026 - Hadiyth Ya 26: Kulea Watoto Wa Kike Ni Kuwa Pamoja na Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) Peponi




عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ  (رضي الله عنه)  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صلى الله عليه و آله وسلم): ((مَنْ عَالَ جَارِيَتَيْنِ حَتَّى تَبْلُغَا جَاءَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَنَا وَهُوَ كَهَاتَيْنِ)) وَضَمَّ أَصَابِعَهُ. رواه مسلم   
 
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه)  kwamba Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayewasimamia [kuwalea na matumizi] mabinti wawili mpaka wabaleghe, atakuja Siku ya Qiyaamah mimi na  yeye ni kama hivi)), Akavishikanisha vidole vyake.[1]
 
 
Mafunzo Na Hidaaya:
 
 
  1. Fadhila za kulea watoto wa kike ambao walikuwa wakidhalilishwa zama za ujaahiliyyah mpaka kufikia kuzikwa wangali hai.
 
وَإِذَا الْمَوْءُودَةُ سُئِلَتْ ﴿٨﴾ بِأَيِّ ذَنبٍ قُتِلَتْ ﴿٩﴾
 
Na mtoto wa kike aliyezikwa akiwa hai atakapoulizwa. Kwa dhambi gani aliuliwa?
 
  1. Hoja kwa makafiri wanaozusha kwamba mwanamke wa Kiislamu hana haki wala hadhi. Bali Uislamu umemnyanyua mwanamke cheo chake na kumpatia hadhi kubwa.
 
  1. Kulea watoto wa kike malezi mema ya Dini ni sababu ya mzazi kuingia Peponi.
 
  1. Sababu mojawapo ya kumjaalia mtu kuwa karibu na Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) Peponi ni kuwalea wasichana vizuri.
 
  1. Ukarimu na upole wa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa watoto na wazazi [At-Tawbah 9: 128].
 
  1. Muislamu anatakiwa awe mwadilifu kwa watoto wake katika malezi bila kubagua wavulana au wasichana.
 
  1. Hii inaonyesha fadhila kubwa ya wasichana katika jamii ya Kiislamu. Ndio mshairi akasema: “Kumlea vyema msichana ni kutengeneza jamii”.



[1]  Muslim.