Al-Mutwaffifiyn (83)

سُورَةُ  الْمُطَفِّفِين
Al-Mutwaffifiyn (83)

(Imeteremka Makka)

 
Imeanzia Sura hii kwa onyo kali kwa huyo anaye jipimia mwenyewe sawa na akampimia mtu mwingine kwa upungufu; na ikaeleza hayo kwa wayatendayo watu katika kutaka watimiziwe haki zao katika vipimo na mizani, na ikaonya mtindo kama huo kwa kuwa ipo Siku ya Hisabu, na ikathibitisha kuwa vitendo vyao vimedhibitiwa katika daftari la hisabu, ambalo halimkadhibishi ila mwenye kupindukia mipaka, mwenye dhambi aliye zuiliwa na rehema za Mola wake Mlezi, na mwisho wake ni Jahannamu.
Tena Aya zikawageukia watu wema, zikawatuza nyoyo kwa vitendo vyao, na zikataja neema zao na alama zao, zikiashiria namna moja wapo katika neema hizo, na kwa ajili ya hizo washindanie wanao shindana. Na Aya zikaeleza walio kuwa wakiyafanya makafiri wakosefu kuwafanyia Waumini wanapo waona, au wanapo kuwa Waumini wanapita mbele yao. Na Sura ikakhitimisha kwa kuwatuliza Waumini kwamba Siku ya Kiyama itawafanyia insafu, wao watakuwa katika neema wakiwacheka makafiri, nao wamekaa juu ya makochi wakiwaangalia, na makafiri watalipwa kwa waliyo kuwa wakiyatenda.


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

وَيْلٌ لِّلْمُطَفِّفِينَ ﴿١﴾

1. Ole kwa wanaopunja.


الَّذِينَ إِذَا اكْتَالُوا عَلَى النَّاسِ يَسْتَوْفُونَ ﴿٢﴾

2. Ambao wanapojipimia kwa watu (wanataka) wapimiwe kamilifu.

وَإِذَا كَالُوهُمْ أَو وَّزَنُوهُمْ يُخْسِرُونَ ﴿٣﴾

3. (Lakini) Wanapowapimia (watu kwa kipimo cha pishi na vyenye kufanana nacho) au kwa mizani (wao) wanapunguza (wanapunja).

أَلَا يَظُنُّ أُولَـٰئِكَ أَنَّهُم مَّبْعُوثُونَ ﴿٤﴾

4. Je, hawadhanii kwamba wao watafufuliwa?

لِيَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿٥﴾

5. Kwenye siku iliyo kuu.

يَوْمَ يَقُومُ النَّاسُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٦﴾

6. Siku watakayosimama watu kwa Rabb (Mola) wa walimwengu.

كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْفُجَّارِ لَفِي سِجِّينٍ ﴿٧﴾

7. Hapana! Hakika kitabu cha waovu bila shaka kimo katika Sijjiyn.

وَمَا أَدْرَاكَ مَا سِجِّينٌ ﴿٨﴾

8. Na lipi litakalokujulisha nini hiyo Sijjiyn?

كِتَابٌ مَّرْقُومٌ ﴿٩﴾

9. (Ni) Kitabu kiloandikwa (matendo).

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿١٠﴾

10. Ole siku hiyo kwa wakadhibishaji.

الَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ ﴿١١﴾

11. Ambao wanaikadhibisha siku ya Malipo.

وَمَا يُكَذِّبُ بِهِ إِلَّا كُلُّ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ ﴿١٢﴾

12. Na haikadhibishi isipokuwa kila mwenye kuruka mipaka, mtendaji dhambi.

إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ آيَاتُنَا قَالَ أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ ﴿١٣﴾

13. Anaposomewa Aayaat Zetu, husema: “Simulizi za (watu) wa kale.”

كَلَّا ۖ بَلْ ۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿١٤﴾

14. Hapana! Bali imefanya kutu juu ya nyoyo zao yale (maovu) waliyokuwa wakiyachuma.

كَلَّا إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّمَحْجُوبُونَ ﴿١٥﴾

15. Hapana! Hakika wao siku hiyo watawekewa kizuizi (wasimuone) Rabb (Mola) wao.

ثُمَّ إِنَّهُمْ لَصَالُو الْجَحِيمِ ﴿١٦﴾

16. Kisha hakika wao bila shaka wataingizwa na waungue katika (Moto wa) Al-Jahiym.

ثُمَّ يُقَالُ هَـٰذَا الَّذِي كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ ﴿١٧﴾

17. Kisha itasemwa: “Haya ndio yale mliyokuwa mkiyakadhibisha.”

كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْأَبْرَارِ لَفِي عِلِّيِّينَ ﴿١٨﴾

18. Hapana! Hakika kitabu cha Al-Abraar (wafanyao wema) bila shaka kiko katika ‘Illiyyiyn.


وَمَا أَدْرَاكَ مَا عِلِّيُّونَ ﴿١٩﴾

19. Na lipi litakalokujulisha nini hiyo ‘Illiyyiyn?

كِتَابٌ مَّرْقُومٌ ﴿٢٠﴾

20. (Ni) Kitabu kilichoandikwa (matendo).

يَشْهَدُهُ الْمُقَرَّبُونَ ﴿٢١﴾

21. Watakishuhudia waliokurubishwa (kwa Allaah).

إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ ﴿٢٢﴾

22. Hakika Al-Abraar bila shaka (watakuwa) kwenye neema.

عَلَى الْأَرَائِكِ يَنظُرُونَ ﴿٢٣﴾

23. Kwenye makochi (ya fakhari) wakitazama.

تَعْرِفُ فِي وُجُوهِهِمْ نَضْرَةَ النَّعِيمِ ﴿٢٤﴾
24. Utatambua nyuso zao kwa kunawiri.

يُسْقَوْنَ مِن رَّحِيقٍ مَّخْتُومٍ ﴿٢٥﴾

25. Watanyweshwa kinywaji safi cha mvinyo kilichotiwa muhuri.

خِتَامُهُ مِسْكٌ ۚ وَفِي ذَٰلِكَ فَلْيَتَنَافَسِ الْمُتَنَافِسُونَ ﴿٢٦﴾

26. Mwisho wake ni Misk. Na katika hayo basi washindane wanaoshindana (kufanya mazuri).

وَمِزَاجُهُ مِن تَسْنِيمٍ ﴿٢٧﴾

27. Na mchanganyiko wake ni kutokana na Tasniym.

عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا الْمُقَرَّبُونَ ﴿٢٨﴾

28. (Ambayo ni) Chemchemu watakayokunywa humo watakaokurubishwa (kwa Allaah).

إِنَّ الَّذِينَ أَجْرَمُوا كَانُوا مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا يَضْحَكُونَ ﴿٢٩﴾

29. Hakika wale waliofanya uhalifu walikuwa (duniani) wakiwacheka wale walioamini.

وَإِذَا مَرُّوا بِهِمْ يَتَغَامَزُونَ ﴿٣٠﴾

30. Na wanapowapitia (karibu yao) wanakonyezana.

وَإِذَا انقَلَبُوا إِلَىٰ أَهْلِهِمُ انقَلَبُوا فَكِهِينَ ﴿٣١﴾

31. Na wanaporudi kwa ahli zao, hurudi (huku wakiwa) wenye kushangilia.

وَإِذَا رَأَوْهُمْ قَالُوا إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ لَضَالُّونَ ﴿٣٢﴾

32. Na wanapowaona, husema: “Hakika hawa bila shaka (yoyote ile) ndio (wale) waliopotea.”

وَمَا أُرْسِلُوا عَلَيْهِمْ حَافِظِينَ ﴿٣٣﴾

33. (Makafiri) hawakupelekwa kuwa ni walinzi juu yao.

فَالْيَوْمَ الَّذِينَ آمَنُوا مِنَ الْكُفَّارِ يَضْحَكُونَ ﴿٣٤﴾

34. Basi leo wale walioamini watawacheka makafiri.

عَلَى الْأَرَائِكِ يَنظُرُونَ ﴿٣٥﴾

35. Kwenye makochi (ya fakhari) wakitazama.

هَلْ ثُوِّبَ الْكُفَّارُ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ ﴿٣٦﴾

36. Je, basi makafiri (leo) wamelipwa (kikamilifu) yale waliyokuwa wakiyafanya?





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com