Aal-‘Imraan: 3


  آل عِمْران
Aal-‘Imraan:  3

(Imeteremka Madina)



MIONGONI mwa mambo inayo yazungumzia Qur'ani ni hadithi za ada ya Mwenyezi Mungu katika uumbaji wake, na mifano na mazingatio yanayo patikana katika hizo hadithi. Na hubainisha katika hadithi hizo mambo mengi yaliyo khusu itikadi, hukumu za sharia na nyendo njema. Katika Sura iliyo pita yametajwa mfano wa mwendo wa Wana wa Israili. Yameelezwa mengi ya walivyo kengeuka. Na katika Sura hii yanatajwa mengine ya upotovu wao na kukengeuka kwao, na vipi Muumini anatakikana aongoke katika itikadi yake na mwenendo wake, na pia unabainishwa humu ukweli wa Dini ya Mbinguni, na inaonyeshwa vipi ziwe adabu za kujadiliana, na zinaelezwa ada za wakati wa kushinda na pengine wakati wa kushindwa. Pia inabainishwa vipi watakuwa wanao kufa Mashahidi Siku ya Kiyama, na yepi malipo yao. Na hayo yote kwa wanaume na wanawake. Na inaelezwa kadhaalika njia ya mafanikio. Sura hii tukufu inaanza kama ilivyo anza iliyo tangulia. 



  
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 الم﴿١﴾
1. Alif Laam Miym.


اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ﴿٢﴾
2. Allaah, hapana ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye, Al-Hayyul-Qayyuwm (Aliyehai daima - Msimamia kila kitu).


 نَزَّلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَأَنزَلَ التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ﴿٣﴾
3. Amekuteremshia Kitabu (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa haki kinachosadikisha yaliyo kabla yake na AkateremshaTawraat na Injiyl.


مِن قَبْلُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَأَنزَلَ الْفُرْقَانَ ۗ إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ ذُو انتِقَامٍ ﴿٤﴾
4. Kabla, ni Mwongozo kwa watu na Akateremsha al-Furqaan (pambanuo la haki na ubatilifu). Hakika wale waliokufuru Aayaat za Allaah watapata adhabu kali. Na Allaah ni Aziyz (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika) Mwenye kulipiza.


إِنَّ اللَّـهَ لَا يَخْفَىٰ عَلَيْهِ شَيْءٌ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ﴿٥﴾
5. Hakika Allaah Hakifichiki Kwake chochote katika ardhi wala katika mbingu.   

 هُوَ الَّذِي يُصَوِّرُكُمْ فِي الْأَرْحَامِ كَيْفَ يَشَاءُ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٦﴾
6. Yeye Ndiye Aliyekuundeni umbo katika matumbo ya uzazi vile Atakavyo. Hapana ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye, Al-‘Aziyzul-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika - Mwenye hikmah wa yote).


هُوَ الَّذِي أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ ۖ فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ ۗ وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلَّا اللَّـهُ ۗ وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٧
7. Yeye Ndiye Aliyeteremsha kwako Kitabu humo mna Aayaat Muhkam (zilizo wazi maana yake) hizo ndio msingi wa Kitabu, na nyinginezo ni mutashaabih (haziko wazi maana yake). Basi wale ambao katika nyoyo zao mna upotovu hufuata zile zilizo mutashaabih kutafuta fitnah (upotofu) na kutafuta tafsiri zake (kuridhisha nafsi zao); na hakuna ajuae tafsiri zake isipokuwa Allaah. Na Ar-Raasikhuwna (wenye msingi madhubuti) katika elimu husema: “Tumeziamini, zote ni kutoka kwa Rabb (Mola) wetu.” Na hawakumbuki ila wenye akili.

رَبَّنَا لَا تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْوَهَّابُ ﴿٨﴾
8.(Ar-Raasikhuwna Husema):Rabb (Mola) wetu, Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kutuongoza na Tutunukie kutoka kwako Rahmah. Hakika Wewe ni Al-Wahhaab (Mwingi wa kutunuku na kuneemesha).”


رَبَّنَا إِنَّكَ جَامِعُ النَّاسِ لِيَوْمٍ لَّا رَيْبَ فِيهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُخْلِفُ الْمِيعَادَ ﴿٩﴾ 
9. “Rabb (Mola) wetu! Hakika Wewe ni Mkusanyaji watu Siku isiyo na shaka ndani yake. Hakika Allaah Havunji miadi.”

 إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَن تُغْنِيَ عَنْهُمْ أَمْوَالُهُمْ وَلَا أَوْلَادُهُم مِّنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمْ وَقُودُ النَّارِ ﴿١٠﴾
10. Hakika wale waliokufuru hazitowafaa kitu mali zao na wala auladi wao mbele ya Allaah, na hao ndio kuni za Moto.

كَدَأْبِ آلِ فِرْعَوْنَ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا فَأَخَذَهُمُ اللَّـهُ بِذُنُوبِهِمْ ۗ وَاللَّـهُ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿١١﴾
11. Kama mwendo wa watu wa Fir’awn na wale walio kabla yao. Wamekadhibisha Aayaat (ishara, dalili n.k) Zetu basi Allaah Aliwachukua kwa madhambi yao, na Allaah ni Mkali wa kuakibu.

قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُوا سَتُغْلَبُونَ وَتُحْشَرُونَ إِلَىٰ جَهَنَّمَ ۚ وَبِئْسَ الْمِهَادُ ﴿١٢
12. Waambie waliokufuru: “Mtashindwa na mtakusanywa katika (Moto wa) Jahannam, na ni pabaya mno mahala pa kupumzika.”


 قَدْ كَانَ لَكُمْ آيَةٌ فِي فِئَتَيْنِ الْتَقَتَا ۖ فِئَةٌ تُقَاتِلُ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَأُخْرَىٰ كَافِرَةٌ يَرَوْنَهُم مِّثْلَيْهِمْ رَأْيَ الْعَيْنِ ۚ وَاللَّـهُ يُؤَيِّدُ بِنَصْرِهِ مَن يَشَاءُ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبْرَةً لِّأُولِي الْأَبْصَارِ ﴿١٣﴾
13. Kwa hakika ilikuwa ni Aayah (ishara, dalili wazi) kwenu katika makundi mawili; yalipokutana (vita vya Badr). Kundi linapigana katika njia ya Allaah na jingine kafiri. (Makafiri) wanawaona, (Waislamu) mara mbili yao kwa kuona kwa macho. Na Allaah Humsaidia kwa nusura Yake Amtakaye. Hakika katika hayo bila shaka ni zingatio kwa wenye macho.

زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ الشَّهَوَاتِ مِنَ النِّسَاءِ وَالْبَنِينَ وَالْقَنَاطِيرِ الْمُقَنطَرَةِ مِنَ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ وَالْخَيْلِ الْمُسَوَّمَةِ وَالْأَنْعَامِ وَالْحَرْثِ ۗ ذَٰلِكَ مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَاللَّـهُ عِندَهُ حُسْنُ الْمَآبِ ﴿١٤﴾
14. Watu wamepambiwa huba ya matamanio miongoni mwa wanawake, na watoto, na mirundi ya mali iliyorundikwa ya dhahabu na fedha na farasi wenye chapa (ya aina bora) na wanyama wa mifugo na mashamba. Hayo ni starehe za uhai wa dunia, na Allaah Kwake kuna marejeo mazuri

 قُلْ أَؤُنَبِّئُكُم بِخَيْرٍ مِّن ذَٰلِكُمْ ۚ لِلَّذِينَ اتَّقَوْا عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَأَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ وَرِضْوَانٌ مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ ﴿١٥﴾
15. Sema: “Je, nikujulisheni yaliyo bora kuliko hayo? Kwa wale waliokuwa na taqwa kwa Rabb (Mola) wao (watapata) Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo na wake waliotakasika na Radhi kutoka kwa Allaah. Na Allaah ni Baswiyr (Mwenye kuona) waja.

الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا إِنَّنَا آمَنَّا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ﴿١٦﴾ 
16. Wale wasemao: “Rabb (Mola) wetu, hakika sisi tumeamini, basi Tughufurie madhambi yetu na Tukinge na adhabu ya Moto.”

 الصَّابِرِينَ وَالصَّادِقِينَ وَالْقَانِتِينَ وَالْمُنفِقِينَ وَالْمُسْتَغْفِرِينَ بِالْأَسْحَارِ﴿١٧﴾
17. Wenye kusubiri na wasemao kweli, na watiifu, na watoaji (mali katika njia ya Allaah) na waombao maghfirah kabla ya Alfajiri.

شَهِدَ اللَّـهُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٨﴾
18. Allaah Ameshuhudia kwamba hapana ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye; na Malaika, na wenye elimu (wote wameshuhudia kwamba Yeye) ni Mwenye kusimamisha (uumbaji Wake) kwa uadilifu. Hapana ilaaha ila Yeye Al-‘Aziyzul-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika - Mwenye hikmah wa yote).


إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّـهِ الْإِسْلَامُ ۗ وَمَا اخْتَلَفَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْعِلْمُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِآيَاتِ اللَّـهِ فَإِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿١٩﴾
19. Hakika Dini mbele ya Allaah ni Uislamu. Na hawakukhitilafiana wale waliopewa Kitabu ila baada ya kuwajia elimu kwa uhusuda baina yao. Na atakayekanusha Aayaat (na ishara, dalili, n.k) za Allaah basi hakika Allaah ni Mwepesi wa kuhesabu.

 فَإِنْ حَاجُّوكَ فَقُلْ أَسْلَمْتُ وَجْهِيَ لِلَّـهِ وَمَنِ اتَّبَعَنِ ۗ وَقُل لِّلَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْأُمِّيِّينَ أَأَسْلَمْتُمْ ۚ فَإِنْ أَسْلَمُوا فَقَدِ اهْتَدَوا ۖ وَّإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا عَلَيْكَ الْبَلَاغُ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ ﴿٢٠﴾
20. Na wakikuhoji, basi sema: “Nimejisalimisha kwa Allaah na (wamesilimu pia) walionifuata” Na waambie waliopewa Kitabu na Al-Ummiyyuwn (wasiojua kusoma na kuandika): “Je mmesilimu?” Wakisilimu basi wameongoka, na wakikengeuka basi hakika juu yako ni kubalighisha. Na Allaah ni Baswiyr (Mwenye kuona) waja.

إِنَّ الَّذِينَ يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَيَقْتُلُونَ النَّبِيِّينَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَيَقْتُلُونَ الَّذِينَ يَأْمُرُونَ بِالْقِسْطِ مِنَ النَّاسِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٢١﴾ 
21. Hakika waliokanusha Aayaat (ishara, dalili, hoja n.k) za Allaah na wakaua Nabiy bila ya haki, na wakaua wale wanaoamrisha haki miongoni mwa watu, basi wabashirie adhabu iumizayo.

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ﴿٢٢﴾
22. Hao ni wale ambao zimebatilika ‘amali zao katika dunia na Aakhirah na hawatopata yeyote mwenye kunusuru.

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يُدْعَوْنَ إِلَىٰ كِتَابِ اللَّـهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ يَتَوَلَّىٰ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ وَهُم مُّعْرِضُونَ﴿٢٣﴾ 
23. Je, hukuzingatia wale waliopewa sehemu katika Kitabu wanaitwa katika Kitabu cha Allaah ili kiwahukumu baina yao; kisha kundi miongoni mwao linageuka na huku wanapuuza.

 ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا لَن تَمَسَّنَا النَّارُ إِلَّا أَيَّامًا مَّعْدُودَاتٍ ۖ وَغَرَّهُمْ فِي دِينِهِم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿٢٤﴾
24. Hivyo ni kwa sababu wamesema: “Hautatugusa Moto isipokuwa siku (chache) za kuhesabika.” Na yakawadanganya katika dini yao yale waliyokuwa wakiyazua.

فَكَيْفَ إِذَا جَمَعْنَاهُمْ لِيَوْمٍ لَّا رَيْبَ فِيهِ وَوُفِّيَتْ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ﴿٢٥﴾
25. Basi itakuwa vipi Tutakapowakusanya katika Siku ambayo haina shaka ndani yake, na kila nafsi italipwa kikamilifu yale iliyochuma; nao hawatodhulumiwa.

قُلِ اللَّـهُمَّ مَالِكَ الْمُلْكِ تُؤْتِي الْمُلْكَ مَن تَشَاءُ وَتَنزِعُ الْمُلْكَ مِمَّن تَشَاءُ وَتُعِزُّ مَن تَشَاءُ وَتُذِلُّ مَن تَشَاءُ ۖ بِيَدِكَ الْخَيْرُ ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٦﴾
26. Sema: “Ee Allaah Mfalme Uliyemiliki ufalme wote, Unampa ufalme Umtakaye, na Unamuondoshea ufalme Umtakaye, na Unamtukuza Umtakaye, na Unamdhalilisha Umtakaye, kheri imo Mkononi Mwako.  Hakika Wewe juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza).

 تُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَتُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ ۖ وَتُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَتُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ ۖ وَتَرْزُقُ مَن تَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٢٧﴾
27. Unauingiza usiku katika mchana na Unauingiza mchana katika usiku; na Unatoa kilicho hai kutokana na kilichomfu na Unatoa kilichomfu kutokana na kilicho hai na Unamruzuku Umtakaye bila ya hesabu.

لَّا يَتَّخِذِ الْمُؤْمِنُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَلَيْسَ مِنَ اللَّـهِ فِي شَيْءٍ إِلَّا أَن تَتَّقُوا مِنْهُمْ تُقَاةً ۗ وَيُحَذِّرُكُمُ اللَّـهُ نَفْسَهُ ۗ وَإِلَى اللَّـهِ الْمَصِيرُ ﴿٢٨﴾ 
28. Waumini hawawafanyi makafiri kuwa wandanai wasaidizi wao badala ya Waumini. Na atakayefanya hivyo, basi hatokua na chochote mbele ya Allaah, isipokuwa mkiwa mnaogopa hatari kutoka kwao. Na Allaah Mwenyewe Anakutahadharisheni Naye. Na kwa Allaah ni mahali pa kuishia.

 قُلْ إِن تُخْفُوا مَا فِي صُدُورِكُمْ أَوْ تُبْدُوهُ يَعْلَمْهُ اللَّـهُ ۗ وَيَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٩﴾
29. Sema: “Mkificha yale yaliyomo katika vifua vyenu au mkiyafichua, Allaah Anayajua. Na Anajua yale yaliyomo katika mbingu na yale yaliyomo katika ardhi. Na Allaah juu ya kila kitu ni Qadiyr.” (Muweza).

يَوْمَ تَجِدُ كُلُّ نَفْسٍ مَّا عَمِلَتْ مِنْ خَيْرٍ مُّحْضَرًا وَمَا عَمِلَتْ مِن سُوءٍ تَوَدُّ لَوْ أَنَّ بَيْنَهَا وَبَيْنَهُ أَمَدًا بَعِيدًا ۗ وَيُحَذِّرُكُمُ اللَّـهُ نَفْسَهُ ۗ وَاللَّـهُ رَءُوفٌ بِالْعِبَادِ ﴿٣٠﴾
30. Siku itayokuta kila nafsi yale iliyoyatenda katika kheri yamehudhurishwa, na yale iliyoyatenda katika maovu, itatamani nafsi lau kama ingelikuwa baina yake na baina hayo (maovu) masafa ya mbali. Na Allaah Anakutahadharisheni Naye (adhabu Yake). Na Allaah ni Rauwf (Mwenye huruma mno) kwa waja.

 قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣١﴾
31. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. Na Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).

قُلْ أَطِيعُوا اللَّـهَ وَالرَّسُولَ ۖ فَإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْكَافِرِينَ ﴿٣٢﴾
32. Sema: “Mtiini Allaah na Rasuli, lakini mkikengeuka basi hakika Allaah Hapendi makafiri.”

إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَىٰ آدَمَ وَنُوحًا وَآلَ إِبْرَاهِيمَ وَآلَ عِمْرَانَ عَلَى الْعَالَمِينَ﴿٣٣﴾
33. Hakika Allaah Amemteua Aadam na Nuwh na kizazi cha Ibraahiym na kizazi cha ‘Imraan juu ya walimwengu.

 ذُرِّيَّةً بَعْضُهَا مِن بَعْضٍ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٣٤﴾
34. Kizazi cha wao kwa wao na Allaah ni Samiy’un-‘Aliym (Mwenye kusikia yote - Mjuzi wa yote).


إِذْ قَالَتِ امْرَأَتُ عِمْرَانَ رَبِّ إِنِّي نَذَرْتُ لَكَ مَا فِي بَطْنِي مُحَرَّرًا فَتَقَبَّلْ مِنِّي ۖ إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٣٥﴾ 
35.  (Taja) Aliposema mke wa ‘Imraan: “Rabb (Mola) wangu, hakika mimi nimeweka nadhiri Kwako kilichomo katika tumbo langu kuwa ni wakfu (kukutumikia), basi nitakabalie. Hakika wewe ni As-Samiy’ul-‘Aliym (Mwenye kusikia yote - Mjuzi wa yote).


 فَلَمَّا وَضَعَتْهَا قَالَتْ رَبِّ إِنِّي وَضَعْتُهَا أُنثَىٰ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا وَضَعَتْ وَلَيْسَ الذَّكَرُ كَالْأُنثَىٰ ۖ وَإِنِّي سَمَّيْتُهَا مَرْيَمَ وَإِنِّي أُعِيذُهَا بِكَ وَذُرِّيَّتَهَا مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ ﴿٣٦﴾
36. Basi alipomzaa akasema: “Rabb (Mola) wangu, hakika mimi nimezaa mwanamke,” na Allaah Anajua zaidi alichokizaa. “Na mwanamme si kama mwanamke. Nami nimemwita Mayram nami namkinga Kwako na kizazi chake kutokana na shaytwaan aliyefukuzwa mbali (na Rahmah ya Allaah).

فَتَقَبَّلَهَا رَبُّهَا بِقَبُولٍ حَسَنٍ وَأَنبَتَهَا نَبَاتًا حَسَنًا وَكَفَّلَهَا زَكَرِيَّا ۖ كُلَّمَا دَخَلَ عَلَيْهَا زَكَرِيَّا الْمِحْرَابَ وَجَدَ عِندَهَا رِزْقًا ۖ قَالَ يَا مَرْيَمُ أَنَّىٰ لَكِ هَـٰذَا ۖ قَالَتْ هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ ۖ إِنَّ اللَّـهَ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٣٧﴾ 
37. Basi Rabb (Mola) wake Akampokea kwa kabuli njema na Akamkuza mkuzo mzuri na Akamfanya Zakariyyaa kuwa mlezi wake. Kila Zakariyyaa alipoingia kwake (katika) chumba cha kuswalia alikuta iko kwake riziki (chakula) Akasema: “Ee Maryam! Umepata wapi hivi? ”Akasema: “Hivi ni kutoka kwa Allaah.  Hakika Allaah Anamruzuku Amtakaye bila ya hesabu.”

 هُنَالِكَ دَعَا زَكَرِيَّا رَبَّهُ ۖ قَالَ رَبِّ هَبْ لِي مِن لَّدُنكَ ذُرِّيَّةً طَيِّبَةً ۖ إِنَّكَ سَمِيعُ الدُّعَاءِ ﴿٣٨﴾
38. Hapo hapo Zakariyyaa akamwomba Rabb (Mola) wake, akasema: “Rabb wangu Nitunukie kutoka Kwako kizazi chema hakika Wewe ni Samiy’u (Mwenye kusikia) du’aa yangu.”

فَنَادَتْهُ الْمَلَائِكَةُ وَهُوَ قَائِمٌ يُصَلِّي فِي الْمِحْرَابِ أَنَّ اللَّـهَ يُبَشِّرُكَ بِيَحْيَىٰ مُصَدِّقًا بِكَلِمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَسَيِّدًا وَحَصُورًا وَنَبِيًّا مِّنَ الصَّالِحِينَ﴿٣٩﴾
39. Basi mara Malaika akamwita (Zakariyyaa) naye akiwa amesimama anaswali katika chumba kwamba: “Hakika Allaah Anakubashiria Yahyaa mwenye kusadikisha Neno (la Kun! Akazaliwa Nabiy ‘Iysaa (عليه السلام kutoka kwa Allaah na ni bwana mwenye sifa nzuri na anayejitenga mbali na matamanio na Nabiy miongoni mwa Swalihina.”

قَالَ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَقَدْ بَلَغَنِيَ الْكِبَرُ وَامْرَأَتِي عَاقِرٌ ۖ قَالَ كَذَٰلِكَ اللَّـهُ يَفْعَلُ مَا يَشَاءُ ﴿٤٠﴾
40. (Zakariyyaa) Akasema: “Nitapataje ghulamu na hali uzee umeshanifikia na mke wangu ni tasa?!” Akasema: “Hivyo ndivyo Allaah Anafanya Atakavyo”

قَالَ رَبِّ اجْعَل لِّي آيَةً ۖ قَالَ آيَتُكَ أَلَّا تُكَلِّمَ النَّاسَ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ إِلَّا رَمْزًا ۗ وَاذْكُر رَّبَّكَ كَثِيرًا وَسَبِّحْ بِالْعَشِيِّ وَالْإِبْكَارِ ﴿٤١﴾ 
41. (Zakariyyaa) Akasema: “Rabb (Mola) wangu niwekee Aayah (ishara, dalili)” Akasema: Aayah yako (kuwa ameshika mimba) ni kwamba hutowasemesha watu siku tatu ila kwa kuashiria tu. Na mdhukuru Rabb wako kwa wingi na msabbih jioni na asubuhi.”

وَإِذْ قَالَتِ الْمَلَائِكَةُ يَا مَرْيَمُ إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَاكِ وَطَهَّرَكِ وَاصْطَفَاكِ عَلَىٰ نِسَاءِ الْعَالَمِينَ﴿٤٢
42. Na (Taja) waliposema Malaika: “Ee Maryam! Hakika Allaah Amekuteua na Amekutakasa na Amekuteua juu ya wanawake wa walimwengu.”

 يَا مَرْيَمُ اقْنُتِي لِرَبِّكِ وَاسْجُدِي وَارْكَعِي مَعَ الرَّاكِعِينَ﴿٤٣﴾
43. “Ee Maryam!  Kuwa mtiifu kwa Rabb (Mola) wako, na sujudu, na rukuu pamoja na wanaorukuu”.

ذَٰلِكَ مِنْ أَنبَاءِ الْغَيْبِ نُوحِيهِ إِلَيْكَ ۚ وَمَا كُنتَ لَدَيْهِمْ إِذْ يُلْقُونَ أَقْلَامَهُمْ أَيُّهُمْ يَكْفُلُ مَرْيَمَ وَمَا كُنتَ لَدَيْهِمْ إِذْ يَخْتَصِمُونَ ﴿٤٤﴾ 
44. Hizo ni habari za ghayb Tunakufunulia Wahy (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).  Na hukuwa pamoja nao walipotupa kalamu zao, (ili) nani kati yao amlee Maryam. Na hukuwa pamoja nao walipokhasimiana.


 إِذْ قَالَتِ الْمَلَائِكَةُ يَا مَرْيَمُ إِنَّ اللَّـهَ يُبَشِّرُكِ بِكَلِمَةٍ مِّنْهُ اسْمُهُ الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ وَجِيهًا فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَمِنَ الْمُقَرَّبِينَ﴿٤٥﴾
45. (Taja) Waliposema Malaika: “Ee Maryam! Hakika Allaah Anakubashiria neno (la Kun!) kutoka Kwake (azaliwe mwana bila ya kujamiiwa) jina lake ni al-Masiyhu ‘Iysaa mwana wa Maryam, mwenye taadhima katika dunia na Aakhirah na ni miongoni mwa waliokurubishwa (kwa Allaah).

وَيُكَلِّمُ النَّاسَ فِي الْمَهْدِ وَكَهْلًا وَمِنَ الصَّالِحِينَ﴿٤٦﴾
46. Na Atawasemesha watu katika utoto wake na utu uzima wake na ni miongoni mwa Swalihina.

قَالَتْ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي وَلَدٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِي بَشَرٌ ۖ قَالَ كَذَٰلِكِ اللَّـهُ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ ۚ إِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٤٧﴾
47. (Maryam) Akasema: “Itakuwaje nipate waladi na hali hakunigusa mtu?” (Malaika) Akasema: “Hivyo ndivyo Allaah Huumba Akitakacho. Anapokidhia jambo basi huliambia: ‘Kun!’ (Kuwa) nalo huwa.”

 وَيُعَلِّمُهُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَالتَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ﴿٤٨﴾
48.  “Na Atamfunza Kitabu na Hikmah na Tawraat na Injiyl.”

 وَرَسُولًا إِلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنِّي قَدْ جِئْتُكُم بِآيَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ ۖ أَنِّي أَخْلُقُ لَكُم مِّنَ الطِّينِ كَهَيْئَةِ الطَّيْرِ فَأَنفُخُ فِيهِ فَيَكُونُ طَيْرًا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۖ وَأُبْرِئُ الْأَكْمَهَ وَالْأَبْرَصَ وَأُحْيِي الْمَوْتَىٰ بِإِذْنِ اللَّـهِ ۖ وَأُنَبِّئُكُم بِمَا تَأْكُلُونَ وَمَا تَدَّخِرُونَ فِي بُيُوتِكُمْ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٤٩﴾
49. “Na ni Rasuli kwa wana wa Israaiyl (akisema), Hakika mimi nimekujieni na Aayah (ishara, dalili n.k) kutoka kwa Rabb (Mola) wenu, kwamba nakuumbieni kutokana na udongo kama umbo la ndege, kisha napuliza humo basi huwa ndege kwa idhini ya Allaah. Na naponyesha vipofu na wenye ubarasi na nahuisha wafu kwa idhini ya Allaah. Na nakujulisheni mtakavyokula na mtakavyoweka akiba majumbani mwenu. Hakika katika hayo bila shaka kuna Aayah kwenu mkiwa Waumini”.

 وَمُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَلِأُحِلَّ لَكُم بَعْضَ الَّذِي حُرِّمَ عَلَيْكُمْ ۚ وَجِئْتُكُم بِآيَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿٥٠﴾
50. “Na mwenye kusadikisha yaliyo kabla yangu katika Tawraat na ili nikuhalalishieni baadhi ya yale yaliyoharamishwa kwenu. Na nimekujieni na Aayah (ishara, hoja n.k) kutoka kwa Rabb (Mola) wenu. Basi mcheni Allaah na nitiini.”

 إِنَّ اللَّـهَ رَبِّي وَرَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۗ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ ﴿٥١﴾
51.  “Hakika Allaah ni Rabb (Mola) wangu na Rabb wenu basi mwabuduni. Hii ndio njia iliyonyooka.”

 فَلَمَّا أَحَسَّ عِيسَىٰ مِنْهُمُ الْكُفْرَ قَالَ مَنْ أَنصَارِي إِلَى اللَّـهِ ۖ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ نَحْنُ أَنصَارُ اللَّـهِ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَاشْهَدْ بِأَنَّا مُسْلِمُونَ ﴿٥٢﴾
52. Basi alipohisi ‘Iysaa ukafiri (umeshitadi) kutoka kwao; alisema: “Nani wanusuruji wangu kwa ajili ya Allaah? Wakasema wafuasi watifu:  “Sisi Answaaru-Allaah. Tumemwamini Allaah na shuhudia kwamba sisi ni Waislamu (tunajisalimisha kwa Allaah).”

رَبَّنَا آمَنَّا بِمَا أَنزَلْتَ وَاتَّبَعْنَا الرَّسُولَ فَاكْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِينَ﴿٥٣﴾
53. “Rabb (Mola) wetu, tumeamini Uliyoyateremsha na tumemfuata Rasuli basi tuandike pamoja na wanaoshuhudia (haki).

وَمَكَرُوا وَمَكَرَ اللَّـهُ ۖ وَاللَّـهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ ﴿٥٤﴾
54. Na wakapanga njama (kumuua Nabiy ‘Iysaa), lakini Allaah Akapanga (kuwalipiza) njama. Na Allaah ni Mbora wa (kurudisha) mipango ya njama.

إِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَىٰ إِنِّي مُتَوَفِّيكَ وَرَافِعُكَ إِلَيَّ وَمُطَهِّرُكَ مِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا وَجَاعِلُ الَّذِينَ اتَّبَعُوكَ فَوْقَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ ۖ ثُمَّ إِلَيَّ مَرْجِعُكُمْ فَأَحْكُمُ بَيْنَكُمْ فِيمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ ﴿٥٥﴾ 
55. (Taja) Aliposema Allaah: “Ee ‘Iysaa, hakika Mimi ni Mwenye kukuchukua na Mwenye kukupandisha Kwangu na Mwenye kukutakasa kutokana na wale waliokufuru na Nitawafanya wale waliokufuata (kujisalimisha kwa Allaah Pekee) kuwa juu ya wale waliokufuru mpaka Siku ya Qiyaamah, kisha Kwangu ndio marejeo yenu Nitahukumu baina yenu katika yale mliyokuwa kwayo mkikhitilafiana.”

فَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا فَأُعَذِّبُهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ﴿٥٦﴾
56. Basi wale waliokufuru, Nitawaadhibu adhabu kali katika dunia na Aakhirah, na hawatopata yeyote mwenye kunusuru.

وَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَيُوَفِّيهِمْ أُجُورَهُمْ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الظَّالِمِينَ ﴿٥٧﴾
57. Ama wale waliomini na wakatenda mema, basi Atawalipa ujira wao kikamilifu. Na Allaah Hapendi madhalimu.

ذَٰلِكَ نَتْلُوهُ عَلَيْكَ مِنَ الْآيَاتِ وَالذِّكْرِ الْحَكِيمِ﴿٥٨﴾
58. Hizo Tunakusomea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika Aayaat (Zetu) na ukumbusho wenye hikmah.


إِنَّ مَثَلَ عِيسَىٰ عِندَ اللَّـهِ كَمَثَلِ آدَمَ ۖ خَلَقَهُ مِن تُرَابٍ ثُمَّ قَالَ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٥٩﴾
59. Hakika mfano wa ‘Iysaa kwa Allaah ni kama mfano wa Aadam. Amemuumba kutokana na udongo kisha Akamwambia: ‘Kun’ (Kuwa) basi akawa.

الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُن مِّنَ الْمُمْتَرِينَ﴿٦٠﴾
60. Haki kutoka kwa Rabb (Mola) wako, basi usiwe miongoni mwa wanaotia shaka.


فَمَنْ حَاجَّكَ فِيهِ مِن بَعْدِ مَا جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ فَقُلْ تَعَالَوْا نَدْعُ أَبْنَاءَنَا وَأَبْنَاءَكُمْ وَنِسَاءَنَا وَنِسَاءَكُمْ وَأَنفُسَنَا وَأَنفُسَكُمْ ثُمَّ نَبْتَهِلْ فَنَجْعَل لَّعْنَتَ اللَّـهِ عَلَى الْكَاذِبِينَ﴿٦١﴾
61. Basi yeyote atakayekuhoji kwayo baada ya kukujia elimu, basi sema: “Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu, na nafsi zetu, na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu, tuifanye laana ya Allaah iwe juu ya waongo (kati yetu).

 إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ الْقَصَصُ الْحَقُّ ۚ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا اللَّـهُ ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٦٢﴾
62. Hakika haya ni masimulizi ya haki. Na hapana ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Allaah. Na hakika Allaah Yeye Ndiye Al-‘Aziyzul-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika - Mwenye hikmah wa yote).


فَإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِالْمُفْسِدِينَ﴿٦٣﴾
63. Wakikengeuka, basi hakika Allaah ni Aliym (Mjuzi) wa mafisadi.

 قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّـهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ ﴿٦٤﴾
64. Sema: “Enyi Ahlal-Kitaabi! Njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu, kwamba tusiabudu isipokuwa Allaah Pekee, na wala tusimshirikishe na chochote, na wala wasichukue baadhi yetu wengine (kuwa) waungu badala ya Allaah.” Wakikengeuka; basi semeni: “Shuhudieni kwamba sisi ni Waislamu. (tunajisalimisha kwa Allaah).”

يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تُحَاجُّونَ فِي إِبْرَاهِيمَ وَمَا أُنزِلَتِ التَّوْرَاةُ وَالْإِنجِيلُ إِلَّا مِن بَعْدِهِ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٦٥﴾
65. Enyi Ahlal-Kitaabi! Kwanini mnahojiana kuhusu Ibraahiym na hali haikuteremshwa Tawraat na Injiyl isipokuwa baada yake? Je, hamtii akilini?

هَا أَنتُمْ هَـٰؤُلَاءِ حَاجَجْتُمْ فِيمَا لَكُم بِهِ عِلْمٌ فَلِمَ تُحَاجُّونَ فِيمَا لَيْسَ لَكُم بِهِ عِلْمٌ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٦٦﴾
66. Ha! Nyinyi ndio hawa mliohojiana katika yale ambayo mnayo elimu nayo, basi kwa nini (sasa) mnahojiana katika yale msiyokuwa na elimu nayo? Na Allaah Anajua na nyinyi hamjui.

مَا كَانَ إِبْرَاهِيمُ يَهُودِيًّا وَلَا نَصْرَانِيًّا وَلَـٰكِن كَانَ حَنِيفًا مُّسْلِمًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ﴿٦٧﴾
67. Hakuwa Ibraahiym Yahudi wala Naswara; lakini alikuwa haniyfaa (aliyejiengua na upotofu akaelemea Dini ya haki), Muislamu na hakuwa miongoni mwa washirikna.

إِنَّ أَوْلَى النَّاسِ بِإِبْرَاهِيمَ لَلَّذِينَ اتَّبَعُوهُ وَهَـٰذَا النَّبِيُّ وَالَّذِينَ آمَنُوا ۗ وَاللَّـهُ وَلِيُّ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٦٨﴾
68. Hakika watu waliokaribu zaidi kwa Ibraahiym ni wale waliomfuata na huyu Nabiy (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na wale walioamini. Na Allaah ni Waliyyu (Mlinzi, Msaidizi) wa Waumini.


وَدَّت طَّائِفَةٌ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَوْ يُضِلُّونَكُمْ وَمَا يُضِلُّونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ﴿٦٩﴾ 
69. Linatamani kundi katika Ahlil-Kitaabi kama wangelikupotezeni, lakini hawapotezi ila nafsi zao na hawahisi.

يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَأَنتُمْ تَشْهَدُونَ﴿٧٠﴾
70. Enyi Ahlal-Kitaabi! Kwanini mnakanusha Aayaat za Allaah na hali nyinyi mnashuhudia?

 يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَلْبِسُونَ الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُونَ الْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ﴿٧١﴾
71. Enyi Ahlal-Kitaabi!  Kwanini mnachanganya haki na batili na mnaficha haki na hali nyinyi mnajua?

وَقَالَت طَّائِفَةٌ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ آمِنُوا بِالَّذِي أُنزِلَ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَجْهَ النَّهَارِ وَاكْفُرُوا آخِرَهُ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ﴿٧٢﴾
72. Na kundi miongoni mwa Ahlil-Kitaabi likasema (kuambiana): “Aminini yale ambayo yameteremshwa kwa wale walioamini mwanzo wa mchana na kanusheni mwisho wake, wapate kurejea (waache dini yao).”

وَلَا تُؤْمِنُوا إِلَّا لِمَن تَبِعَ دِينَكُمْ قُلْ إِنَّ الْهُدَىٰ هُدَى اللَّـهِ أَن يُؤْتَىٰ أَحَدٌ مِّثْلَ مَا أُوتِيتُمْ أَوْ يُحَاجُّوكُمْ عِندَ رَبِّكُمْ ۗ قُلْ إِنَّ الْفَضْلَ بِيَدِ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٧٣﴾ 
73. “Na wala msimwamini isipokuwa yule anayefuata dini yenu”. Sema: “Hakika mwongozo wa (kweli) ni Mwongozo wa Allaah, (mnakhofu) kwamba atapewa mmoja (elimu) mfano wa yale mliyopewa au wakuhojini mbele ya Rabb (Mola) wenu” Sema: “Hakika fadhila zi Mkononi mwa Allaah; Humpa Amtakaye. Na Allaah ni Waasi’un-‘Aliym (Mwenye wasaa - Mjuzi wa yote).

يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿٧٤﴾
74. Humchagua kwa Rahmah Yake Amtakaye; na Allaah ni Mwenye fadhila adhimu.

وَمِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ مَنْ إِن تَأْمَنْهُ بِقِنطَارٍ يُؤَدِّهِ إِلَيْكَ وَمِنْهُم مَّنْ إِن تَأْمَنْهُ بِدِينَارٍ لَّا يُؤَدِّهِ إِلَيْكَ إِلَّا مَا دُمْتَ عَلَيْهِ قَائِمًا ۗ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا لَيْسَ عَلَيْنَا فِي الْأُمِّيِّينَ سَبِيلٌ وَيَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٧٥﴾
75. Na katika Ahlil-Kitaab yuko ambaye ukimpa amana ya mrundi (wa mali) atakurejeshea, na katika wao yuko ambaye ukimpa amana ya dinari moja (tu) hatoirudisha kwako isipokuwa utakapodumisha kumsimamia (kumdai). Hilo ni kwa sababu wao wamesema: “Hakuna juu yetu lawama kwa ummiyyiyn (wasiojua kusoma na kuandika)” na wanamsingizia uongo Allaah, na hali wao wanajua.

بَلَىٰ مَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِ وَاتَّقَىٰ فَإِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَّقِينَ﴿٧٦﴾
76. Bali sivyo! Atakayetimiza ahadi yake akawa na taqwa, basi hakika Allaah Anapenda wamchao Allaah.

إِنَّ الَّذِينَ يَشْتَرُونَ بِعَهْدِ اللَّـهِ وَأَيْمَانِهِمْ ثَمَنًا قَلِيلًا أُولَـٰئِكَ لَا خَلَاقَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ اللَّـهُ وَلَا يَنظُرُ إِلَيْهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٧٧﴾
77. Hakika wale wanaobadili ahadi ya Allaah na viapo vyao kwa thamani ndogo; hao hawana sehemu yoyote katika Aakhirah na wala Allaah Hatowasemesha na wala Hatowatazama Siku Ya Qiyaamah na wala Hatowatakasa na watapata adhabu iumizayo.

 وَإِنَّ مِنْهُمْ لَفَرِيقًا يَلْوُونَ أَلْسِنَتَهُم بِالْكِتَابِ لِتَحْسَبُوهُ مِنَ الْكِتَابِ وَمَا هُوَ مِنَ الْكِتَابِ وَيَقُولُونَ هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ وَمَا هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ وَيَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ وَهُمْ يَعْلَمُونَ﴿٧٨﴾
78. Na hakika miongoni mwao kuna kundi wanaopinda ndimi zao kwa (kusoma) Kitabu ili mdhanie kuwa hayo ni yanayotoka katika Kitabu, na hali hayo si yenye kutoka katika Kitabu, na wanasema: “Hayo ni kutoka kwa Allaah”; na hali hayo si kutoka kwa Allaah na wanamsingizia uongo Allaah na wao wanajua.

مَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُؤْتِيَهُ اللَّـهُ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ ثُمَّ يَقُولَ لِلنَّاسِ كُونُوا عِبَادًا لِّي مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَـٰكِن كُونُوا رَبَّانِيِّينَ بِمَا كُنتُمْ تُعَلِّمُونَ الْكِتَابَ وَبِمَا كُنتُمْ تَدْرُسُونَ﴿٧٩﴾
79. Haiwi (mustahili) kwa mtu kwamba Allaah Amempa Kitabu na Al-Hukma (hukumu, mamlaka, ufakihi wa shariy’ah n.k) na Unabii kisha awaambie watu: “Kuweni wenye kuniabudu mimi badala ya Allaah” Bali (atawaambia): “Kuweni Rabbaaniyyiyn (‘Ulamaa wenye taqwa wanaofanyia kazi elimu zao) kwa yale mliyokuwa mkiyafundisha ya Kitabu na kwa yale mliyokuwa mkiyasoma.”

وَلَا يَأْمُرَكُمْ أَن تَتَّخِذُوا الْمَلَائِكَةَ وَالنَّبِيِّينَ أَرْبَابًا ۗ أَيَأْمُرُكُم بِالْكُفْرِ بَعْدَ إِذْ أَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿٨٠﴾ 
80. Na wala hakuamuruni kuwachukua Malaika na Manabii kuwafanya miungu. Je anakuamrisheni ukafiri baada ya nyinyi kuwa Waislamu (waliojisalimisha kwa Allaah)?

وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ النَّبِيِّينَ لَمَا آتَيْتُكُم مِّن كِتَابٍ وَحِكْمَةٍ ثُمَّ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مُّصَدِّقٌ لِّمَا مَعَكُمْ لَتُؤْمِنُنَّ بِهِ وَلَتَنصُرُنَّهُ ۚ قَالَ أَأَقْرَرْتُمْ وَأَخَذْتُمْ عَلَىٰ ذَٰلِكُمْ إِصْرِي ۖ قَالُوا أَقْرَرْنَا ۚ قَالَ فَاشْهَدُوا وَأَنَا مَعَكُم مِّنَ الشَّاهِدِينَ ﴿٨١﴾
81. Na (kumbukeni enyi watu wa Kitabu) Alipochukua Allaah fungamano kwa Manabii (akawaambia) “Kwa yale niliyokupeni kutoka kitabu na hikmah, kisha akakujieni Rasuli (ambaye ni Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) mwenye kusadikisha yaliyo pamoja nanyi; ni juu yenu kumwamini na kumnusuru.” (Kisha Allaah): Akasema “Je, mmekiri na mmekubali kuchukua juu ya hayo fungamano zito Langu?” Wakasema: “Tumekiri”. (Allaah) Akasema: “Basi shuhudieni na Mimi Niko pamoja nanyi katika wenye kushuhudia.

فَمَن تَوَلَّىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ﴿٨٢﴾
82. Basi atakayekengeuka baada ya hayo, basi hao ni mafasiki.

أَفَغَيْرَ دِينِ اللَّـهِ يَبْغُونَ وَلَهُ أَسْلَمَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَإِلَيْهِ يُرْجَعُونَ﴿٨٣﴾
83. Je, wanataka dini isiyokuwa ya Allaah, na hali amejisalimisha Kwake kila aliye katika mbingu na katika ardhi akipenda asipende na Kwake watarejeshwa.

قُلْ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ عَلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ عَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَالنَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ﴿٨٤﴾
84. Sema: “Tumemwamini Allaah, na yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwa Ibraahiym, na Ismaa’iyl na Is-haaq, na Ya’quwb na al-Asbaatw (Makabila ya wana wa Ya’quwb عليه السلام waliotoka Manabii) na yale aliyopewa Muwsaa na ‘Iysaa na Manabii kutoka kwa Rabb (Mola) wao, hatutofautishi baina ya mmoja yeyote miongoni mwao, nasi Kwake tumejisalimisha (katika Uislamu).

 وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ﴿٨٥﴾
85. Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake; naye katika Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.


كَيْفَ يَهْدِي اللَّـهُ قَوْمًا كَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ وَشَهِدُوا أَنَّ الرَّسُولَ حَقٌّ وَجَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٨٦﴾ 
86. Vipi Allaah Atawaongoza watu waliokufuru baada ya kuamini kwao na wakashuhudia kwamba Rasuli ni haki na zikawajia hoja bayana? Na Allaah Hawaongozi watu madhalimu.

 أُولَـٰئِكَ جَزَاؤُهُمْ أَنَّ عَلَيْهِمْ لَعْنَةَ اللَّـهِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ﴿٨٧﴾
87. Hao jazaa yao ni kwamba juu yao ipo laana ya Allaah na ya Malaika na watu wote.

خَالِدِينَ فِيهَا لَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ﴿٨٨﴾
88. Wenye kudumu humo hawatopunguziwa adhabu wala hawatopewa muda wa kuakhirishwa adhabu.

إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ وَأَصْلَحُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٨٩﴾
89. Isipokuwa wale waliotubu baada ya hayo na wakatengenea, basi hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ ثُمَّ ازْدَادُوا كُفْرًا لَّن تُقْبَلَ تَوْبَتُهُمْ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الضَّالُّونَ﴿٩٠﴾ 
90. Hakika wale waliokufuru baada ya kuamini kwao kisha wakazidi kukufuru; haitokubaliwa tawbah yao, na hao ndio waliopotoka.

 إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَمَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ فَلَن يُقْبَلَ مِنْ أَحَدِهِم مِّلْءُ الْأَرْضِ ذَهَبًا وَلَوِ افْتَدَىٰ بِهِ ۗ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٩١﴾
91. Hakika wale waliokufuru na wakafa nao wakiwa makafiri, basi haitakubaliwa kutoka kwa mmoja wao (fidia ya) dhahabu ya kujaza dunia nzima lau wakitaka kujikombolea nayo. Hao watapata adhabu iumizayo na hawatopata mwenye kuwanusuru.

 لَن تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّىٰ تُنفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِن شَيْءٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٩٢﴾
92. Hamtoweza kuufikia wema (thawabu za kupata Jannah) mpaka mtoe (katika njia ya Allaah) katika vile mnavyovipenda. Na kitu chochote mnachotoa basi hakika Allaah kwacho ni ‘Aliym (Mjuzi).

 كُلُّ الطَّعَامِ كَانَ حِلًّا لِّبَنِي إِسْرَائِيلَ إِلَّا مَا حَرَّمَ إِسْرَائِيلُ عَلَىٰ نَفْسِهِ مِن قَبْلِ أَن تُنَزَّلَ التَّوْرَاةُ ۗ قُلْ فَأْتُوا بِالتَّوْرَاةِ فَاتْلُوهَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٩٣﴾
93. Kila chakula kilikuwa halaal kwa wana wa Israaiyl, isipokuwa kile alichojiharamishia Israaiyl (Ya’quwb) mwenyewe kabla ya kuteremshwa Tawraat. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Basi leteni Tawraat kisha muisome mkiwa wakweli.”


فَمَنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ﴿٩٤﴾
94. Na yeyote atakayemtungia Allaah uongo baada ya hayo; basi hao ndio madhalimu.

قُلْ صَدَقَ اللَّـهُ ۗ فَاتَّبِعُوا مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٩٥﴾
95. Sema: “Allaah Amesema kweli.” Basi fuateni millah ya Ibraahiym haniyfaa (aliyejiengua na upotofu akaelemea Dini ya haki) na hakuwa miongoni mwa washirikina.

إِنَّ أَوَّلَ بَيْتٍ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِي بِبَكَّةَ مُبَارَكًا وَهُدًى لِّلْعَالَمِينَ﴿٩٦﴾ 
96. Hakika nyumba ya awali iliyowekwa kwa ajili ya watu (kufanya ‘ibaadah) ni ile ambayo iko Bakkah (Makkah), yenye barakah na mwongozo kwa walimwengu.

فِيهِ آيَاتٌ بَيِّنَاتٌ مَّقَامُ إِبْرَاهِيمَ ۖ وَمَن دَخَلَهُ كَانَ آمِنًا ۗ وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ ﴿٩٧﴾ 
97. Ndani yake kuna Aayaat (ishara, dalili) zilizo wazi; mahali pa kisimamo cha Ibraahiym. Na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Allaah ni wajibu kwa watu watekeleze Hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo. Na atakayekufuru, basi hakika Allaah ni Ghaniyy (Mkwasi) kwa walimwengu.


قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَاللَّـهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا تَعْمَلُونَ﴿٩٨﴾ 
98. Sema: “Enyi Ahlal-Kitaabi! Kwa nini mnakanusha Aayaat za Allaah; na hali Allaah ni Shahiyd (Mwenye kushuhudia) juu ya myatendayo?”

قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ مَنْ آمَنَ تَبْغُونَهَا عِوَجًا وَأَنتُمْ شُهَدَاءُ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٩٩﴾ 
99. Sema: “Enyi Ahlal-Kitaabi! Kwanini mnamzuilia aliyeamini njia ya Allaah mnaitafutia upotofu na hali nyinyi mashahidi (juu ya haki)? Na Allaah si Mwenye kughafilika kuhusu myatendayo.”

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تُطِيعُوا فَرِيقًا مِّنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ يَرُدُّوكُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ كَافِرِينَ﴿١٠٠﴾
100. Enyi mlioamini! Mkilitii kundi la waliopewa Kitabu watakurudisheni baada ya kuamini kwenu (muwe) makafiri.

وَكَيْفَ تَكْفُرُونَ وَأَنتُمْ تُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ آيَاتُ اللَّـهِ وَفِيكُمْ رَسُولُهُ ۗ وَمَن يَعْتَصِم بِاللَّـهِ فَقَدْ هُدِيَ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿١٠١﴾
101. Na vipi mkufuru na hali mnasomewa Aayaat za Allaah na Rasuli yuko kati yenu? Na atakayeshikamana na Allaah basi kwa yakini ameongozwa kuelekea njia iliyonyooka.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ﴿١٠٢﴾
102. Enyi mlioamini! Mcheni Allaah kama apasavyo kuogopwa na wala msife isipokuwa nyinyi (mmeshakuwa) ni Waislamu (wanaojisalimisha kwa Allaah).

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا ۚ وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِ إِخْوَانًا وَكُنتُمْ عَلَىٰ شَفَا حُفْرَةٍ مِّنَ النَّارِ فَأَنقَذَكُم مِّنْهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ﴿١٠٣﴾ 
103. Na shikamaneni kwa kamba ya Allaah nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Allaah kwenu, pale mlipokuwa maadui (kati yenu); kisha Akaunganisha nyoyo zenu, mkawa kwa neema Yake ndugu; na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto Akakuokoeni humo. Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat Zake mpate kuongoka.

وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿١٠٤﴾
104. Na uweko (watokeze) kutoka kwenu umati (wa watu) unaolingania kheri na unaoamrisha ma’-ruwf (mema) na unaokataza munkari. Na hao ndio waliofaulu.

وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ تَفَرَّقُوا وَاخْتَلَفُوا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ ۚ وَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١٠٥﴾
105. Na wala msiwe kama wale waliofarikiana na wakakhitilafiana baada ya kuwajia hoja bayana. Na hao watapata adhabu kuu.


يَوْمَ تَبْيَضُّ وُجُوهٌ وَتَسْوَدُّ وُجُوهٌ ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ اسْوَدَّتْ وُجُوهُهُمْ أَكَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ ﴿١٠٦﴾ 
106. Siku (baadhi ya) nyuso zitakuwa nyeupe na (nyingine) zitakuwa nyeusi. Basi wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeusi (wataambiwa): “Je mlikufuru baada ya kuamini kwenu?!  Basi onjeni adhabu kwa yale mliyokuwa mkikufuru.”

 وَأَمَّا الَّذِينَ ابْيَضَّتْ وُجُوهُهُمْ فَفِي رَحْمَةِ اللَّـهِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴿١٠٧﴾
107. Na wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeupe; basi (watakuwa) katika Rahmah ya Allaah. Wao humo ni wenye kudumu.

تِلْكَ آيَاتُ اللَّـهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِالْحَقِّ ۗ وَمَا اللَّـهُ يُرِيدُ ظُلْمًا لِّلْعَالَمِينَ ﴿١٠٨﴾
108. Hizi ni Aayaat za Allaah Tunakusomea kwa haki (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na Allaah Hataki dhulma kwa walimwengu.


وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ وَإِلَى اللَّـهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ ﴿١٠٩﴾
109. Na ni vya Allaah Pekee vilivyomo katika mbingu na katika ardhi. Na kwa Allaah Pekee mambo (yote) yatarejeshwa.

 كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ ۗ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم ۚ مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿١١٠﴾
110.  Mmekuwa Ummah bora kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu; mnaamrisha ma’-ruwf (mema) na mnakataza munkari na mnamwamini Allaah. Na lau wangeliamini Ahlul-Kitaabi ingelikuwa ni bora kwao, miongoni mwao wanaoamini na wengi wao ni mafasiki.

لَن يَضُرُّوكُمْ إِلَّا أَذًى ۖ وَإِن يُقَاتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنصَرُونَ ﴿١١١﴾
111. Hawatokudhuruni isipokuwa udhia tu, na wakikupigeni vita watakupeni migongo, kisha hawatonusuriwa.

ضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ أَيْنَ مَا ثُقِفُوا إِلَّا بِحَبْلٍ مِّنَ اللَّـهِ وَحَبْلٍ مِّنَ النَّاسِ وَبَاءُوا بِغَضَبٍ مِّنَ اللَّـهِ وَضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الْمَسْكَنَةُ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانُوا يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَيَقْتُلُونَ الْأَنبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ ۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ ﴿١١٢﴾ 
112. Wamepigwa na udhalili, popote wanapopatikana isipokuwa kwa ahadi ya Allaah na kwa (kushika) kamba ya watu (Waislamu) na wakastahiki ghadhabu kutoka kwa Allaah, na wakapigwa na umasikini. Hivyo kwa kuwa walikuwa wakikanusha Aayaat (na ishara, hoja n.k) za Allaah; na wakiua Nabiy pasi na haki. Hivyo ni kwa sababu ya kuasi kwao na walikuwa wanataadi.

لَيْسُوا سَوَاءً ۗ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَائِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللَّـهِ آنَاءَ اللَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ ﴿١١٣﴾
113. Hawako sawa sawa; miongoni mwa Ahlil-Kitaabi (wako) watu wenye kusimama (kwa utiifu) wanasoma Aayaat za Allaah nyakati za usiku na wao wanasujudu (katika Swalaah).

يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَأُولَـٰئِكَ مِنَ الصَّالِحِينَ﴿١١٤﴾
114. Wanamwamini Allaah na Siku ya Mwisho na wanaamrisha ma’-ruwf (mema) na wanakataza munkari na wanakimbilia katika mambo ya kheri, na hao ni miongoni mwa Swalihina.

وَمَا يَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَلَن يُكْفَرُوهُ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالْمُتَّقِينَ ﴿١١٥﴾
115. Na kheri yoyote waifanyayo hawatakanushiwa (thawabu zake).  Na Allaah ni ‘Aliym (Mjuzi) wa wenye taqwa.

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَن تُغْنِيَ عَنْهُمْ أَمْوَالُهُمْ وَلَا أَوْلَادُهُم مِّنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۖ وَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۚ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿١١٦﴾
116.  Hakika wale waliokufuru hazitowafaa kitu mali zao na wala auladi wao mbele ya Allaah; na hao ni watu wa Motoni wao humo ni wenye kudumu.


مَثَلُ مَا يُنفِقُونَ فِي هَـٰذِهِ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَثَلِ رِيحٍ فِيهَا صِرٌّ أَصَابَتْ حَرْثَ قَوْمٍ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ فَأَهْلَكَتْهُ ۚ وَمَا ظَلَمَهُمُ اللَّـهُ وَلَـٰكِنْ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿١١٧﴾ 
117. Mfano wa vile wanavyovitoa katika uhai (wao) huu wa duniani ni kama mfano wa upepo ndani yake mna baridi ya barafu, ukasibu shamba lilolimwa la watu waliojidhulumu nafsi zao ukaliangamiza. Na Allaah Hakuwadhulumu lakini wamejidhulumu nafsi zao.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا بِطَانَةً مِّن دُونِكُمْ لَا يَأْلُونَكُمْ خَبَالًا وَدُّوا مَا عَنِتُّمْ قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاءُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ ۚ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الْآيَاتِ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ ﴿١١٨﴾
118. Enyi mlioamini! Msifanye rafiki mwandani na msiri (wenu) wasiokuwa nyinyi. Hawatoacha kukuharibieni. Wanatamani kama mngetaabika. Imekwishajitokeza bughudha kutoka midomoni mwao. Na yale yanayoficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni Aayaat (na ishara, hoja, dalili) mkiwa mtatia akilini.

هَا أَنتُمْ أُولَاءِ تُحِبُّونَهُمْ وَلَا يُحِبُّونَكُمْ وَتُؤْمِنُونَ بِالْكِتَابِ كُلِّهِ وَإِذَا لَقُوكُمْ قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَوْا عَضُّوا عَلَيْكُمُ الْأَنَامِلَ مِنَ الْغَيْظِ ۚ قُلْ مُوتُوا بِغَيْظِكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿١١٩﴾ 
119. Ha! Nyinyi ndio wale mnaowapenda na wala wao hawakupendeni, na mnaamini Kitabu chote; na wanapokukuteni husema: “Tumeamini” na wanapokuwa peke yao wanakutafunieni ncha za vidole kutokana na chuki. Sema: “Kufeni kwa chuki zenu.” Hakika Allaah ni ‘Aliym (Mjuzi) kwa yaliyomo vifuani.

إِن تَمْسَسْكُمْ حَسَنَةٌ تَسُؤْهُمْ وَإِن تُصِبْكُمْ سَيِّئَةٌ يَفْرَحُوا بِهَا ۖ وَإِن تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا لَا يَضُرُّكُمْ كَيْدُهُمْ شَيْئًا ۗ إِنَّ اللَّـهَ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطٌ ﴿١٢٠﴾
120. Ikikuguseni hasanah (nusura, ushindi, ghanima) inawachukiza, na likikusibuni baya hulifurahia; na mkisubiri na mkawa na taqwa haitokudhuruni chochote katika hila zao. Hakika Allaah kwa wayatendayo ni Muhiytw (Mwenye kuzunguka vyote kwa ujuzi Wake).

وَإِذْ غَدَوْتَ مِنْ أَهْلِكَ تُبَوِّئُ الْمُؤْمِنِينَ مَقَاعِدَ لِلْقِتَالِ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿١٢١﴾ 
121. Na (kumbuka ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) pale ulipotoka asubuhi mapema ukaacha ahli zako uwapange Waumini vituo vya kupigana (vita vya Uhud). Na Allaah ni Samiy‘un-‘Aliym (Mwenye kusikia yote - Mjuzi wa yote).


إِذْ هَمَّت طَّائِفَتَانِ مِنكُمْ أَن تَفْشَلَا وَاللَّـهُ وَلِيُّهُمَا ۗ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١٢٢﴾
122. Pale walipofanya wasiwasi makundi mawili miongoni mwenu kwamba watashindwa na Allaah ni Waliyy (Mlinzi, Msaidizi) wao; basi kwa Allaah pekee na watawakali Waumini.

وَلَقَدْ نَصَرَكُمُ اللَّـهُ بِبَدْرٍ وَأَنتُمْ أَذِلَّةٌ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿١٢٣﴾
123. Kwa yakini Alikunusuruni Allaah katika (vita vya) Badr na hali nyinyi mlikuwa dhaifu (idadi chache). Basi mcheni Allaah mpate kushukuru.

إِذْ تَقُولُ لِلْمُؤْمِنِينَ أَلَن يَكْفِيَكُمْ أَن يُمِدَّكُمْ رَبُّكُم بِثَلَاثَةِ آلَافٍ مِّنَ الْمَلَائِكَةِ مُنزَلِينَ﴿١٢٤﴾
124. (Kumbuka) Pale ulipowaambia Waumini: “Je, haikutosheni ikiwa Rabb (Mola) wenu Atakuongezeeni nguvu kwa Malaika elfu tatu walioteremshwa?”

بَلَىٰ ۚ إِن تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا وَيَأْتُوكُم مِّن فَوْرِهِمْ هَـٰذَا يُمْدِدْكُمْ رَبُّكُم بِخَمْسَةِ آلَافٍ مِّنَ الْمَلَائِكَةِ مُسَوِّمِينَ ﴿١٢٥﴾ 
125. Ndio! Mkisubiri mkawa na taqwa na wakakujieni kwa ghafla hivi (kukutekeni); Rabb (Mola) wenu Atakuongezeeni nguvu kwa Malaika elfu tano waliotiwa alama (ya ubora).

 وَمَا جَعَلَهُ اللَّـهُ إِلَّا بُشْرَىٰ لَكُمْ وَلِتَطْمَئِنَّ قُلُوبُكُم بِهِ ۗ وَمَا النَّصْرُ إِلَّا مِنْ عِندِ اللَّـهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ ﴿١٢٦﴾
126. Na hakujaalia hayo Allaah isipokuwa ni bishara kwenu na ili zitue nyoyo zenu kwayo. Na hakuna ushindi isipokuwa kutoka kwa Allaah ‘Aziyzil-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika   - Mwenye hikmah wa yote).

لِيَقْطَعَ طَرَفًا مِّنَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَوْ يَكْبِتَهُمْ فَيَنقَلِبُوا خَائِبِينَ﴿١٢٧﴾ 
127. Ili Akate sehemu ya waliokufuru au Awafedheheshe, warudi nyuma wakiwa wametaka tamaa.

 لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ﴿١٢٨﴾
128. Si juu yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم bali ni juu ya Allaah) kuamua; ima Apokee tawbah yao au Awaadhibu, kwani wao ni madhalimu.


وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ يَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٢٩﴾
129. Na ni vya Allaah Pekee vilivyomo katika mbingu na katika ardhi. Anamghufuria Amtakaye na Anamuadhibu Amtakaye. Na Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria -  Mwenye kurehemu)

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَأْكُلُوا الرِّبَا أَضْعَافًا مُّضَاعَفَةً ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿١٣٠﴾
130. Enyi mlioamini! Msile ribaa mkizidisha maradufu juu ya maradufu. Na mcheni Allaah mpate kufaulu.

وَاتَّقُوا النَّارَ الَّتِي أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ﴿١٣١﴾ 
131. Na uogopeni Moto ambao umeandaliwa kwa makafiri.

وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَالرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ﴿١٣٢﴾
132. Na mtiini Allaah na Rasuli mpate kurehemewa.

وَسَارِعُوا إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ﴿١٣٣﴾ 
133. Na kimbilieni maghfirah kutoka kwa Rabb (Mola) wenu na Jannah upana wake ni wa mbingu na ardhi imeandaliwa kwa wenye taqwa. 

الَّذِينَ يُنفِقُونَ فِي السَّرَّاءِ وَالضَّرَّاءِ وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٣٤﴾ 
134. Ambao wanatoa (katika njia ya Allaah) katika (hali ya) wasaa na katika (hali ya) shida, na wanazuia ghadhabu, na wenye kusamehe watu. Na Allaah Anapenda wafanyao ihsaan.

وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّـهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّـهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ﴿١٣٥﴾
135. Na wale ambao wanapofanya machafu au wakajidhulumu nafsi zao (kwa maasi), humdhukuru Allaah wakaomba maghfirah kwa madhambi yao. Na nani anayeghufuria madhambi isipokuwa Allaah. Na hawaendelei katika waliyoyafanya na wao wanajua.

أُولَـٰئِكَ جَزَاؤُهُم مَّغْفِرَةٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَجَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَنِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ ﴿١٣٦﴾
136. Hao jazaa yao ni maghfirah kutoka kwa Rabb (Mola) wao na Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo.  Uzuri ulioje ujira wa watendaji (wema).

قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِكُمْ سُنَنٌ فَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ﴿١٣٧﴾
137. Kwa hakika zimekwishapita kabla yenu nyendo (kama zenu), basi tembeeni katika ardhi kisha mtazame vipi ilikuwa hatima ya wenye kukadhibisha.

هَـٰذَا بَيَانٌ لِّلنَّاسِ وَهُدًى وَمَوْعِظَةٌ لِّلْمُتَّقِينَ﴿١٣٨﴾
138. Hii (Qur-aan) ni ubainisho kwa watu (wote) na Mwongozo na mawaidha kwa wenye taqwa.

وَلَا تَهِنُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَنتُمُ الْأَعْلَوْنَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿١٣٩﴾ 
139. Na wala msilegee na wala msihuzunike na ilhali nyinyi mko juu mkiwa Waumini (wa kweli).

 إِن يَمْسَسْكُمْ قَرْحٌ فَقَدْ مَسَّ الْقَوْمَ قَرْحٌ مِّثْلُهُ ۚ وَتِلْكَ الْأَيَّامُ نُدَاوِلُهَا بَيْنَ النَّاسِ وَلِيَعْلَمَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَيَتَّخِذَ مِنكُمْ شُهَدَاءَ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الظَّالِمِينَ ﴿١٤٠﴾
140. Inapokuguseni majeraha basi yamekwisha wagusa watu majeraha kama hayo. Na hizo ni siku (za mabadiliko ya hali) Tunazizungusha zamu baina ya watu na ili Allaah Adhihirishe waloamini na Afanye miongoni mwenu mashahidi. Na Allaah Hapendi madhalimu.

وَلِيُمَحِّصَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَيَمْحَقَ الْكَافِرِينَ﴿١٤١﴾ 
141. Na ili Allaah Awasafishe walioamini (dhambi kwa mitihani inayowasibu)  na Awafute (waondoke duniani) makafiri.

 أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَعْلَمِ اللَّـهُ الَّذِينَ جَاهَدُوا مِنكُمْ وَيَعْلَمَ الصَّابِرِينَ﴿١٤٢﴾
142. Je! Mnadhani kwamba mtaingia Jannah na hali Allaah Hakudhihirisha wale waliofanya jihaad miongoni mwenu na Akadhihirisha wenye kusubiri?

وَلَقَدْ كُنتُمْ تَمَنَّوْنَ الْمَوْتَ مِن قَبْلِ أَن تَلْقَوْهُ فَقَدْ رَأَيْتُمُوهُ وَأَنتُمْ تَنظُرُونَ﴿١٤٣﴾
143. Na kwa yakini mlikuwa mnatamani mauti (muwe mashuhadaa) kabla hamjakutana nayo, basi mmekwishayaona na huku mnayatazama. 

وَمَا مُحَمَّدٌ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ ۚ أَفَإِن مَّاتَ أَوْ قُتِلَ انقَلَبْتُمْ عَلَىٰ أَعْقَابِكُمْ ۚ وَمَن يَنقَلِبْ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ فَلَن يَضُرَّ اللَّـهَ شَيْئًا ۗ وَسَيَجْزِي اللَّـهُ الشَّاكِرِينَ ﴿١٤٤﴾
144. Na Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) si yeyote isipokuwa ni Rasuli tu. Wamekwishapita kabla yake Rasuli. Je, akifa au akiuawa mtageuka nyuma ya visigino vyenu (mrudi katika ukafiri)? Na atakayegeuka nyuma ya visigino vyake, basi hatomdhuru Allaah kitu chochote. Na Allaah Atawalipa wenye kushukuru.


وَمَا كَانَ لِنَفْسٍ أَن تَمُوتَ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ كِتَابًا مُّؤَجَّلًا ۗ وَمَن يُرِدْ ثَوَابَ الدُّنْيَا نُؤْتِهِ مِنْهَا وَمَن يُرِدْ ثَوَابَ الْآخِرَةِ نُؤْتِهِ مِنْهَا ۚ وَسَنَجْزِي الشَّاكِرِينَ ﴿١٤٥﴾ 
145. Na haiwi kwa nafsi yeyote kufa isipokuwa kwa idhini ya Allaah, imeandikwa muda wake maalumu. Na yeyote anayetaka thawabu za dunia Tutampa katika hizo. Na yeyote anayetaka thawabu za Aakhirah Tutampa katika hizo; na Tutawalipa wanaoshukuru. 

وَكَأَيِّن مِّن نَّبِيٍّ قَاتَلَ مَعَهُ رِبِّيُّونَ كَثِيرٌ فَمَا وَهَنُوا لِمَا أَصَابَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَمَا ضَعُفُوا وَمَا اسْتَكَانُوا ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الصَّابِرِينَ ﴿١٤٦﴾
146. Na Nabiy wangapi (kila mmoja alipigina vita na maadui na) pamoja naye walipigana Ribbiyyuwna (Wanavyuoni wanaomwabudu mno Rabb, wenye taqwa), basi hawakulegea kwa yaliyowasibu katika njia ya Allaah, wala hawakudhoofika na wala hawakunyong’onyea. Na Allaah Anapenda wanaosubiri.

وَمَا كَانَ قَوْلَهُمْ إِلَّا أَن قَالُوا رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَإِسْرَافَنَا فِي أَمْرِنَا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ﴿١٤٧﴾
147. Na haikuwa kauli yao isipokuwa walisema: “Rabb (Mola) wetu Tughufurie madhambi yetu na upindukaji mipaka katika mambo yetu, na Ithibitishe miguu yetu na Tunusuru dhidi ya watu makafiri.”

فَآتَاهُمُ اللَّـهُ ثَوَابَ الدُّنْيَا وَحُسْنَ ثَوَابِ الْآخِرَةِ ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٤٨﴾ 
148. Basi Allaah Akawalipa thawabu za dunia na thawabu nzuri za Aakhirah.  Na Allaah Anapenda wafanyao ihsaan. 


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تُطِيعُوا الَّذِينَ كَفَرُوا يَرُدُّوكُمْ عَلَىٰ أَعْقَابِكُمْ فَتَنقَلِبُوا خَاسِرِينَ﴿١٤٩﴾
149. Enyi mlioamini! Mkiwatii wale waliokufuru watakurudisheni (nyuma) juu ya visigino vyenu, kisha mtageuka mkiwa wenye kukhasirika.

بَلِ اللَّـهُ مَوْلَاكُمْ ۖ وَهُوَ خَيْرُ النَّاصِرِينَ ﴿١٥٠﴾
150. Bali Allaah ndio Mawlaa (Mola, Mlinzi) wenu.  Naye ni Mbora kabisa wa wenye kunusuru.

سَنُلْقِي فِي قُلُوبِ الَّذِينَ كَفَرُوا الرُّعْبَ بِمَا أَشْرَكُوا بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا ۖ وَمَأْوَاهُمُ النَّارُ ۚ وَبِئْسَ مَثْوَى الظَّالِمِينَ ﴿١٥١﴾
151. Tutavurumisha kizaazaa katika nyoyo za waliokufuru kwa sababu ya kumshirikisha Allaah na ambayo Hakuyateremshia mamlaka. Na makazi yao ni Moto, na ubaya ulioje maskani ya madhalimu.

وَلَقَدْ صَدَقَكُمُ اللَّـهُ وَعْدَهُ إِذْ تَحُسُّونَهُم بِإِذْنِهِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا فَشِلْتُمْ وَتَنَازَعْتُمْ فِي الْأَمْرِ وَعَصَيْتُم مِّن بَعْدِ مَا أَرَاكُم مَّا تُحِبُّونَ ۚ مِنكُم مَّن يُرِيدُ الدُّنْيَا وَمِنكُم مَّن يُرِيدُ الْآخِرَةَ ۚ ثُمَّ صَرَفَكُمْ عَنْهُمْ لِيَبْتَلِيَكُمْ ۖ وَلَقَدْ عَفَا عَنكُمْ ۗ وَاللَّـهُ ذُو فَضْلٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٥٢﴾
152. Na kwa yakini Allaah Amekwisha kusadikishieni ahadi Yake mlipowaua vikali kwa idhini Yake; mpaka mliposhindwa na mkazozana katika amri (aliyokupeni Rasuli) na mkaasi baada ya Yeye kukuonyesheni yale mnayoyapenda.  Miongoni mwenu (wako) wenye kutaka dunia, na miongoni mwenu (wako) wenye kutaka Aakhirah. Kisha Akakugeuzeni nyuma mbali nao (hao maadui) ili Akujaribuni. Na kwa yakini Amekwisha kusameheni. Na Allaah ni Mwenye fadhila kwa Waumini.

إِذْ تُصْعِدُونَ وَلَا تَلْوُونَ عَلَىٰ أَحَدٍ وَالرَّسُولُ يَدْعُوكُمْ فِي أُخْرَاكُمْ فَأَثَابَكُمْ غَمًّا بِغَمٍّ لِّكَيْلَا تَحْزَنُوا عَلَىٰ مَا فَاتَكُمْ وَلَا مَا أَصَابَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ ﴿١٥٣﴾
153. (Kumbuka) Pale mlipopanda (mlima na kukimbia) na wala hamgeuki nyuma kumtazama yeyote, na Rasuli anakuiteni nyuma yenu, kisha Akakulipeni dhiki juu ya dhiki ili msihuzunike kwa yaliyokupiteni (ghanima) na wala kwa yaliyokusibuni (majeraha na vifo). Na Allaah ni Khabiyr (Mjuzi wa yaliyodhahiri na yaliyofichikana) kwa myatendayo.

ثُمَّ أَنزَلَ عَلَيْكُم مِّن بَعْدِ الْغَمِّ أَمَنَةً نُّعَاسًا يَغْشَىٰ طَائِفَةً مِّنكُمْ ۖ وَطَائِفَةٌ قَدْ أَهَمَّتْهُمْ أَنفُسُهُمْ يَظُنُّونَ بِاللَّـهِ غَيْرَ الْحَقِّ ظَنَّ الْجَاهِلِيَّةِ ۖ يَقُولُونَ هَل لَّنَا مِنَ الْأَمْرِ مِن شَيْءٍ ۗ قُلْ إِنَّ الْأَمْرَ كُلَّهُ لِلَّـهِ ۗ يُخْفُونَ فِي أَنفُسِهِم مَّا لَا يُبْدُونَ لَكَ ۖ يَقُولُونَ لَوْ كَانَ لَنَا مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ مَّا قُتِلْنَا هَاهُنَا ۗ قُل لَّوْ كُنتُمْ فِي بُيُوتِكُمْ لَبَرَزَ الَّذِينَ كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقَتْلُ إِلَىٰ مَضَاجِعِهِمْ ۖ وَلِيَبْتَلِيَ اللَّـهُ مَا فِي صُدُورِكُمْ وَلِيُمَحِّصَ مَا فِي قُلُوبِكُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿١٥٤﴾
154. Kisha Akakuteremshieni baada ya dhiki, amani (utulivu kwa) usingizi unaofunika kundi miongoni mwenu na kundi likawashughulisha nafsi zao wakamdhania Allaah pasi na haki dhana ya kijahili; wanasema: “Je, tuna amri yoyote sisi katika jambo hili?”  Sema: “Hakika amri yote ni ya Allaah” Wanaficha katika nafsi zao yale wasiyokubainishia. Wanasema: “Lau tungelikuwa tuna amri yoyote katika jambo basi tusingeliuliwa hapa”.  Sema: “Lau mngelikuwa majumbani mwenu, bila shaka wangejitokeza wale walioandikiwa kuuwawa kwenye mahali pa kuangukia wafe.” Ili Allaah Ayajaribu yale yaliyomo katika vifua vyenu na Atakase yale yaliyomo katika nyoyo zenu. Na Allaah ni ‘Aliym (Mjuzi) kwa yaliyomo vifuani.

إِنَّ الَّذِينَ تَوَلَّوْا مِنكُمْ يَوْمَ الْتَقَى الْجَمْعَانِ إِنَّمَا اسْتَزَلَّهُمُ الشَّيْطَانُ بِبَعْضِ مَا كَسَبُوا ۖ وَلَقَدْ عَفَا اللَّـهُ عَنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿١٥٥﴾ 
155. Hakika wale waliokengeuka miongoni mwenu siku yalipokutana (kwa kupambana) makundi mawili, hakika hapana ila shaytwaan (ndiye) aliyewatelezesha kwa baadhi ya yale waliyoyachuma. Na kwa yakini Allaah Aliwasamehe. Hakika Allaah ni Ghafuwrun-Haliym (Mwingi wa kughufuria - Mpole wa kuwavumilia waja).


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ كَفَرُوا وَقَالُوا لِإِخْوَانِهِمْ إِذَا ضَرَبُوا فِي الْأَرْضِ أَوْ كَانُوا غُزًّى لَّوْ كَانُوا عِندَنَا مَا مَاتُوا وَمَا قُتِلُوا لِيَجْعَلَ اللَّـهُ ذَٰلِكَ حَسْرَةً فِي قُلُوبِهِمْ ۗ وَاللَّـهُ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿١٥٦﴾ 
156. Enyi mlioamini! Msiwe kama wale waliokufuru na wakasema kwa ndugu zao; waliposafiri katika ardhi au walipokuwa vitani: “Lau wangelikuwa kwetu wasingelikufa na wala wasingeliuawa,” ili Allaah Afanye hayo (yaliyoeleweka vibaya) majuto katika nyoyo zao. Na Allaah Anahuisha na Anafisha. Na Allaah kwa myatendayo ni Baswiyr (Mwenye kuona).

وَلَئِن قُتِلْتُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَوْ مُتُّمْ لَمَغْفِرَةٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرَحْمَةٌ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ﴿١٥٧﴾
157. Na kama mtauliwa katika njia ya Allaah au mtakufa; bila shaka maghfirah kutoka kwa Allaah na Rahmah ni bora kuliko yale wanayoyakusanya (duniani).

وَلَئِن مُّتُّمْ أَوْ قُتِلْتُمْ لَإِلَى اللَّـهِ تُحْشَرُونَ﴿١٥٨﴾
158. Na kama mtakufa au mtauliwa; bila shaka kwa Allaah mtakusanywa.

فَبِمَا رَحْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ لِنتَ لَهُمْ ۖ وَلَوْ كُنتَ فَظًّا غَلِيظَ الْقَلْبِ لَانفَضُّوا مِنْ حَوْلِكَ ۖ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاسْتَغْفِرْ لَهُمْ وَشَاوِرْهُمْ فِي الْأَمْرِ ۖ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَوَكِّلِينَ ﴿١٥٩﴾
159. Basi ni kwa Rahmah kutoka kwa Allaah umekuwa mpole kwao (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).  Na lau ungelikuwa mjeuri mwenye moyo mgumu wangelitawanyika mbali nawe (wakakukimbia). Basi wasamehe na waombee maghfirah na washauri katika mambo. Na unapoazimia basi tawakali kwa Allaah. Hakika Allaah Anapenda wanaotawakali.


إِن يَنصُرْكُمُ اللَّـهُ فَلَا غَالِبَ لَكُمْ ۖ وَإِن يَخْذُلْكُمْ فَمَن ذَا الَّذِي يَنصُرُكُم مِّن بَعْدِهِ ۗ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١٦٠﴾ 
160. Akikunusuruni Allaah, basi hakuna wa kukushindeni. Na Akikutelekezeni, basi nani atakunusuruni baada Yake? Na kwa Allaah Pekee watawakali Waumini.

 وَمَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَغُلَّ ۚ وَمَن يَغْلُلْ يَأْتِ بِمَا غَلَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿١٦١﴾
161. Na haikuwa (ni tabia) kwa Nabiy yeyote kukhini (ghanima; mali ya vita). Na yeyote atakayekhini atakuja na kile alichokikhini Siku ya Qiyaamah. Kisha italipwa kamilifu kila nafsi yale iliyoyachuma nao hawatodhulumiwa.

أَفَمَنِ اتَّبَعَ رِضْوَانَ اللَّـهِ كَمَن بَاءَ بِسَخَطٍ مِّنَ اللَّـهِ وَمَأْوَاهُ جَهَنَّمُ ۚ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿١٦٢﴾ 
162. Je aliyefuata Radhi za Allaah ni kama aliyestahiki ghadhabu kutoka kwa Allaah?!  Na makazi yake ni (Moto wa) Jahannam; na ubaya ulioje mahali pa kuishia.

هُمْ دَرَجَاتٌ عِندَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ ﴿١٦٣﴾
163. Wao wana vyeo (mbali mbali) mbele ya Allaah. Na Allaah ni Baswiyr (Mwenye kuona) yale wayatendayo.

لَقَدْ مَنَّ اللَّـهُ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ إِذْ بَعَثَ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْ أَنفُسِهِمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿١٦٤﴾
164. Kwa yakini Allaah Amewafanyia ihsaan Waumini pale Alipomtuma kwao, Rasuli miongoni mwao, anawasomea Aayaat Zake na anawatakasa na anawafunza Kitabu na Hikmah; japokuwa walikuwa kabla katika upotofu bayana.

أَوَلَمَّا أَصَابَتْكُم مُّصِيبَةٌ قَدْ أَصَبْتُم مِّثْلَيْهَا قُلْتُمْ أَنَّىٰ هَـٰذَا ۖ قُلْ هُوَ مِنْ عِندِ أَنفُسِكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٦٥﴾
165. (Mna nini?) Ulipokusibuni msiba (siku ya vita vya Uhud) ingawa mliwasibu mara mbili yake (maadui siku ya vita vya Badr); mlisema: “Umetoka wapi huu?” Sema: “Huo ni kutoka kwenu wenyewe”. Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza).

وَمَا أَصَابَكُمْ يَوْمَ الْتَقَى الْجَمْعَانِ فَبِإِذْنِ اللَّـهِ وَلِيَعْلَمَ الْمُؤْمِنِينَ﴿١٦٦﴾
166. Na yale yaliyokusibuni siku yalipokutana makundi mawili (Waislamu na makafiri katika vita vya Uhud), basi ni kwa idhini ya Allaah; na ili Adhihirishe Waumini (wakweli).

وَلِيَعْلَمَ الَّذِينَ نَافَقُوا ۚ وَقِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا قَاتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَوِ ادْفَعُوا ۖ قَالُوا لَوْ نَعْلَمُ قِتَالًا لَّاتَّبَعْنَاكُمْ ۗ هُمْ لِلْكُفْرِ يَوْمَئِذٍ أَقْرَبُ مِنْهُمْ لِلْإِيمَانِ ۚ يَقُولُونَ بِأَفْوَاهِهِم مَّا لَيْسَ فِي قُلُوبِهِمْ ۗ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا يَكْتُمُونَ ﴿١٦٧﴾
167. Na ili Adhihirishe wale walionafiki na kuambiwa: “Njooni mpigane katika njia ya Allaah au (angalau) lindeni”. (Waambiapwo hivyo) Husema: “Lau tungelijua (kuwa kuna) kupigana bila shaka tungelikufuateni”. Wao siku hiyo kwa ukafiri (walikuwa wako) karibu zaidi kuliko iymaan. Wanasema kwa midomo yao, yale yasiyokuwemo katika nyoyo zao. Na Allaah Anajua zaidi wanayoyaficha.

الَّذِينَ قَالُوا لِإِخْوَانِهِمْ وَقَعَدُوا لَوْ أَطَاعُونَا مَا قُتِلُوا ۗ قُلْ فَادْرَءُوا عَنْ أَنفُسِكُمُ الْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٦٨﴾ 
168. Wale waliowaambia ndugu zao nao wakakaa (hawakwenda vitani): “Lau wangelitutii basi wasingeliuawa.” Sema: “Basi ziondoleeni nafsi zenu mauti mkiwa ni wakweli.

وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتًا ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ ﴿١٦٩﴾ 
169. Na wala usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika njia ya Allaah ni wafu, bali wahai, kwa Rabb (Mola) wao wanaruzukiwa.

فَرِحِينَ بِمَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ وَيَسْتَبْشِرُونَ بِالَّذِينَ لَمْ يَلْحَقُوا بِهِم مِّنْ خَلْفِهِمْ أَلَّا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴿١٧٠﴾ 
170. Wanafurahia kwa Aliyowapa Allaah kwa fadhila Zake na wanawashangilia (watakaokufa mashahidi) ambao hawajaungana nao, walio nyuma yao, kwamba: “Hakuna khofu juu yao na wala hawatohuzunika.”

يَسْتَبْشِرُونَ بِنِعْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَفَضْلٍ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُؤْمِنِينَ﴿١٧١﴾
171. Wanashangilia kwa neema za Allaah na fadhila na kwamba Allaah Hapotezi ujira wa Waumini.

الَّذِينَ اسْتَجَابُوا لِلَّـهِ وَالرَّسُولِ مِن بَعْدِ مَا أَصَابَهُمُ الْقَرْحُ ۚ لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا مِنْهُمْ وَاتَّقَوْا أَجْرٌ عَظِيمٌ ﴿١٧٢﴾
172. Wale (Waumini) waliomwitikia Allaah na Rasuli baada ya kuwasibu majeraha. Kwa wale waliofanya ihsaan miongoni mwao na wakawa na taqwa watapa ujira adhimu.

الَّذِينَ قَالَ لَهُمُ النَّاسُ إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُوا لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَانًا وَقَالُوا حَسْبُنَا اللَّـهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ﴿١٧٣﴾
173. Wale walioambiwa na watu: “Hakika watu wamejumuika dhidi yenu, basi waogopeni” (Haya) Yakawazidishia iymaan; na wakasema: “Allaah Anatutosheleza, Mzuri Alioje Al-Wakiyl (Mdhamini Anayetegemewa kwa yote).”

فَانقَلَبُوا بِنِعْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَفَضْلٍ لَّمْ يَمْسَسْهُمْ سُوءٌ وَاتَّبَعُوا رِضْوَانَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ ذُو فَضْلٍ عَظِيمٍ ﴿١٧٤﴾
174. Basi wakarudi na neema kutoka kwa Allaah na fadhila; halijawagusa ovu lolote; na wakafuatilia Radhi za Allaah.  Na Allaah ni Mwenye fadhila adhimu.

 إِنَّمَا ذَٰلِكُمُ الشَّيْطَانُ يُخَوِّفُ أَوْلِيَاءَهُ فَلَا تَخَافُوهُمْ وَخَافُونِ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿١٧٥﴾
175. Hakika huyo ni shaytwaan anawakhofisha marafiki wake wandani. Basi msiwakhofu, na nikhofuni Mimi mkiwa ni Waumini (kweli).

وَلَا يَحْزُنكَ الَّذِينَ يُسَارِعُونَ فِي الْكُفْرِ ۚ إِنَّهُمْ لَن يَضُرُّوا اللَّـهَ شَيْئًا ۗ يُرِيدُ اللَّـهُ أَلَّا يَجْعَلَ لَهُمْ حَظًّا فِي الْآخِرَةِ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١٧٦﴾ 
176. Wala wasikuhuzunishe kabisa (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) wale wanaokimbilia katika ukafiri. Hakika wao hawamdhuru Allaah kitu chochote. Allaah Anakusudia Asiwawekee fungu lolote Aakhirah; na watapa adhabu kuu.


إِنَّ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الْكُفْرَ بِالْإِيمَانِ لَن يَضُرُّوا اللَّـهَ شَيْئًا وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿١٧٧﴾ 
177. Hakika wale waliokhiari ukafiri badala ya iymaan, hawatomdhuru kitu chochote Allaah; nao watapata adhabu iumizayo.

وَلَا يَحْسَبَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا أَنَّمَا نُمْلِي لَهُمْ خَيْرٌ لِّأَنفُسِهِمْ ۚ إِنَّمَا نُمْلِي لَهُمْ لِيَزْدَادُوا إِثْمًا ۚ وَلَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿١٧٨﴾
178. Na wala wasidhanie kabisa wale waliokufuru kwamba muhula Tunaowapa (wa kustarehe) ni kheri kwao. Hakika Tunawapa muhula ili wazidi (kufanya) dhambi. Nao watapata adhabu ya kudhalilisha.


مَّا كَانَ اللَّـهُ لِيَذَرَ الْمُؤْمِنِينَ عَلَىٰ مَا أَنتُمْ عَلَيْهِ حَتَّىٰ يَمِيزَ الْخَبِيثَ مِنَ الطَّيِّبِ ۗ وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُطْلِعَكُمْ عَلَى الْغَيْبِ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَجْتَبِي مِن رُّسُلِهِ مَن يَشَاءُ ۖ فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ ۚ وَإِن تُؤْمِنُوا وَتَتَّقُوا فَلَكُمْ أَجْرٌ عَظِيمٌ ﴿١٧٩﴾
179. Haiwi kwa Allaah kuwaacha Waumini katika hali mliyo nayo mpaka Apambanue khabiyth (mbaya) kutoka kwa twayyib (mema) Na haiwi kwa Allaah Akujulisheni ya ghayb; lakini Allaah Humteua katika Rasuli Wake Amtakaye (Akamjulisha baadhi ya hayo ya ghayb). Basi mwaminini Allaah na Rasuli Wake. Na mkiamini na mkawa na taqwa mtapata ujira adhimu.

 وَلَا يَحْسَبَنَّ الَّذِينَ يَبْخَلُونَ بِمَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ هُوَ خَيْرًا لَّهُم ۖ بَلْ هُوَ شَرٌّ لَّهُمْ ۖ سَيُطَوَّقُونَ مَا بَخِلُوا بِهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ وَلِلَّـهِ مِيرَاثُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿١٨٠﴾
180. Wala wasidhani kabisa wale wanaofanya ubakhili kwa yale Aliyowapa Allaah katika fadhila Zake kwamba hayo ni kheri kwao, bali ni shari kwao. Watafungwa kongwa yale waliyoyafanyia ubakhili Siku ya Qiyaamah. Na ni Wake Allaah Pekee urithi wa mbingu na ardhi.  Na Allaah kwa myatendayo ni Khabiyr (Mjuzi wa yaliyodhahiri na yaliyofichikana).

لَّقَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ فَقِيرٌ وَنَحْنُ أَغْنِيَاءُ ۘ سَنَكْتُبُ مَا قَالُوا وَقَتْلَهُمُ الْأَنبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَنَقُولُ ذُوقُوا عَذَابَ الْحَرِيقِ ﴿١٨١﴾
181. Kwa yakini Allaah Ameisikia kauli ya wale (Mayahudi) waliosema: “Hakika Allaah ni fakiri na sisi ni matajiri.” Tutayaandika waliyoyasema na kuua kwao Nabiy pasi na haki na Tutasema: “Onjeni adhabu ya kuungua.”

ذَٰلِكَ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيكُمْ وَأَنَّ اللَّـهَ لَيْسَ بِظَلَّامٍ لِّلْعَبِيدِ﴿١٨٢﴾
182. Hivyo ni kwa sababu ya yale iliyotanguliza mikono yenu na kwamba Allaah si dhalimu kabisa kwa waja.

الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ عَهِدَ إِلَيْنَا أَلَّا نُؤْمِنَ لِرَسُولٍ حَتَّىٰ يَأْتِيَنَا بِقُرْبَانٍ تَأْكُلُهُ النَّارُ ۗ قُلْ قَدْ جَاءَكُمْ رُسُلٌ مِّن قَبْلِي بِالْبَيِّنَاتِ وَبِالَّذِي قُلْتُمْ فَلِمَ قَتَلْتُمُوهُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٨٣﴾
183. (Hao ndio) Wale waliosema: “Hakika Allaah Ametuahidi kwamba tusimwamini Rasuli yeyote mpaka atuletee qurbaan (kafara kutoka mbinguni) iliwe na moto.  Sema: “Kwa yakini walikujieni Rasuli kabla yangu kwa hoja bayana na (hata) kwa yale ambayo mmesema; basi kwa nini mliwaua mkiwa ni wakweli?”

فَإِن كَذَّبُوكَ فَقَدْ كُذِّبَ رُسُلٌ مِّن قَبْلِكَ جَاءُوا بِالْبَيِّنَاتِ وَالزُّبُرِ وَالْكِتَابِ الْمُنِيرِ﴿١٨٤﴾
184. Basi wakikukadhibisha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), kwa yakini wamekadhibishwa Rasuli kabla yako. Walikuja kwa hoja bayana na Az-Zubur (vitabu vya waadhi) na Kitabu chenye Nuru.


كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ ۗ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۖ فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ ۗ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ ﴿١٨٥﴾
185. Kila nafsi itaonja mauti. Na hakika mtalipwa kikamilifu ujira wenu Siku ya Qiyaamah. Basi atakayewekwa mbali na Moto na akaingizwa Jannah kwa yakini amefuzu. Na uhai wa dunia si lolote ila ni starehe ya udanganyifu.

لَتُبْلَوُنَّ فِي أَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ وَلَتَسْمَعُنَّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ وَمِنَ الَّذِينَ أَشْرَكُوا أَذًى كَثِيرًا ۚ وَإِن تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ ذَٰلِكَ مِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ ﴿١٨٦﴾
186. Bila shaka mtajaribiwa katika mali zenu na nafsi zenu; na bila shaka mtasikia kutoka kwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu na kutoka kwa wale walioshirikisha udhia mwingi. Lakini mkisubiri na mkawa na taqwa basi hakika hayo ni mambo ya (thamani yapasayo) kuazimiwa.

 وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَتُبَيِّنُنَّهُ لِلنَّاسِ وَلَا تَكْتُمُونَهُ فَنَبَذُوهُ وَرَاءَ ظُهُورِهِمْ وَاشْتَرَوْا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۖ فَبِئْسَ مَا يَشْتَرُونَ ﴿١٨٧﴾
187. Na (taja ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) pale Alipochukua Allaah fungamano la wale waliopewa Kitabu (Allaah Akawaambia): “Bila shaka mtakibainisha kwa watu na wala hamtokificha.” Lakini walikitupa nyuma ya migongo yao na wakabadilisha kwayo thamani ndogo.  Basi ubaya ulioje yale wanayoyanunua.

لَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ يَفْرَحُونَ بِمَا أَتَوا وَّيُحِبُّونَ أَن يُحْمَدُوا بِمَا لَمْ يَفْعَلُوا فَلَا تَحْسَبَنَّهُم بِمَفَازَةٍ مِّنَ الْعَذَابِ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٨٨﴾ 
188. Usiwadhanie kabisa wale wanaofurahia kwa waliyopewa na wanapenda wasifiwe kwa wasiyoyatenda. Usiwadhanie kabisa kuwa watasalimika na adhabu. Nao watapata adhabu iumizayo.

وَلِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٨٩﴾
189. Ni Wake Allaah Pekee ufalme wa mbingu na ardhi. Na Allaah juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza).

إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ﴿١٩٠﴾ 
190. Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na mabadiliko (ya mfuatano) ya usiku na mchana; bila shaka ni Aayaat (ishara, dalili, zingatioa n.k) kwa wenye akili.

الَّذِينَ يَذْكُرُونَ اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمْ وَيَتَفَكَّرُونَ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ رَبَّنَا مَا خَلَقْتَ هَـٰذَا بَاطِلًا سُبْحَانَكَ فَقِنَا عَذَابَ النَّارِ﴿١٩١﴾ 
191. Ambao wanamdhukuru Allaah (kwa) kusimama, na (kwa) kukaa na (kwa) kulala ubavuni mwao na wanatafakari katika kuumbwa mbingu na ardhi (wakisema): “Rabb (Mola) wetu, Hukuumba haya bure. Subhaanak! (Utakasifu ni Wako!) Tukinge na adhabu ya Moto.

رَبَّنَا إِنَّكَ مَن تُدْخِلِ النَّارَ فَقَدْ أَخْزَيْتَهُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ ﴿١٩٢﴾
192. Rabb (Mola) wetu, hakika Umuingizaye Motoni, kwa yakini Umemhizi. Na madhalimu hawana yeyote mwenye kuwanusuru.

رَّبَّنَا إِنَّنَا سَمِعْنَا مُنَادِيًا يُنَادِي لِلْإِيمَانِ أَنْ آمِنُوا بِرَبِّكُمْ فَآمَنَّا ۚ رَبَّنَا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَكَفِّرْ عَنَّا سَيِّئَاتِنَا وَتَوَفَّنَا مَعَ الْأَبْرَارِ ﴿١٩٣﴾
193. Rabb (Mola) wetu, hakika sisi tumemsikia mwitaji anaita kwenye iymaan kwamba ‘mwaminini Rabb wenu’ basi tukaamini.  Rabb (Mola) wetu, Tughufurie madhambi yetu na Tufutie makosa yetu na Tufishe pamoja na Al-Abraar (Waumini wema).

 رَبَّنَا وَآتِنَا مَا وَعَدتَّنَا عَلَىٰ رُسُلِكَ وَلَا تُخْزِنَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ إِنَّكَ لَا تُخْلِفُ الْمِيعَادَ ﴿١٩٤﴾
194. Rabb (Mola) wetu na Tupe Uliyotuahidi kupitia Rasuli Wako, wala Usituhizi Siku ya Qiyaamah; hakika Wewe Huendi kinyume na miadi”.

فَاسْتَجَابَ لَهُمْ رَبُّهُمْ أَنِّي لَا أُضِيعُ عَمَلَ عَامِلٍ مِّنكُم مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ ۖ بَعْضُكُم مِّن بَعْضٍ ۖ فَالَّذِينَ هَاجَرُوا وَأُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَأُوذُوا فِي سَبِيلِي وَقَاتَلُوا وَقُتِلُوا لَأُكَفِّرَنَّ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَلَأُدْخِلَنَّهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ثَوَابًا مِّنْ عِندِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عِندَهُ حُسْنُ الثَّوَابِ ﴿١٩٥﴾
195. Basi Rabb (Mola) wao Akawaitikia (maombi yao kwa kusema) “Hakika Mimi Sipotezi amali za mtendaji yeyote yule miongoni mwenu akiwa mwanamume au mwanamke, nyinyi kwa nyinyi. Basi wale waliohajiri (kwa ajili ya dini) na wakatolewa majumbani mwao na wakaudhiwa katika njia Yangu, wakapigana na wakauliwa; bila shaka Nitawafutia makosa yao na bila shaka Nitawaingiza Jannaat zipitazo chini yake mito, ni thawabu kutoka kwa Allaah.  Na kwa Allaah kuna thawabu nzuri kabisa.”


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com 



 لَا يَغُرَّنَّكَ تَقَلُّبُ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي الْبِلَادِ﴿١٩٦﴾
196. Isikudanganye kabisa kutangatanga kwa wale waliokufuru katika nchi.

مَتَاعٌ قَلِيلٌ ثُمَّ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۚ وَبِئْسَ الْمِهَادُ ﴿١٩٧﴾ 
197. Ni starehe ndogo, kisha makazi yao ni (Moto wa) Jahannam. Na ni mahala pabaya mno pa kupumzikia.

 لَـٰكِنِ الَّذِينَ اتَّقَوْا رَبَّهُمْ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا نُزُلًا مِّنْ عِندِ اللَّـهِ ۗ وَمَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ لِّلْأَبْرَارِ ﴿١٩٨﴾
198. Lakini wale waliomcha Rabb (Mola) wao watapata Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo, mapokezi kutoka kwa Allaah. Na vilioko kwa Allaah ni bora kabisa kwa ajili ya Al-Abraar (Waumini wema).

وَإِنَّ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَمَن يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْكُمْ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْهِمْ خَاشِعِينَ لِلَّـهِ لَا يَشْتَرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۗ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿١٩٩﴾
199. Na miongoni mwa Ahlil-Kitaabi wamo wanaomwamini Allaah na yaliyoteremshwa kwenu, na yaliyoteremswha kwao, wananyenyekea kwa Allaah hawabadili Aayaat za Allaah kwa thamani ndogo. Hao watapata ujira wao kwa Rabb (Mola) wao. Hakika Allaah ni Mwepesi wa kuhesabu.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اصْبِرُوا وَصَابِرُوا وَرَابِطُوا وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ﴿٢٠٠﴾
200. Enyi mlioamini! Subirini na zidini kuvuta subira na bakieni imara na mcheni Allaah ili mpate kufaulu.