007 - Hadiyth Ya 7: Kumwamini Allaah Na Kuwa Na Istiqaamah عَنْ أبي عَمْرَةَ سُفْيَانَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ (رضي الله عنه) قَالَ: قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ قُلْ لِي فِي الإسْلاَمِ قَوْلاً لاَ أَسْأَلُ عَنْهُ أَحَدًا غَيْرَكَ)) قَالَ: ((قُلْ آمَنْتُ بِاللَّهِ ثُمَّ َاسْتَقِمْ)) رواه مسلم Imepokelewa kutoka kwa Abu ‘Amrah Sufyaan bin ‘Abdillaah (رضي الله عنه) amesema: Nilisema: “Ee Mjumbe wa Allaah! Niambie neno katika Uislamu ambalo sitomuuliza yeyote badala yako”. Akasema: ((Sema: Nimemwamini Allaah kisha uwe na istiqaamah [msimamo])).[1] Mafunzo Na Hidaaya: Hadiyth hii ni miongoni mwa ‘Jawaami’ul-Kalim’ (Mjumuisho wa maana nyingi katika maneno machache) aliyopewa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) unaohusiana na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى). [Fusw-swilat 41: 30-32]. إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ. أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ خَالِدِينَ فِيهَا جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ Hakika wale waliosema: “Mola wetu ni Allaah,” kisha wakanyooka (kuthibitisha Tawhiyd na taqwa), basi hakutokuwa na khofu juu yao, na wala hawatohuzunika. Hao ndio watu wa Jannah, watadumu humo milele, jazaa kwa yale waliyokuwa wakitenda[2] Umuhimu wa tawhiyd, kumpwekesha Allaah bila ya kumshirikisha [Al-An’aam 6: 102, Al-Baqarah 2: 163, Twaahaa 20: 14, Al-Qaswas 28: 88, Ghaafir 41: 65]. [Rejea Hadiyth namba 11]. Kuwa na msimamo kunapeleka kufikia cheo cha juu na ukamilifu wa Iymaan. Amesema ‘Umar bin al-Khattwaab(رضي الله عنه) : Istiqaamah ni kutekeleza amri na kuacha yaliyokatazwa, wala msimili na kugeuka geuka mgeuko wa fisi. Hii inaashiria kuwa Istiqaamah ina fadhila kubwa mpaka imekuja baada tu ya Iymaan. Na bila shaka Iymaan yenyewe haiwezi kusimama bila ya Istiqaamah. [1] Muslim. [2] Al-Ahqaaf (46: 13-14).

007 - Hadiyth Ya 7: Kumwamini Allaah Na Kuwa Na Istiqaamah


عَنْ أبي عَمْرَةَ سُفْيَانَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ (رضي الله عنه)  قَالَ: قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ قُلْ لِي فِي الإسْلاَمِ قَوْلاً لاَ أَسْأَلُ عَنْهُ أَحَدًا غَيْرَكَ)) قَالَ:  ((قُلْ آمَنْتُ بِاللَّهِ  ثُمَّ َاسْتَقِمْ)) رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abu ‘Amrah Sufyaan bin ‘Abdillaah (رضي الله عنه) amesema: Nilisema: “Ee Mjumbe wa Allaah! Niambie neno katika Uislamu ambalo sitomuuliza yeyote badala yako”. Akasema: ((Sema: Nimemwamini Allaah kisha uwe na istiqaamah [msimamo])).[1]
 
Mafunzo Na Hidaaya:
 
  1. Hadiyth hii ni miongoni mwa ‘Jawaami’ul-Kalim’ (Mjumuisho wa maana nyingi katika maneno machache) aliyopewa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) unaohusiana na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى). [Fusw-swilat 41: 30-32].
 
إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ. أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ خَالِدِينَ فِيهَا جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ
Hakika wale waliosema: “Mola wetu ni Allaah,” kisha wakanyooka (kuthibitisha Tawhiyd na taqwa), basi hakutokuwa na khofu juu yao, na wala hawatohuzunika.  Hao ndio watu wa Jannah, watadumu humo milele, jazaa kwa yale waliyokuwa wakitenda[2]
 
  1. Umuhimu wa tawhiyd, kumpwekesha Allaah bila ya kumshirikisha [Al-An’aam 6: 102, Al-Baqarah 2: 163, Twaahaa 20: 14, Al-Qaswas 28: 88, Ghaafir 41: 65]. [Rejea Hadiyth namba 11].
 
  1. Kuwa na msimamo kunapeleka kufikia cheo cha juu na ukamilifu wa Iymaan.
 
  1. Amesema ‘Umar bin al-Khattwaab(رضي الله عنه) : Istiqaamah ni kutekeleza amri na kuacha yaliyokatazwa, wala msimili na kugeuka geuka mgeuko wa fisi.
 
  1. Hii inaashiria kuwa Istiqaamah ina fadhila kubwa mpaka imekuja baada tu ya Iymaan. Na bila shaka Iymaan yenyewe haiwezi kusimama bila ya Istiqaamah.



[1] Muslim.
[2] Al-Ahqaaf (46: 13-14).