011 - Hadiyth Ya 11: Daraja Za Iymaan Ni Sabini Na Kitu; Ya Juu Ni Tawhiyd, Ya Chini Ni Kuondosha Taka Njiani

011 - Hadiyth Ya 11: Daraja Za Iymaan Ni Sabini Na Kitu; Ya Juu Ni Tawhiyd, Ya Chini Ni Kuondosha Taka Njiani


عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ  (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صلى الله عليه و آله وسلم):  ((الإيمَانُ بِضْعٌ وَسَبْعُونَ)) أَوْ ((بِضْعٌ وَسِتُّونَ شُعْبَةً, فَأَفْضَلُهَا قَوْلُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ,  وَأَدْنَاهَا إِمَاطَةُ الأَذَى عَنْ الطَّرِيقِ, وَالْحَيَاءُ شُعْبَةٌ مِنْ الإِيمَانِ)) متفق عليه.
Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه) amesema: Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Iymaan ni sabiini na kitu[1])) au alisema ((Tanzu sitiini na kitu. Ilio bora kabisa ni kauli ya ‘Laa ilaaha illa-Allaah’, na ya chini kabisa ni kuondosha taka njiani. Na kuona hayaa ni utanzu katika tanzu za Iymaan).[2]
 
 
  1. Waumini wanatofautiana katika daraja za Iymaan zao.
 
  1. Umuhimu na fadhila ya tawhiyd (kumpwekesha Allaah سبحانه وتعالى) ambayo ni asili ya Iymaan [Al-An’aam 6: 102, Al-Baqarah 2: 163, Twaahaa 20: 14, Al-Qaswas 28: 88, Ghaafir 41: 65].
 
وَلَا تَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ ۘ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ كُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ ۚ لَهُ الْحُكْمُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ .
Na wala usiombe pamoja na Allaah ilaah mwingine. Hapana ilaaha ila Yeye. Kila kitu ni chenye kuhiliki isipokuwa Wajihi Wake. Ana Hukumu (ya mambo yote) na Kwake mtarejeshwa[3]
 
  1. Iymaan na vitendo vinakwenda sambamba, ni vitu viwili ambavyo haviwezi kutengana.
 
  1. Kuona hayaa ni katika Sifa za Waumini. Haya inahusiana na tabia njema kwa sababu inamzuia mtu kutenda maasi yote na inamweka kwenye hali ya utiifu wakati wote. [Rejea Hadiyth namba 69]. 

  1. Kuwa na hayaa ni dalili ya ukweli wa Iymaan ya Muislamu.
 
  1. Asidharau Muumin kutenda jambo jema lolote hata dogo mno vipi kama kuondosha taka njiani. [Al-Ambiyaa 21: 47, Al-Zalzalah 99: 7].
 
  1. Kukosekana haya ni kukosekana Iymaan, hivyo kunamfanya mja afanye lolote atakalo. Imepokewa kwa Abu Mas’uwd ‘Uqbah bin ‘Amr al-Answaar al-Badriy (رضي الله عنه) amesema: Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hakika katika maneno yaliyopatikana na watu kutokana na Mitume ni: Usipokuwa na hayaa, basi fanya utakalo)).[4]
 
 
 



[1]  "Bidhw’" ni idadi baina ya tatu na tisa.
[2]  Al-Bukhaariy na Muslim.
[3]  Al-Qaswasw (28: 88).
[4]  Al-Bukhaariy.