At-Tahriym (66)


سُورَةُ  التَّحْرِيم
At-Tahriym (66)

(Imeteremka Madina)


Sura hii inaashiria jambo ambalo lilimuudhi Nabii s.a.w. katika baadhi ya wake zake; akajizuilia na baadhi ya mambo ambayo nafsi huyapenda na Mwenyezi Mungu amehalalisha. Na inawahadharisha wake zake na matokeo ya waliyo yatenda. Kisha Sura ikaingia kuwaamrisha Waumini wajikinge nafsi zao na ahali zao na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Na ikabainisha kwamba haukubalii udhuru wa makafiri Siku ya Kiyama. Na inawataka Waumini watubu kweli kweli, na Mtume s.a.w. ende kupambana kwa Jihadi na makafiri na wanaafiki, na awe mgumu kwao. Na inakhitimisha kwa kupiga mifano kwamba wema wa waume hautazuia adhabu isiwafikie wake zao wakiwa wao wamepotoka, na kwamba uharibifu wa waume hauwadhuru wake zao ikiwa hao wake wamesimama sawa sawa.  Kwani kila nafsi ina dhamana kwa vitendo vyake mwenyewe.

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكَ ۖ تَبْتَغِي مَرْضَاتَ أَزْوَاجِكَ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١﴾

1. Ee Nabii! Kwa nini unaharamisha kile Alichokuhalalishia Allaah? Unataka kuwaridhisha wake zako; na Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).

قَدْ فَرَضَ اللَّـهُ لَكُمْ تَحِلَّةَ أَيْمَانِكُمْ ۚ وَاللَّـهُ مَوْلَاكُمْ ۖ وَهُوَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ ﴿٢﴾

2. Allaah Amekwishakufaridhishieni (nyinyi Waislamu Shari’ah) ya kufungua viapo vyenu, na Allaah ni Mawlaa wenu Naye Ndiye Al-‘Aliymul-Hakiym (Mjuzi wa yote daima - Mwenye hikmah wa yote daima).

وَإِذْ أَسَرَّ النَّبِيُّ إِلَىٰ بَعْضِ أَزْوَاجِهِ حَدِيثًا فَلَمَّا نَبَّأَتْ بِهِ وَأَظْهَرَهُ اللَّـهُ عَلَيْهِ عَرَّفَ بَعْضَهُ وَأَعْرَضَ عَن بَعْضٍ ۖ فَلَمَّا نَبَّأَهَا بِهِ قَالَتْ مَنْ أَنبَأَكَ هَـٰذَا ۖ قَالَ نَبَّأَنِيَ الْعَلِيمُ الْخَبِيرُ ﴿٣﴾

3. Na (pale) Nabii alipotoa hadiyth ya siri kwa mmoja wa wake zake, na (huyo mke) alipoijulisha (alipoivujisha hiyo hadiyth), na Allaah Akamdhihirishia (Mtume صلى الله عليه وآله وسلم), akaijulisha baadhi yake na akaacha nyingine. Basi alipomjulisha (huyo mkewe aliyevujisha siri) akasema: “Nani aliyekujulisha haya?” (Mtume صلى الله عليه وآله وسلم), Akasema: “Amenijulisha Al-‘Aliymul-Khabiyr (Mjuzi wa yote daima - Mjuzi wa vilivyodhahiri na vilivyofichikana).”

إِن تَتُوبَا إِلَى اللَّـهِ فَقَدْ صَغَتْ قُلُوبُكُمَا ۖ وَإِن تَظَاهَرَا عَلَيْهِ فَإِنَّ اللَّـهَ هُوَ مَوْلَاهُ وَجِبْرِيلُ وَصَالِحُ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَالْمَلَائِكَةُ بَعْدَ ذَٰلِكَ ظَهِيرٌ ﴿٤﴾

4. Ikiwa nyinyi wawili mtatubia kwa Allaah (ni kheri kwenu) kwani kwa hakika nyoyo zenu zimeelemea (kupotoka). Na mkisaidiana dhidi yake, basi hakika Allaah Ndiye Mawlaa wake na Jibriyl na Waumini wema, na zaidi ya hayo, Malaika pia watasaidia.

عَسَىٰ رَبُّهُ إِن طَلَّقَكُنَّ أَن يُبْدِلَهُ أَزْوَاجًا خَيْرًا مِّنكُنَّ مُسْلِمَاتٍ مُّؤْمِنَاتٍ قَانِتَاتٍ تَائِبَاتٍ عَابِدَاتٍ سَائِحَاتٍ ثَيِّبَاتٍ وَأَبْكَارًا ﴿٥﴾

5. Akikutalikini, huenda Rabb (Mola) Wake Akambadilishia wake bora kuliko nyinyi; Muslimaat (Waislamu), Muuminaat (Waumini), Qaanitaat (watiifu), Taaibaat (wanaotubia), ‘Aabidaat (wenye kufanya ‘ibaadah), Saaihaat (wanaotembea huku na kule kwa ajili ya njia ya Allaah au wanaofunga Swawm) Thayyibaat (wajane), na Abkaar (bikra).

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَّا يَعْصُونَ اللَّـهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ ﴿٦﴾

6. Enyi mlioamini! Jikingeni nafsi zenu na ahli zenu na Moto (ambao) mafuta (kuni) yake ni watu na mawe; juu yake wako Malaika washupavu, shadidi hawamuasi Allaah kwa yale Anayowaamrisha na wanafanya yale wanayoamrishwa.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ كَفَرُوا لَا تَعْتَذِرُوا الْيَوْمَ ۖ إِنَّمَا تُجْزَوْنَ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٧﴾

7. Enyi mliokufuru! Msitoe nyudhuru Leo! Hakika mtalipwa yake mliyokuwa mkiyafanya.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّـهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يُكَفِّرَ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَيُدْخِلَكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ يَوْمَ لَا يُخْزِي اللَّـهُ النَّبِيَّ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ ۖ نُورُهُمْ يَسْعَىٰ بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَبِأَيْمَانِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَتْمِمْ لَنَا نُورَنَا وَاغْفِرْ لَنَا ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٨﴾

8. Enyi mlioamini! Tubieni kwa Allaah tawbah ya kwelikweli; huenda Rabb (Mola) wenu Akakufutieni maovu yenu, na Akakuingizeni Jannaat zipitazo chini yake mito. Siku ambayo Allaah Hatomfedhehesha Nabii (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)  na wale walioamini pamoja naye. Nuru yao itatembea mbele yao na kuliani mwao, watasema: “Rabb wetu! Tutimizie Nuru yetu, na Tughufurie, hakika Wewe juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza).

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ جَاهِدِ الْكُفَّارَ وَالْمُنَافِقِينَ وَاغْلُظْ عَلَيْهِمْ ۚ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿٩﴾

9. Ee Nabii! Pambana jihaad na makafiri na wanafiki na kuwa mshupavu kwao, na makazi yao ni (Moto wa) Jahannam, (napo ni) mahali pabaya mno pa kuishia.

ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا لِّلَّذِينَ كَفَرُوا امْرَأَتَ نُوحٍ وَامْرَأَتَ لُوطٍ ۖ كَانَتَا تَحْتَ عَبْدَيْنِ مِنْ عِبَادِنَا صَالِحَيْنِ فَخَانَتَاهُمَا فَلَمْ يُغْنِيَا عَنْهُمَا مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا وَقِيلَ ادْخُلَا النَّارَ مَعَ الدَّاخِلِينَ ﴿١٠﴾

10. Allaah Amewapigia mfano wale waliokufuru; mke wa Nuwh na mke wa Luwtw. Wote wawili walikuwa chini ya waja wawili miongoni mwa waja Wetu wema; wakawafanyia hiana, basi (Manabii hao wawili) hawakuwafaa chochote mbele ya Allaah, na ikasemwa: “Ingieni Motoni pamoja na wenye kuingia

وَضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا لِّلَّذِينَ آمَنُوا امْرَأَتَ فِرْعَوْنَ إِذْ قَالَتْ رَبِّ ابْنِ لِي عِندَكَ بَيْتًا فِي الْجَنَّةِ وَنَجِّنِي مِن فِرْعَوْنَ وَعَمَلِهِ وَنَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿١١﴾

11. Na (pia) Allaah Amewapigia mfano wale walioamini; mke wa Fir’awn, aliposema: “Rabb (Mola) wangu! Nijengee nyuma Kwako kwenye Jannah na niokoe na Fir’awn na vitendo vyake na niokoe na watu madhalimu.”

وَمَرْيَمَ ابْنَتَ عِمْرَانَ الَّتِي أَحْصَنَتْ فَرْجَهَا فَنَفَخْنَا فِيهِ مِن رُّوحِنَا وَصَدَّقَتْ بِكَلِمَاتِ رَبِّهَا وَكُتُبِهِ وَكَانَتْ مِنَ الْقَانِتِينَ ﴿١٢﴾

12. Na Maryam binti wa ‘Imraan ambaye amehifadhi tupu yake, Tukampulizia humo kutoka Roho Yetu, na akasadikisha Maneno ya Rabb (Mola) wake, na Vitabu Vyake, na akawa miongoni mwa Al-Qaanitiyn (watiifu).


 

[1] Kumwambia mke: wewe kwangu sawa na mgongo wa mama yangu na na kuwapelekea kujitenga na kutowajimai
[2] Kumdhukuru Allaah kwa kila aina; kukumbuka Utukufu Wake, neema Zake, ihsani Yake kwa kutaja jina Lake; kumsabbih, kumpwekesha, kumshukuru, kumsifu, kumtukuza, kuomba maghfirah, kusoma Qu-raan, kumswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), na kwa kuzingatia na kuyataamali Majina Yake Matukufu.

[3] Kumdhukuru Allaah kwa kila aina; kukumbuka Utukufu Wake, neema Zake, ihsani Yake kwa kutaja jina Lake; kumsabbih, kumpwekesha, kumshukuru, kumsifu, kumtukuza, kuomba maghfirah, kusoma Qu-raan, kumswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), na kwa kuzingatia na kuyataamali Majina Yake Matukufu.

[4] Kumdhukuru Allaah kwa kila aina; kukumbuka Utukufu Wake, neema Zake, ihsani Yake kwa kutaja jina Lake; kumsabbih, kumpwekesha, kumshukuru, kumsifu, kumtukuza, kuomba maghfirah, kusoma Qu-raan, kumswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), na kwa kuzi




Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com