsabbih Allaah Pekee (kila) kilichokuweko katika mbingu na katika ardhi, Al-Malik (Mfalme) Al-Qudduws (Mtakatifu) Al-‘Aziyzil-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwenye hikmah wa yote daima).

هُوَ الَّذِي بَعَثَ فِي الْأُمِّيِّينَ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٢﴾

2. Yeye Ndiye Aliyepeleka Rasuli kwa Al-Ummiyyiyn (watu wasiojua kusoma wala kuandika) miongoni mwao anawasomea Aayaat Zake na Anawatakasa, na Anawafunza Kitabu (Qur-aan) na Hikmah (Sunnah), na japo walikuwa kabla katika upotofu bayana.

وَآخَرِينَ مِنْهُمْ لَمَّا يَلْحَقُوا بِهِمْ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٣﴾

3. Na wengineo ambao bado hawajakutana nao. Naye Ndiye Al-‘Aziyzul-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwenye hikmah wa yote daima).

ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿٤﴾

4. Hiyo ni fadhila ya Allaah Humpa Amtakaye, na Allaah ni Mwenye fadhila adhimu.

مَثَلُ الَّذِينَ حُمِّلُوا التَّوْرَاةَ ثُمَّ لَمْ يَحْمِلُوهَا كَمَثَلِ الْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًا ۚ بِئْسَ مَثَلُ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٥﴾

5. Mfano wa wale waliobebeshwa Tawraat, kisha wasiibebe (kwa kutotekeleza amri zake) ni kama mfano wa punda abebaye mijalada ya vitabu. Ubaya ulioje mfano wa watu waliokadhibisha Aayaat za Allaah, na Allaah Haongoi watu madhalimu.

قُلْ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ هَادُوا إِن زَعَمْتُمْ أَنَّكُمْ أَوْلِيَاءُ لِلَّـهِ مِن دُونِ النَّاسِ فَتَمَنَّوُا الْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٦﴾

6. Sema: Enyi Mayahudi! Mkidai kuwa nyinyi ni awliyaa (vipenzi) wa Allaah pasina watu wengine, basi tamaneni mauti, mkiwa ni wasemao kweli.

وَلَا يَتَمَنَّوْنَهُ أَبَدًا بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ ۚ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ ﴿٧﴾

7. Na wala hawatayatamani (hayo mauti) abadani kwa sababu ya yale (maovu) yaliyotanguliza mikono yao, na Allaah ni ‘Aliym (Mjuzi) wa madhalimu.

قُلْ إِنَّ الْمَوْتَ الَّذِي تَفِرُّونَ مِنْهُ فَإِنَّهُ مُلَاقِيكُمْ ۖ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٨﴾

8. Sema: “Hakika (hayo) mauti mnayoyakimbia, hakika ni yenye kukuteni tu! Kisha mtarudishwa kwa ‘Aalimu (Mjuzi) wa ghayb na dhahiri. Atakujulisheni kwa yale mliyokuwa mkiyatenda.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٩﴾

9. Enyi mlioamini! Inaponadiwa (adhana ya) Swalaah siku ya Ijumaa, kimbilieni kwenye dhikri[3] ya Allaah na acheni kuuza na kununua. Hivyo ni kheri kwenu mkiwa mnajua.

فَإِذَا قُضِيَتِ الصَّلَاةُ فَانتَشِرُوا فِي الْأَرْضِ وَابْتَغُوا مِن فَضْلِ اللَّـهِ وَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَثِيرًا لَّعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿١٠﴾

10. Na inapomalizika Swalaah, tawanyikeni katika ardhi, na tafuteni katika fadhila za Allaah, na mdhukuruni Allaah sana ili mpate kufaulu.

وَإِذَا رَأَوْا تِجَارَةً أَوْ لَهْوًا انفَضُّوا إِلَيْهَا وَتَرَكُوكَ قَائِمًا ۚ قُلْ مَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ مِّنَ اللَّـهْوِ وَمِنَ التِّجَارَةِ ۚ وَاللَّـهُ خَيْرُ الرَّازِقِينَ ﴿١١﴾

11. Na wanapoona tijara au pumbao wanaikimbilia, na wanakuacha umesimama. Sema: “Yaliyoko kwa Allaah ni bora zaidi kuliko pumbao na tijara, na Allaah ni Mbora wa wenye kuruzuku.



Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com