Hadiyth
Ya 44
Ninayempenda
Zaidi Ni Lofa, Mwenye Swalah Nyingi, Ananiabudu Kwa Siri, Si Maarufu,
Anastahmili Hali Ya Uduni
عَنْ
أَبِي أُمَامَةَ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((إِنَّ أَغْبَطَ أَوْلِيَائِي عِنْدِي لَمُؤْمِنٌ
خَفِيفُ الْحَاذِ ذُو حَظٍّ مِنْ الصَّلَاةِ أَحْسَنَ عِبَادَةَ رَبِّهِ
وَأَطَاعَهُ فِي السِّرِّ وَكَانَ غَامِضًا فِي النَّاسِ لَا يُشَارُ إِلَيْهِ
بِالْأَصَابِعِ وَكَانَ رِزْقُهُ كَفَافًا فَصَبَرَ عَلَى ذَلِكَ)) ثُمَّ نَقَرَ بِيَدِهِ
فَقَالَ: ((عُجِّلَتْ مَنِيَّتُهُ قَلَّتْ
بَوَاكِيهِ قَلَّ تُرَاثُهُ)) الترمذي
(وكذلك أحمد وابن ماجه ) وإسناده حسن
Kutoka kwa
Abu Umaamah رضي الله عنه kwambe Mtume صلى الله عليه وسلم amesema: (([Allah Amesema}] Kwa kweli katika
wale wanaoniabudu, Ninayempenda zaidi ni yule muuminu lofa, mwenye Swalah
nyingi mwenye kujitahidi kumuabudu Mola wake kwa siri (bila ya kujionyesha kwa
watu), ambaye si maarufu kwa watu, na wala hatajiki, na ambaye hali yake ya
maisha ni duni lakini anaistahamili hali hiyo)) Tena hapo صلى الله عليه وسلم
akasema: ((Kama mauti yangekuwa mapema kwake asingekuwa na watu wengi wa
kumlilia, na urithi wake ungelikuwa mdogo sana)) [ At-Tirmidhiy
(vilevile Ahmad na Ibn Maajah) Mapokezi
yake ni mazuri]