Jinsi ya Kujipanga Safu Wakisali Wanaume na Wanawake kwa Pamoja.
Watakaposali
wanawake na wanaume sala ya jamaa pamoja (na kama kuna na watoto ) ikiwa ni nyumbani
au msikitini basi mistari (safu) za mwanzo zitatakiwa ziwe za wanaume
kisha zifuate za watoto wa kiume kama wapo na mwisho zije safu za wanawake.
Kwa
mujibu wa hadithi ya Mtume (Salla Allahu ‘Alayhi
Wasallam) iliyosimuliwa na Bukhari na Muslim na kupokelewa na Anas bin
Malik Allah amuwie radhi kwamba :
Bibi
yake anas alimualika Mtume (Salla Allahu ‘Alayhi
Wasallam) kwa ajili ya chakula alichomuandalia. Mtume (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam) akala kidogo kisha
akasema : simameni nikuongozeni kwenye sala. Anas akasema: Nikaenda kuchukua
msala wetu ambao tayari umejaa weusi(kwa kutumika sana) nikauchurizia maji
kuusafisha . Kisha Mtume(Salla Allahu ‘Alayhi
Wasallam) akasimama na (alikuwepo ) yatima na mimi tukasimama nyuma yake
na bibi akasimama nyuma yetu Na Mtume(Salla Allahu
‘Alayhi Wasallam) Akatusalisha rakaa mbili kisha akaondoka.
Na
kwa mujibu wa hadithi nyengine ya Mtume(Salla Allahu
‘Alayhi Wasallam)
قال صلى الله عليه وآله وسلم (( خَيْرُ صُفُوف
الرَّجْلُ أَوَّلُهَا وَشَرُّهَا أَخِرُهَا وَخَيْر صُفُوف النِّسَاء
أَخِرُهَا وَشَرُّهَا أَوَّلُهَا )) رواه مسلم
Amesema Mtume (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam) katika
hadithi iliyosimuliwa na Abu Hurayrah, Allah amuwie radhi:
“Safu iliyo bora kwa wanaume ni ile ya mwanzo na safu iliyo mbaya ni
ile ya mwisho, Na bora ya safu (ya sala) kwa mwanamke ni ile ya mwisho na iliyo
mbaya ni ile ya mwanzo”
Imesimuliwa na Muslim
Na ikiwa kama wanawake wanasali na wanaume kwenye sehemu kama msikiti
au kwenye ukumbi (hall) na ukuta au kizuizi ndio kinachowatenganisha
lakini wanasali kama bega kwa bega pia sala hii ni sahihi almuradi kuna kitu
kinawatenganisha lakini inavyotakikana kiutaratibu safu hizi ziwe nyuma ya safu
za wanaume .