Al-Bayyinah (98)

سُورَةُ  الْبَيِّنَة
Al-Bayyinah (98)

(Imeteremka Madina)

Watu wa Kitabu, yaaani Mayahudi na Wakristo, wamejua kutokana na Vitabu vyao, na  washirikina wa Makka wakajua kutokana nao sifa za Nabii wa zama za mwisho. Na yalikuwa yanatakikana kutokana na hayo ni kuwa wamuamini huyo Nabii pindi akiteuliwa. Lakini alipo teuliwa miongoni mwao Mtume wa Mwenyezi Mungu mwenye kuungwa mkono na Qur'ani, walikhitalifiana na wakaacha ahadi yao. Na vitendo vya Watu wa Kitabu katika hayo vilikuwa viovu zaidi kuliko vya washirikina. Na hukumu ya watu hawa wote Akhera ni kukaa milele katika Moto. Na Waumini, watu wa vyeo vya juu kwa fadhila, ndio bora wa viumbe. Malipo yao ni kukaa milele Peponi, na kuridhika kwa kuyapata wayatakayo na kupewa wanayo yapenda. Hii ndiyo neema ya mwenye kumkhofu Mola wake Mlezi.  

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

لَمْ يَكُنِ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ مُنفَكِّينَ حَتَّىٰ تَأْتِيَهُمُ الْبَيِّنَةُ ﴿١﴾

1. Hawakuwa wale waliokufuru miongoni mwa ahlil-Kitaabi (Mayahudi na Manaswara) na washirikina wenye kuacha (waliyonayo) mpaka iwafikie hoja bayana.

رَسُولٌ مِّنَ اللَّـهِ يَتْلُو صُحُفًا مُّطَهَّرَةً ﴿٢﴾

2.  Rasuli kutoka kwa Allaah anawasomea sahifa zilotwaharika.


فِيهَا كُتُبٌ قَيِّمَةٌ ﴿٣﴾

3. Ndani yake humo mna maandiko yanayosimama imara.

وَمَا تَفَرَّقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَةُ ﴿٤﴾

4. Na hawakufarikiana wale waliopewa kitabu isipokuwa baada ya kuwajia hoja bayana.

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ ۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ ﴿٥﴾

5. Na hawakuamrishwa (chochote kile) isipokuwa wamwabudu Allaah mukhliswiyn (wenye kumtakasia) Dini, hunafaa (wenye kujiengua na upotofu kuelemea Dini ya haki) na wasimamishe Swalaah na watoe Zakaah; na hiyo ndiyo Dini iliyosimama imara.

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ أُولَـٰئِكَ هُمْ شَرُّ الْبَرِيَّةِ ﴿٦﴾

6. Hakika wale waliokufuru miongoni mwa watu wa kitabu na washirikina watakuwa katika Moto wa Jahannam, ni wenye kudumu humo; hao ndio waovu wa viumbe.

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَـٰئِكَ هُمْ خَيْرُ الْبَرِيَّةِ ﴿٧﴾

7. Hakika wale walioamini na wakatenda mazuri, hao ndio wema wa viumbe.


جَزَاؤُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتُ عَدْنٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۖ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ۚ ذَٰلِكَ لِمَنْ خَشِيَ رَبَّهُ ﴿٨﴾

8. Jazaa yao iko kwa Rabb (Mola) wao, (nayo ni) Jannaat za ‘Adn zipitazo chini yake mito ni wenye kudumu humo abadi. Allaah Ataridhika nao, nao wataridhika Naye; hayo ni kwa yule anayemkhofu Rabb wake.

 


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com