Al-Mujaadalah (58)

سُورَةُ  الْمُجَادلَة
Al-Mujaadalah (58)

(Imeteremka Madina)


Sura imeanza kwa kueleza khabari za mwanamke anaye tengwa na mumewe, na ikafuatia kubainisha hukumu za kutengana. Na Mwenyezi Mungu katika sura hii katika zaidi ya Aya moja amewatia makosani wanao ifanyia uadui Dini yake, na amewahadharisha na kunong'ona nong'ona kwa ajili ya madhambi na uadui. Na amewaongoza Waumini juu ya adabu za kunong'ona baina yao kwa wao, na baina yao na Mtume s.a.w. Kama vile vile alivyo watia makosani wanaafiki kwa kushirikiana na makafiri, na akawaeleza kuwa hao ni kundi la Shetani lenye kuingia khasarani.
Na Sura ikakhitimisha kwa kueleza kwa jumla yaliyo ya waajibu juu ya  Waumini ya kupendelea kumridhi Mwenyezi Mungu na Mtume wake kuliko wengine wasio kuwa wao, hata wangeli kuwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Na akawasifu Waumini hao kuwa ni Hizbu-Llahi, Kundi la Mwenyezi Mungu, lenye kufanikiwa.
 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

قَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّتِي تُجَادِلُكَ فِي زَوْجِهَا وَتَشْتَكِي إِلَى اللَّـهِ وَاللَّـهُ يَسْمَعُ تَحَاوُرَكُمَا ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ ﴿١﴾

1. Allaah Amekwishasikia kauli ya yule (mwanamke) anayejadiliana nawe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu mumewe, na anamshitakia Allaah; na Allaah Anayasikia majibizano yenu. Hakika Allaah ni Samiy’um-Baswiyr (Mwenye kusikia yote daima - Mwenye kuona yote daima).

الَّذِينَ يُظَاهِرُونَ مِنكُم مِّن نِّسَائِهِم مَّا هُنَّ أُمَّهَاتِهِمْ ۖ إِنْ أُمَّهَاتُهُمْ إِلَّا اللَّائِي وَلَدْنَهُمْ ۚ وَإِنَّهُمْ لَيَقُولُونَ مُنكَرًا مِّنَ الْقَوْلِ وَزُورًا ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ لَعَفُوٌّ غَفُورٌ ﴿٢﴾

2. Wale wanaotamka dhwihaar[1] miongoni mwenu kwa wake zao, hao (wake zao) si mama zao. Hawakuwa mama zao isipokuwa wale waliowazaa. Na hakika wao bila shaka wanasema kauli ya kuchukiza katika kauli na uongo. Na hakika Allaah bila shaka ni ‘Afuwun-Ghafuwr (Mwenye kusamehe - Mwingi wa kughufuria).

وَالَّذِينَ يُظَاهِرُونَ مِن نِّسَائِهِمْ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا قَالُوا فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مِّن قَبْلِ أَن يَتَمَاسَّا ۚ ذَٰلِكُمْ تُوعَظُونَ بِهِ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿٣﴾

3. Na wale wanaotamka dhwihaar kwa wake zao, kisha wakarudi katika waliyoyasema (wakaitengua kauli yao ya dhwihaar), basi (kafara yao ni) kuacha huru mtumwa kabla ya kugusana. Hivyo kwenu mnawaidhiwa kwayo (ili msirudie jambo) hilo. Na Allaah kwa yale myatendayo ni Khabiyr (Mjuzi wa vilivyodhahiri na vilivyofichikana).

فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ مِن قَبْلِ أَن يَتَمَاسَّا ۖ فَمَن لَّمْ يَسْتَطِعْ فَإِطْعَامُ سِتِّينَ مِسْكِينًا ۚ ذَٰلِكَ لِتُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۚ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ ۗ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٤﴾

4. Na yule asiyepata (mtumwa), basi (afunge) Swawm miezi miwili mfululuzo kabla ya kugusana. Na yule asiyeweza, basi alishe chakula masikini sitini. Hivyo ili mumuamini Allaah na Rasuli Wake. Na hiyo ni mipaka ya Allaah. Na makafiri watapata adhabu iumizayo.

إِنَّ الَّذِينَ يُحَادُّونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ كُبِتُوا كَمَا كُبِتَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ وَقَدْ أَنزَلْنَا آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ ۚ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿٥﴾

5. Hakika wale wanaopinzana na Allaah na Rasuli Wake wamefedheheshwa kama walivyofedheheshwa wale wa kabla yao. Na Tumekwishateremsha Aayaat bayana, na makafiri watapata adhabu ya kudhalilisha.

يَوْمَ يَبْعَثُهُمُ اللَّـهُ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوا ۚ أَحْصَاهُ اللَّـهُ وَنَسُوهُ ۚ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿٦﴾

6. Siku Atakayowafufua Allaah wote, Awajulishe yale (yote) waliyoyatenda, Allaah Ameyadhibiti nao wameyasahau; na Allaah juu ya kila kitu ni Shahiyd (Mwenye kushuhudia).

أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَىٰ ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ وَلَا خَمْسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمْ وَلَا أَدْنَىٰ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمْ أَيْنَ مَا كَانُوا ۖ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٧﴾

7. Je, huoni kwamba Allaah Anajua yale (yote) yaliyomo mbinguni na yale (yote) yaliyomo ardhini? Hauwi mnong’ono wa (watu) watatu isipokuwa Yeye ni wa nne wao (kwa ujuzi Wake), na wala (hauwi mnong’ono wa) watano isipokuwa Yeye ni wa sita wao (kwa ujuzi Wake), na wala (hauwi mnong’ono wa) chini (kuliko) ya hivyo, na wala (wa) wengi zaidi isipokuwa Yeye Yu pamoja nao (kwa ujuzi Wake) popote watakapokuwa; kisha Atawajulisha kwa yale (yote) waliyoyatenda Siku ya Qiyaamah. Hakika Allaah kwa kila kitu ni ‘Aliym (Mjuzi).

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ نُهُوا عَنِ النَّجْوَىٰ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا نُهُوا عَنْهُ وَيَتَنَاجَوْنَ بِالْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَمَعْصِيَتِ الرَّسُولِ وَإِذَا جَاءُوكَ حَيَّوْكَ بِمَا لَمْ يُحَيِّكَ بِهِ اللَّـهُ وَيَقُولُونَ فِي أَنفُسِهِمْ لَوْلَا يُعَذِّبُنَا اللَّـهُ بِمَا نَقُولُ ۚ حَسْبُهُمْ جَهَنَّمُ يَصْلَوْنَهَا ۖ فَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿٨﴾

8. Je, huwaoni wale waliokatazwa kunong’ona, kisha wanarudia yale waliyokatazwa nayo, na wananong’onezana kwa (mambo yanayohusu) dhambi na uadui na kumuasi Rasuli na wanapokujia wanakuamkia kwa (maamkizi) Asiyokuamkia kwayo Allaah; na wanasema katika nafsi zao: “Mbona Allaah Hatuadhibu kwa yale tunayoyasema?” (Moto wa) Jahannam unawatosheleza, watauingia waungue, na pabaya mno mahali pa kuishia mwishoni.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا تَنَاجَيْتُمْ فَلَا تَتَنَاجَوْا بِالْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَمَعْصِيَتِ الرَّسُولِ وَتَنَاجَوْا بِالْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٩﴾

9. Enyi mlioamini! Mnaponong’onezana, basi msinong’onezane kwa (mambo yanayohusu) dhambi na uadui na kumuasi Rasuli (lakini) nong’onezaneni kwa (mambo yanayohusu) wema na taqwa; na mcheni Allaah Ambaye Kwake Pekee mtakusanywa (nyote).

إِنَّمَا النَّجْوَىٰ مِنَ الشَّيْطَانِ لِيَحْزُنَ الَّذِينَ آمَنُوا وَلَيْسَ بِضَارِّهِمْ شَيْئًا إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١٠﴾

10. Hakika mnong’ono ni kutoka kwa shaytwaan ili awahuzunishe wale walioamini, na wala hawezi kuwadhuru chochote isipokuwa kwa idhini ya Allaah. Na kwa Allaah (Pekee) watawakali Waumini.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قِيلَ لَكُمْ تَفَسَّحُوا فِي الْمَجَالِسِ فَافْسَحُوا يَفْسَحِ اللَّـهُ لَكُمْ ۖ وَإِذَا قِيلَ انشُزُوا فَانشُزُوا يَرْفَعِ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَالَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ دَرَجَاتٍ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿١١﴾

11. Enyi mlioamini! Mnapoambiwa: “Fanyeni nafasi katika majlisi,” basi (sogeeni) mfanye nafasi; Allaah Atakufanyieni nafasi. Na mnapoambiwa: “Inukeni,” basi inukeni; Allaah Atawainua wale walioamini miongoni mwenu na waliopewa elimu daraja za juu. Na Allaah kwa yale myatendayo ni Khabiyr (Mjuzi wa vilivyodhahiri na vilivyofichikana).

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نَاجَيْتُمُ الرَّسُولَ فَقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيْ نَجْوَاكُمْ صَدَقَةً ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ لَّكُمْ وَأَطْهَرُ ۚ فَإِن لَّمْ تَجِدُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٢﴾

12. Enyi mlioamini! Mnapotaka kunong’ona (kushauriana kwa siri na)   Rasuli basi kadimisheni swadaqah kabla ya mnong’ono wenu. Hivyo ni kheri kwenu na (ni) utakaso zaidi. Na msipopata, basi hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).

أَأَشْفَقْتُمْ أَن تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيْ نَجْوَاكُمْ صَدَقَاتٍ ۚ فَإِذْ لَمْ تَفْعَلُوا وَتَابَ اللَّـهُ عَلَيْكُمْ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ وَاللَّـهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ ﴿١٣﴾

13. Je, mnaogopa kukadimisha swadaqah kabla ya mnong’ono wenu? Ikiwa hamjafanya na Allaah Akapokea tawbah yenu; basi simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah, na mtiini Allaah na Rasuli Wake; na Allaah ni Khabiyr (Mjuzi wa vilivyodhahiri na vilivyofichikana) kwa myatendayo

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ تَوَلَّوْا قَوْمًا غَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مَّا هُم مِّنكُمْ وَلَا مِنْهُمْ وَيَحْلِفُونَ عَلَى الْكَذِبِ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿١٤﴾

14. Je, huwaoni wale waliofanya urafiki na watu (ambao) Allaah Ameghadhibika nao, wao si miongoni mwenu (ni wanafiki), na wala si miongoni mwao (ni unafiki tu). Na wanaapia uongo, nao wanajua (kuwa ni uongo).


أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا ۖ إِنَّهُمْ سَاءَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٥﴾

15. Allaah Amewaandalia adhabu kali, hakika waliyokuwa wakiyatenda ni maovu mno.

اتَّخَذُوا أَيْمَانَهُمْ جُنَّةً فَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ فَلَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿١٦﴾

16. Wamechukua viapo vyao (vya uongo) kuwa ni kinga (ya vitendo vyao), (hivyo) wakazuia (watu) njia ya Allaah, basi watapa adhabu idhalilishayo.


لَّن تُغْنِيَ عَنْهُمْ أَمْوَالُهُمْ وَلَا أَوْلَادُهُم مِّنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۚ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿١٧﴾

17. Hazitowafaa kitu chochote mali zao na wala auladi wao mbele ya Allaah, hao ni watu wa Motoni, wao humo ni wenye kudumu.

يَوْمَ يَبْعَثُهُمُ اللَّـهُ جَمِيعًا فَيَحْلِفُونَ لَهُ كَمَا يَحْلِفُونَ لَكُمْ ۖ وَيَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ عَلَىٰ شَيْءٍ ۚ أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ الْكَاذِبُونَ ﴿١٨﴾

18. Siku Atakayowafufua Allaah wote, watamwapia kama wanavyokuapieni nyinyi, na watadhania kwamba wamesimamia juu ya kitu (hoja). Tanabahi!  Hakika wao ni waongo.

اسْتَحْوَذَ عَلَيْهِمُ الشَّيْطَانُ فَأَنسَاهُمْ ذِكْرَ اللَّـهِ ۚ أُولَـٰئِكَ حِزْبُ الشَّيْطَانِ ۚ أَلَا إِنَّ حِزْبَ الشَّيْطَانِ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿١٩﴾

19. Shaytwaan amewatawala, akawasahaulisha dhikri[2] ya Allaah, hao ndio kundi la shaytwaan. Tanabahi! Hakika kundi la shaytwaan ndio lenye kukhasirika.

إِنَّ الَّذِينَ يُحَادُّونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ أُولَـٰئِكَ فِي الْأَذَلِّينَ ﴿٢٠﴾

20. Hakika wale wanaopinzana na Allaah na Rasuli Wake hao ndio kati ya (wale) waliodhalilishwa.

كَتَبَ اللَّـهُ لَأَغْلِبَنَّ أَنَا وَرُسُلِي ۚ إِنَّ اللَّـهَ قَوِيٌّ عَزِيزٌ ﴿٢١﴾

21. Allaah Amekwishaandika kwamba: “Bila shaka Nitashinda Mimi na Rasuli Wangu.”  Hakika Allaah ni Qawiyyun-‘Aziyz (Mwenye nguvu zote daima - Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima).

لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ ۚ أُولَـٰئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ الْإِيمَانَ وَأَيَّدَهُم بِرُوحٍ مِّنْهُ ۖ وَيُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ رَضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ۚ أُولَـٰئِكَ حِزْبُ اللَّـهِ ۚ أَلَا إِنَّ حِزْبَ اللَّـهِ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٢٢﴾

22. Hutokuta watu wanaomuamini Allaah na Siku ya Mwisho (kuwa) wanawapenda wale wanaopinzana na Allaah na Rasuli Wake, japo wakiwa (ni) baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao (Allaah) Amewaandikia katika nyoyo zao iymaan, na Akawatia nguvu kwa Roho kutoka Kwake, na Atawaingiza Jannaat zipitazo chini yake mito ni wenye kudumu humo. Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Hao ndio kundi la Allaah. Tanabahi! Hakika kundi la Allaah ndio lenye kufaulu.



Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com