الحديث
الحادي والثلاثون
"ازهد في الدنيا
يحبك الله"
عَنْ أَبِي العَبّاسِ سَهلِ
بْن سَعْدٍ السّاعِدِيِّ رضي الله عنه قَالَ : جَاءَ رَجُلُ إِلى النَبِي
صلى الله عليه وسلم فَقَالَ : يَا رَسُولَ اللَّهِ دُلَّنِي
عَلَى عَمَلٍ إِذَا عَمِلْتُهُ أَحَبَّنِي اللَّهُ وَأَحَبَّنِي النَّاسُ .
فَقَالَ: (( ازْهَدْ فِي الدُّنْيَا يُحِبُّكَ اللَّهُ وَازْهَدْ فِيمَا
عِنْدَ النَّاسِ يُحِبُّكَ النّاسُ)).
رَوَاهُ
ابْنُ مَاجَهْ وَغَيْرُهُ
بِأَسَانِيدَ حَسَنَةٍ.
HADITHI YA 31
UPE ULIMWENGU KISOGO ALLAAH ATAKUPENDA
Kutoka kwa Abu
Al-‘Abbaas Sahl bin Sa'ad As-Saa'idiy رضي الله عنه ambaye alisema:
Mtu alikuja kwa
Mtume صلى الله عليه وسلم
na akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu, nielekeze kitendo ambacho
nikitenda kitasababisha Mola kunipenda na watu kunipenda.
Akasema (صلى الله عليه وسلم ) : Upe ulimwengu kisogo na Mwenyeezi Mungu atakupenda, na
jiepushe na mali za watu na watu watakupenda.
Imesimuliwa na Ibn
Maajah na wengineo kwa mtiririko mzuri wa mapokezi.*
*Hata hivyo
wanachuoni wa Hadiyth wameeleza kuwa Hadiyth hii ni dhaifu kutokana na udhaifu
wa sanad yake japo An-Nawawiy kaitumia na kasema ina sanad nzuri.