Al-Qiyaamah (75)


سُورَةُ  الْقِيَامَة
Al-Qiyaamah (75)
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

لَا أُقْسِمُ بِيَوْمِ الْقِيَامَةِ ﴿١﴾
1. Naapa kwa siku ya Qiyaamah.


وَلَا أُقْسِمُ بِالنَّفْسِ اللَّوَّامَةِ ﴿٢﴾

2. Na Naapa kwa nafsi inayojilaumu.


أَيَحْسَبُ الْإِنسَانُ أَلَّن نَّجْمَعَ عِظَامَهُ ﴿٣﴾

3.  Je, anadhani insani kwamba Hatutoikusanya mifupa yake?

بَلَىٰ قَادِرِينَ عَلَىٰ أَن نُّسَوِّيَ بَنَانَهُ ﴿٤﴾

4. Ndio! Tuna uwezo wa (hata) kusawazisha ncha za vidole vyake (zikiwemo alama zake).

بَلْ يُرِيدُ الْإِنسَانُ لِيَفْجُرَ أَمَامَهُ ﴿٥﴾

5. Bali anataka insani aendelee kutenda dhambi mbele yake.

يَسْأَلُ أَيَّانَ يَوْمُ الْقِيَامَةِ ﴿٦﴾

6. Anauliza (kwa istihzai) ni lini (hiyo) siku ya Qiyaamah?

فَإِذَا بَرِقَ الْبَصَرُ ﴿٧﴾

7. Basi jicho litakapoduwaa.

وَخَسَفَ الْقَمَرُ ﴿٨﴾

8. Na mwezi utakapopatwa.

وَجُمِعَ الشَّمْسُ وَالْقَمَرُ ﴿٩﴾

9. Na itakapojumuishwa jua na mwezi.

يَقُولُ الْإِنسَانُ يَوْمَئِذٍ أَيْنَ الْمَفَرُّ ﴿١٠﴾

10. Atasema insani siku hiyo: “Wapi pa kukimbilia?”

كَلَّا لَا وَزَرَ ﴿١١﴾

11. Hasha! Hapana mahali pa kukimbilia.

إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ الْمُسْتَقَرُّ ﴿١٢﴾

12. Kwa Rabb (Mola) wako siku hiyo ndio makazi ya kustakiri.

يُنَبَّأُ الْإِنسَانُ يَوْمَئِذٍ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ ﴿١٣﴾

13. Siku hiyo insani atajulishwa yale aliyoyakadimisha na aliyoyaakhirisha.

بَلِ الْإِنسَانُ عَلَىٰ نَفْسِهِ بَصِيرَةٌ ﴿١٤﴾

14. Bali insani (atakuwa) shahidi dhidi ya nafsi yake.

وَلَوْ أَلْقَىٰ مَعَاذِيرَهُ ﴿١٥﴾

15. Japo akitoa nyudhuru.

لَا تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ ﴿١٦﴾

16. Usitikise lisani yako ili kuiharakiza (Qur-aan ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).

إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَهُ وَقُرْآنَهُ ﴿١٧﴾

17. Hakika ni juu Yetu kuikusanya (moyoni mwako), na (kuiwezesha) kuisoma kwake.

فَإِذَا قَرَأْنَاهُ فَاتَّبِعْ قُرْآنَهُ ﴿١٨﴾

18. Basi Tunapoisoma (kupitia Jibriyl), fuata kusomwa kwake.

ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُ ﴿١٩﴾

19. Kisha ni juu Yetu kuibainisha (kwako).

كَلَّا بَلْ تُحِبُّونَ الْعَاجِلَةَ ﴿٢٠﴾
20. Sivyo katu! Bali mnapenda (uhai wa dunia) unaopita haraka kwa muda tu.

وَتَذَرُونَ الْآخِرَةَ ﴿٢١﴾

21. Na mnaiacha Aakhirah (yenye kudumu abadi).

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاضِرَةٌ ﴿٢٢﴾

22. (Baadhi ya) Nyuso siku hiyo zitanawiri.

إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ ﴿٢٣﴾

23. Zikimtazama Rabb (Mola) wake.

وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ بَاسِرَةٌ ﴿٢٤﴾

24. Na (baadhi ya) nyuso siku hiyo zitakunjana (kwa kusononeka).

تَظُنُّ أَن يُفْعَلَ بِهَا فَاقِرَةٌ ﴿٢٥﴾

25. Zitaelewa yakini kuwa zitafikiwa na msiba unaovunja uti wa mgongo.

كَلَّا إِذَا بَلَغَتِ التَّرَاقِيَ ﴿٢٦﴾
321
26. Hasha! Itakapofika (roho) mafupa ya koo.

وَقِيلَ مَنْ ۜ رَاقٍ ﴿٢٧﴾

27. Na itasemwa:  “Ni nani wa kumzingua (kumtibu)?”

وَظَنَّ أَنَّهُ الْفِرَاقُ ﴿٢٨﴾

28. Na ataelewa yakini kwamba ni (wakati wa) kufariki.


وَالْتَفَّتِ السَّاقُ بِالسَّاقِ ﴿٢٩﴾

29. Na utakapoambatanishwa muundi kwa muundi.

إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ الْمَسَاقُ ﴿٣٠﴾

30. Siku hiyo kwa Rabb (Mola) wako ndio kuendeshwa (kupelekwa huko).


فَلَا صَدَّقَ وَلَا صَلَّىٰ ﴿٣١﴾

31. (Kwani) Hakusadikisha (hii Qur-aan) na wala hakuswali.

وَلَـٰكِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ﴿٣٢﴾

32. Lakini (badala yake) alikadhibisha na akakengeuka.

ثُمَّ ذَهَبَ إِلَىٰ أَهْلِهِ يَتَمَطَّىٰ ﴿٣٣﴾

33. Kisha akaenda kwa watu wake akijigamba.

أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰ ﴿٣٤﴾

34. Ole kwako! Ole kwako (ewe kafiri)!

ثُمَّ أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰ ﴿٣٥﴾

35. Kisha ole kwako! Tena ole kwako!

أَيَحْسَبُ الْإِنسَانُ أَن يُتْرَكَ سُدًى ﴿٣٦﴾

36. Je, anadhani insani ataachwa bila ya lengo (bure)?

أَلَمْ يَكُ نُطْفَةً مِّن مَّنِيٍّ يُمْنَىٰ ﴿٣٧﴾

37. Kwani hakuwa tone kutokana na manii lilotonwa?

ثُمَّ كَانَ عَلَقَةً فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ ﴿٣٨﴾

38. Kisha akawa pande la damu, (Allaah) Akamuumba na Akamsawazisha?

فَجَعَلَ مِنْهُ الزَّوْجَيْنِ الذَّكَرَ وَالْأُنثَىٰ ﴿٣٩﴾

39. Akamjaalia jozi; dume na jike.

أَلَيْسَ ذَٰلِكَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يُحْيِيَ الْمَوْتَىٰ ﴿٤٠﴾

40. Je, hivyo Hakuwa (Huyo Muumbaji) Qaadir (Muweza) wa kuhuisha wafu?





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com