16. SUURAT AN NAH'L

 النَّحْل

16. SUURAT AN NAH'L

(Imeteremka Makka)


Sura hii ni ya Makka, isipo kuwa Aya tatu za mwisho. Hizo ni za Madina.  Idadi ya Aya zake ni mia na ishirini na nane. Sura hii tukufu imeanzia kutilia mkazo maonyo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwapa washirikina, na kubainisha uwezo wake Subhanahu wa Taa'la katika kutimiza ahadi hiyo, kwa dalili ya kuumba kwake mbingu na ardhi. Kisha kawabainishia watu wote kumuumba kwake ngamia, na kuotesha kwake makulima, na aliyo yaumba baharini, kama samaki wa kuliwa, na majohari ya mapambo. Kisha akaashiria yanayo wajibikia kwa neema hizo, nayo ni kumshukuru Subhanahu, na waajibu wa kumuabudu Yeye peke yake, na kuwakabili washirikina kwa kuwaita watambue Upweke wa Mwenyezi Mungu; na imetaja uzushi wa washirikina kuizulia Qur'ani Tukufu, na kudai kuwa hiyo ni hadithi za uwongo za kale. Kisha Subhanahu ameashiria adhabu ya washirikina Siku ya Kiyama na starehe za Waumini. Baadaye Subhanahu akataja kukanya kwa washirikina kukhusu kufufuliwa na kushikilia kwao kukanya. Naye Subhanahu anapinga ukafiri wao kwa kubainisha uwezo wake, na anatilia mkazo ahadi yake kwa wachamngu na vitisho vyake kwa makafiri. Kisha anakaribisha  kufufuliwa kwa kueleza uwezo wake juu yao, na kuwa viumbe vyote vinamnynyekea Yeye Aliye takasika, na anabainisha kuwa ni Yeye Subhanahu ndiye anaye kashifu. Na anabainisha upotovu wa washirikina katika itikadi yao kuamini vitu visivyo weza kuleta nafuu wala madhara, na uovu wa maoni yao kwa wanawake wote, watoto na watu wazima. Naye Subhanahu ameashiria khabari za Mitume walio tangulia, akataka tuuzingatie  uumbaji wake wa vitu na faida ziliomo ndani yake kwa ajili ya watu, na kutafautiana riziki, kuwa matajiri wanapewa zaidi kuliko masikini, na neema zake kwa watu kuwa wengine wanaume na wengine wanawake, na kuzaliana kwa kuoana. Naye Subhanahu akaingia kupiga mifano ili kueleza kudra yake. Kisha akataka watu waangalie vipi ubora wa kuumba unavyo onyesha ubora wa Mwenye kuumba na kuenea neema zake. Na vipi washirikina wanavyo zipinga neema hizi tukufu. Na baada ya kueleza matakwa ya Uislamu kuleta uadilifu, na kuunganisha udugu kwa kutimiza ahadi, na muujiza wa Qur'ani, na ukafiri wa washirikina kuikataa Qur'ani, na kuizulia uwongo, Aliye takasika ameashiria hali ya washirikina Siku ya Kiyama. Amebainisha vipi walivyo kuwa wakihalalisha na wakiharimisha bila ya hoja. Akaashiria vipi Mayahudi walivyo wakaribia washirikina, na akabainisha kuwa yapasa wasiadhibiwe isipo kuwa kwa kadiri ya walivyo tenda, na kuwa ni waajibu wa Waumini wasubiri, na washikamane na uchamngu na kufanya ihsani.
 



بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


أَتَىٰ أَمْرُ اللَّـهِ فَلَا تَسْتَعْجِلُوهُ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿١﴾
1. Amri ya Allaah (ya Qiyaamah) itafika tu basi msiihimize. Subhaanahu wa Ta’aala (Utakasifu ni Wake na Ametukuka kwa ‘Uluwa) kutokana na yale wanayomshirikisha nayo.


يُنَزِّلُ الْمَلَائِكَةَ بِالرُّوحِ مِنْ أَمْرِهِ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ أَنْ أَنذِرُوا أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاتَّقُونِ﴿٢﴾
2. Anateremsha Malaika na Ruwh (Wahy) kwa amri Yake (Allaah) juu ya Amtakaye miongoni mwa waja Wake, kwamba: “Onyeni: Hakika hapana ilaah (muabudiwa wa haki) ila Mimi basi Nicheni.


خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۚ تَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٣﴾
3.  Ameumba mbingu na ardhi kwa haki. Ta’aala (Ametukuka kwa Uluwa) kutokana na yale wanayomshirikisha nayo.


خَلَقَ الْإِنسَانَ مِن نُّطْفَةٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ مُّبِينٌ﴿٤﴾
4. Amemuumbainsani kutokana na tone la manii tahamaki yeye ni mbishani bayana.


وَالْأَنْعَامَ خَلَقَهَا ۗ لَكُمْ فِيهَا دِفْءٌ وَمَنَافِعُ وَمِنْهَا تَأْكُلُونَ﴿٥﴾
5. Na wanyama wa mifugo Amewaumba. Mnapata humo (vifaa vya kutia) vuguvugu (la joto) na manufaa (mengine) na mnakula humo (wengine).


وَلَكُمْ فِيهَا جَمَالٌ حِينَ تُرِيحُونَ وَحِينَ تَسْرَحُونَ﴿٦﴾
6. Na mnapata humo (raha ya) uzuri wakati wa mnaporudisha jioni na mnapopeleka machunganiasubuhi.


وَتَحْمِلُ أَثْقَالَكُمْ إِلَىٰ بَلَدٍ لَّمْ تَكُونُوا بَالِغِيهِ إِلَّا بِشِقِّ الْأَنفُسِ ۚ إِنَّ رَبَّكُمْ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿٧﴾
7. Na (wanyama hao) hubeba mizigo yenu kupeleke nchi msizoweza kuzifikia isipokuwa kwa mashaka ya nafsi. Hakika Rabb (Mola) wenu bila shaka ni Rauwfur-Rahiym (Mwenye huruma mno - Mwenye kurehemu).


وَالْخَيْلَ وَالْبِغَالَ وَالْحَمِيرَ لِتَرْكَبُوهَا وَزِينَةً ۚ وَيَخْلُقُ مَا لَا تَعْلَمُونَ﴿٨﴾
8. Na (Ameumba pia) farasi na baghala (nyumbu) na punda ili muwapande na wawe mapambo. Na Anaumba msivyovijua.


وَعَلَى اللَّـهِ قَصْدُ السَّبِيلِ وَمِنْهَا جَائِرٌ ۚ وَلَوْ شَاءَ لَهَدَاكُمْ أَجْمَعِينَ﴿٩﴾
9. Na juu ya Allaah kubainisha njia (iliyonyooka), na humo ziko miongoni mwazo za kupotoka. Na kama Angetaka Angekuongoeni nyote.


هُوَ الَّذِي أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً ۖ لَّكُم مِّنْهُ شَرَابٌ وَمِنْهُ شَجَرٌ فِيهِ تُسِيمُونَ﴿١٠﴾
10. Yeye Ndiye Yule Aliyeteremesha kutoka mbinguni maji, katika hayo mnapata kinywaji na kwa hayo (inatoa) miti ambayo humo mnalisha (wanyama).


يُنبِتُ لَكُم بِهِ الزَّرْعَ وَالزَّيْتُونَ وَالنَّخِيلَ وَالْأَعْنَابَ وَمِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴿١١﴾
11. Anakuotesheeni mimea kwayo (hayo maji) na mizaytuni na mitende na mizabibu na kila (aina ya) mazao. Hakika katika hayo (kuna) Aayah (ishara, dalili, hoja, zingatio n.k) kwa watu wanaotafakari.


وَسَخَّرَ لَكُمُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ ۖ وَالنُّجُومُ مُسَخَّرَاتٌ بِأَمْرِهِ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ﴿١٢﴾
12. Na Amekutiishieni usiku na mchana, na jua na mwezi, na nyota zinazotiishwa kwa amri Yake. Hakika katika hayo (kuna) Aayaat (ishara, dalili, n.k) kwa watu wanaotia akilini.


وَمَا ذَرَأَ لَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُخْتَلِفًا أَلْوَانُهُ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَذَّكَّرُونَ﴿١٣﴾
13. Na (Ametiisha pia) Alivyoviumba katika ardhi vya rangi tofauti. Hakika katika hayo ni Aayah (ishara, dalili, zingatio n.k) kwa watu wanaokumbuka.


وَهُوَ الَّذِي سَخَّرَ الْبَحْرَ لِتَأْكُلُوا مِنْهُ لَحْمًا طَرِيًّا وَتَسْتَخْرِجُوا مِنْهُ حِلْيَةً تَلْبَسُونَهَا وَتَرَى الْفُلْكَ مَوَاخِرَ فِيهِ وَلِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ﴿١٤﴾
14. Naye Ndiye Ambaye Ametiisha bahari ili mle humo kitoweo kipya (freshi), na mtoe humo mapambo mnayoyavaa (lulu, marijani n.k), na utaona merikebu zikipasua (maji) humo; (Amezitiisha) ili mtafute katika fadhila Zake, na ili mpate kushukuru.

وَأَلْقَىٰ فِي الْأَرْضِ رَوَاسِيَ أَن تَمِيدَ بِكُمْ وَأَنْهَارًا وَسُبُلًا لَّعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ﴿١٥﴾
15. Na Ameweka katika ardhi milima iliyosimama imara ili isiyumbeyumbe kwenu, na (Akaweka) mito na njia ili mpate kujiongoza.


وَعَلَامَاتٍ ۚ وَبِالنَّجْمِ هُمْ يَهْتَدُونَ﴿١٦﴾
16. Na alama za kutambulisha (njia), na kwa nyota wanaojiongoza (njia).


أَفَمَن يَخْلُقُ كَمَن لَّا يَخْلُقُ ۗ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ﴿١٧﴾
17. Je, yule Anayeumba (Naye ni Allaah) ni (sawa) kama asiyeumba? Je, basi hamkumbuki (na kuwaidhika?).


وَإِن تَعُدُّوا نِعْمَةَ اللَّـهِ لَا تُحْصُوهَا ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١٨﴾
18. Na mkihesabu neema za Allaah hamtoweza kuzihesabu (zote). Hakika Allaah bila shaka ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).


وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعْلِنُونَ﴿١٩﴾
19. Na Allaah Anajua mnayoyafanya siri na mnayoyadhihirisha.


وَالَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ لَا يَخْلُقُونَ شَيْئًا وَهُمْ يُخْلَقُونَ﴿٢٠﴾
20. Na wale wanaowaomba badala ya Allaah hawaumbi kitu chochote, bali wao wanaumbwa.


أَمْوَاتٌ غَيْرُ أَحْيَاءٍ ۖ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ﴿٢١﴾
21. Ni wafu si wahai; na hawatambui lini watafufuliwa.


إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۚ فَالَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ قُلُوبُهُم مُّنكِرَةٌ وَهُم مُّسْتَكْبِرُونَ﴿٢٢﴾
22. Ilaah (Muabudiwa wa haki) wenu ni Ilaah Mmoja (Pekee). Basi wale wasioamini Aakhirah nyoyo zao ni zenye kukanusha nao wanatakabari.


لَا جَرَمَ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْتَكْبِرِينَ﴿٢٣﴾
23. Hapana shaka kwamba Allaah Anajua wanayoyafanya siri na wanayayoyadhihirisha. Hakika Yeye Hapendi wanaotakabari.


وَإِذَا قِيلَ لَهُم مَّاذَا أَنزَلَ رَبُّكُمْ ۙ قَالُوا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ﴿٢٤﴾
24. Na (pale) wanapoambiwa: “Nini Ameteremsha Rabb (Mola) wenu (kwa Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)?” Husema: “Hekaya za watu wa kale.”


لِيَحْمِلُوا أَوْزَارَهُمْ كَامِلَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۙ وَمِنْ أَوْزَارِ الَّذِينَ يُضِلُّونَهُم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ أَلَا سَاءَ مَا يَزِرُونَ﴿٢٥﴾
25. Ili wabebe mizigo (ya madhambi) yao kamili Siku ya Qiyaamah, na mizigo ya wale waliowapoteza bila ya elimu. Tanabahi!  Uovu ulioje wanayoyabeba.


قَدْ مَكَرَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَأَتَى اللَّـهُ بُنْيَانَهُم مِّنَ الْقَوَاعِدِ فَخَرَّ عَلَيْهِمُ السَّقْفُ مِن فَوْقِهِمْ وَأَتَاهُمُ الْعَذَابُ مِنْ حَيْثُ لَا يَشْعُرُونَ﴿٢٦﴾
26. Walikwishafanya njama wale wa kabla yao, basi Allaah Aliyasukua majengo yao kwenye misingi, sakafu ikawaporomokea juu yoa, na ikawajia adhabu kutoka pande wasizozitambua.


ثُمَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يُخْزِيهِمْ وَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَائِيَ الَّذِينَ كُنتُمْ تُشَاقُّونَ فِيهِمْ ۚ قَالَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ إِنَّ الْخِزْيَ الْيَوْمَ وَالسُّوءَ عَلَى الْكَافِرِينَ﴿٢٧﴾
27. Kisha Siku ya Qiyaamah (Allaah) Atawahizi na Atasema: “Wako wapi (mnaodai kuwa ni) washirika Wangu ambao mlikuwa kwa ajili yao mnapingana (kuwahasimu Rasuli na Waumini)?” Watasema waliopewa elimu: “Hakika hizaya leo na uovu ni juu ya makafiri.”


الَّذِينَ تَتَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ ۖ فَأَلْقَوُا السَّلَمَ مَا كُنَّا نَعْمَلُ مِن سُوءٍ ۚ بَلَىٰ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٢٨﴾
28. Ambao Malaika huwafisha wakiwa wamejidhulumu nafsi zao, watasalimu amri (watasema): “Hatukuwa tukitenda uovu.” (Wataambiwa): “Hapana! (waongo, kwani) hakika Allaah ni ‘Aliym (Mjuzi) kwa yale mliyokuwa mkitenda.”


فَادْخُلُوا أَبْوَابَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا ۖ فَلَبِئْسَ مَثْوَى الْمُتَكَبِّرِينَ﴿٢٩﴾
29. “Basi ingieni milango ya (Moto wa) Jahannam ni wenye kudumu humo. Basi uovu ulioje makazi ya wanaotakabari.”


وَقِيلَ لِلَّذِينَ اتَّقَوْا مَاذَا أَنزَلَ رَبُّكُمْ ۚ قَالُوا خَيْرًا ۗ لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةٌ ۚ وَلَدَارُ الْآخِرَةِ خَيْرٌ ۚ وَلَنِعْمَ دَارُ الْمُتَّقِينَ﴿٣٠﴾
30. Na wanapoambiwa wale waliokuwa na taqwa: “Nini Ameteremsha Rabb (Mola) wenu?” Husema: “Kheri.” Kwa wale waliofanya mazuri katika dunia hii watapata hasanah (mazuri). Na bila shaka nyumba ya Aakhirah ni bora. Na uzuri ulioje nyumba ya wenye taqwa.


جَنَّاتُ عَدْنٍ يَدْخُلُونَهَا تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ لَهُمْ فِيهَا مَا يَشَاءُونَ ۚ كَذَٰلِكَ يَجْزِي اللَّـهُ الْمُتَّقِينَ﴿٣١﴾
31. Jannaat za‘Adn wataziingia humo, zipitazo chini yake mito. Watapata humo wayatakayo. Hivyo ndivyo Allaah Anavyowalipa wenye taqwa.


الَّذِينَ تَتَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ طَيِّبِينَ ۙ يَقُولُونَ سَلَامٌ عَلَيْكُمُ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٣٢﴾
32. Ambao Malaika huwafisha katika hali nzuri (Malaika) watasema: (kuwaambia Waumini): “Salaamun ‘Alaykum (amani iwe juu yenu)! Ingieni Jannah kwa yale mliyokuwa mkitenda.”


هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن تَأْتِيَهُمُ الْمَلَائِكَةُ أَوْ يَأْتِيَ أَمْرُ رَبِّكَ ۚ كَذَٰلِكَ فَعَلَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ وَمَا ظَلَمَهُمُ اللَّـهُ وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ﴿٣٣﴾
33. Je, wanangojea lolote isipokuwa wawafikie Malaika (kuwatoa roho) au iwafikie amri ya Rabb (Mola) wako (ya adhabu). Hivyo ndivyo walivyofanya wale wa kabla yao. Na Allaah Hakuwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu nafsi zao wenyewe.


فَأَصَابَهُمْ سَيِّئَاتُ مَا عَمِلُوا وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ﴿٣٤﴾
34. Basi ikawasibu maovu ya waliyoyatenda, na ikawazunguka yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.


وَقَالَ الَّذِينَ أَشْرَكُوا لَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا عَبَدْنَا مِن دُونِهِ مِن شَيْءٍ نَّحْنُ وَلَا آبَاؤُنَا وَلَا حَرَّمْنَا مِن دُونِهِ مِن شَيْءٍ ۚ كَذَٰلِكَ فَعَلَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ فَهَلْ عَلَى الرُّسُلِ إِلَّا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ﴿٣٥﴾
35. Na wale washirikina wakasema: “Kama Angelitaka Allaah tusingeliabudu chochote pasi Naye, sisi wala baba zetu; wala tusingeliharamisha chochote bila (ya amri) Yake.” Hivyo ndivyo walivyofanya wale wa kabla yao. Basi je, kuna lolote juu ya Rasuli isipokuwa ubalighisho bayana wa ujumbe?


وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ ۖ فَمِنْهُم مَّنْ هَدَى اللَّـهُ وَمِنْهُم مَّنْ حَقَّتْ عَلَيْهِ الضَّلَالَةُ ۚ فَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ﴿٣٦﴾
36. Na kwa yakini Tulituma katika kila ummah Rasuli (awaamrishe watu wake) kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na twaaghuwt (miungu ya uongo). Basi miongoni mwao ambao Allaah Amewaongoa, na miongoni mwao ambao umethibiti kwake upotofu. Basi nendeni katika ardhi kisha mtazame vipi ilikuwa hatima ya wenye kukadhibisha.


إِن تَحْرِصْ عَلَىٰ هُدَاهُمْ فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي مَن يُضِلُّ ۖ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ﴿٣٧﴾
37. Ukiwa na hima ya kutaka kuwaongoza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi hakika Allaah Hamuongozi aliyepotea. Na hawatopata mwenye kunusuru yeyote.


وَأَقْسَمُوا بِاللَّـهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ ۙ لَا يَبْعَثُ اللَّـهُ مَن يَمُوتُ ۚ بَلَىٰ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴿٣٨﴾
38. Na wakaapa kwa Jina la Allaah nguvu ya viapo vyao kwamba: “Allaah Hatomfufua aliyekufa.” Ndio!  Ahadi Yake ni haki (ya kuwa Atafufua kila kiumbe); lakini watu wengi hawajui.


لِيُبَيِّنَ لَهُمُ الَّذِي يَخْتَلِفُونَ فِيهِ وَلِيَعْلَمَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَنَّهُمْ كَانُوا كَاذِبِينَ﴿٣٩﴾
39. (Atawafufua) Ili Awabainishie yale waliyokhitilafiana kwayo, na ili wajue wale waliokufuru kwamba wao walikuwa waongo.


إِنَّمَا قَوْلُنَا لِشَيْءٍ إِذَا أَرَدْنَاهُ أَن نَّقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ﴿٤٠﴾
40. Hakika Kauli Yetu juu ya kitu Tunapokitaka (kiwe); Tunakiambia: “Kun” (Kuwa) basi kinakuwa!


وَالَّذِينَ هَاجَرُوا فِي اللَّـهِ مِن بَعْدِ مَا ظُلِمُوا لَنُبَوِّئَنَّهُمْ فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً ۖ وَلَأَجْرُ الْآخِرَةِ أَكْبَرُ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ﴿٤١﴾
41. Na wale waliohajiri kwa ajili ya Allaah baada ya kudhulumiwa, Tutawapa makazi mazuri duniani. Na bila shaka ujira wa Aakhirah ni mkubwa zaidi lau wangelikuwa wanajua.


الَّذِينَ صَبَرُوا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ﴿٤٢﴾
42. (Hao ndio) Wale waliosubiri na wakatawakali kwa Rabb (Mola) wao.


وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِي إِلَيْهِمْ ۚ فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ﴿٤٣﴾
43. Na Hatukutuma (Rasuli) kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa ni wanaume Tunawafunulia Wahy. Basi (enyi makafiri) ulizeni watu wenye kumbukumbu (ya vitabu vilivyotangulia) ikiwa hamjui.


بِالْبَيِّنَاتِ وَالزُّبُرِ ۗ وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ﴿٤٤﴾
44. (Tumewatuma) Kwa hoja bayana navitabu. Na Tumekuteremshia Adh-Dhikra (Qur-aan) ili uwabainishie watu (kwa Sunnah) yaliyoteremshwa kwao na huenda wakapata kutafakari.


أَفَأَمِنَ الَّذِينَ مَكَرُوا السَّيِّئَاتِ أَن يَخْسِفَ اللَّـهُ بِهِمُ الْأَرْضَ أَوْ يَأْتِيَهُمُ الْعَذَابُ مِنْ حَيْثُ لَا يَشْعُرُونَ﴿٤٥﴾
45. Je, wameaminisha wale waliopanga njama za uovu kwamba Allaah Hatowadidimiza katika ardhi au haitowafikia adhabu kutoka wasipotambua?


أَوْ يَأْخُذَهُمْ فِي تَقَلُّبِهِمْ فَمَا هُم بِمُعْجِزِينَ﴿٤٦﴾
46. Au (Allaah) Hatowachukuwa katika harakati zao? Basi wao si wenye kushinda kukwepa (adhabu).


أَوْ يَأْخُذَهُمْ عَلَىٰ تَخَوُّفٍ فَإِنَّ رَبَّكُمْ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿٤٧﴾
47. Au (Allaah) Hatowachukuwa katika hali ya khofu (kuwapunguzia mali na afya), basi hakika Rabb (Mola) wako bila shaka ni Rauwfur-Rahiym (Mwenye huruma mno - Mwenye kurehemu).


أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَىٰ مَا خَلَقَ اللَّـهُ مِن شَيْءٍ يَتَفَيَّأُ ظِلَالُهُ عَنِ الْيَمِينِ وَالشَّمَائِلِ سُجَّدًا لِّلَّـهِ وَهُمْ دَاخِرُونَ﴿٤٨﴾
48. Je, hawaoni vile vitu Alivyoumba Allaah ambavyo vivuli vyake vinaelemea kulia na kushoto vikimsujudia Allaah na huku vinanyenyekea?


وَلِلَّـهِ يَسْجُدُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ مِن دَابَّةٍ وَالْمَلَائِكَةُ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ﴿٤٩﴾
49. Na ni kwa Allaah pekee vinasujudia vyote vilivyomo mbinguni na ardhini katika viumbe vitembeavyo, na Malaika, nao hawatakabari.


يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوْقِهِمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ ۩﴿٥٠﴾
50. Wanamkhofu Rabb (Mola) wao Aliye juu yao, na wanafanya yale wanayoamrishwa.


وَقَالَ اللَّـهُ لَا تَتَّخِذُوا إِلَـٰهَيْنِ اثْنَيْنِ ۖ إِنَّمَا هُوَ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ فَإِيَّايَ فَارْهَبُونِ﴿٥١﴾
51. Na Allaah Anasema: “Msijichukulie waungu wawili; hakika Yeye Ndiye Ilaah (Muabudiwa wa haki) Mmoja (Pekee) basi niogopeni Mimi tu.


وَلَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَهُ الدِّينُ وَاصِبًا ۚ أَفَغَيْرَ اللَّـهِ تَتَّقُونَ﴿٥٢﴾
52. Na ni Vyake Pekee vyote viliomo katika mbingu na ardhi, na Kwake Pekee inastahiki Ad-Diywnu waaswibaa (‘ibaadah ya kudumu ya ikhlaasw na utiifu). Je, basi mtamcha asiyekuwa Allaah.


وَمَا بِكُم مِّن نِّعْمَةٍ فَمِنَ اللَّـهِ ۖ ثُمَّ إِذَا مَسَّكُمُ الضُّرُّ فَإِلَيْهِ تَجْأَرُونَ﴿٥٣﴾
53. Na neema yoyote mliyo nayo, basi ni kutoka kwa Allaah. Kisha inapokuguseni dhara Kwake mnamlilia msaada.


ثُمَّ إِذَا كَشَفَ الضُّرَّ عَنكُمْ إِذَا فَرِيقٌ مِّنكُم بِرَبِّهِمْ يُشْرِكُونَ﴿٥٤﴾
54. Kisha Anapokuondosheeni dhara tahamaki kundi miongoni mwenu wanamshirikisha Rabb (Mola) wao.


لِيَكْفُرُوا بِمَا آتَيْنَاهُمْ ۚ فَتَمَتَّعُوا ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ﴿٥٥﴾
55. (Baada ya hayo) Ili wakufuru (bila kushukuru neema) kwa yale Tuliyowapa. Basi stareheni kidogo, mtakuja kujua.


وَيَجْعَلُونَ لِمَا لَا يَعْلَمُونَ نَصِيبًا مِّمَّا رَزَقْنَاهُمْ ۗ تَاللَّـهِ لَتُسْأَلُنَّ عَمَّا كُنتُمْ تَفْتَرُونَ﴿٥٦﴾
56. Na wanaweka (miungu yao) wasiojua (wanayofanyiwa), sehemu ya yale Tuliyowaruzuku. Ta-Allaahi (Naapa kwa Jina la Allaah), bila shaka mtaulizwa juu ya yale mliyokuwa mkiyatunga.


وَيَجْعَلُونَ لِلَّـهِ الْبَنَاتِ سُبْحَانَهُ ۙ وَلَهُم مَّا يَشْتَهُونَ﴿٥٧﴾
57. Na wanamfanyia Allaah mabinti Subhaanah! (Utakasifu ni Wake!) na hali wao wanao (wana wa kiume) wanaowatamani


وَإِذَا بُشِّرَ أَحَدُهُم بِالْأُنثَىٰ ظَلَّ وَجْهُهُ مُسْوَدًّا وَهُوَ كَظِيمٌ﴿٥٨﴾
58. Na anapopewa bishara mmoja wao ya (kuzaliwa mwana wa) kike, husawijika uso wake naye huku amezuia ghaidhi (na majonzi).


يَتَوَارَىٰ مِنَ الْقَوْمِ مِن سُوءِ مَا بُشِّرَ بِهِ ۚ أَيُمْسِكُهُ عَلَىٰ هُونٍ أَمْ يَدُسُّهُ فِي التُّرَابِ ۗ أَلَا سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ﴿٥٩﴾
59. Anajificha kwa watu kwa ubaya aliobashiriwa nao. Je, akae naye (huyo mwana wa kike) kwa fedheha au amfukie udongoni (amzike mzimamzima). Tanabahi! Uovu ulioje wanayohukumu.


لِلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ مَثَلُ السَّوْءِ ۖ وَلِلَّـهِ الْمَثَلُ الْأَعْلَىٰ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٦٠﴾
60. Kwa wale wasioamini Aakhirah (wana) mfano mbaya (ya kupigiwa); na Allaah Ana Sifa tukufu. Naye ni Al-‘Aziyzul-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika - Mwenye hikmah wa yote).


وَلَوْ يُؤَاخِذُ اللَّـهُ النَّاسَ بِظُلْمِهِم مَّا تَرَكَ عَلَيْهَا مِن دَابَّةٍ وَلَـٰكِن يُؤَخِّرُهُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۖ فَإِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ لَا يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً ۖ وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ﴿٦١﴾
61. Na kama Allaah Angeliwachukuwa watu (kuwaadhibu) kwa dhulma zao, Asingeliacha juu ya ardhi kiumbe chochote; lakini Anawaakhirisha mpaka muda maalumu uliokadiriwa. Basi utakapofika muda wao hawaakhirishi saa na wala hawatangulizi.


وَيَجْعَلُونَ لِلَّـهِ مَا يَكْرَهُونَ وَتَصِفُ أَلْسِنَتُهُمُ الْكَذِبَ أَنَّ لَهُمُ الْحُسْنَىٰ ۖ لَا جَرَمَ أَنَّ لَهُمُ النَّارَ وَأَنَّهُم مُّفْرَطُونَ﴿٦٢﴾
62. Na wanamfanyia Allaah yale wanayoyachukia (wao wenyewe kama kuwa na watoto wa kike). Na ndimi zao zinaeleza uongo kwamba watapata Al-Husnaa (hali nzuri duniani na Aakhirah). Hapana shaka kwamba watapata Moto, na kwamba wao wataachwa humo wapuuzwe.


تَاللَّـهِ لَقَدْ أَرْسَلْنَا إِلَىٰ أُمَمٍ مِّن قَبْلِكَ فَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ أَعْمَالَهُمْ فَهُوَ وَلِيُّهُمُ الْيَوْمَ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٦٣﴾
63. Ta-Allaahi (Naapa kwa Jina la Allaah) kwa yakini Tumepeleka (Rasuli) kwa umati kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi shaytwaan akawapambia ‘amali zao, basi yeye leo ni rafiki mwandani wao, na watapata adhabu iumizayo.


وَمَا أَنزَلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ إِلَّا لِتُبَيِّنَ لَهُمُ الَّذِي اخْتَلَفُوا فِيهِ ۙ وَهُدًى وَرَحْمَةً لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ﴿٦٤﴾
64. Na Hatukukuteremshia Kitabu (Qur-aan) isipokuwa uwabainishie yale waliyokhitilafiana kwayo, na (pia kiwe) Mwongozo na Rahmah kwa watu wanaoamini.


وَاللَّـهُ أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ﴿٦٥﴾
65. Na Allaah Ameteremsha kutoka mbinguni maji Akahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake. Hakika katika hayo (kuna) Aayah (ishara, dalili, zingatio n.k) kwa watu wanaosikia.


وَإِنَّ لَكُمْ فِي الْأَنْعَامِ لَعِبْرَةً ۖ نُّسْقِيكُم مِّمَّا فِي بُطُونِهِ مِن بَيْنِ فَرْثٍ وَدَمٍ لَّبَنًا خَالِصًا سَائِغًا لِّلشَّارِبِينَ﴿٦٦﴾
66. Na hakika katika wanyama wamifugo mna ibra (zingatio) kwenu. Tunakunywisheni katika yale yaliyomo matumboni mwao yaliyo baina ya kinyesi na damu (nayo ni) maziwa safi ya ladha kwa wanywaji.


وَمِن ثَمَرَاتِ النَّخِيلِ وَالْأَعْنَابِ تَتَّخِذُونَ مِنْهُ سَكَرًا وَرِزْقًا حَسَنًا ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ﴿٦٧﴾
67. Na katika matunda ya mitende na mizabibu mnafanya humo vinywaji vikali (vya ulevi vinavyokatazwa) na riziki nzuri. Hakika katika hayo (kuna) Aayah (ishara, dalili, zingatio n.k) kwa wanaotia akilini.


وَأَوْحَىٰ رَبُّكَ إِلَى النَّحْلِ أَنِ اتَّخِذِي مِنَ الْجِبَالِ بُيُوتًا وَمِنَ الشَّجَرِ وَمِمَّا يَعْرِشُونَ﴿٦٨﴾
68. Na Rabb (Mola) wako Akamtia ilhamu nyuki kwamba: “Jitengenezee nyumba katika majabali, na katika miti, na katika (vinginevyo) wanavyojenga.”


ثُمَّ كُلِي مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ فَاسْلُكِي سُبُلَ رَبِّكِ ذُلُلًا ۚ يَخْرُجُ مِن بُطُونِهَا شَرَابٌ مُّخْتَلِفٌ أَلْوَانُهُ فِيهِ شِفَاءٌ لِّلنَّاسِ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴿٦٩﴾
69. “Kisha kula katika kila matunda, na fuata njia za Rabb (Mola) wako zilizofanywa nyepesi (kuzipita). Kinatoka katika matumbo yao kinywaji cha rangi mbali mbali (asali) ndani yake mna shifaa (ya magonjwa) kwa watu. Hakika katika hayo (kuna) Aayah (ishara, dalili, zingatio n.k.) kwa watu wanaotafakari.


وَاللَّـهُ خَلَقَكُمْ ثُمَّ يَتَوَفَّاكُمْ ۚ وَمِنكُم مَّن يُرَدُّ إِلَىٰ أَرْذَلِ الْعُمُرِ لِكَيْ لَا يَعْلَمَ بَعْدَ عِلْمٍ شَيْئًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ قَدِيرٌ﴿٧٠﴾
70. Na Allaah Amekuumbeni, kisha Anakufisheni. Na miongoni mwenu (wapo) wanaorudishwa katika umri wa udhalilifu kabisa (wa uzee) awe hajui kitu chochote baada ya elimu (aliyokuwa nao). Hakika Allaah ni ‘Aliymun-Qadiyr (Mjuzi wa yote   – Muweza wa yote).


وَاللَّـهُ فَضَّلَ بَعْضَكُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ فِي الرِّزْقِ ۚ فَمَا الَّذِينَ فُضِّلُوا بِرَادِّي رِزْقِهِمْ عَلَىٰ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَهُمْ فِيهِ سَوَاءٌ ۚ أَفَبِنِعْمَةِ اللَّـهِ يَجْحَدُونَ﴿٧١﴾
71. Na Allaah Amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengineo katika riziki. Basi wale waliofadhilishwa hawarudishi (hawagawi) riziki zao kwa wale iliowamiliki mikono yao ya kulia (watumwa wao), ili wawe sawa katika hiyo (riziki). Je, basi wanakanusha neema za Allaah?


وَاللَّـهُ جَعَلَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا وَجَعَلَ لَكُم مِّنْ أَزْوَاجِكُم بَنِينَ وَحَفَدَةً وَرَزَقَكُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ ۚ أَفَبِالْبَاطِلِ يُؤْمِنُونَ وَبِنِعْمَتِ اللَّـهِ هُمْ يَكْفُرُونَ﴿٧٢﴾
72.  Na Allaah Amekufanyieni wake katika jinsi yenu; na Amekufanyieni katika wake zenu wana na wajukuu; na Amekuruzukuni vizuri.Je, basi wanaamini ya ubatilifu na wanakufuru neema za Allaah?


وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَمْلِكُ لَهُمْ رِزْقًا مِّنَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ شَيْئًا وَلَا يَسْتَطِيعُونَ﴿٧٣﴾
73. Na wanaabudu pasina Allaah (miungu ya uongo) wasiowamilikia riziki ya kitu chochote kutoka mbinguni wala (kutoka katika) ardhi na wala hawawezi.


فَلَا تَضْرِبُوا لِلَّـهِ الْأَمْثَالَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ﴿٧٤﴾
74. Basi msimpigie mifano Allaah (kwani hakuna kinachofanana Naye kabisa!) Hakika Allaah Anajua nanyi hamjui.


ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا عَبْدًا مَّمْلُوكًا لَّا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَيْءٍ وَمَن رَّزَقْنَاهُ مِنَّا رِزْقًا حَسَنًا فَهُوَ يُنفِقُ مِنْهُ سِرًّا وَجَهْرًا ۖ هَلْ يَسْتَوُونَ ۚ الْحَمْدُ لِلَّـهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿٧٥﴾
75. Allaah Amepiga mfano wa (waja wawili) mja anayemilikiwa hana uwezo juu ya chochote na (mfano mwingine) ambaye Tumemruzuku kutoka Kwetu riziki nzuri; naye anatoa katika (riziki hiyo) kwa siri na (kwa) dhahiri. Je, wanalingana sawa? (Haiwezekani kabisa!) AlhamduliLLaah (Himidi zote Anastahiki Allaah). Bali wengi wao hawajui.


وَضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا رَّجُلَيْنِ أَحَدُهُمَا أَبْكَمُ لَا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَيْءٍ وَهُوَ كَلٌّ عَلَىٰ مَوْلَاهُ أَيْنَمَا يُوَجِّههُّ لَا يَأْتِ بِخَيْرٍ ۖ هَلْ يَسْتَوِي هُوَ وَمَن يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ ۙ وَهُوَ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٧٦﴾
76. Na Allaah amepiga mfano (mwingine) wa watu wawili; mmoja ni bubu asiye na uwezo juu ya chochote naye ni mzigo kwa bwana wake, popote unapomuelekeza haleti kheri. Je, analingana sawa yeye na yule anayeamrisha uadilifu, naye yuko juu ya njia iliyonyooka.


وَلِلَّـهِ غَيْبُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَمَا أَمْرُ السَّاعَةِ إِلَّا كَلَمْحِ الْبَصَرِ أَوْ هُوَ أَقْرَبُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٧٧﴾
77. Na ni ya Allaah Pekee ghayb ya mbingu na ardhi. Na wala haikuwa amri ya Saa (kusimama Qiyaamah) isipokuwa kama upepeso wa jicho au karibu zaidi. Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza).


وَاللَّـهُ أَخْرَجَكُم مِّن بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ لَا تَعْلَمُونَ شَيْئًا وَجَعَلَ لَكُمُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَالْأَفْئِدَةَ ۙ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ﴿٧٨﴾
78. Na Allaah Amekutoeni kutoka matumboni mwa mama zenu (hali ya kuwa) hamjui lolote, na Amekujaalieni kusikia na kuona na nyoyo ili mpate kushukuru.


أَلَمْ يَرَوْا إِلَى الطَّيْرِ مُسَخَّرَاتٍ فِي جَوِّ السَّمَاءِ مَا يُمْسِكُهُنَّ إِلَّا اللَّـهُ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ﴿٧٩﴾
79. Je, hawaoni ndege wanavyotiishwa katika anga la mbingu, hakuna anayewashika (wasianguke) isipokuwa Allaah (Aliyewapa uwezo wa kuruka). Hakika katika hayo (kuna) Aayaat (ishara, dalili, zingatio n.k) kwa watu wanaoamini.


وَاللَّـهُ جَعَلَ لَكُم مِّن بُيُوتِكُمْ سَكَنًا وَجَعَلَ لَكُم مِّن جُلُودِ الْأَنْعَامِ بُيُوتًا تَسْتَخِفُّونَهَا يَوْمَ ظَعْنِكُمْ وَيَوْمَ إِقَامَتِكُمْ ۙ وَمِنْ أَصْوَافِهَا وَأَوْبَارِهَا وَأَشْعَارِهَا أَثَاثًا وَمَتَاعًا إِلَىٰ حِينٍ﴿٨٠﴾
80. Na Allaah Amekufanyieni majumba yenu yawe maskani, na Amekujaalieni kutokana na ngozi za wanyama wa mifugo nyumba nyepesi (mahema mnayachukua) wakati wa safari zenu na wakati wa kutua kwenu (safarini); na kutokana na sufi zao na manyoya yao, na nywele zao (hao wanyama mnafanya) fanicha na vifaa (mfano mazulia, mablanketi, mabegi) vya kutumia kwa muda.


وَاللَّـهُ جَعَلَ لَكُم مِّمَّا خَلَقَ ظِلَالًا وَجَعَلَ لَكُم مِّنَ الْجِبَالِ أَكْنَانًا وَجَعَلَ لَكُمْ سَرَابِيلَ تَقِيكُمُ الْحَرَّ وَسَرَابِيلَ تَقِيكُم بَأْسَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُتِمُّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تُسْلِمُونَ﴿٨١﴾
81. Na Allaah Amekufanyieni katika Alivyoumba (vinavyoleta) vivuli, na Akakujaalieni katika majabali mahali pa kukimbilia (mapangoni), na Amekujaalieni mavazi yanakukingeni na joto (na baridi) na mavazi (ya chuma) yanakukingeni (maadui) katika vita vyenu. Hivyo ndivyo Anavyotimiza neema Yake juu yenu huenda mkapata kujisalimisha.


فَإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا عَلَيْكَ الْبَلَاغُ الْمُبِينُ﴿٨٢﴾
82. Wakikengeuka, basi hakika ni juu yako ubalighisho (wa ujumbe) bayana.


يَعْرِفُونَ نِعْمَتَ اللَّـهِ ثُمَّ يُنكِرُونَهَا وَأَكْثَرُهُمُ الْكَافِرُونَ﴿٨٣﴾
83. Wanazijua neema za Allaah, kisha wanazikanusha; na wengi wao ni makafiri.


وَيَوْمَ نَبْعَثُ مِن كُلِّ أُمَّةٍ شَهِيدًا ثُمَّ لَا يُؤْذَنُ لِلَّذِينَ كَفَرُوا وَلَا هُمْ يُسْتَعْتَبُونَ﴿٨٤﴾
84. Na (taja ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Siku Tutakapowafufua katika kila ummah shahidi kisha haitoruhusiwa kwa wale waliokufuru (kutoa nyudhuru) na wala hawataachiliwa kuomba kuridhisha (kwa Allaah).


وَإِذَا رَأَى الَّذِينَ ظَلَمُوا الْعَذَابَ فَلَا يُخَفَّفُ عَنْهُمْ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ﴿٨٥﴾
85. Na wale waliodhulumu watakapoiona adhabu, basi hawatopunguziwa hiyo adhabu, na wala hawatopewa muhula.


وَإِذَا رَأَى الَّذِينَ أَشْرَكُوا شُرَكَاءَهُمْ قَالُوا رَبَّنَا هَـٰؤُلَاءِ شُرَكَاؤُنَا الَّذِينَ كُنَّا نَدْعُو مِن دُونِكَ ۖ فَأَلْقَوْا إِلَيْهِمُ الْقَوْلَ إِنَّكُمْ لَكَاذِبُونَ﴿٨٦﴾
86. Na wale waliomshirikisha (Allaah) watakapowaona washirika wao watasema: “Rabb (Mola) wetu! Hawa ni washirikishwa wetu ambao tulikuwa tunawaomba badala Yako.” Basi (wale washirikishwa) watawatupia kauli: “Hakika nyinyi ni waongo.”


وَأَلْقَوْا إِلَى اللَّـهِ يَوْمَئِذٍ السَّلَمَ ۖ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ﴿٨٧﴾
87. Na watajisalimisha kwa Allaah Siku hiyo. Na yatawapotea waliyokuwa wakiyatunga.


الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ زِدْنَاهُمْ عَذَابًا فَوْقَ الْعَذَابِ بِمَا كَانُوا يُفْسِدُونَ﴿٨٨﴾
88. Wale waliokufuru na wakazuia (watu) njia ya Allaah, Tutawazidishia adhabu juu ya adhabu kwa yale waliyokuwa wakifanya ufisadi.


وَيَوْمَ نَبْعَثُ فِي كُلِّ أُمَّةٍ شَهِيدًا عَلَيْهِم مِّنْ أَنفُسِهِمْ ۖ وَجِئْنَا بِكَ شَهِيدًا عَلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ ۚ وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ تِبْيَانًا لِّكُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً وَبُشْرَىٰ لِلْمُسْلِمِينَ﴿٨٩﴾
89. Na (taja) Siku Tutakayofufua katika kila ummah shahidi kutokana na jinsi zao (kuwashuhudia) dhidi yao. Na Tutakuleta (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uwe shahidi juu ya hawa (ummah wako). Na Tumekuteremshia Kitabu kikiwa ni kielezo bayana cha kila kitu na ni Mwongozo na Rahmah na bishara kwa Waislamu.


إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚ يَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ﴿٩٠﴾
90. Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (mahitajio na msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini huenda mkapata kukumbuka (na kuwaidhika).


وَأَوْفُوا بِعَهْدِ اللَّـهِ إِذَا عَاهَدتُّمْ وَلَا تَنقُضُوا الْأَيْمَانَ بَعْدَ تَوْكِيدِهَا وَقَدْ جَعَلْتُمُ اللَّـهَ عَلَيْكُمْ كَفِيلًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا تَفْعَلُونَ﴿٩١﴾
91. Na timizeni ahadi ya Allaah mnapoahidi, na wala msivunje viapo baada ya kuvithibitisha; na mmekwishamfanya Allaah kuwa ni Mdhamini wenu.  Hakika Allaah Anajua yale mnayoyafanya.


وَلَا تَكُونُوا كَالَّتِي نَقَضَتْ غَزْلَهَا مِن بَعْدِ قُوَّةٍ أَنكَاثًا تَتَّخِذُونَ أَيْمَانَكُمْ دَخَلًا بَيْنَكُمْ أَن تَكُونَ أُمَّةٌ هِيَ أَرْبَىٰ مِنْ أُمَّةٍ ۚ إِنَّمَا يَبْلُوكُمُ اللَّـهُ بِهِ ۚ وَلَيُبَيِّنَنَّ لَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ﴿٩٢﴾
92. Na wala msiwe kama yule mwanamke aliyezongoa uzi wake vipande vipande baada ya (kuusokota na) kuwa mgumu, mnafanya viapo vyenu kuwa njia ya kudaganyana baina yenu, kwa kuwa taifa moja lina nguvu zaidi kuliko jingine (kwa wingi au mali). Hakika Allaah Anakujaribuni kwa njia hiyo (kujua atakayemtii na kutimiza ahadi Yake na atakayeasi). Na bila shaka Atakubainishieni Siku ya Qiyaamah yale mliyokuwa mkikhitilafiana nayo.


وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَجَعَلَكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَلَـٰكِن يُضِلُّ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَلَتُسْأَلُنَّ عَمَّا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٩٣﴾
93. Na kama Allaah Angelitaka Angelikufanyeni ummah mmoja, lakini Humpotoa Amtakaye na Anamwongoa Amtakaye. Na bila shaka mtaulizwa kuhusu yale mliyokuwa mkiyatenda.


وَلَا تَتَّخِذُوا أَيْمَانَكُمْ دَخَلًا بَيْنَكُمْ فَتَزِلَّ قَدَمٌ بَعْدَ ثُبُوتِهَا وَتَذُوقُوا السُّوءَ بِمَا صَدَدتُّمْ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۖ وَلَكُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿٩٤﴾
94. Na wala msifanye viapo vyenu kuwa ni njia ya kudanganyana baina yenu ukateleza mguu baada ya kuthibitika kwake, na mkaonja uovu wenu (duniani) kwa sababu ya kuwazuilia (watu) nia ya Allaah. Na mtapata adhabu kuu.


وَلَا تَشْتَرُوا بِعَهْدِ اللَّـهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۚ إِنَّمَا عِندَ اللَّـهِ هُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ﴿٩٥﴾
95. Na wala msibadilishe ahadi ya Allaah kwa thamani ndogo. Hakika yaliyoko kwa Allaah ni bora kwenu, mgelikuwa mnajua.


مَا عِندَكُمْ يَنفَدُ ۖ وَمَا عِندَ اللَّـهِ بَاقٍ ۗ وَلَنَجْزِيَنَّ الَّذِينَ صَبَرُوا أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٩٦﴾
96. Mlivyo navyo nyinyi vinatoweka, na vilioko kwa Allaah ni vya kubakia. Na kwa yakini Tutawalipa wale waliosubiri ujira wao kwa mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wakitenda.


مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً ۖ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٩٧﴾
97. Mwenye kutenda mema miongoni mwa wanamume au wanawake naye ni Muumin, Tutamhuisha uhai mzuri, na bila shaka Tutawalipa ujira wao kwa mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wakitenda.


فَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ﴿٩٨﴾
98. Unapotaka kusoma Qur-aan basi (anza kwa) omba kinga kwa Allaah dhidi ya shaytwaan aliyefukuzwa mbali (na Rahmah ya Allaah).

إِنَّهُ لَيْسَ لَهُ سُلْطَانٌ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ﴿٩٩﴾
99. Hakika yeye (shaytwaan) hana mamlaka juu ya wale walioamini na kwa Rabb (Mola) wao wanatawakali.


إِنَّمَا سُلْطَانُهُ عَلَى الَّذِينَ يَتَوَلَّوْنَهُ وَالَّذِينَ هُم بِهِ مُشْرِكُونَ﴿١٠٠﴾
100. Hakika mamlaka yake (shaytwaan) ni juu ya wale wanaomfanya rafiki mlinzi, na ambao wao wanamshirikisha (Allaah) naye.


وَإِذَا بَدَّلْنَا آيَةً مَّكَانَ آيَةٍ ۙ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا يُنَزِّلُ قَالُوا إِنَّمَا أَنتَ مُفْتَرٍ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿١٠١﴾
101. Na Tunapobadilisha Aayah mahala pa Aayah nyingine, na Allaah Anajua zaidi Anayoyateremsha, (makafiri) husema: “Hakika wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ni mtungaji (uongo).” Bali wengi wao hawajui.


قُلْ نَزَّلَهُ رُوحُ الْقُدُسِ مِن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ لِيُثَبِّتَ الَّذِينَ آمَنُوا وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُسْلِمِينَ﴿١٠٢﴾
102. Sema: Ameiteremsha Ruwhul-Qudus (Jibriyl) kutoka kwa Rabb (Mola) wako kwa haki ili iwathibitishe walo walioamini na ni Mwongozo na bishara kwa Waislamu.


وَلَقَدْ نَعْلَمُ أَنَّهُمْ يَقُولُونَ إِنَّمَا يُعَلِّمُهُ بَشَرٌ ۗ لِّسَانُ الَّذِي يُلْحِدُونَ إِلَيْهِ أَعْجَمِيٌّ وَهَـٰذَا لِسَانٌ عَرَبِيٌّ مُّبِينٌ﴿١٠٣﴾
103. Na kwa yakini Tunajua kwamba wao wanasema: “Hakika hapana isipokuwa mtu anamfundisha (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم Qur-aan).” Lisani wanaomnasibishia nao ni ya kigeni, na hii ni lisani ya Kiarabu bayana.


إِنَّ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ لَا يَهْدِيهِمُ اللَّـهُ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿١٠٤﴾
104. Hakika wale wasioamini Aayaat za Allaah, Allaah Hatowaongoa, na watapata adhabu iumizayo.


إِنَّمَا يَفْتَرِي الْكَذِبَ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَاذِبُونَ﴿١٠٥﴾
105. Hakika wanaotunga uongo ni wale ambao hawaamini Aayaat za Allaah. Na hao ndio waongo.


مَن كَفَرَ بِاللَّـهِ مِن بَعْدِ إِيمَانِهِ إِلَّا مَنْ أُكْرِهَ وَقَلْبُهُ مُطْمَئِنٌّ بِالْإِيمَانِ وَلَـٰكِن مَّن شَرَحَ بِالْكُفْرِ صَدْرًا فَعَلَيْهِمْ غَضَبٌ مِّنَ اللَّـهِ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿١٠٦﴾
106. Atakayemkufuru Allaah baada ya iymaan yake (atapata adhabu) isipokuwa yule aliyekirihishwa (kukanusha Dini ya Kiislamu) na huku moyo wake umetua juu ya iymaan. Lakini aliyekifungulia ukafiri kifua chake, basi hao juu yao ni ghadhabu kutoka kwa Allaah na watapata adhabu kuu.


ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ اسْتَحَبُّوا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا عَلَى الْآخِرَةِ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ﴿١٠٧﴾
107. Hivyo kwa sababu wao wamestahabu uhai wa dunia kuliko wa Aakhirah; na kwamba Allaah Haongoi watu makafiri.


أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ طَبَعَ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَسَمْعِهِمْ وَأَبْصَارِهِمْ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْغَافِلُونَ﴿١٠٨﴾
108. Hao ni wale ambao Allaah Amepiga chapa juu ya nyoyo zao, na masikio yao, na macho yao. Na hao ndio walioghafilika.


لَا جَرَمَ أَنَّهُمْ فِي الْآخِرَةِ هُمُ الْخَاسِرُونَ﴿١٠٩﴾
109. Hakuna shaka kwamba wao Aakhirah niwenye kukhasirika.


ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ هَاجَرُوا مِن بَعْدِ مَا فُتِنُوا ثُمَّ جَاهَدُوا وَصَبَرُوا إِنَّ رَبَّكَ مِن بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١١٠﴾
110. Kisha hakika Rabb (Mola) wako, kwa wale waliohajiri baada ya kutiwa katika mtihani kisha wakafanya jihaad na wakasubiri; hakika Rabb wako baada ya hayo bila shaka ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).


يَوْمَ تَأْتِي كُلُّ نَفْسٍ تُجَادِلُ عَن نَّفْسِهَا وَتُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا عَمِلَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ﴿١١١﴾
111. Siku itakapokuja kila nafsi kutetea nafsi yake na kila nafsi italipwa kikamilifu yale iliyofanya; nao hawatodhulumiwa.


وَضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا قَرْيَةً كَانَتْ آمِنَةً مُّطْمَئِنَّةً يَأْتِيهَا رِزْقُهَا رَغَدًا مِّن كُلِّ مَكَانٍ فَكَفَرَتْ بِأَنْعُمِ اللَّـهِ فَأَذَاقَهَا اللَّـهُ لِبَاسَ الْجُوعِ وَالْخَوْفِ بِمَا كَانُوا يَصْنَعُونَ﴿١١٢﴾
112. Na Allaah Amepiga mfano wa mji uliokuwa katika amani na utulivu, inaifikia riziki yake maridhawa kutoka kila mahali; (mji huo) ukakufuru neema za Allaah basi Allaah Akauonjesha funiko la njaa na khofu kwa yale waliyokuwa wakitenda.



وَلَقَدْ جَاءَهُمْ رَسُولٌ مِّنْهُمْ فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَهُمُ الْعَذَابُ وَهُمْ ظَالِمُونَ﴿١١٣﴾
113. Na kwa yakini aliwajia Rasuli miongoni mwao wakamkadhibisha, basi ikawachukuwa dhabu hali ya kuwa ni madhalimu.


فَكُلُوا مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّـهُ حَلَالًا طَيِّبًا وَاشْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ﴿١١٤﴾
114. Basi kuleni katika vile Alivyokuruzukuni Allaah vya halaal vizuri na shukuruni neema za Allaah ikiwa (kweli) mnamwabudu Yeye Pekee.


إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةَ وَالدَّمَ وَلَحْمَ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ ۖ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١١٥﴾
115. Hakika (Allaah) Amekuharamishieni nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na kilichotajiwa katika kuchinjwa kwake ghairi ya Allaah. Basi atakayefikwa na dharura bila ya kutamani wala kuvuka mipaka; basi hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).


وَلَا تَقُولُوا لِمَا تَصِفُ أَلْسِنَتُكُمُ الْكَذِبَ هَـٰذَا حَلَالٌ وَهَـٰذَا حَرَامٌ لِّتَفْتَرُوا عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ لَا يُفْلِحُونَ﴿١١٦﴾
116. Na wala msiseme zinayotetea ndimi zenu uongo; hii halaal na hii haraam ili mumtungie Allaah uongo. Hakika wale wanaomtungia Allaah uongo hawafaulu.


مَتَاعٌ قَلِيلٌ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿١١٧﴾
117. Ni starehe ndogo (tu hapa duniani), na watapata adhabu iumizayo.


وَعَلَى الَّذِينَ هَادُوا حَرَّمْنَا مَا قَصَصْنَا عَلَيْكَ مِن قَبْلُ ۖ وَمَا ظَلَمْنَاهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ﴿١١٨﴾
118. Na wale Mayahudi Tuliwaharamishia yale Tuliyokusimulia kabla (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na Hatukuwadhulumu, lakini walikuwa wanajidhulumu nafsi zao wenyewe.


ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ عَمِلُوا السُّوءَ بِجَهَالَةٍ ثُمَّ تَابُوا مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ وَأَصْلَحُوا إِنَّ رَبَّكَ مِن بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١١٩﴾
119. Kisha hakika Rabb (Mola) wako, kwa wale waliotenda uovu kwa ujahili, kisha wakatubu baada yake, na wakatengenea (kwa kufanya ‘amali nzuri); hakika Rabb wako baada ya hayo bila shaka ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).


إِنَّ إِبْرَاهِيمَ كَانَ أُمَّةً قَانِتًا لِّلَّـهِ حَنِيفًا وَلَمْ يَكُ مِنَ الْمُشْرِكِينَ﴿١٢٠﴾
120. Hakika Ibraahiym alikuwa Imaam mtiifu kwa Allaah, haniyfaa (aliyejiengua na upotofu akaelemea Dini ya haki) na wala hakuwa miongoni mwa washirikina.


شَاكِرًا لِّأَنْعُمِهِ ۚ اجْتَبَاهُ وَهَدَاهُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿١٢١﴾
121. (Alikuwa daima) Mwenye kushukuru neema Zake (Allaah); (Naye Allaah) Akamteua na Akamuongoza kuelekea njia iliyonyooka.


وَآتَيْنَاهُ فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً ۖ وَإِنَّهُ فِي الْآخِرَةِ لَمِنَ الصَّالِحِينَ﴿١٢٢﴾
122. Na Tukampa duniani mazuri. Na hakika yeye Aakhirah bila shaka ni miongoni mwa Swalihina.


ثُمَّ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ أَنِ اتَّبِعْ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۖ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ﴿١٢٣﴾
123. Kisha Tukakufunulia Wahy (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba fuata millah ya Ibraahim haniyfaa (aliyejiengua na upotofu akathibitika katika Dini ya haki) na hakuwa miongoni mwa washirikina.


إِنَّمَا جُعِلَ السَّبْتُ عَلَى الَّذِينَ اخْتَلَفُوا فِيهِ ۚ وَإِنَّ رَبَّكَ لَيَحْكُمُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ﴿١٢٤﴾
124. Hakika As-Sabt (Shariy’ah ya Jumamosi) imefanywa kwa wale waliokhitilafiana kwayo. Na hakika Rabb (Mola) wako Atawahukumu baina yao Siku ya Qiyaamah katika yale waliyokuwa wanakhitilafiana kwayo.


ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ ۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِ ۖ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ﴿١٢٥﴾
125. Waite (watu) katika njia ya Rabb (Mola) wako kwa hikmah na mawaidha mazuri. Na jadiliana nao kwa ambayo ni mazuri zaidi. Hakika Rabb wako Yeye Anamjua zaidi aliyepotea njia Yake, Naye Anawajua zaidi walioongoka.


وَإِنْ عَاقَبْتُمْ فَعَاقِبُوا بِمِثْلِ مَا عُوقِبْتُم بِهِ ۖ وَلَئِن صَبَرْتُمْ لَهُوَ خَيْرٌ لِّلصَّابِرِينَ﴿١٢٦﴾
126. Na mkilipiza, basi lipizeni kulingana na vile mlivyoadhibiwa. Na mkisubiri, basi bila shaka hivyo ni bora kwa wenye kusubiri.


وَاصْبِرْ وَمَا صَبْرُكَ إِلَّا بِاللَّـهِ ۚ وَلَا تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَلَا تَكُ فِي ضَيْقٍ مِّمَّا يَمْكُرُونَ﴿١٢٧﴾
127. Na subiri (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), na haiwi subira yako isipokuwa kupitia kwa Allaah. Na wala usiwahuzunukie, na wala usiwe katika dhiki kutokana na njama wanazozifanya.


إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوا وَّالَّذِينَ هُم مُّحْسِنُونَ﴿١٢٨﴾
128. Hakika Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa, na wale ambao wao ni wenye kufanya ihsaan.


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com