Al-Layl (92)


سُورَةُ  اللَّيْل
Al-Layl (92)

(Imeteremka Makka)


 Mwenyezi Mungu Mtukufu ameapa kwa viapo vitatu juu ya kuwa vitendo vya watu vinakhitalifiana, baadhi yake ni vya uwongofu, na baadhi yake ni vya upotofu. Mwenye kutoa, na akamchamngu, na akawafiki tabia yenye kukusanya kheri, basi Mwenyezi Mungu atamsahilishia mambo yake kwa wepesi. Na mwenye kufanya ubakhili, na akajiona hana haja na mtu, na akakanusha tabia zenye kukusanya kheri Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi kuingia mashakani.  Na wala mali yake hayatamfaa kitu kumwokoa akitumbukia katika adhabu! Na Aya zikabainisha baada ya hayo kwamba hakika Mwenyezi Mungu amechukua jukumu kubainisha njia za uwongofu kwa fadhila zake, na kwake yapo mambo ya maisha mawili, ya Akhera na ya duniani. Na kwamba hakika Yeye amekwisha onya kwamba Moto watauingia waovu na watauepuka walio wema.


 
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَىٰ ﴿١﴾

1. Naapa kwa usiku unapofunika.

وَالنَّهَارِ إِذَا تَجَلَّىٰ ﴿٢﴾

2. Na (Naapa kwa) mchana unapodhihirika (mwanga).

وَمَا خَلَقَ الذَّكَرَ وَالْأُنثَىٰ ﴿٣﴾

3. Na (Naapa kwa) Aliyeumba dume na jike.

إِنَّ سَعْيَكُمْ لَشَتَّىٰ ﴿٤﴾

4. Hakika juhudi zenu bila shaka ni tofauti tofauti.

فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَاتَّقَىٰ ﴿٥﴾

5. Basi yule anayetoa, na akawa na taqwa.

وَصَدَّقَ بِالْحُسْنَىٰ ﴿٦﴾

6. Na akasadikisha Al-Husnaa (tamshi la Tawhiyd – laa ilaaha illa-Allaah).

فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْيُسْرَىٰ ﴿٧﴾

7. “Basi Tutamuwepesishia kwa (yale yaliyo) mepesi ”

وَأَمَّا مَن بَخِلَ وَاسْتَغْنَىٰ ﴿٨﴾

8. Ama yule afanyaye ubakhili na (anayejidhania kuwa) amejitosheleza.

وَكَذَّبَ بِالْحُسْنَىٰ ﴿٩﴾

9. Na akakadhibisha Al-Husnaa (tamshi zuri la Tawhiyd - laa ilaaha illa-Allaah).

فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْعُسْرَىٰ ﴿١٠﴾

10. Na Tutamuwepesishia kwa (yale yaliyo) magumu”.

وَمَا يُغْنِي عَنْهُ مَالُهُ إِذَا تَرَدَّىٰ ﴿١١﴾

11. Na mali yake haitomfaa, atakapoporomoka (kuangamia Motoni).

إِنَّ عَلَيْنَا لَلْـهُدَىٰ ﴿١٢﴾
12. Hakika ni juu Yetu (kubainisha) mwongozo.

وَإِنَّ لَنَا لَلْآخِرَةَ وَالْأُولَىٰ ﴿١٣﴾

13. Na hakika ni Yetu Sisi (ya) Aakhirah na (uhai) wa awali.

فَأَنذَرْتُكُمْ نَارًا تَلَظَّىٰ ﴿١٤﴾

14. Basi Nimekutahadharisheni Moto uwakao kwa ghadhabu.

لَا يَصْلَاهَا إِلَّا الْأَشْقَى ﴿١٥﴾

15. Hauingii (yeyote) isipokuwa muovu kabisa.

الَّذِي كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١٦﴾

16. Ambaye amekadhibisha na akakengeuka.

وَسَيُجَنَّبُهَا الْأَتْقَى ﴿١٧﴾

17. Na ataepushwa nao mwenye taqwa.

الَّذِي يُؤْتِي مَالَهُ يَتَزَكَّىٰ ﴿١٨﴾

18. Ambaye anatoa mali yake kujitakasa.

وَمَا لِأَحَدٍ عِندَهُ مِن نِّعْمَةٍ تُجْزَىٰ ﴿١٩﴾

19. Na hali hakuna mmoja yeyote (yule) aliyemfanyia fadhila yoyote hata amlipe.

إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ رَبِّهِ الْأَعْلَىٰ ﴿٢٠﴾

20. Isipokuwa kutaka Wajihi wa Rabb (Mola) wake Aliyetukuka.

وَلَسَوْفَ يَرْضَىٰ ﴿٢١﴾

21. Na bila shaka atakuja kuridhika.





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com