Asw-Swaff (61)


سُورَةُ  الصَّف
Asw-Swaff (61)

(Imeteremka Madina)



Sura hii imefunguka kwa kutoa khabari kwamba viliomo katika mbingu na katika ardhi vinamsabihi Mwenyezi Mungu. Na kwamba haiwaelekei Waumini kusema wasiyo yatenda. Na hakika Mwenyezi Mungu anapenda wawe mkono mmoja. Kisha Sura imewashutumu Wana wa Israili kuwa ni wenye inda na ukafiri kwa kauli za Mitume wawili watukufu, nao ni Musa na Isa s.a.w. Na kwamba wao wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuitimiza nuru yake. Na ndani ya hii Sura ipo ahadi ya Mwenyezi Mungu - na ahadi yake ni ya kweli - kuwa ataifanya Dini hii ishinde dini zote nyenginezo, hata walau washirikina wakichukia. Na ikakhitimishia kwa kuhimiza Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa hali na mali, na kuwaahidi wenye kupigana Jihadi, Mujahidina, kupata msamaha na Pepo, na mengineyo wayapendayo Waumini, nayo ni msaada utokao kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi wa karibu. Na wanahimizwa Waumini wawe wenye kumsaidia Mwenyezi Mungu, kama walivyo kuwa wanafunzi wa Isa bin Mariamu. Na kwamba Mwenyezi Mungu atawaunga mkono Waumini kwa msaada wake, na Yeye ni Mwenye kushinda katika kila kitu, Mwenye hikima ya ukomo.

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

سَبَّحَ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١﴾

1. Kinamsabbih Allaah Pekee (kila) kilichokuweko katika mbingu na katika ardhi, Naye ndiye Al-‘Aziyzul-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwenye hikmah wa yote daima).

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لِمَ تَقُولُونَ مَا لَا تَفْعَلُونَ ﴿٢﴾

2. Enyi mlioamini!  Kwanini mnasema yale msiyoyafanya?

كَبُرَ مَقْتًا عِندَ اللَّـهِ أَن تَقُولُوا مَا لَا تَفْعَلُونَ ﴿٣﴾

3. Ni chukizo kubwa mno mbele ya Allaah kwamba mnasema yale msiyoyafanya.

إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِهِ صَفًّا كَأَنَّهُم بُنْيَانٌ مَّرْصُوصٌ ﴿٤﴾

4. Hakika Allaah Anapenda wale wanaopigana katika njia Yake safusafu kama kwamba wao ni jengo linalokamatana barabara.

وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ لِمَ تُؤْذُونَنِي وَقَد تَّعْلَمُونَ أَنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ ۖ فَلَمَّا زَاغُوا أَزَاغَ اللَّـهُ قُلُوبَهُمْ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ ﴿٥﴾

5. Na (taja pale) Muwsaa alipowaambia watu wake: “Enyi watu wangu! Kwanini mnaniudhi na hali mmekwishajua kwamba hakika mimi ni Rasuli wa Allaah kwenu?” Basi walipopotoka, Allaah Akapotosha nyoyo zao; na Allaah Haongoi watu mafasiki.

وَإِذْ قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُم مُّصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَمُبَشِّرًا بِرَسُولٍ يَأْتِي مِن بَعْدِي اسْمُهُ أَحْمَدُ ۖ فَلَمَّا جَاءَهُم بِالْبَيِّنَاتِ قَالُوا هَـٰذَا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿٦﴾

6. Na (taja pale) ‘Iysaa mwana wa Maryam aliposema: “Enyi wana wa Israaiyl! Hakika mimi ni Rasuli wa Allaah kwenu mwenye kusadikisha yaliyo kabla yangu katika Tawraat na mwenye kubashiria kuja kwa Rasuli baada yangu jina lake: Ahmad.” Basi alipowajia kwa hoja bayana, walisema: “Hii ni sihiri bayana.”

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ وَهُوَ يُدْعَىٰ إِلَى الْإِسْلَامِ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٧﴾

7. Na nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia Allaah uongo na (hali) yeye analinganiwa katika Uislamu? Na Allaah Haongoi watu madhalimu.

يُرِيدُونَ لِيُطْفِئُوا نُورَ اللَّـهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَاللَّـهُ مُتِمُّ نُورِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ ﴿٨﴾

8. Wanataka kuizima Nuru ya Allaah kwa midomo yao, (lakini) Allaah ni Mwenye kuitimiza Nuru Yake japo makafiri watachukia.

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ ﴿٩﴾

9. Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa mwongozo na Dini ya haki ili Aidhihirishe (Aishindishe) juu ya dini zote, japo washirikina watachukia.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ تِجَارَةٍ تُنجِيكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿١٠﴾

10. Enyi mlioamini! Nikujulisheni biashara itakayokuokoeni na adhabu iumizayo?


تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَتُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿١١﴾

11. Mumuamini Allaah na Rasuli Wake, na mfanye jihaad katika njia ya Allaah kwa mali zenu, na nafsi zenu. Hivyo ndiyo bora kwenu mkiwa mnajua.

يَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَيُدْخِلْكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١٢﴾

12. (Allaah) Atakughufurieni madhambi yenu, na Atakuingizeni Jannaat zipitazo chini yake mito na masikani mazuri katika Jannaat za ‘Adn. Huko ndiko kufuzu kukubwa.

وَأُخْرَىٰ تُحِبُّونَهَا ۖ نَصْرٌ مِّنَ اللَّـهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ ۗ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٣﴾

13. Na (Atakupeni neema) nyinginezo mzipendazo; nusura kutoka kwa Allaah na ushindi wa karibu. Na wabashirie Waumini.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا أَنصَارَ اللَّـهِ كَمَا قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ لِلْحَوَارِيِّينَ مَنْ أَنصَارِي إِلَى اللَّـهِ ۖ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ نَحْنُ أَنصَارُ اللَّـهِ ۖ فَآمَنَت طَّائِفَةٌ مِّن بَنِي إِسْرَائِيلَ وَكَفَرَت طَّائِفَةٌ ۖ فَأَيَّدْنَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَىٰ عَدُوِّهِمْ فَأَصْبَحُوا ظَاهِرِينَ ﴿١٤﴾

14. Enyi mlioamini! Kuweni Answaar (wenye kunusuru Dini ya) Allaah kama (vile alivyosema) ‘Iysa mwana wa Maryam kuwaambia Al-Hawariyyiyn (wafuasi wake): “Nani Answaar wangu kwa (ajili ya) Allaah?” Al-Hawariyyuwn wakasema: “Sisi ni Answaaru-Allaah (wenye kunusuru Dini ya Allaah)” Basi likaamini kundi miongoni mwa wana wa Israaiyl na likakufuru kundi. Tukawatia nguvu wale walioamini dhidi ya maadui zao, wakapambaukiwa wakiwa washindi




Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com